Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/1

Bangili ya shanga

Sammlung Braun
r 2018 / 18201
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18201
Kichwa
Bangili ya shanga
Vipimo
Kipenyo: 9cm
Nyenzo
Kioo shanga,
Ngozi
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_d5eb2734-9f44-42b8-bf59-9f17d68a7d9b
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uainishaji
vito vya kikabila  
Uzalishaji
Wakati
mpaka 1904-04-28
Mtu
  • Person (Mtengenezaji)
Mahali
  • Tansania
Kununua / Uuzaji
Wakati
1904-11-28
Maelezo
"Jumatatu 28. Mwezi wa kumi na moja 1904 [imepigwa mstari] nimepata tena mapambo kadhaa [...] [?]: 9. Mkanda wa Massai kama u. 103 [1] N° 8 lakini wenye shanga za kijani nyeupe buluu & nyekundu & ukiunganishwa na kimori cha kawaida chenye shanga (= 1 Rupie) 10. Bangili ya Massai, imetengenezwa kama N°9 [2] shanga: nyekundu, nyeupe, kijani, buluu iliyokolea, buluu iliyopauka. (= ½ Rupie) 11. Kimbao cha kuwekea masikioni cha Maßai kimechongwa na mbao & kimepakwa udongo mwekundu, upande moja umepambwa. (= 10 Pesa) [Michoro miwili yenye maelezo ya mtazamo] mbele upande / zawadi kutoka mama Oberst [3] Kühne v. u. 111, vg. shajara [4] 46. u.107. 12. Ala ya Waswahili huitwa "zezi". Mchoro unaofanana kwa kiasi fulani hupatikana: Ratzel, Völkerkunde, Leipzig 1887, kitabu 1. u. 449. Unaitwa fidla ya Wanika. Kifaa kimetengenezwa kwa ubao uliochongwa upande mmoja ukiwa na nyuzi za waya upande mwingine. [u. 105] kuna kibuyu kwa ajili ya utoaji sauti. Ubao umepambwa. (= 1/2 Rupie) [mchoro] angalia. Shajara 52. u. 75" [Utafsiri] [1] ukurasa. [2] nambari. [3] cheo kwenye jeshi ya wakoloni wanawake enzi zile waliitwa kwa cheo ya waume wao. [4] kitabu cha kumbukumbu cha kila siku.

chanzo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 43 (104)
mwandishi: Karl Braun
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mnunuzi)
    GND Explorer
  • Person (Mchuuzi)
Mahali
  • Amani
Malipo
Wakati
kutoka 1904-11-28
Maelezo
„10. Bangili ya Masai / shanga nyekundu,nyeupe,kijani, buluu iliyolokolea, buluu iliyopauka/Amani, 28. mwezi wa kuminamoja 1904 (= ½ Rp.) / TB 43,103 [sic! 43,104]" [Utafsiri]

chanzo: Museen Stade, r 2018 / 18566
mwandishi: Karl Braun
Mtu
Nambari za hesabu za zamani
  • 10
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
  • Hansestadt Stade (Mkopeshaji)
  • Bohmbach, Jürgen (* 1944) (Mkopeshaji)
    GND Explorer
  • Museum Schwedenspeicher (Mkopaji)
    GND Explorer
  • Gerd Mettjes (Mkopaji)
Mahali
  • Stade
Scientific use:
Wakati
2023-09-28
Maelezo
I: Sawa nina picha nyingine hapa ambayo imesajiliwa kwa namba 2018_18201_1 hebu mama […] iangalie na mama […] mnaweza kutuambia hicho ni nini? R1: Hii inaitwa kamba ya kufungia Engeene I: Engeene ni kamba ya kufungia nini? R1: Kama hii hapa lakini hiyo ni kamba ya ngozi I: Kwahiyo hii unafungia hiyo orkelaa? R1: Eeeeeh unafungia orkelaa I: Na hiyo ilikuwa inatengenezwa kwa ngozi ya nini? R1: Na ngozi ya ng’ombe siunaona ni ngumu I: Kwanini walitumia ngozi ya ng’ombe wakati hii ilikuwa imetumia ngozi ya kondoo mama […]? R1: Hii hapa ukitumia ngozi ya kondoo inakatika haraka kwa hapa I: Kwasababu hiyo ni ngumu? R1: Eeeh hii imekuwa nzito siumeona imeshonwa na ikishonewa inakuwa nzito eeh sasa ndiyo wanatumia hizi I: Ndiyo inaitwa Engeene? R1: Eeeeh I: Na hizo shanga shanga hizo mama […]? R1: Ni urembo tu ni urembo kama huu hapa anaweka rangi hii anaweka na rangi nyingine kama ameamua kuweka rangi tatu anaweka rangi tatu kama ameamua kuweka rangi mbili anaweka rangi mbili I: Na hizo zilikuwa zinauzwa shilingi ngapi hizo mtu akikuambia nitengenezee hiyo bado zinatengenezwa kama hizo siku hizi? R1: Eeeeh hii zinatengenezwa I: Sasa hivi zikitengenezwa kama hizo mnatumia mnatumia nini kufungia? R1: Tunafungia nguo alafu na ushanga nyingine unaitwa Engimeita ya kiunoni ndiyo tunafungia hapo I: Hiyo ni Engeene? R1: Eeeh Engeene

chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 03
mwandishi: I: Mohamed Seif, R1: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Mnazi
Scientific use:
Wakati
2023-09-29
Maelezo
I: Nina picha nyingine ambayo imesajiliwa kwa namba 2018_18201_1 bibi […] tuambie hiyo inaitwaje? R2: Hii ni ya mkono Arkataa I: Kwenye kuvaa anavaa sehemu gani? R2: Hapa mkono wa kulia wanaume I: Wanaume wa umri gani? R2: Hawa vijana ambao wana visinga I: Morani? R2: Eeeh Morani I: Kwahiyo hiyo ni kwa ajili ya vijana wa kiume tu? R2: Eeeh hata wasichana kama hawa wa zamani anavaa hapa I: Hapo mkononi? R2: Eeeeeh mkono huu I: Mkono wa kulia? R2: Eeeeh I: Ilikuwa ina maana gani ukivaa hapo? R2: Ni urembo tu wakupendeza tu I: Sasa hivi bado inatumika kuvaa? R2: Eeeh ipo nyingine sasa hivi haiwekwi kwenye ngozi anashona tu na nyuzi ya dukani anashona kama hivi lakini haiwekwi kamba I: Haiwekwi kwenye ngozi? R2: Hapana I: Kwanini hawaweki kwenye ngozi tena? R2: Watoto wa siku hizi ndiyo hawataki mwanangu unajua dunia imeshabadilika sana siku hizi siyo kama zamani I: Kwahiyo hiyo ni kwa ajili ya mkono tu? R2: Eeeeh I: Tena mkono wa kulia? R2: Eeeeh I: Na Morani ndiyo wanavaa? R2: Morani ndiyo wanavaa hiyo hii ni Arkataa ya mkono I: Waliokuwa wanatengeneza hizi zote pia ni wakina mama? R2: Wakina mama tu hakuna mwanaume ambaye anatengeneza hizi zote ni kazi za kina mama walikuwa wanafanya I: Na hiyo ilikuwa ni ngozi ya mbogo pia? R2: Eeeeh sasa hii ameshonea ya ng’ombe I: Kwahiyo ukikosa ya mbogo unashonea ya ng’ombe? R2: Eeeeh I: Na kwanini sanasana ilikuwa inatumika ni ngozi ya mbogo au ng’ombe? mama […] hebu tuambie R2: Ile Engosokwa imekuwa mzee hata zamani wazee walikuwa wanaweka mguuni bila ushanga anafungia tu maana wanasema inasaidia miguu ya wazee kuumwa umwa ukifunga ile inasaidia haiumi I: Inasaidia inakuwa haiumi umi inaponesha? R2: Eeeeh I: Kwahiyo ngozi ya mbogo lakini? R2: Eeeeeh I: Kwahiyo ukifunga ngozi ya ng’ombe inakuwa haisaidii kuponyesha? R2: Hapana haiwezi lakini hii Arkataa ni ngozi ya ng’ombe hii I: Sasa hivi wanatengeneza lakini hawatumii ngozi? R2: Hata kama unataka lakini hawa watoto wa karne hii hawatumii ngozi wanashona na uzi na sindano tu basi lakini hawaweki ngozi lakini kama mtu anasema anataka hii ya kitamaduni anashonewa I: Kwahiyo kazi yake kubwa ilikuwa ni kwa ajili ya urembo tu? R2: Eeeeh I: Kupendezesha? R2: Eeeh

chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 05
mwandishi: I: Mohamed Seif, R2: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Mnazi
Scientific use:
Wakati
2023-10-03
Maelezo
I: Haya asante sana nina picha nyingine hapa ambayo imesajiliwa kwa namba 2018_18201_1 namba moja uliitambua hii hiyo ni nini? R1: Hii tunasema Ndalama I: Maana yake ni nini Ndalama? R1: Maana yake hii ni ngozi lakini ngozi inaewekwa ushanga kurembesha kuweka urembo lakini ni ngozi I: Ni ngozi ya mnyama gani? R1: Ni ngozi ya ng’ombe inashonwa alafu inawekwa kwa wanaume lakini siyo wanawake ni wanaume tu wa kimasai ndiyo walikuwa wanavaa mguuni lakini katika hao wanaume siyo wanaume wote ni mwanaume ambaye ametahiriwa ameacha utoto maana kabla ya kutahiriwa wewe bado ni mtoto hata kama ni mkubwa kiasi gani hujaingizwa jandoni wewe ni mtoto kwahiyo ni wanaume walikuwa wanavaa na siyo watoto ambao bado hawajaenda jando na kutahiriwa I: Miguu gani walikuwa wanavaa? R1: Miguu yote ni urembo I: Ni vijana tu ndiyo walikuwa wanavaa waliotahiriwa tena? R1: Eeeeh mwanaume anavaa I: Kwanini wanawake walikuwa hawavai? R1: Wanawake walikuwa hawavai kwasababu hii ilikuwa inaashiria kwamba huyu ni mwanaume, wanawake nao walikuwa na kitu wanavaa wanawake walikuwa wanavaa vyuma miguuni yani unafungwa zamani mguu unafungwa chuma mpaka hapa alafu ikija hapa wanaiachia sasa kuiremba wanaiachia itanuke hivi ukienda inatatamka ta, ta, ta ndiyo inaashiria kwamba hawa ni wanawake I: Na bado inatumika hivi sasa ndalama? R1: Ndalama kuna watu wanaotumia sasa hivi kabila letu la wamasai ila wamegawanyika mimi ninaoona sasa hivi bado wanavaa ni upande wa Kenya wale wanapenda kuvaa wanavaa miguuni sawa na hata hawa wakwetu huku wanavaa lakini siyo hii sasa hivi wanavaa sijui niseme ni utandawazi umekuja sasa wao wanashona tofauti na hizi za sasa hivi hawapendelei R3: Sasa hivi wanavaa hizi siunaona zina utofauti wanasuka sasa hivi hii ni kwamba imesukwa na manila siyo ngozi hawatumii ngozi tena wanatumia vitu vya kisasa eeh hii ni manila ndiyo wanatumia sasa hivi hawatumii ngozi I: Bado jina hilo hilo ndalama? R3: Ndiyo ndalama I: Na waliokuwa wanashona hizo jinsia gani wanawake au wanaume? R3: Wanawake I: Wakuanzia umri gani hasa? R3: Rika kuanzia miaka 20 ndiyo wanaanza kujua kushona na kuendelea hapo ndiyo walikuwa wanashona I: Kwahiyo ilikuwa inatengenezwa kwa kutumia shanga na shanga kwa kimasai inaitwaje namba tatu tuambie? R3: Isae iko hapa ndogondogo tunaita isayeni na ipo kubwa tunaita orureshi kwahiyo zimegawanyika sana zipo za aina mbalimbali kuna isayeni na kuna nyingine orureshi na hii ni isayeni imeshonea hapa I: Isaye nini ndogondogo na orureshi ni kubwa kubwa? R3: Eeeeeh I: Kwahiyo sasa hivi hawatumii ngozi wanatumia kamba za manila? R3: Ndiyo kamba za manila mtu akija akisema anataka ya ngozi bado watu wana huo uwezo tu wa kushona tu na ngozi maana sahivi kuna watu tu ambao hawataki ya manila kuna watu sasa hivi asilimia kubwa wanasema mimi nataka mnishonee kwa kutumia ngozi kwahiyo watu bado wanauwezo tu wakutumia I: Na kwa mfano hii ndalama ikitengenezwa kama hivi inaweza ikauzwa shilingi ngapi namba moja hebu tuambie? R1: Kwasasa hivi maana zamani kulikuwa hakuna mambo ya kuuza sasa hivi ndiyo tumekuja kujanjaruka mwanamke alikuwa anamshona hivi basi anamshonea mume wake au rafiki yake lakini sasa hivi tumejanjaruka sasa hivi tunashona na tunauza pia imekuwa kama biashara sasa hivi I: Mmekuwa wajanja? R1: Eeeeh tumeacha ule ujinga wa zamani sasa hivi unashona na unauza na unajipatia hela nzuri tu ya kujikimu I: Ikishonwa kama hiyo inaweza ikauzwa shilingi ngapi? R1: Inategemea na upana ushanga itakayochukua I: Kwahiyo bei itatofautiana kulingana malighafi iliyotumika? R1: Eeeeh

chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 07
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Longido
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1904-11-28, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 43 (104)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1904-11-28, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566 (10)jifunze zaidi

Rejeo la ndani la kitu

Kijitabu cha hesabu

Kijitabu cha hesabu

r 2018 / 18566
Rejeo la ndani la kitu
Kuhusiana na
Kamba ya ngozi yenye shanga

Kamba ya ngozi yenye shanga

r 2018 / 18362
Rejeo la ndani la kitu
Mazingira/Muktadha wa upataji/Upatikanaji
Kamba ya ngozi yenye shanga

Kamba ya ngozi yenye shanga

r 2018 / 18202
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Bendi ya magoti ya ngozi na kamba ya bodice

Bendi ya magoti ya ngozi na kamba ya bodice

r 2018 / 18441 b
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Bendi ya magoti ya ngozi na kamba ya bodice

Bendi ya magoti ya ngozi na kamba ya bodice

r 2018 / 18441 a
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Kamba ya ngozi

Kamba ya ngozi

r 2018 / 18222
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:40:33+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji