Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/1

Bangili

Sammlung Braun
r 2018 / 18407
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18407
Kichwa
Bangili
Vipimo
Urefu: 9cm, Upana: 11,5cm
Nyenzo
Ngozi,
Pembe
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_a028cd7d-7337-4eb9-b5b1-2332a7411d9c
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uainishaji
vito vya kikabila  
Uzalishaji
Wakati
mpaka 1905-11-30
Mtu
  • Person (Mtengenezaji)
Mahali
  • Tansania
Ethnolojia
  • Massai  
Kununua / Uuzaji
Wakati
1905-11-30
Maelezo
„Alhamisi 30. Mwezi wa kuminamoja 1905 [imepigwa mstari] Kutoka kwa [?] Massai wawili nimenunua ngao kwa 4 ½ Rupie, kamba mbili za magoti tepe nyembamba zilizowekewa shanga utepe mwingine kama hii ya kuvaliwa mwilini mwenyewe ni kubwa zaidi pambo moja la mkononi kama shajara 43. u.103 kwa hela 50 & hela 75 & na mkufu uliotengenezwa na mbao unaonukia & umepakwa na udongo mwekundu (hela 50) angalia. u. 108. [mchoro, wenye rangi ngao]" [Utafsiri]

chanzo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 46 (41)
mwandishi: Karl Braun
Mtu
  • Mtu, haijulikani (Mchuuzi)
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mnunuzi)
    GND Explorer
Mahali
  • Amani
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
Mahali
  • Stade
Scientific use:
Wakati
2023-09-29
Maelezo
I: Hahahhaha sawasawa nina picha nyingine hapa ambayo imesajiliwa kwa namba 2018_18407_1 mzee [anonymous] wewe uliitambua picha hii hebu nikumbushe jina la hicho kinaitwaje? R2: Hichi ni kitu cha urembo. I: Kinaitwaje hicho? R2: Emburunoti kwasababu hii wewe hujui ni ngozi imesukwa lakini ni ngozi nyepesi imesokotwa, sokotwa kwa ajili ya kuweka kama urembo ya kuweka ile kisinga kama tulivyokuambia kisinga vipo vya design mbili kuna kile kinachoenda mpaka huku huna kinachoishia kichwani tu ambayo hiyo anavaa morani ambaye ndiye tu kiongozi labda kwenye sherehe ndiyo anaweza kuongoza hata morani mia sita ndiyo anakwenda mbele na emburunoti yake. I: Kwa kabila la wamasai ilikuwa inatengenezwa kwa kutumia kitu gani ukiachia ngozi mzee [anonymous]? R2: Kwasisi hakuna njia nyingine ya kutengeneza hii ila ni ngozi ila kupitia upembe wa kondoo hapana labda kuna kabila lingine wametengeneza kupitia kondoo. R1: Na hata pembe ya kondoo huwezi kuipata ukaikunja hivyo siyo rahisi haiwezekani huwezi kukunja pembe ya kondoo mpaka inakaa hivi. I: Kwahiyo hii ni emburunoti kwa ajili ya kubania kisinga? R2: Eeeh kama atabania kisinga. I: Kiongozi wa morani anayeongoza ndiyo anaivaa hiyo? R2: Eeeh anayeongoza kwenye ngoma. I: Ilikuwa ni kwenye ngoma ndiyo anavaa? R2: Kwenye ngoma, kwenye sherehe eeeh. I: Kwahiyo hapa kunaweza kukawa na morani mia sita yeye ndiyo kiongozi mzee [anonymous] hebu tuambie? R2: Eeeh anachaguliwa anaambiwa ongoza wenzako eeh tuingie kwenye boma tucheze na ingiza wenzako kwenye boma kwasababu wanakuwa nje alafu anachaguliwa yeye anawaongoza anawaleta wenzake nyumbani waje wacheze ndani ya boma kwenye sherehe au sikukuu yoyote inayofanyika. I: Sawasawa na hizi emburunoti bado zinatengenezwa hata hivi sasa namba mbili hebu tuambie kama bado zinatengenezwa. R2: Sasa hivi imekufa hii imepotea hamna kwasababu ile kisinga hamna tena ile kisinga imepotea hata mkuki umepotea mikuki utakayo ikuta sasa hivi ni ndogo ndogo nyeusi siyo kama ile nyeupe. I: Ile ndefu? R2: Hakuna ile ndefu tena. I: Sawasawa na waliokuwa wanavaa hizo ni morani tu? R2: Ndiyo ni morani peke yake haruhusiwi mzee au mvulana ambaye hajaingia jandoni ni morani peke yake. I: Na labda kama sasa hivi mtu anakitaka hicho japo kimepotea akataka kitengenezwe kinaweza kikatengenezwa kwa shilingi ngapi? R2: Hii inataka ufundi siyo kila mtu anaweza akasuka hii ikawa hivi siyo rahisi kwahiyo fundi ndiye anaweza akaithaminisha mimi naweza nikaithaminisha nikawa ni muongo kwasababu nitataja bei ambayo siyo hahha. I: Hahhahaha na waliokuwa wanatengeneza ni hao hao morani au mzee [anonymous] hebu tuambie hapo? R2: Hata wazee lakini ni ufundi siyo wote wanajua inawezekana hata kwenye watu mia wakajua watatu eeh wakawa ndiyo mafundi sasa fundi ndiye anajua hii inachukua muda gani na gharama yake ni ipi hadi ikamilike ila mimi ni vigumu kujua kwasababu sio fundi kwahiyo sijui vitu vitagharimu kiasi gani. I: Kwahiyo ni wazee wakiume ndiyo walikuwa wanatengeneza hii? R2: Eeeh wakiume kwahiyo mafundi hawawezi kushindwa kutengeneza hiyo ukimuonyesha tu basi anakutengenezea.

chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 04
mwandishi: I: Mohamed Seif, R1, R2: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Lunguza
Scientific use:
Wakati
2023-10-03
Maelezo
I: Hahhahha sawasawa nina picha nyingine hapa imesajiliwa kwa namba 2018_18407_1 namba mbili hii uliitambua vizuri sana hebu tueleze kwa undani tuambie kwanza jina lake hiko kifaa kinaitwaje? R2: Erapu I: Ehe ilikuwa na kazi gani hiyo erapu? R2: Inaitwa erapu ambayo ni pembe ya mbogo inachongwa na kwa huku wanaweka na ushanga unavalishwa hapa na hii ni kamba ya kufungia kwenye mkono wa juu ili morani acheze nayo na aendelee kuimba itikisike aimbe nayo kama kifaa ambacho kinaonyesha kwamba ya kuchezea nayo I: Ilikuwa ni kwa ajili ua kuchezea tu? R2: Ni mchezo tu ni urembo I: Ilikuwa ni kwa ajili ya morani tu? R2: Eeeh ni morani tu eeh kwa ajili ya kuchezea I: Kuchezea ngoma? R2: Eeeeh I: Kwahiyo umesema ilikuwa ni pembe ya mbogo? R2: Eeeeh pembe ya mbogo I: Unaweza ukatuambia inatengenezaje? R2: Ile pembe ya mbogo kuna eneo unajua inanyooka alafu huku mbele kuna sehemu inajikunja sasa mtaalamu wa uchongaji alikuwa anaichonga alafu anaitengenezea size ya mkono alafu anaitengeneza anaitoa sasa kwa namna hiyo kwahiyo ni kuchongwa ile pembe ya mbogo na kutoa hiyo size ya mkono I: Na ni kitu gani kingine kilikua kinatumika ukiachia hiyo pembe? R2: Hakuna kitu kingine isipokuwa hizi shanga ndiyo zinaongezeka kwa pande zote mbili nani shanga ndiyo zilikuwa zinawekwa huku kwasababu ya kufungia kwahiyo I: Hii ni kamba ya kitu gani? R2: Hii ni kamba ya kufungia na hii ni pembe tu na huku kulikuwa hakuna kitu ila ni rafuness tu ya pembe hakuna kitu kingine cha kuwekwa ni upande tu wa hapa ndiyo unaongezewa shanga tu basi I: Ukiangalia hapa unaona kuna kamba imezungushwa? R2: Hii inakwanguliwa alafu inapakwa rangi I: Kwahiyo ni pembe ya mbogo? R2: Eeeeeh I: Kwahiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kuchezea ngoma tu? R2: Niyakuchezea lakini siyo wote ni wale tu wachache ambao wanapenda kujiremba tu niyo walikuwa wanachezea I: Hii ilikuwa haina junior na senior? R2: Hapana haina R1: Naongezea kwamba kuna watu wanatengeneza na kuuza lakini wanauza kwa mbuzi mmoja yani wanabadilishana kwa mbuzi ndiyo biashara yao hiyo I: Kwahiyo kwa hivi sasa bado zinatengenezwa hizi? R2: Hakuna I: Kwanini zimepotea? R3: Sasa hivi mambo mengi kwa kweli ya mila na desturi zinapotea mambo mengi sana mimi nilikuwa nimejiandaa kueleza mengi lakini naona haya mambo haya tulipofika sisi rika hii maana sisi ni rika moja mimi na huyu I: Rika yenu inaitwaje sasa hivi? R3: Seuri na haya mambo yaliishia kwetu hawa waliofuata huku hawana chochote tena hawafuati hii wameshaacha kabisa na mambo mengi yamepotea kwamfano kuna mambo mengi mimi huwa napata wageni wa kutoka nje wanakuja kwangu kwahiyo nakuwa lecture wao nawapa mambo mengi ya mila na desturi na kuna vitu vingi wanauliza wanakuta vimeshapotea muda sana I: Nani ngoma gani walikuwa wakianza kucheza lazima morani wavae hii erapu namaba tatu hebu tuambie? R3: Ngoma yoyote ile ilimradi ni ngoma inayochenzwa na morani maana wazee wana nyimbo zao nawa mama wana nyimbo zao na morani wana nyimbo zao na wasichana wana nyimbo zao maana morani wakiwa wanacheza lazima watakuwa na wasichana wao ambao watakuwa wanacheza wote I: Wawe na kina ndito? R3: Eeeeh ndito kwahiyo wana hizo ngoma zao na wana nyimbo nyingi tu I: Labda ni ngoma gani ya kimasai ambayo ni maarufu sana ambayo ilikuwa wakiincheza wawe wamevaa hii? R2: Kuna wimbo ulikuwa unawekwa unaitwa emborokoi ulikuwa ni maarufu maana hata miaka ya wazee umri uliopita mbele yao waliimba na waliofuata waliimba na hata wao walikuta waliimba ulikuwa maarufu na mwingine ulikuwa unaitwa elongishu ambao walikuwa wanaimba morani na wasichana wao kwahiyo lazima wasichana wawepo wawaimbie ilikuwa ni nyimbo maarufu sana na wameimba mpaka juzi juzi tu lakini anasema kwa sasa imebadilika kwa mfano sasa hivi vijana wa sasa ni hizi gitaa tu wanapiga hakuna wakuitikia kama wasichana kwahiyo ni gitaa lina pigwa tu basi na hizi mila zimepotea R1: Kuna nyimbo aina tatu zilikuwa maarufu kama alivotaja namba mbili kuna emburugoi, elongishu na punyaa sasa kipindi hicho akiwa na hiki kifaa ndiyo hizo nyimbo zilikuwa maarufu na ndiyo zilikuwa zinatumika sasa ndiyo baadae hizi nyimbo nyingine ndiyo zikafuata lakini hakuna hii kitu tena I: Na kilikuwa kinavaliwa mkono gani hasa? R1: Hiki kilikuwa maarufu sana kuvalishwa mkono wa kushoto na siyo mkono mwingine wowote ule I: Kwanini walikuwa wanavaa mkono wa kushoto? R2: Ndiyo ulikuwa mkono maarufu mtu alikuwa rahisi kuutikisa kwasababu morani anavyoenda kuimba au kuruka ni rahisi sana mkono huu kutikisika alivokuwa anaruka na hii inatikisika, tikisika I: Kwahiyo ilikuwa inatoa sauti? R2: Inatikisika tu I: Sawasawa na waliokuwa wanatengeneza hizi erapu ni wanaume au wanawake ni jinsia gani hasa? R3: Wanaume ila kwa nyongeza walitaka kuweka shanga na kupamba zaidi wa mama ndiyo wanaweka zile shanga kwasababu ndiyo wanajua kupamba kwa kutumia shanga lakini kuichonga na kuiweka katika muonekano mzuri ni wanaume ndiyo walikuwa wanafanya kazi ya kuchonga I: Na kwanini walikuwa wanatumia pembe ya mbogo peke yake? R3: Walikuwa wanapenda kutumia hiyo kwasababu haivunjiki ile haivunjiki vunjiki ni ngumu ni hiyo tu kwasababu haivunjiki inaweza kukaa miaka mingi bila kuvunjika na hata kwa nyongeza morani wanatumia ngao na ngao wanayotumia wanatumia ngozi ya mbogo kwasababu ni ngumu ikikakuka ikitengenezwa ikikaa vizuri unaweza ukapiga mkuki hapa haiwezi kuingia kwahiyo ni vitu hivyo lakini wanaamini ngozi ya mbogo ni ngumu sana maana ngozi ya ng’ombe haifai ukipiga tu inatoboa inamkuta aliyeshika au ngozi ya mnyama mwingine yeyote ila ngozi ya mbogo ni ngumu zaidi kwahiyo hiyo pembe wanaitumia kwasababu haivunjiki ni ngumu sana inaweza ikakaa miaka na miaka

chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 08
mwandishi: I: Mohamed Seif, R1-3: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Longido
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1905-11-30, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 46 (41)jifunze zaidi

Rejeo la ndani la kitu

Ngao

Ngao

r 2018 / 18340
Rejeo la ndani la kitu
Kuhusiana na
Bangili ya sehemu ya juu ya mkono

Bangili ya sehemu ya juu ya mkono

r 2018 / 18447
Rejeo la ndani la kitu
Mazingira/Muktadha wa upataji/Upatikanaji
Bendi ya magoti ya ngozi na kamba ya bodice

Bendi ya magoti ya ngozi na kamba ya bodice

r 2018 / 18441 a
Rejeo la ndani la kitu
Kuhusiana na
Bendi ya magoti ya ngozi na kamba ya bodice

Bendi ya magoti ya ngozi na kamba ya bodice

r 2018 / 18441 b
Rejeo la ndani la kitu
Kuhusiana na
Shanga ya mkufu wa mbao na kishaufu

Shanga ya mkufu wa mbao na kishaufu

r 2018 / 18426 a
Rejeo la ndani la kitu
Kuhusiana na
Mkufu

Mkufu

r 2018 / 18426 c
Rejeo la ndani la kitu
Kuhusiana na
Mkufu wa vipande vitatu

Mkufu wa vipande vitatu

r 2018 / 18426 b
Rejeo la ndani la kitu
Kuhusiana na
Mkufu

Mkufu

r 2018 / 18426 d
Rejeo la ndani la kitu
Kuhusiana na

Rejeo la ndani la kitu

Oberarmklammer (Schmuck) - Staatliche Museen zu Berlin

Rejeo la ndani la kitu
ist ähnliches Objekt
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:38:58+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji