Wakati
2023-09-15
Maelezo
I: Sawa tunaenda kwenye picha nyingine ambayo imesajiliwa kwa namba 2018_18542-1 hii mlisema inaitwa?
R1: Ingimeta
I: Ingimeta hii ya kwanza hapa
R1: Eeeh hii ya kwanza
I: Sawa hii ingimeta inatumikaje?
R2: Hii niya wasichana na ndiyo mkanda wao ukishafikisha miaka 9 msichana anatengenezewa hii anaanza kuivaa na ndiyo mkanda wake kabisa
I: Hii ya emutha
R1: Hii emutha emborosi anaifunga kiunoni ndani yake wanavaa wanawake wa kawaida tu ndiyo wanavaa
I: Kuanzia umri gani hii ya kufunga kiunoni?
R1: Kuvaa akiwa na miaka 10, 15, 20 ila akishafika umri wa kuolewa anaacha zote mbili anaingia kwenye utu uzima eeh anaenda ukubwani kwahiyo havai tena hizo anawaachia watoto ndiyo wavae
I: Kuna nyingine anavaa tofauti na hizo?
R1: Mkanda, sikioni na ushanga
I: Kwahiyo hizi ni bado akiwa binti?
R1: Bado ni msichana ukimkuta nayo hii bado ni mtoto bado hajaolewa
I: Kwahiyo utoto unaisha akiwa na umri gani?
R2: Akiwa na miaka 15, 20 sema akipata bwana wake anaachana na hii
I: Kwahiyo hii ingimeta inavaliwa nje?
R1: Eeeeeeh
I: Lakini emutha emborosi?
R1: Inavaliwa ndani
I: Sawasawa nani kwa ajili ya wasichana tu?
R1: Wasichana tu
I: Sawasawa na ilikuwa na umuhimu gani hasa?
R1: Ni mapambo tu ni urembo tu msichana anavaa ile anapendeza kijana akiona sijui atamfata hahaha
I: Hhahahha kwahiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kuwafanya wapendeze?
R2: Ndiyo
I: Na kuvutia kwenye jamii
R2: Ndiyo
I: Sawasawa bado zinatumika hivi sasa?
R1: Mpaka leo zinatumika
I: Wanaotengeza hizi ni akina nani?
R1: Ni akina mama ni mafundi tena sasa hivi ndiyo wameongeza kuboresha wanatengeneza vizuri zaidi siyo kama huko nyuma saa hivi wakitengeneza wanatengeneza kitu kizuri sana na bora
I: Wakina mama kuanzia umri gani ndiyo wanaanza kutengeneza hizi?
R1: Yani kuanzia miaka 20 yani hii haina kiwango ni ile ufundi tu wa kujua hata akijua na miaka 15 basi anatengeneza unaweza ukakuta mkubwa lakini hajui kutengeneza ni ule ufundi tu umri wowote unaweza ukatengeneza
I: Na hizi zilikuwa zikitengenezwa kwa kutumia nini?
R2: Ngozi
I: Ngozi?
R2: Eeeh hii ni ngozi hii sasa hivi hapa siunaona ni ngozi imegeuzwa huku juu ndiyo inayotumika
I: Alafu hii ni shanga?
R2: Ni shanga hizo
I: Alivochanganya changanya hizo rangi ilikuwa kuna maana yoyote?
R1: Yeye sianatengeneza mapambo shanga inawekwa sehemu yake hii sehemu yake na hii pia sehemu yake
I: Kwahiyo ilikuwa yakuifanya ipendeze zaidi?
R1: Ipendeze zaidi kama hii sahivi siunaona hii
I: Ndiyo
R2: Hiyo bado ina urembo hivyo hivo
I: Na ngozi ni ngozi ya aina gani?
R1: Ni ng’ombe
I: Emutha emborosi?
R1: Eeeeh ushanga wa kiunoni
I: Lakini sasa mke wangu kashatoka kwenye huuu umri hahhhaha
R1: Hahhahhah ukitaka hii sianavaa kwa ndani wewe unakwenda kumshika shika mke wako hahaha
I: Sawasawa na hizi sasa mtu akitaka kununua atazinunua kwa shilingi ngapi?
R1: Hii sasa hivi engimeta inauzwa kuanzia elfu sabini ukikuta ambayo imeshonwa eeh ila fundi yupo hapa kwetu ukimwambia mama nataka kitu kama hiki unishonee ni elfu sabini kama ni hela kama ni mbuzi mbarika inayofikia makamu lakini kama ni hela ni elfu sabini sasa hivi ndiyo inauzwa hivyo
I: Kwahiyo sasa watoto wakiwa kwenye umri wa wasichana wanaowanunulia hizi ni akina nani kwenye jamii?
R2: Mzazi wake
I: Wa kike au wa kiume?
R2: Wa kike haswa mama yake au au mtoto anaweza kwenda kwa baba yake kwamba baba hebu ninunulie basi mama yake atakwenda kumtengenezea kwasababu wanaume hawajui kutengeneza na kama mke hajui inabidi umuite anaye jua ili amutengenezee vizuri akishamaliza msichana wako anaenda kuvaa sasa
I: Hela nyingi sana elfu sabini?
R1: Eeeh hii elfu sabini
I: Na hii emutha emborosi shilingi ngapi?
R1: Hii ushonaji wake siyo wa muda mrefu kama hii hii inachukua siku tano tu anakuwa kashamaliza
I: Siku tano inakuwa imeisha?
R1: Hata wiki imeisha lakini hii mpaka miezi miwili yote hiyo anaitumia katika kutengeneza tu hiyo
I: Ndiyo maana inauzwa bei nyingi sana?
R2: Ndiyo maana unaweza ukaweka hii ukishamaliza mwenyewe akasema ibadilishwe awekewe anaoupenda ndiyo maana inakuwa ngumu kidogo
I: Na hii naona ni shanga na hii inatengenezwa na ngozi pia emutha?
R2: Kuna nyingine inatengenezwa na ngozi kuna nyingine inasukwa sukwa tu na kamba huoni sasa hivi kama hii siyo ngozi imesukwa tu eeh
I: Ni kamba gani wanatumia kusuka?
R1: Manila fulani unanunua dukani nyembamba eeh
I: Lakini hii niya miaka ya 1905 kamba zilikuwa zinapatikana?
R1: Wanajua bado kuna kamba au labda ngozi
I: Hebu iangalie mzee [anonymous] vizuri hizo kamba zinaweza kuwa kamba za nini kama unaweza kuzitambua?
R1: Si kuna hii mkonge wananyofoa kwanza wanatoa ganda yake ya nje alafu nyuzi zake ndiyo wanatengenezea hii wanashonea
chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 01
mwandishi: I: Mohamed Seif, R1, R2: Anonymous
Mtu
-
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
-
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali