Wakati
2023-06-14
Maelezo
I: mzee [Anonym] nina picha nyingine hapa imesajiliwa kwa namba 2018_18301_001, hebu angalia unaweza ukatambua hiki ni kitu gani
R: hiki ni kitu cha kutolea moto
I: kinaitwaje
R: kwa kipare kinaitwa 'linyindi', hii kuna mti maalum na mti unaitwa 'mvumo', lakini kuna mti mwingine wa pili ambao ndio unatumika hivyo 'mkonde', iko hiyo miti, unapata uliyokauka ndio unachukua unafanya hivi unatengeneza kitu cha duara unapikicha mpaka unaoa moshi moto unatoka, lakini kuna mti unaitwa 'mzumba nkhozo wautei', huo mti ndio unaochukua…wenyewe umekaa kama kamba hivi, ni wingi sana hata huku tunauona, sasa unachukua yale yaliokauka ndio ukiyafikicha hivi unapata ule unga wake unatumbukiza hapa, ukifanya hivi unalipuka moto haraka sana
I: kipare umesema inaitwa
R: 'lunyindi'
I: na kisambaa
R: 'unyindi', yani una geuka geuka hapo hapo
I: na ni makabila gani hasa walikuwa wakitumia lunyindi
R: ni wasambaa, wapare, wambugu na makabila mengine wasafwa, wangoni kwa sababu kule walikuwa wapo wengi
I: wasafwa wanapatikana mkoa gani
R: wasafwa wanapatikana mkoa wa mara, tarime bara huko
I: na wangoni
R: wangoni ni songea
I: kwa hiyo ilikuwa ni maalum kwa ajili ya kuwashia moto
R: porini mkienda ndio kibiriti
I: na mti mwingine ambao ulikuwa unaendana sambamba
R: miti ninayoijua ni hiyo miwili, 'mvumo' na huo 'mkonde',
I: na waliokuwa wanatumia lunyindi ni wa jinsia gani na umri gani hasa
R: hii hasa zaidi ilikuwa inatumiwa na wazee wanaoenda kuwinda, na wazee wanaoenda shambani hawana haja ya kubeba moto wanabeba hii, au ametengeneza kabanda kake vinakaa huko, ndio ilikuwa inatumiwa na watu wa namna hiyo, lakini baada ya tuseme wazee kuzeeka sana wakatumia vijana sasa wanapoenda kuwinda wanabeba hii, au wanaenda kuchonga huko porini, yani unaweza kuchonga halafu ukafanya ukapata moto
I: unachoma kwa mti ulio kauka au mbichi
R: mti uliokauka, uliokauka tena umepewa jina 'khunge', yani umekauka ni wa muda mrefu sana, lakini kwa kipare wanasema 'ikulunge'
I: na ni lazima uwe na mti mwingne ndio upikiche upate moto
R: ee
I: na kulikuwa kina umuhimu gani hasa kwa tamaduni hizo za watu uliowataja
R: ni umuhimu wa kuepuka kununua vibiriti kutoka dukani
wote: wanacheka
I: kulikuwa kuna vibiriti kipindi hicho
R: ee vibiriti vinaitwa vya 'nyota'
I: ni miaka gani hiyo
R: ni miaka ya 61,62
I: kwa sasa lunyindi inatengenezwa
R: labda mtu anayependa kama hivi nyinyi mmependa labda mmekumbuka labda mkaona niwarithishe, maana wamesema ‘tuhifathi tuwarithishe’, tulirithishwa na mababu na sisi tuwarithishe, labda mimi niseme nina wajukuu na watoto niwafundishe lakini hawataki, kazi za namna hii hawataki hizi kazi
I: wanapenda nini sana
R: kununua vibiriti vya gesi...
wote: wanacheka
I: mzee [Anonym] lunyindi kama hiyo ikiletwa kwenye mazingira yetu ya sasa, unaweza ukainunua shilingi ngapi
R: labda elfu 5, kwa sababu mali ghafi zake sio sana kama vile vingine nilivyowaelezea
chanzo: Amani-Stade Proejct / Amani Field Research 2023, Interview No. 19
mwandishi: I: Mohamed Seif, R. Anonymous
Mtu
-
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
-
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali