Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/1

Mundu

Sammlung Braun
r 2018 / 18486
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18486
Kichwa
Mundu
Vipimo
Urefu: 19cm
Nyenzo
Chuma
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_596405a9-6f9c-4d4f-97f7-4c1abe70f90c
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uainishaji
Zana/vifaa (ujenzi wa meli)  
Uzalishaji
Wakati
mpaka ca. 1920
Mtu
  • Person (Mtengenezaji)
Mahali
  • Tansania
Acquisition:
Wakati
ca. 1904 - ca. 1920
Mtu
Mahali
  • Tansania
Malipo
Mtu
Nambari za hesabu za zamani
  • 294
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
Mahali
  • Stade
Scientific use:
Wakati
2023-06-09
Maelezo
I: Hapa nina picha ya mwisho kwako ambayo imesajiliwa kwa namba 2018_18486_001 hebu angalia hicho ni kitu gani? R: Hii picha inanijia I: Angalia tu vizuri hata usiwe na haraka R: Hiki wanaita nyengo I: Wanaita kama? R: Kuna kitu kinaitwa nyengo R: Maana hapa kina kata hapa na nyengo ninayo humu ndani I: Wewe angalia vizuri hiyo sasa niya miaka hiyo siunajua vitu vinaenda vinabadilika badilika sasa wewe angalia? R: Hiki ni kisu bwana kinaitwa nyengo I: Nyengo? R: Eeeeh I: Ahaa hahahha haya hebu tuambie nyengo ni kilugha gani? R: Nyengo bwana ni jina la watu wa bara I: Watu wa bara kabila gani? R: Sanasana tuliowazoea sisi walikuwa ni wabena I: Wabena? R: Eeeeeh I: Ambayo maana yake ni nini nyengo? R: Nyengo ni aina ya kisu kilichopindishwa hapa juu eeh I: Kinatumikaje? R: Hiki kwa kufyekea, kukatia kama majani kufyekea kwenye maua hii nyengo hili jina la nyengo nila kuja I: Kwa mazingira ya Amani inajulikana kwa jina gani? R: Hiyo hiyo nyengo I: Nyengo? R: Eeeeh I: Kwahiyo jina hilohilo liliendelea? R: Liliendelea hilo mpaka kesho I: Mpaka leo inaitwa nyengo? R: Nyengo eeeh sanasana kwa watu wanaofanyakwenye michai I: Kwenye michai wanatumia zaidi kufanyia nini? R: Pruning wakati wa pruning ile anashika hapa maana ile pruning ya mchai haitakiwi ikatwe level inatakiwa ikatwe hivi ili kwasababu maji pale yasitue eeh sasa walikuwa wanatumia visu hivi I: Kukatia michai? R: Eeeeh kukatia chai I: Sawasawa na watu gani hasa walikuwa wakitumia nyengo kati ya wanawake na wanaume mzee [anonymous]? R: Wanaume I: Kwanini wanaume? R: Unajua baadhi ya kazi zamani tuligawana sasa hii kazi ya kutumia nguvu kidogo walikua wanafanya wanaume eeh I: Kwahiyo inahitaji mtu mwenye nguvu? R: Eeeeh mwenye nguvu I: Hakukuwa na wanawake wenye nguvu kipindi hicho hahhha maana siku hizi kuna wanawake wanapiga kazi kuzidi wanaume? R: Hapo zamani kazi ya udereva lakini dereva mwanamke utamkuta wapi sasa hivi hapa pia nyengo uchukue hiyo anakata hivi hapa I: Kwahiyo sasa hivi wanaweza wakatumia? R: Wanatumia wanakata I: Lakini kwa kipindi hicho? R: Mwanamke alikuwa hashiki nyengo I: Kuanzia umri gani walikuwa wanatumia nyengo? R: Tuseme kuanzia miaka tusemae ukishakuwa mtu ambaye sanasana vijana kwenda mbele vijana eeh miaka 30 kwenda mbele I: Sawasawa unadhani ikafika wakati nyengo ikawa haina thamani ya kuhitajika katika maisha yetu kwasasa? R: Kwa kazi tulizo nazo bado itatumika I: Kama kazi gani ambazo zinahitaji kutumia nyengo? R: kwamfano kama mifugo kukata majani ya ng’ombe I: Ndiyo R: Maana hizi ziko aina mbili kunai le iko kama ina meno kama msumeno siunaitambua hiyo eeh I: Ndiyo R: Na hii eeh zinatumika zote I: Kwahiyo sababu ya kuendelea kufuga kukatia majani itaendelea kutumika na kuhitajika kwenye jamii? R: Itaendelea kuhitajika kwasababu mchai mpaka leo upo I: Ndiyo R: Utaendelea kuhitajika nyengo I: Nyengo zinaendelea kutengenezwa kwa hapa Amani zinaweza zikawa zinatengenezwa wapi nyengo? R: Hapa umpate fundi umpelekee chuma chako bwana nitengenezee nyengo hapa lakini kukuta mtu tu anatengeneza nyengo anauza pale bado hatujaona kwa wakati huu kwenye hii jamii yetu ya saivi I: Kwahiyo mpaka uihitaji? R: Mpaka uihitaji au usubiri zitoke hukohuko zilikotengenezewa I: Na hasa kwa watu wa Amani wanazipatia wapi? R: Kwa hawa watu wanaokuja nazo kwa mfano kule kwenye mashamba ya mpunga siwanatumia zile zenye msumeno humu I: Zenye msumeno, msumeno? R: Eeeeh kule kwenye mashamba ya mpunga kwa ajili ya kukatia mpunga kwahiyo kwenye mashamba hayo zinatumika sana I: Zinatokea mkoa gani hasa nyengo? R: Kwa wastani kama zinatoka kwa wenzetu I: Sawasawa na unadhani nyengo zilikuwa zinatengenezwa na watu gani wa kike au wakiume mzee [anonymous]? R: Wanaume eeh I: Kwasababu ya hizo R: Eeeeh I: Hahahhahha sawasawa na unaweza ukasema unaweza ukatuambia kitu gani kilikua kinatumika kutengenezea nyengo? R: Ni chuma kama hivi na mti unaweka mpini I: Mti wa aina yoyote? R: Mti wa aina yoyote kwa sisi huku ulikuwa unaitwa mkabera, mkabera unavumilia msumari hata ukigongwa I: Hata ukigonga? R: Eeeeh I: Sawasawa nyenzo zilizokuwa zinatumika kutengenezea nyengo zilikuwa zikibadilika au miaka yote mpaka sasa hivohivo chuma na mti? R: Jinsi mambo yanavokwenda kuna mabadiliko yanayojitokeza material wanatumia material wanatumia material hizo kuwa hii bwana ni nzito hii bwana inashika kutu hii bwana haishiki makali inapukutika tumia hii I: Kitu gani kinapelekea watumie vitu ambavyo havishiki kutu au nini hebu tuelezee hapo mzee [anonymous]? R: Na kazi unayoifanya kuna kazi za majimaji kazi nyingine yani ni kavu I: Ndiyo R: Eeeeeh hazina maji kazi nyingine I: Nyengo hiyo unaiona ya miaka 100 iliyopita kwasasa ikiletwa kulingana na mabadiliko inaweza ikauzwa shilingi ngapi kwa jinsi ilivo hapa hahhaha hebu tuambie mzee [anonymous]? R: Ukipata fundi mtundu hapa anatoa mbili hahhahha I: Hahhahhahha kwahiyo hii inaweza ikauzwa shilingi ngapi hhahhha kwa jinsi unavyoiona hapo mzee [anonymous]? R: Hahhahha kwa sasa I: Eeeeeeh R: Linaonekana ni zito hili lakini ninavoelewwa siku hizi wanajeuri wanaweza wakasema sinunui anaweza akakuuzia bei ya panga elfu 7 I: Kutokana na material yake? R: Eeeeeh anaweza akakuambia shilingi elfu 7 I: Sawasawa basi mzee [anonymous] sisi tunashukuru kwako wewe tutakuwa tumemaliza R: Vizuri sana I: Asante sana kwa ushiriki wako R: Na mimi nashukuru I: Haya

chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023, Interview No. 04
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
Mahali
  • Amani
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1909-04-05, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 53 (43 )jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566 (123)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1905-02-24, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 44 (68)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Baun, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1905-02-24, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 44 (68)jifunze zaidi
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:41:30+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji