Wakati
2023-06-08
Maelezo
I: naomba nikubadilishie picha, nimeshka picha imesajiliwa 2018_18369_001, hebu angalia hiki ni kitu gani
R: hii ni kofia, kofia hii ilikuwa inaitwa kitunga
I: manake ni nini na kwanini iliitwa kitunga
R: ni jina tu kutokana na haka kajiurembo ka hapa juu ndio ikaitwa jina hilo kitunga
I: na ilikuwa inapatikana zaidi maeneo gani katika nchi yetu ya tanzania
R: lilikuwa ni vazi la watu wa pwani, islamic
I: unaweza ukatutajia ni mikoa gani
R: ni mkanda wa coast wote, na kigoma kule islamic wamekaa, na wakati huo mtu akivaa kofia hizi uh! akiingia mahali lazima watu wasimame
I: kwa nini
R: kila zama wana mambo yake, ilikuwa ndio mavazi ya hadhi
I: kwa hiyo mtu akivaa hiyo inakuwa ni mtu mwenye hadhi kubwa, ila sio mtu yeyote alikuwa anaweza akavaa hiyo kofia
R: hapana, una habar zamani hela ilikuwa iko chini na kuna baadhi ya vitu... na wakati huo pengine utakuta bei yake ni senti tano, lakini huyo anayepata senti 5 mpaka anainunua lazima akuambie yanazungumzika, na wengine wlikuwa wanavaa kutokana na uwezo wa uchumi wao
I: kwa hiyo kitunga kilikuwa kinauzwa kwa gharama kubwa kidogo kwa kipindi chicho
R: ee
I: na ilikuwa inavaliwa kipindi gani
R: ndio nimekuambia ni vazi la watu wa pwani haswa islamic,
I: ilikuwa ni kwenye matukio maaluma au ni muda wowote mtu anaweza akavaa
R: ni muda wowote, lakini mavazi yake kitunga wewe leo huwezi kuvaa na suruali ya kuchonga, hii lazima upate kanzu na koti
I: koti la namna gani
R: koti la kawaida, halafu ilikuwa raha yake saa nyingine ilkuwa iweke upande
I: kwa hiyo mtu anayevaa kitunga lazima avae kanzu na koti katika muonekano
R: ni katika muonekano tu
I: labda ilikuwa na masharti ya aina ya viatu pia maana kuna baadhi ya vazi huwezi ukavaa kanzu
R: kipindi cha matumizi kama hivi likuwa viatu vyake vikubwa ni makubadhi, viatu vya wazi
I: na kitunga kwa hali ya sasa kinatumika
R: ah, tunakiona lakini kwa umbali sana, halafu kuna baadhi ya vijana wakikuta vya marehemu babu zao wanavaa kama fashen lakini sio vinavaliwa kuwa ni vazi, enzi yake imepita
I: nayo haiwezi ikarudi
R: sio rahisi
I: kwa nini sio rahisi
R: unajua sasa hivi tunakokwenda...lakini kuna siku moja nilisema ifike wakati hizi tawala kuna vitu lazima waviangalie, kwa mfano kama sasa hivi ukifungulia tv unaambiwa oh sijui maji lakini nani wa kulinda maji, mimi nilitegemea mama samia tangia ameingia madarakani leo ilikuwa akemee wasichana wanaotembea uchi, yeye kwa vile ni mwanamke ilikuwa aone uchungu na akemee, sasa mama nini utakaoyatengenezwe na yatatengenezwa vipi, anakuja makamu wa rais kuna kuja watoto wa shule wanafunga migomba uchi tunamuona, sasa hayo maadili mnayoyataka ni yapi, serikali kwanza ikae iangalie kama inataka irudishe mfumo wa maadili, serikali ndio isimamie hili, mimi ninasema hata kwenye mataasisi ya dini pia inachangia kuharibu maadili, mimi kwa umri wangu nilishaona ukristo wa nyuma, unakuta mtoto wa kikristo anaenda kanisani mwili wake unamtosheleza kabisa kwa nguo anajua anakwenda mahali pazuri patakatifu, unaangalia wale mabinti I wanaokwenda kwenye ibada halafu naked kabisa na mchungaji unasimama unaangalia unazungumza huku mate yanakutoka, kwa nini hukemei vitu kama hivi, kwa hiyo hizi zama z maadili zilishapita
I: kitunga bado kinatengenezwa hivi sasa
R: watumiaji hawapo, utengenezaji wake pia...
I: umepungua au umeisha
R: itakuwa umeisha
I: kwa hiyo leo hii mimi nikihitaji kitunga...
R: unaweza ukakipata bangladesh huko kidogo kinatumika
I: na je kwa tanzania au vinginezo aagize au mtu aje nacho
R: ee au mtu aje nacho
I: na kwa tanzania kipindi hicho ni watu gani walikuwa wakitengeneza vitunga
R: vilikuwa imported
I: kutoka nchi gani
R: huko huko bangladesh ndio kwenye ambako walikuwa wanakitumia sana, kilikuwa ni kitu cha biashara
I: japo kilikuwa kinaingizwa kutoka nje, je unaweza ukazungumzia nyenzo zilizokuwa zinatumika kutengeneza kitunga
R: kitunga ilikuwa ukikiangalia ni kama pamba iliyochatwa, lakini katika mchakato wa kitambaa sio pamba kama pamba, lakini imechakazwa katika mchakato wa kitambaa, ilikuwa ni kitu kama hicho
I: kwa kipindi hicho umeseme kitunga kilikuwa ni kivazi cha thamani na chenye hadhi kwa anaevaa, thamani iliyokuwa inauzwa kipindi kile ukiileta katika maisha yetu ya sasa, inaweza ikawa ni shilingi ngapi
R: kama elfu 5 au elfu 10 kitu kama hicho
chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023 / Interview No. 02
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
-
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
-
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali