Wakati
1909-04-05
Maelezo
„Jumatatu 5. Mwezi wa nne 1909 [imepigwa mstari] Kwenye maabara asubuhi nimefanyia kazi mzigo wa mimea, mchana mafaili. – nimepata rungu zuri liliochongwa lilizungishwa na misumari ya shaba. (= 1 Rp. 50) mapambo ya kuchonga ni kama yale yanayopatikana kwa N* [1] wa hapa hasahasa kwenye vitu vya ""Lewa"". Kigeni kwangu yalikuwa mapambo yale ya mawimbi na pinde. Mnyama ni kenge (Kenge [?]) kama wanavyoishi porini. Mpini umegongeshwa na fedha au shaba nyeupe kwa chini. Kitu hicho ni kuukuu kina rangi ya kawia iliyokolea na kinatoa harufu ya mafuta amabayo wa Masai wanayapaka kwenye vitu vyao. Kwa vyovyote vile umetengenezwa kwa umakini usio wa kawaida (mchoro na vipimo 36 cm, 20 cm. Kofia mbaja masai wetu wa farasi aliyeniuzia kitu hicho akadai ni fimbo ya sultani wa ki Masai na kinaitwa ""es sēre"". Neno hilo linapatikana kwa Merker, Die Masai, Berlin 1904, u. 130 lakini hakuna picha ya fimbo kama hicho. Nategemea ikiwa Merker angeiona angeichora. Hayo yananifanya nifikiri kwamba pamoja na kwamba nimeinunua kwa Masai labda inatoka kwingineko. " [Utafsiri]
[1] The N-word (N*) is a highly racist term used to refer to Black people. The term originated in the context of ""racial"" theories and is closely linked to the history of slavery and colonialism. In the transcription of original sources, it has not been reproduced but instead marked as a racist, derogatory, and offensive term.
chanzo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 53 (44)
mwandishi: Karl Braun
Mtu
-
unknown actor
(Mchuuzi)
-
Braun, Karl (* 1870 † 1935)
(Mnunuzi)
GND Explorer
Mahali