Wakati
2023-09-09
Maelezo
I: Sawa sawa, ngoja tujadili tena picha nyingine, nina picha nyingine imesajiliwa kwa namba 2018_18368_001, hebu angalia unaweza ukatuambia ni nini hicho?
R: Hiki nacho ni ‘Kiko’ lakini kimerembeshwa zaidi kulikoni kile cha kwanza, unajua mtu akianza kutengeneza ‘Kiko’ cha kwanza atakapotengeneza ‘Kiko’ cha pili ni tofauti na kile cha kwanza atakuwa amepata ufundi zaidi, anakiweka mapambo zaidi ili kuvutia wavutaji
I: Labda tuangalie kile cha kwanza mdomo wake ni mfupi kidogo wa kuwekea tumbaku ukilinganisha na hicho ulichoshika, unadhani ni kitu gani kilepekea vikatengenezwa tofauti kwenye mdomo wa kuwekea tumbaku
R: Unajua hawa mafundi wanadizini wenye kuvutia hao wanunuzi, naona wanatengeneza kutokana na wakati, hiki kimefanyiwa maringo zaidi lakini uso ni ule ule
I: Ukiangalia hapo mbele kinaonekana kama kina sura ya mtu, unaweza ukahisi ilikuwa sababu gani kuwekea sura ya mtu kwenye hicho kichwa cha kuwekea tumbaku
R: Hapo ninaweza kusema kwamba hiki kitu kinatumika kuvutwa na mtu ndio sababu kina sura ya mtu ndio kwa sababu kna sura ya mtu, wao wanatengeneza sura ya mtu kutokana na ufundi wao, maana hata ukiangalia unaona hiki na hiki kinakwenda sawa sawa kwa nini, kwa sababu hapa ni pembamba na hapa napo ni pembamba lakini ni tofauti, huu ni ufundi wao wanadizaini wenyewe hawa wahunzi
I: Ukikiangalia unaweza kusema ni nyenz ganizilitumika kutengeneza hicho
R: Huu ni mpingo huu, maana unaona wamekwaruza kwaruza hivi, hiki cha udongo hakina mpango zaidi kulikoni hiki, ndio kina maringo zaidi kulikoni hiki, kwa hiyo hii ni ya kumvutia mvutaji
I: Kwa hiyo hii ni ya kumvutia mvutaji
R: Eee
I: Kwa hiyo inawezekana ilikuwa ni mti wa mpingo
R: Inawezekana ni mti wa mpingo, maana mpingo hauungui ukiweka mkaa hivi hauungui kabisa
I: Sawa sawa, na labda ukiangalia huo mrija wa kuvutia unaweza ukawa ulitengenezwa kwa mti gani?
R:Mimi naona kuna miti fulani ambayo ina nafasi katikati, inakuwa kama bomba
I: Unaitwaje huo mti
R: Kama muanzi, kuna miti fulani ambayo ukiuchonga huku juu huko ndani kuna njia, kwa hiyo unafanya kuchokoa na kijiti
I: Sifa yake ni mgumu au ni mlaini
R: Ni mgumu,mpaka upige chini ndio upasuke
I: Na ukilinganisha na kile ‘Kiko’ cha kwanza, kwahicho ulichokishika unadhani kikiletwa sokoni leo hii kikakutana n mvutaji
R: Hiki ni imara zaidi kulikoni hiki
I: Hiyo kamba yake tunaiona ni tofauti na ile ya kwanza, unadhani hiyo inaweza ikawa ni kamba ya aina gani
R: Ni kama kamba ya manila ile nyembamba, lakini kufunga hivi ni kwa sababu ya kuimarisha huu ‘Mtemba’, hapa na hapa na hapa kwa ajili ya kuimarisha
I: Kwa hali ya sasa kingeuzwa shilingi ngapi hicho ulichokishika
R: Hiki hapa kwa wakati huu, hata shilingi elfu kumi unaweza ukauziwa maana ni kizuri zaidi, lakini sasa kwa wakati huu hakitakua na bei kwa sababu havitumiki
I: tu assume umekutanan na mtu ambaye anatumia ‘Kiko’ kungekuwa tayari kulipa hiyo shilingi elfu kumi
R: Anganipa hiyo shilingi elfi kumi kwa sababu amezoea kuvuta kwa kutumia ‘Kiko’
chanzo: Amani-Stade Project / Mlalo Field Research 2023, Interview No. 05
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
-
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
-
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali