Wakati
2023-06-09
Maelezo
I: Sawa sasa kuna picha nyingine hapa hii picha imesajiliwa kawa namba 2018_18312_1 hebu angalia picha hiyo unaweza ukafahamu ni kitu gani?
R: Hiki ni kitu kilichosukwa na minyaa
I: Kinaitwaje unaweza ukafahamu Jina Lake?
R: Jina lake kwetu tulikua tunaita kome
I: Kome?
R: Eee Kome
I: Kome kilikua kinaitwa kome inamaanisha nini?
R: Hii ikimaanisha yani ilikuwa kazi yake hiki wale watu wa zamani walikuwa wanasaga pombe kwenye mabati muwa ule unachongwa kuna bati limetobolewa tobolewa wanasaga kinatoka laini laini halafu sasa wanatumbukiza humu wanakamua ndiyo chujio yao watu wa zamani walikuwa wanachujia pombe
I: Ndiyo wanachujia?
R: Eeeeeh nilikuwa naona mimi hata mama yangu hiyo kazi alikuwa anaifanya wanasaga miwa kwenye bati wanaweka maji kidogo au ya wastani kulinganisha kwamba kama haya machicha ya muwa kama ni debe litoke maji kiasi gani sasa wanatumbukiza humu alafu ndiyo sasa kazi ni kukamua mpaka yakauke na yale ya kutengenezea pombe
I: Ilikuwa inatengenezea tu pombe peke yake?
R: Yani pombe Zaidi pombe maana kule nazi zilikua hazipo nilikua naona sasa kwenye kuchujia pombe sasa kwa wenzetu wengine sijui walikua wanachujia nini
I: Ni kabila gani walikua wakichujia pombe?
R: Wasambaa
I: Wasambaa?
R: Eeeeeh
I: Kwahiyo hicho kilikua kinapatikana kwa mikoa gani hasa kilikua kikipatikana?
R: Sana sana Lushoto wilaya ya Lushoto ndiyo nilivoviona sana hivi
I: Miaka gani hiyo uliona?
R: Mimi kuanzia mwaka hamsini na tisa kwenda sitini ndiyo nilikua na akili ya kuona hivi vitu kwasababu nilikua nishakuwa msichana mkubwa mkubwa
I: Sawasawa
R: Eeeeeh
I: Sawa kwahiyo kilikua kinatumika kuchuja pombe?
R: Eeeeh kuchujia pombe eeh
I: Au?
R: Au kuchujia mahindi kuna mahindi haya machanga wakati huo wakati yanaanza hayajakomaa vizuri yanapondwa kwenye kinu yanakuwa kama uji kabla hayajawa uji ili wasipike na chenga kwasababu ya uji wa watoto kipindi cha hali ya shida zamani shida ya njaa ikiingia ni njaa haswa haina maarifa ya dukani wala nini kwahiyo mahindi yanaiva sasa wanatwanga kwenye kinu alafu wanatumbukiza humu wana kamua yale maji yake wanaya chemsha yakichemshwa tayari ni uji watoto wanakunywa zile chenga chenga za maganda ya mahindi zinatupwa eeeh ni uji laini sasa kwa watoto ndiyo hivo nilikua naona sasa sijui kwa nyinyi wenzetu
I: Hahahaha kwahiyo ilikua ni kwa ajili ya kutengenezea uji wa watoto?
R: Eheeee kutengenezea uji wa watoto na kutengenezea pombe eehe
I: Sawa na ukikiangalia kitu hicho waliokuwa wanatumia hasa ni watu gani kina mama kina baba?
R: Kina mama Zaidi
I: Kina mama?
R: Eeeeeh ndiyo Zaidi waliokuwa wanatumia kukamua hizo pombe za kusaga
I: Akina mama kuanzia umri gani?
R: Hata wasichana wa miaka kumi na mbili mnafundishwa maana kama hawezi kukamua peke yake hiyo kila siku kuanzia miaka kumi na mbili kwenda kumi na tano kuendelea mpaka miaka arobaini watu wazima
I: Kwanini walikua wanatumia Zaidi akina mama?
R: Akina mama kwenye hizi kazi zilikua zinaonekana kule kusaga miwa wababa wanasaga bali kwenye kukamua ni wamama sababu ni kazi ya wamama hii eeh na sijaona wababa wakikamua ni wamama, wamama ndiyo wenye kuhimili sana hizi shughuli za mikono hasa kukamua pombe ilikua ni kina mama
I: Kifaa hicho bado kinatumika au hakitumiki tena?
R: Kwasasa sikioni
I: Hakitumiki tena
R: Hakitumiki tena sasa hivi watu wanatumia machujio eeh ya bati yametobolewa ndiyo wanatumia eeh zamani hata kwa nazi hizi mtu anatumbukiza anakamulia lakini sasa hivi havipo hivi vitu vimepotea hivi
I: Kwahiyo kwa kabila la wasambaa kitu hiko hakina thamani tena?
R: Kwa muda nilioona sasa sikioni ni muda mrefu tuseme tu hakina thamani hawana thamani nacho tena eeh
I: Kwasababu hakitumiki tena?
R: Kwasababu vitu vya kisasa vimeshatokea vimepoteza hivi vitu vya asili
I: Kwahiyo hata kutengenezwa havitengenezwi tena vilikua vinatengenezwa wapi?
R: Hivi kwa watu wa bara vipo lakini vifupi kwa ajili ya kuwekea unga eeh naviona na hivi sasa kwa ajili ya kubadilisha maana siyo tena cha kukamulia wana tengeneza vikapu vya kwendea sokoni
I: Lakini kwa hicho cha kuchujia kwa sasa hakitengenezwi tena?
R: Sasa sivioni
I: Kwanini havitengenezwi?
R: Watu sasa ni wakisasa wanatumia vitu vya kisasa
I: Vya kisasa hahahhahhaha
R: Eeeeh hahahhahha
I: Sawasawa
R: Wanatumia vitu vya kisasa
I: Na ni watu gani walikuwa wakitengeneza sana hivyo?
R: Hivi ni wazee wa kisambaa
I: Wa kike au wakiume?
R: Wakiume
I: Wakiume?
R: Eeeh
I: Kwahiyo walikua wanatengeneza wao lakini watumiaji wakubwa ni akina nani?
R: Ni wanawake
I: Wazee siyo vijana?
R: Wazee ndiyo walikuwa wanatengeneza hivi
I: Kwanini ilikuwa ni wazee na siyo vijana?
R: Wazee Zaidi walikuwa wabunifu wazee wazamani alafu kwa ajili na wenyewe wanauza siyo kwamba walikuwa wanavitengeneza bure walikua wanaviuza eeh
I: Ukiangalia vitu gani vilitumika kutengenezea hicho kitu ukikiangalia?
R: Hiki ni minyaa tu
I: Minyaa ni nini?
R: Minyaa ni ukindu
I: Ukindu?
R: Eeeh kuna ule ukindu mdogo na ukindu mkubwa lakini hiki naona ni ukindu mkubwa ule eeh ni ukindu ukisema minyaa ni ukindu tuseme ukindu
I: Na ukiangalia kifaa hicho kikiletwa katika mazingira ya sasa hivi kinaweza kikawa na thamani ya shilingi ngapi?
R: Kwasasa kama kinaweza kununuliwa kama kilivo unaweza kununua elfu mbili, elfu tatu hata elfu nne eeh
I: Sawasawa haya asante sana hiyo tumemaliza
R: Ni bei ndogo tu
chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023, Interview No. 03
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
-
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
-
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali