Wakati
2023-06-08
Maelezo
I: sasa twende picha ningine, nimeshika picha iliyosajiliwa kwa namba 2018_18440_1, hebu iangalie picha hii unaweza ukatambua ni kitu gani hicho
R: hapa nimeona 'kiko' au 'mtembe', na hii hapa ni taa ya kandili, na hivi vingine pia ni viko dizaini tofauti, hiki hapa unaweza ukaunganisha kitu kama hicho, sijui kama niko sahihi
I: uko sahihi, sasa turudi kwenye hii picha, hizo zimetengenezwa nyingi hiyo ni ya mwaka 1902 mpaka 1928, na unaweza ukatuambia unadhani kiko inaweza ikahusishwa na watu wa tamaduni gani
R: kiko kilikuwa kinavutwa sana katika wazee wa kisambaa, na kipindi hicho mwanaume asiyevuta kiko alikuwa hana hadhi mbele ya wanaume wenzie
wote: wanacheka
R: yani ilikuwa ni kitu cha kijivunia sana
I: na kilikuwa kinatumikaje kiko
R: hiki ni kuweka tumbaku na kuvuta, halafu kuna vingine vilikuwa vinaitwa 'buruma' uvutaji wake mpaka kuwe na mtungi wenye maji, lakini hicho kusema kweli sijui ni watu gani wanatumia hapa kwetu kilikuwa hakitumiki sana
I: lakini kiko kimetumika
R: sana sana, wasambaa wamekitumia sana
I: kwa sasa vipi hali ya utumiaji wa kiko
R: watumiaji hawapo, hata ulaya nafikiri pia watumiaji hawapo, zamani hasa mjerumani ailikuwa ndio uvutaji wake huo, anavuta hivi akitaka kumwaga tumbaku anapiga kwenye kichwa chako, wakati huo yeye kabebwa hivi anavuta sigara yake kwenye kiko ikizima akitaka kutoa tumbaku anapiga kwenye kichwa cha yule anayembeba, walipta tabu sana
I: na tofauti na kuvuta tumbaku, kifaa hiki kinaweza kikatumika kwenye matumizi mengine
R: ni hiyo tu
I: unadani ni kitu gani kimepelekea kiko kutokutumika sasa hivi
R: watumiaji hawapo
I: ukisema watumiaji unamaanisha nini, ni watu waliokipa thamani...
R: waliokipa thamani hawapo, waliokuwa wanakijua ubora wake hawapo, manake hivi viko vilikwa vina tumbaku yake maalum, sasa hivi zile tumbaku pia hazipatikani, kwa vile watumiaji hawapo ilikuwa ikitiwa tumbaku ya kiko zamani akipita mtu unasikia 'lo ile ladha yake', lakini sasa hivi hawapo
I: umesema ilikuwa ni hadhi kwa mtu kipindi hicho kuvuta kiko, ni kitu gani kilikuwa kinasababisha mtu anayevuta kiko kuonekana ana hadhi kubwa kuliko yule ambaye havuti kiko
R: ilikuwa ni hivyo tu,
I: ilikuwa kwa ajili ya muonekano au kinatumika na watu wakubwa
R: kwanza ninaweza nikasema kwanza kilikuwa hakimsumbui mvutaji, manake unahabari kuishika sigara hutaimaliza mpaka ujisikie raha kuwa ladha inafikia wakati unaweza ukaitupa aidha imebakia robo au nusu kwisha, lakini kiko wewe unaringa nacho tu mpaka unamaliza tumbaku yako
I: je kuna ladha tofauti kati ya sigara na kiko
R: inategemea kama tumbaku ya sigara na ya kiko kama itakuwa inawiana test itakuwa ni moja, lakini ilikuwa tumbaku ya kiko ilikuwa ni ya aina yake na ya sigara ilikuwa na aina yake
I: sasa hivi imekuwa watumiaji wa kiko hawapo, hawaioni umuhimu wake
R: sijui labda tuanze tena
wote: wanacheka
I: na kwa siku za leo kuna watu wanatngeneza kwa kweli, mtu akitaka kutafuta kiko anaweza akakipata
R: itamuia ngumu kwa vile kwa sababu watumiaji pia naona hawapo
I: kwa hiyo hata watu inawezekana hata majumbani kwao wanaweza wasiwe nacho, na labda ni jinsia gani walikuwa wakitumia zaidi kiko na wenye umri gani
R: ni wakina babu kuanzia umri wa 60 kwenda juu, ilikuwa so vijana kusema kweli, na wakati watu walipokuwa wanatumia hivi viko, una habari watu wa zamani walikuwa na age kubwa kuliko sasa hivi, mimi miaka niliyokuwa nayo leo 77, pengine wakati wa nyuma nilikuwa ni mtoto wa kutumwa dukani, kwa zamani nilikuwa naonekana bwana mdogo kwa vile watu wanaishi miaka 500 600, 800, ndio mpaka siku ile nikasema kuwa serikali kusema msichana kuolewa chini ya miaka 18 ni jinai, mbona kama wanakosea, manake zamani ilikuwa mwanamke anaolewa kwenye miaka 30, 50 na kuendelea mbele na anazaa, na kw vile walikuwa wanaishia muda mrefu , sasa kama mtu anaishi miaka 300 au 400 aolewe na umri gani, lakini sasa leo mtu anawezakua miaka 40 awe kashakufa kazaa na kashaacha mtoto, sasa kwa nini asiolewe chini ya miaka 18, manake 40 kashaacha mjukuu, serkali pia inahaja ya kuangalia hiki kitu
I: na tukirudi kwenye kiko ni nyenzo gani zilikuwa zinatmika kutengenezea kiko
R: ilikuwa ni mti
I: ni mti wa aina gani
R: kuna hardwood ambazo ukitia tumbaku kwa kipindi cha kuvuta tu bado haijaathirika
I: unaweza kututajia ilikuwa ni miti gani
R: kuna mpingo, mkura, yani ile miti ambayo ni hardwood, unapiga panga inatoka cheche
I: hebu tukadirie ya hicho kifaa unachokiona, kwa sasa hivi kingepewa thamani na wazee wa sasa, kifaa hicho kingenunuliwa kwa kiasi gani
R: kama hao wanaokitumia hicho mpaka leo, sijui kingetolewa bure, manake thamani ya kitu ni kweli ile zama yake
I: sawa, sawa, kwa zama hizo ingekwa ni sasa ingekuwa shilingi ngapi
R: hiyo zama tunaizungumza ingekuwa ni shilingi moja
I: lakini sasa hivi hatuna shilingi moja tuna kuanzia elfu
R: tukiuze mia tano
chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023 / Interview No. 02
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
-
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
-
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali