Wakati
2023-10-04
Maelezo
I: Nina picha nyingine hapa ambayo imesajiliwa kwa namba 2018_18205_1 hii kuna mmoja wenu aliitambua pia inaitwaje hii?
R3: Engimeta
I: Nani anaweza kutuambia engimeta inatumikaje?
R2: Hii engimeta ni mama ndiyo anashona na enopini ndiyo anashonea msichana kwahiyo unashona kama niya msichana wako unashona hiyo unaweka lukaria alafu unampa msichana avae.
I: Msichana ambaye ameolewa au ambaye hajaolewa au msichana kwa kimasai ni yule ambaye hajaolewa?
R2: Ni msichana ambaye hajaolewa.
I: Anaivaa sehemu gani?
R2: Kiunoni.
I: Anavaa kiunoni?
R2: Eeeeh.
I: Kwa ndani ya mwili au nje ya mwili?
R2: Anavaa nje ya nguo.
I: Na unaweza kutuambia huo mshono unaitwaje?
R2: Hauna jina huu mshono.
I: Anavaa mpaka muda gani akiolewa bado anaendelea kuivaa hiyo engimeta au anaachana nayo?
R2: Akishaolewa siyo msichana tena kwahiyo anaitoa.
R3: Engimeta mama ukishamzaa binti utamuangalia akishafikia umri wa miaka 10 utaona kwamba huyu anahitaji kuwa na engimeta kwahiyo unaanza kuandaa ngozi yako na kukata ili umtengenezee engimeta ukishatoa kiasi ya kiuno chake unaishonea ushanga alafu unampa anavaa akishafika ule umri wa kuwa siangiki sasa siyo binti tena na hafai kuvaa tena hiyo engimeta kwasababu sasa nimaandalizi ya kuolewa sasa anaacha nyumbani yeye anaenda kuolewa.
I: Anamwachia nani?
R3: Msichana mwingine ambaye ni mdogo wake.
I: Kwahiyo akiolewa haiendi nayo kwa mume wake?
R3: Eeeh haendi nayo.
I: Ilikuwa ina umuhimu gani engimeta?
R1: Engimeta ina maana kadhaa engimeta msichana akiwa mkubwa haruhusiwi tena kwenda sehemu inaitwa esoto kwenda kuungana na morani bila engimeta hiyo ndiyo maana yake katika jamii ya kimasai.
I: Inaitwaje?
R1: Esoto, na esoto ni sehemu ya mkusanyiko wa morani na wasichana, msichana kama anenda kulala na morani anaweza kutoa ile engimeta ataiweka juu ya kitanda kuna mbao ambayo iko juu ya kitanda zamani sisi ambavyo ilikuwa nyumba ya matope siyo sasa kwa ambaye ana ya majani au mabati hapana zamani kuna nyumba za matope ambayo inatengenezwa inawekwa matope na majani hivi na unafunika na matope huyo msichana anaenda kuiweka kwenye kitanda ambacho analala naye na morani pamoja hairuhusiwi msichana ambaye amekuwa kwenda kulala na morani lakini awe na engimeta inatakiwa iwe inaninginia kwenye kitanda kwahiyo engimeta hakuna mama ambaye anaona mtoto wake amekuwa lazima anatoa ngozi yake anapasua anatoa hii ngozi anashonea msichana wake engimeta baada ya kumaliza anafanya kama hivyo namba tatu anaweka udongo ambao unaitwa lukaria anatengeneza lukaria alafu anaweka kwanza mafuta ndani siyo nje ya shanga ndani ya ngozi ataweka lukaria ataweka kamba nyingine ndefu itakuwa tayari anampa mtoto wake avae hairuhusiwi kama mtoto amekuwa ameenda kwa mume wake haruhusiwi tena kuvaa ushanga kama waswahili maana waswahili sasahivi mwanamke ambaye ni mwanamke wa mtu anavaa ushanga ndani ya sketi ndani ya kiuno lakini wamasai hawaruhusiwi mpaka sasa hivi kwahiyo ina maana sana kwa msichana wa jamii ya kimasai hii engimeta.
R3: Engimeta ina mambo mengi mazuri na engimeta ina umuhimu mwingi kwa mfano pia kwa wanaume wanavopelekwa jandoni akiwa bado hajawa morani akiwa kwenye stage ya sipolio sasa ndiyo ameshaenda tu jando sasa lazima avae engimeta na hiyo ndiyo inamfanya sasa huyu mwanaume kuonekana tayari ameshaenda jando na amekuwa na vile vile kwa msichana akivaa anaonekana pia amekuwa mkubwa kwahiyo ina baraka kama hizo katika vijana wa jamii hii ya kimasai.
I: Kwahiyo hiyo inavaliwa na mtu ambaye ameshaenda jando?
R3: Kwa wanaume ndiyo anavaa akienda jando lakini kwa wasichana ni kwamba ni ile hali ya kuonekana tu amekua lakini hajafanyiwa tohara na morani akishatolewa nywele spolio na yeye anarudisha hii.
I: Kwahiyo akisha nyolewa anavua hii?
R3: Eeeeh.
I: Na umesema inavaliwa juu ya nguo?
R3: Eeeh juu ya nguo.
I: Ni nguo aina yoyote anaweza akavaa?
R3: Eeeeh nguo yoyote kama orekelaa maana orekelaa ni ngozi maana kuna watu wanavaa ngozi anafunga kiunoni.
R1: Kwasababu zamani sisi kama tunavaa engimeta na orekelaa tunaenda sikukuu hatutavaa nyingine juu hivi hata kama ana matiti kiasi gani anavaa ushanga anavaa orekelaa hapa kiunoni na anaweka engimeta ili aende kwenye sikukuu kwahiyo ina maana sana katika jamii yetu hii ya kimasai.
I: Bado hii inatengenezwa mpaka sasa hivi?
R1: Mpaka sasa hivi.
I: Na inatumika kwa utaratibu huo huo mlioueleza?
R1: Kabisa.
I: Kwahiyo wanaoshona hii ni wakina mama?
R1: Ni mama.
I: Mama yake na binti?
R1: Mama yake binti au kama yeye mwenyewe ana kazi nyingine anaweza kumuomba rafiki yake amsaidie kumshonea binti yangu engimeta analeta na ushanga wenyewe wanasaidia kushona lakini wanasaidiana tu siyo kwa namna nyingine tunasaidia tu kama kazi nyingine kwenye jamii.
chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 10
mwandishi: I: Mohamed Seif, R1, 2: Anonymous
Mtu
-
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
-
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali