Wakati
2023-06-10
Maelezo
I: sawa, nina picha nyingine hapa imeajiliwa kwa 2018_18256_001
R: kimekaa mfano wa kisu lakini ni ”Nyengo”
I: anha, kuna “Nyengo“ ambazo zina roundi kwa nyuma
R: hapana zinakuwa kama sehemu ya kuwekea kampini
I: kwa hiyi iyo inawezekana ikawa ni aina nyingine ya “Nyengo“
R: ee
I: sawa, na umewezaje kutambua kama ni „Nyengo“
R: nimeweza kuitambua kwa jinsi ilivyotengenezwa hapa
I: “Nyengo“ ni jina la lugha gani
R: “Nyengo“ naona wanaita makabila ya huku ya wabena lakini inaitwa „fauna“
I: „fauna“ ni lugha gani
R: „fauna“ ni kiingereza
I: lakini kibena ni „Nyengo“
R: ee wanaita “Nyengo“
I: sawa sawa, na “Nyengo“ inatumiwa zaidi katika mikoa gani
R: “Nyengo“ ziko za aina....nafikiri mimi ninazozijua ziko za aina mbili, iko “Nyengo“ moja kama kisu cha kufyekea chai na aina ya pili ni “Nyengo“ kubwa ambayo unaweka mpini mkubwa kama wa jembe wanafyekea pori, kwa hiyo kuna “Nyengo“ ndogo kwa ajili ya kufyekea chai na “Nyengo“ kubwa unakuta kabisa ina mpini mkubwa kama wa jembe na ndio unaona wanatumia wabena
I: kwa hiyo wabena wanapatikana mikoa gani zaidi
R: mkoa wa iringa, mbea lakini huku walikuja kufanya kazi kwenye chai
I: kwa hiyo“Nyengo“ inatumika zaidi kwenye kukatia chai
R: ndio
I: tofauti na kukatia chai ni sehemu gani nyingine inatumika
R: kama hii unaweza ukatumia hata kukatia majani
I: na unadhani inaweza ikafika wakati “Nyengo“ ikawa haina matumizi tena katika maisha ya wanadamu labda kwa mkabila ambayo wanatumia “Nyengo“ kama wabena ulivosema
R: kwa wabena nao ni kama jadi maana wanatengeneza kubwa,kwa hiyo kukata chai naona kidogo visu vinapotea ndio kwa sababu wameleta mashine, sasa hivi wanakata chai kwa mashine ambapo ilikuwa inatumika hizi “Nyengo“
I: kwa hiyo kutokana na maendeleo ya teknolojia zinapotea, mashine zimeondoa “Nyengo“ sasa hivi hazitumiki tena
R: ah, tena mashine inakata, watu wawili tu wanakata mbuga
I: kwa hiyo matumizi ya “Nyengo“ yamepungua
R: ndio
I: labda kwa wanaokatia majani unadhani zitaendelea kutumika au na wao wanaweza kuhamia kwenye mashine pia
R: zitatumika tusemem kwenye kukatia majani lakini sana sana wengine wanatumia panga kwa sababu huwezi kwenda kukata majani porini ukatumia kale kamashine kanakotumia petroli, maana ni kama kamashine ka pikipiki halafu mbele kana kishani hivi kina kisu
I: na “Nyengo“ zinatumiwa zaidi na watu wa jinsia gani, wa kike au wa kiume
R: “Nyengo“ wanatumia wanaume
I: wa umri gani
R: ni kuanzia vijana, mwenyewe akienda zake shamba anachukua anatumia
I: kwa nini wanaume ndio wanatumia zaidi „Nyengo“
R: wanazitumia kwa sababu shughuli zake nyingi sana ni kama zinatumika na wanaume
I: kwa nini wanaume nataka kufahamu
R: wanaume ndio wanaozitumia sana kwa sababu mfano kwenye kukata chai wanawake hawahusiki, na shughuli za shamba pia ni mara chache sana kuitumia mwanamke labda kama kuna kazi ndogo ndogo kule shambani ndio anaweza akatumia „Nyengo“
I: kwa hiyo kwenye chai wanaume kwa sababu wana nguvu au kuna sababu nyingine
R: mimi ninafikiri ni sehemu tu ya wanaume kutumia hiyo
Wote: wanacheka
I: sawa sawa, na ili utumie “Nyengo“ unatakiwa uwe na kitu gani kingine
R: kwa mfano kwenye kukata chai ni “Nyengo“ tu, maana hayo majani ya chai yako saizi ya kifua, kwa hiyo unashika tu majani tofauti na kufyeka chini hujui chini kuna kitu gani, hata hivyo pia unaweza kushika bila “Nyengo“ lakini “Nyengo“ inakusaidia kuyashika majani vizuri kwa sababu imejipinda, ukishika unavuta unakata tofauti na kutumia hivi hivi au panga
I: sawa sawa, na“Nyengo“ bado zinaendelea kutengenezwa sasa hivi
R:“Nyengo“ sasa hivi sijui kwa lakini naona hazijawahi kuletwa, mara nyingi sana zinatumika kwa huku mashambani kwetu kunatumika mashine
I: mara ya mwisho kutumia “Nyengo“ ilikuwa ni mwaka gani kama unakumbuka
R: mimi nilikua ninatumia kazini lakini hivi sasa ninayo kuna moja hapo nyumbani nimeiacha
I: unaitumia
R: nikiwa na kashughuli kanakohitaji “Nyengo“ ninaitumia
I: mara chache chache sana
R: ee
I: mara ya mwisho kuletwa kazini kwenu ilikuwa ni mwaka gani
R: hapo kwa sababu mimi ni dereva sijajua itakuwa ni mwaka gani lakini kwa miaka ambayo nilikuwa nafanyia kazi ni tangia 2017 ndio nafikiri ndio zilikuja hizo,wakati huo mimi ninaendesha naona tu pale zinaletwa watu wanazitumia, na sasa hivi wengine wanajinunulia, kwenye kampuni zinaweza zisiletwe mtu akaamua kwenda kujinunulia mwenyewe “Nyengo“
I: wanazinunua wapi
R: wananunua mjini, tuseme kwa mfano tanga pale maduka ya pemejeo zipo zile “Nyengo“ na sana sana ni kwa ajili ya kukatia majani ya ng'ombe
I: anha, kwa hiyo wengi sasa hivi wananunua kwa ajili kukatia majani ya ng'ombe
R: ee una nunua pale kwa ajili ya kukatia majani ya ng'ombe au hata kama unashughuli zako nyingine za nymbani
I: na unadhani ni jinsia gani wanatengeneza hizi „Nyengo“
R: sifahamu kwa sababu zinafanya kuletwa nyingine kutoka nje, unakuta zimeandikwa apale kama ujerumani na nini
I: kwa maana wajerumani waliziona huku pengine walituibia teknolojia yetu na kupeleka kwao wakaenda kuboresha kidogo
R: ee ni kweli
I: na unaweza ukatambua kitu kilichotumika kutengenezea hiyo nyenzo
R: hii ni aina ya chuma
I: unaweza ukajua ni chuma ya aina gani
R: sielewi
I: labda kulingana na mabadiliko ya hivi sasa umewahi kuona “Nyengo“ nyingine tofauti na chuma
R: hapana
I: kwa hiyo zote ni za chuma
R: ee nilizowahi kuona, labda kama urembo maana vijana wa sasa hivi na ile mikufu yao wanayovaa, anaweza kuvaa kitu kama hiki anaweza akatengeneza dizaini
I: ni dizaini ya “Nyengo“ lakini ikavaliwa shingoni
R: ee, kwenye maduka haya wanaouza mikufu mikufu, utakuta kila dizaini
I: wewe unatumia Nyengo, na ukikuta “Nyengo“ kama hii unaweza ukainunua kwa shilingi ngapi kama hiyo unayoiona
R: sasa hivi kwenye 12,000/=
I: unadhani ni kwa sababu inaweza ikawa inaweza ikauzwa elfu kumi na mbili sasa hivi
R: ni kutokana na kupanda kwa bei, unakuta miaka ya nyuma ni hiyo hiyo umenunua kwa bei ya chini sasa ni hiyo hiyo utainunua kwa bei ya juu
chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
-
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
-
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali