„Jumapili 13. Mwezi wa kumi na moja 1904 [imepigwa mstari] [...] hivi karibuni nimepata mapambo ya mikono: 1. Bangili ya Schenzi [Schenzi = Suaheli], nimeikuta kijijini ni kuukuu na mg‘ao, [mchoro] 2. Bangili ya kuvaliwa mkononi kwa juu [masahihishao: bangili, bangili ya paja] waya wa shaba (kamba ya utumbo iliyozungushwa waya zimeletwa kutoka Bondei na huitwa "dodi" [masahihisho Madodi ] kwa Wa Schenzi na "Talli" kwa Kiswahili). Zawadi kutoka kwa Bwana Krockenberger pale Derema [mchoro] 3. bangili,kibanda kinene cha shaba kilichozungushwa kimenunuliwa kwa Rupie 1 kutoka kwa Mswahili inaitwa „Talli“ . Kwa ufahamu wangu mimi Waswahili wanaita utepe wa waya Madodi au Dodi na bangili ya shaba nzito huitwa Talli (Baumann, O. Usambara. Berlin 1891. u. 31) [mchoro] [...]" [Utafsiri]
chanzo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 43 (95) mwandishi: Karl Braun
“2. Bangili ya kuvaliwa juu karibu na bega dodi shaba / Amani 13 mwezi wa kumi na moja.1904 / kamba ya utumbo imezungukwa na waya imetengenezwa Bondei „talli“. „dodi = bondei“. TB 43,95 [mchoro]" [Utafsiri]
chanzo: Museen Stade, r 2018 / 18566 mwandishi: Karl Braun
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).
chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:14:22+01:00
Maoni
Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.