Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/1

Pembe yenye kamba ya ngozi

Sammlung Braun
r 2018 / 18284
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18284
Kichwa
Pembe yenye kamba ya ngozi
Vipimo
Urefu: 31cm
Nyenzo
Ngozi,
Pembe
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_66a2c32d-9284-45cc-8a56-7b5db483d952
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uzalishaji
Wakati
mpaka ca. 1920
Mtu
  • Mtu, haijulikani (Mtengenezaji)
Mahali
  • Tansania
Acquisition:
Wakati
ca. 1904 - ca. 1920
Mtu
Mahali
  • Tansania
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
Mahali
  • Stade
Scientific use:
Wakati
2023-09-29
Maelezo
I: Sawa asante nina picha nyingine hapa ambayo imesajiliwa kwa namba 2018_18284_1 hebu ishike mzee [anonymous] hiyo nikumbushe jina lake hicho kitu? R1: Hii ni chupa ya pembe ya kubebea baruti inaitwa esekekwa engiteni yani engiteni ni ng’ombe. I: Kwahiyo ni pembe ya ng’ombe? R1: Eeeh pembe ya ng’ombe imetengenezwa kama chupa na hii naona imefungwa kabisa mkanda hii niya kufunga mkanda kubeba hivi kwa ajili ya kubebea baruti tu na siyo kwa matumizi mengine. I: Na kabila la kimasai walikuwa wanatumia pia baruti? R1: Eeeh waliokuwa Wanakaa Handeni walikuwa wanatumia pia baadhi ya huku baada ya kujua kuna kitu hiki kinaitwa bunduki nao kutoka huku baadhi walienda kuchukua wakaja nayo mpaka huku. I: Aha esekekwa engiteni? R1: Na ndiyo sisi kwasababu tumeona kwasababu sisi hatukuishi Handeni na baba yetu pia hakuishi Handeni lakini babu yetu mzaa baba alikuwa yupo Handeni na ndiyo maana wakajua kitu kama hiki eeeh. I: Na ulishawahi kuiona kwa macho? R1: Ndiyo nilishawahi kuiona kwa macho. I: Kwahiyo inatengenezwa na pembe peke yake na kitu gani kingine? R1: Pembe na ngozi. I: Ngozi? R1: Eeeh. I: Ya mnyma gani ngozi? R1: Huwa sisi tunatumia sana ngozi ya ng’ombe. I: Kwasababu ni ngumu? R1: Eeeh ngozi ya ng’ombe na ndiyo tuko nayo hatuna ngozi nyingine ng’ombe, mbuzi na kondoo sasa ngozi ambayo ni ngumu ni ngozi ya ng’ombeni imara hata ukitengeneza inakaa kwa muda mrefu. I: Kwahiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kubebea baruti tu? R1: Eeeeeh ila kuna kingine kama hiki ambacho kina bebea ugoro lakini ni kidogo siyo kikubwa kama hichi na pia kinatengenezwa kwa upembe na ngozi pia. I: Kwahiyo ikiwa kubwa kama hiyo ni kwa ajili ya baruti? R1: Eeeh ikiwa kubwa kama hii ni kwa ajili ya baruti ndogo ni kwa ajili ya ugoro hayo ndiyo matumizi yake. R2: Ni kama hii inatengenezwa kwa kulishia watoto wa kimasai mafuta wewe ushawahi kusikia watoto wa kimasai wanalishwa mafuta? I: Samli? R2: Samli lakini ni mbichi haijachemshwa inatingishwa inatolewa hii nyeupe ni siagi inakuwa na pembe kama hivi. I: Inatengenezwa hivohivo pia? R2: Eeeeh inahifadhia chakula cha mtoto mdogo mwenye mwaka 1 kuendelea mbele ndiyo kinachotumika kutunza mafuta. I: Kwahiyo utengenezaji ni huo huo matumizi ndiyo tofauti? R2: Eeeeh matumizi tofauti kwasababu kama ile ya mtoto isingekuwa na huu mkanda ingekuwa ipo kama hivi peke yake. I: Kwahiyo kinachotofautisha ni huo mkanda? R2: Eeeeh ni huo mkanda. I: Esikweka engiteni? R2: Eeeh esikweka engiteni. I: Sawasawa kwahiyo kwahiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kubebea baruti au kuwekea mafuta ya mtoto? R2: Eeeh ya mtoto mchanga yule ambaye ananyonya na pia kuwekea ugoro ndiyo inatumika hivyo. I: Kwahiyo hiyo ya kuwekea mafuta ilikua ni mtoto kuanzia umri gani mpaka umri gani mzee [anonymous]? R2: Anapozaliwa tu mpaka miaka 3 unaweza ukampa tu. I: Wakati huo ananyonya pia? R2: Eeeh ananyonya. I: Na kazi yake nini hayo mafuta? R2: Yanajenga afya ya mtoto ni chakula kwa mtoto kwasababu kulikuwa hamna uji wala nini kwahiyo kwahiyo ni yeye na maziwa ya mama alafu analishwa na mama yake kwasababu ni mtoto mama anamlisha kwa kidole analishwa analishwa na mtoto anameza hadi anashiba kabisa mtoto. I: Ni siagi ya ng’ombe hiyo? R2: Eeeh siagi ya ng’ombe yanakamuliwa maziwa yanagandishwa alafu yakishagandishwa yanatingishwa yanagawanyika maziwa na yanabaki siagi yanakuwa meupe hayajakangwa yanaekwa hapa alafu analishwa mtoto. I: Sawasawa na bado inatumika hii esekekwa kwa sasa hivi? R1: Kwasasa hivi haitumiwi. I: Kwanini haitumiwi kwasasa hivi? R1: Vitu vimekuwa ni vingi kuna vitu vimechukua mbadala wake wachina wanaleta esekekwa siyo kuchonga tena hahahhha unavikuta special tu kwahiyo watu wanasahau vya kitamaduni wananubua special. I: Wachina sahivi mzee [anonymous] wanaharibu mila? R2: Wanaharibu mila kweli kulikuwa na hot pot zamani sasa hivi wameleta hot pot zao na contena za kuwekea vitu vingi hata vile vya asili vimetoweka wamasai kulikuwa kuna nyama wanaweka kwenye contena zao inachukua hata miezi sita nyama bado ipo vizuri sasa hivi wameleta friji. I: Haina kazi tena hiyo hahha? R2: Haina washa haribu. I: Kwahiyo hii kwa ajili ya kubebea baruti walikuwa wanabeba wanaume au wanawake katika jamii yenu ya kimasai? R2: Wanaume. I: Wa umri gani hasa? R2: Mtu yoyote mwenye nguvu ya kuweza kutumia bunduki haichagui ni mzee ni kijana ni mtu wa umri wowote mwenye uwezo na nguvu ya kutumia hiko kifaa ana tumia katika jamii yetu ua kijamii. I: Sawasawa na wanaotengeneza walikuwa wa kike au wakiume? R2: Wakiume. I: Hawana umri maalumu pia? R2: Hawana umri maalumu ni kulingana tu na ufundi wako. I: Kwahiyo ilikuwa pembe ya ng’ombe tu na ngozi yake? R2: Eeeh anachonga yani ni ufundi kweli kweli.

chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 04
mwandishi: I: Mohamed Seif, R1, R2: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Lunguza

Rejeo la ndani la kitu

Pembe yenye kamba za ngozi

Pembe yenye kamba za ngozi

r 2018 / 18296
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:35:33+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji