Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/1

Manyanga

Sammlung Braun
r 2018 / 18279
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18279
Kichwa
Manyanga
Vipimo
Upana: 13cm, Urefu: 18cm
Nyenzo
Fiber ya mimea
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_724c7066-8844-4850-bab2-07c453f12e37
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uainishaji
Vyombo vya muziki  
Uzalishaji
Wakati
mpaka ca. 1920
Mahali
  • Tansania
Acquisition:
Wakati
ca. 1904 - ca. 1920
Mtu
Mahali
  • Tansania
Malipo
Mtu
Nambari za hesabu za zamani
  • 275
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
Mahali
  • Stade
Scientific use:
Wakati
2023-06-10
Maelezo
I: Sawa nina picha nyingine hapa imesajiliwa kwa namba 2018_18279_001 hebu angalia unaweza ukatambua ni kitu gani hichi mama? R: Mkoba I: Ni nini? R: Mkoba I: Mkoba ni kilugha gani hicho? R: La kisasa lakini zamani tunaita mfuko I: Mfuko kwanini mlikuwa mnaita mfuko? R: Hawa wenzetu wanavyoita mkoba hivyohivyo ee I: Kwahiyo mfuko na mkoba ni kitu hichohicho? R: Kimoja I: Ni kabila gani wanaita mkoba? R: Kisambaa I: Kisambaa wanaita mfuko? R: Eeeeh I: Ni ulikuwa unapatikana zaidi mikoa gani mifuko kama hii? R: Tulikua tunanunua sehemu za Muheza, Tanga I: Muheza na Tanga? R: Eeeeh I: Ulikuwa unatumikaje huo mfuko? R: Ni mkoba tu wa kutembelea kwenda sokoni basi I: Unatembelea kwenda sokoni, sokoni unaenda kufanyia nini? R: Kuwekea vitu I: Vitu kama nini? R: Mboga, kuna nazi kuna vitu vyote vinavyotumika ndani I: Mkoba kama huo unaweza ukatumikaje kwa namna nyingine ukiachia kwendea sokoni? R: Huu I: Eeee R: Kwa namna nyingine sijui mimi najua kuwekea vitu tu I: Kuwekea vitu tu? R: Eeeeh kuna mikoba ya uchawi sasa hiii sisi tunatumia kwa kuwekea vitu I: Lakini wengene wanatumia kufanyia nini? R: Kwa uchawi I: Uchawi? R: Eeh anaweka vitu vyake humo ndiyo unakuwa ni mfuko sasa I: Mfuko? R: Eeeeh I: Hebu tuweke tofauti ukiwa ni mkoba ni kwa matumizi ya nini? R: Ndani I: Ukiwa ni mfuko? R: Ni hivyo hivyo matumizi ya ndani I: Ya ndani? R: Eeeh I: Umesema mfuko unawekewa uchawi? R: Eeeeh I: Na mfuko nao unawekwa uchawi? R: Eeeeh lakini zamani walikuwa wanatumia sana vikoba hivi eeh kuwekea vitu vyao vya kiganga I: Vya uganga? R: Eeeeh I: Ahaaah R: Lakini sisi tunatumia kuendea sokoni na kuwekea vitu vyako basi I: Kwenye vya uganga walikuwa wanatia nini sana humo R: Humo ndani I: Eeeeeh R: Kuna yale mapembe uliyoyaona sisi situmeuguliwa maana kwa kuuguliwa tumepitia kwa kweli lakini saivi sasa hata I: Kwahiyo ulikuwa unatumika kwa matumizi mawali R: Eeeeh I: Kununulia vitu masokoni? R: Na wengine wanawekea uganga wao wasili I: Uganga wao? R: Eeeeh I: Kwahiyo wanaowekea uganga ni wale wanaotibu kwa kutumia waganga wa jadi? R: Eeeeh waganga wa jadi I: Inakuwa kama nini hasa? R: Wanahifadhia vitu vyao I: Na jinsia gani walikua wanatumia Zaidi mikoba hii? R: Wakike I: Wa kike? R: Eeeeh I: Wa kike wa umri gani? R: Wa kina mama wazee tu I: Wazee? R: Ndiyo wanaofanya kazi hii eeh I: Eeeeh I: Na wanaounda watu gani? R: Watu wa bara? I: Makabila gani hasa? R: Hao hao niliokutajia I: Nikumbushe umenitajia makabila mengi kidogo nimeshayasahau? R: Wafipa wamambwe, wanyakyusa, na wanyamwanga I: Wafipa ni sumbawanga, na wanyakyusa? R: Ni huko wanaita sikujui I: Mbeya ni mbeya au Iringa wanyakyusa Mbeya, wanyamwanga R: Na wamambwe I: Wamambwe ndiyo walikuwa wakitumia zaidi hiyo R: Eeeeh I: Wao walikua wanatumia zaidi kwa ajili gani? R: Kama hapo Monga walikuwa wanauza I: Kwenye masoko? R: Eeeeh I: Soko la siku gani walikua wanauza Monga? R: Jumamosi na jumatano I: Jumamosi na jumatano? R: Eeeh I: Waneleta mpaka leo? R: Saivi ahhh ni muda taingia sijafikisha watoto wangu wawili I: Lakini soko bado lipo? R: Soko lipo si hilo banda hapo lile banda kubwa pale I: Ila mikoba kama hiyo hailetwi? R: Hamna saivi I: Aaaaah R: Saivi hata mkeka hauukuti I: Kwahiyo kwa mawazo yako unadhani haitumiki tena au? R: Haitumiki imekufa I: Kwahiyo hata watu wa uganga hawaitumii pia? R: Sijui sasa kwa waganga ee maana saivi siwanasema wanaenda na mtandao I: Hahahahah hata kwenye uganga napo wanatumia mtandao? R: Mtandao eeh kwasababu kila kitu kinabadilika I: Hahahaha R: Maana akiuweka mkoba wake anajulikana anasafiri kumbe anaenda kutibu I: Hahahahah ni mtandao siku hizi? R: Eeeeh maana akiweka hivi atajulikana ni mganga hahahhahah I: Hahaaha kwahiyo humo ndani walikuwa wanahifadhia mapembe ana kitu gani kingine walikuwa wanaweka humo? R: Humo kuna vichupa, mapembe sisi tumeuguliwa kwahiyo vikitolewa unaona I: kilikuwa na umuhimu gani mkoba huu ulikuwa na umuhimu gani kwa makabila uliyoyataja? R: Wao ni kwendea sokoni kwa kweli I: Sawasawa kwasasa havitengenezwi? R: Sahivi hamna I: Na waliokuwa wanatengeneza mikoba kama hiyo ni jinsia gani wa kike au wakiume? R: Wa kike I: Wa kike? R: Eeeeh I: Kwanini walikuwa wanatengeneza wa jinsia ya kike? R: Wanatafuta hela I: Wanatafuta hela? R: Eeeh I: Wakiume walikua hawatafuti hela? R: Mwanaume ni pombe na yeye I: Hahahaha kwahiyo akina mama ndiyo walikuwa wanatafuta hela kipindi hicho cha zamani ndiyo watafutaji? R: Eeeeh I: Wanaume wao kazi yao ni kunywa pombe tena kwenye pembe? R: Eeeeh I: Hahahahah sawasawa na unaweza ukatambua walikuwa wanatengeneza kwa kutumia vifaa gani? R: Walikua wanatengeneza sindano lakini siyo sindano hizi za kushonea kuna sinda no zenyewe wanazotumia eeh I: Na haya material gani wametumia hapa? R: Wamesuka hapa wamezungusha siyo ukindu lakini ni huu niliokuambia wanashona virago I: Virago? R: Eeeeh madude yako humo mtoni I: Wanaitaje? R: Sijui Jina Lake I: Sawasawa na miaka yote mpaka mara ya mwisho unaacha kuona vitu vilivokua vinatumika vilikuwa ni hivo hivo? R: Eeeeh I: Haujawahi kuja wa tofauti? R: Hapana I: Maana siku hizi kuna plastiki R: Eeeeh saivi hamna I: Mkoba kama huo ukiukuta sokoni kwa sasa hivi na wewe unaujua vizuri unaweza ukaununua kwa shilingi ngapi? R: Saivi wanakuuzia wanakwambia elfu tano zamani tulikuwa ni elfu moja, au elfu tatu ndiyo mwisho eeh I: Kwahiyo saivi umepanda bei? R: Eeeh utaambiwa elfu tano I: Kwanini bei inakuwa imepanda saivi? R: Si mtandao I: Hhahahaha mtandao ndiyo umepandisha bei? R: Eeeh watu wanaenda na mtandao I: Mtandao? R: Eeeeh I: Sawa basi mama sisi tuchukue muda huu kukushukuru kwa ushiriki wako umetusaidia kweli tumepata taarifa ya baadhi ya picha zetu hapa umechangia kwa kiasi kikubwa sana R: Au siyo I: Eeeee asante sana kwa ushiriki wako tukikugongea tena wakati mwingine utupokee kwa mikono miwili R: Si ndiyo sawa I: Hahahahah

chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Amani

Rejeo la ndani la kitu

Manyanga

Manyanga

r 2018 / 18272
Rejeo la ndani la kitu
Kuhusiana na
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:13:15+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji