Wakati
2023-06-09
Maelezo
I: sawa, tunaenda kwenye picha nyingine, tuna picha nyingine hapa imesajiliwa kwa namba 2018_18293_001, hebu angalia unaweza ukatambua ni kitu gani hiki
R: hiki ni kisu, lakini hiki kisu kilikuwa ni cha mzee haswa, yani ukiambia 'kaniletee giatu ni jangu' yani unaambiwa kalete kile kisu changu, ni hiki
I: ilikuwa inaitwaje
R: 'tuni'
I: ni kabila gani hiyo
R: hicho ni kisambaa, kipare 'kahandwi', sasa haka ni kahandwi maalum, na kisu hiki hiki kinaweza kikawa cha kushevia watu kwenye kumaliza msiba, lakini visu hivi sasa vinmeandaliwa vinakuwa na wazee maalum wazee wa mila, sio kwamba utavikuta kwa mtu yoyote, lakini vilienda vikafikia sasa walipoingia vijana vikatengenezwa kwa wingi, wakati mwingine wazee waganga wa kienyeji wanachanjia chale navyo hivi, ni vikali mno sana, vinanolewa kwenye mawe maalum yale unayoniambia ni meusi
I: kwa hiyo walikuwa wanatumia wazee
R: wazee
I: wa kuanzia umri gani
R: miaka 60, 70 mpaka 90 unamkuta anacho amekaa nacho, akashindwa kukitumia lakini anacho, na anaweza akaacha usia nkifa amani kisu changu apewe karedio, sasa hapo haibadiliki, wewe labda uchukue useme na mimi nampa fulani basi, lakini hivi hivi hata huko kitawekwa mpaka uje
I: kilikuwa kimeunganishwa na mila moja kwa moja
R: ee
I: na umesema kwa kila mtu sasa hivi anaweza kuwa nacho
R: ndio
I: unadhani ni kwa sababu gani imekuwa rahisi kila mtu kuwa nacho tofauti na miaka hiyo
R: maadili yale ya mila yameporomoka hakuna kujali ile mila sasa, kwa sababu sasa hivi ukimwambia mtu kisu kitengenezwe usikipeleke kwenye cherehe ukinoe tu kwenye jiwe anakuambia we utaniua, amaezoea ‘chwaaaa’ akigeuza huku kimekuwa kikali anaondoka anaenda zake, zamani hamna cherehe, kuna mawe ya kunoa na kuna mawe ya kugongea........
I: hayo mawe maalum ya kunolea yalikuwa yanaitwaje
R: 'ibwe'
I: maana yake
R: ni jiwe, yani ukiambiwa 'kaniendie ibwe maalum, unaagizwa na sehemu ya kulipata, hayapatikani patikani hovyo
I: sawa sawa, na unaweza ukatuambia kitu hiki kilikuwa kinatengenezwa na akina nani hasa
R: kilikuwa kinatengenezwa na wazee wazamani mababu wakarithishana hivyo hivyo, vikaenda vikafikia na watu wengine wanarithishwa kama hivi tunavyoongea mkasema kama mimi ninaweza kutengeneza hicho na mimi nikawarithisha
I: na unaweza ukatuambia kisu hicho kilitengenezwa kwa kutumia nyenzo gani hasa
R: ni vyuma ambavyo vinatengenezwa kwa kuchoma kwenye moto, yani hiyo miamba inayoenda kubomolewa ndio inawekwa kwenye huo tunaita 'mvuo', wanasema 'uvugwithwa' yana unavugizwa mpaka kinakuwa chekundu halafu anaweka kwenye jiwe wanapiga mpaka kinatokea hiki
I: kwa hiyo ni chuma na kitu gani kingine ambacho kinaenda sambamba kwenye kutenganeza hiki
R: labda mpini ndio kitu kingine kinaingia, maana huku kimetengenezwa kikawekwa chambamba ndio mpini wake na kujaribu kuboreshwa na vitu vingine, mwingine anavalisha ngozi ya........kuna mnyama kwa kipare anaitwa 'sunipaa', wale digidigi, vitu kama hivyo ndio ilikuwa ngozi zake zinachukuliwa kuvalishwa kwenye visu maalum kama hivi
I: kwa nini mnyama huyo
R: wanasema mnyama yule ana aina fulani ya baraka, ndio kama vile watu wanavyosema ukimpata kakakuona umepata kitu fulani au kuna baraka, au wakati mwingine wanasema kakakuona ukimuona mazingira ambayo sio ni balaa, sasa hivi vinyama unaweza ukakaa hapo nje hakuna pori hapo ukakaona kamesimama hapo, sasa wazee wakikaa wakutolea tafsiri kwamba ile ni balaa nenda katambikie, au ni neema wanategemea kimetokea muda gani
I: sawa sawa, kwa hiyo ilikuwa inaashiria baraka, na huo mpini ulikuwa ni mti gani hasa ulikuwa ukitumika kutengenezea hiyo
R: kuna mti unaitwa 'mzuu' kwa kipare wanaita 'mthuluu', hiyo ndio miti niliyokuwa ninaiona inatumika kwenye mipini ya visu maalumu na fimbo ya hao wazee, akitengenezewa fimbo yake ya kutembelea huku sijawahi kuuona
I: kwa nini walikuwa wanatumia mti huo tu
R: wanasema ni mti mgumu halafu ni mti wenye baraka
I: kwa hiyo ni mgumu lakini unabaraka, na ndio maana wakatumia hata ngozi ya hivyo vinyama kwa sababu na vyenyewe vina baraka
R: ndio vinaendana na kuleta baraka, unajua watu wa zamani wanatofauti, mimi marehemu babu yangu, nyoka mweusi anaingia ndani 'nyoka huyo, nyoka huyo' anasema hapana msimuue muacheni huyo nyoka, anaingia anakuja anatembea hapo baba anachukua chupa ya samli anammwagia yule nyoka, nyoka akatoka, anasema msimuue, kwa nini, anasema ameleta baraka, lakini ni mweusi, lakini kama ni wa kijani anasema ueni, wakijani akiingia anasema ni balaa ueni, kwa mfano hawa digidigi ninaosema anafukuzwa anakuja anaingia kwenye zizi, mara mbili mara tatu mimi nilishuhudia kwa marehemu babu yangu, anafukuzwa anaingia kwenye zizi la mbuzi, wawindaji wakija anawambia 'tafadhalini jamani angalia beberu hii na hii inayomfaa chukueni mmoja yule muacheni,' mzee mnyama wetu, yeye anawambia 'chukueni huyu yule muacheni amejisalimisha na ameleta baraka kwenye zizi langu la mbuzi, atakaa hapo na mbuzi mkifungua wanatoka wote wanaenda porini, sasa sisi hatuli yule mnyama kwa sababu hizo, anasema amekuja kwetu kujisaliisha haifai kumla.
I: tuni kama hiyo, kwa sasa unaweza ukainunua shilingi ngapi
R: hii sasa hivi labda shilingi elfu 5, haikuwa na vitu vingi sana vya usumbufu, ni vichache vichache kama nilivyokueleza
chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research, Interview No. 5
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
-
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
-
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali