Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/2

Chanuo la mbao

Sammlung Braun
r 2018 / 18470 b
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18470 b
Kichwa
Chanuo la mbao
Vipimo
Upana: 8cm, Urefu: 24,5cm
Nyenzo
Mbao
Fasihi
Eichhorn, A. Beiträge zur Kenntnis der Waschambaa, (nach hinterlassenen Aufzeichnungen von A. Karasek) I, 1911, GVK
Luschan, Felix von Beiträge zur Völkerkunde der deutschen Schutzgebiete, mit 48 Tafeln und 46 Textabbildungen, 1897, GVK
F. Ratzel, Völkerkunde, Bd. 1. Verl. des Bibliogr. Inst., Leipzig, 1894. 447
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_da7a270d-ce0e-43f1-aa64-12755b94ec81
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uainishaji
Utunzaji wa nywele na ndevu  
Uzalishaji
Wakati
mpaka ca. 1905-02-24
Mtu
  • Person (Mtengenezaji)
Mahali
  • Tansania
Kununua / Uuzaji
Wakati
1905-02-24
Maelezo
"[Safari ya kwenda Tanga kuanzia u. 64] Ijuma mwezi wa pili 1905 [imepigiwa mstari, u. 66] [...] [u. 67] wakati wa [...] [?] safari hii nimepata baadhi ya vitu vya kimila: [u. 68] 20. Vitambaa viwili vya kihindi. Vimetengenezwa na vitambaa vyeupe na vimepigwa chapa mapambo yenye rangi nyekundu nyeusi buluu na njano Kimoja kina upinde wenye mapambo halafu baadhi ya wanyama labda deers Wapanda farasi & wapanda tembo halafu wanaume. Kila kitu kimetengenezwa kikawaida mno, Kwa chini kuna upinde wa mimea na mungu wa kihindi nisiyemjua mwenye kichwa cha tembo . (= 13 Rupie) 21. Moa-Mkeka. Unatokana na viwanda vya mikeka vinavyoendeshwa na wazawa viko karibu na Moa,karibu na mpaka wa uingereza . Mikeka husukwa kwa kutumia Phoenix reclinata rangi ni nyeusi na njano. Mapambo yanabadilikabadilika sana. Biashara hufanyika na mikeka midogo tu. Mkeka wangu ni kubwa sana nimeupata kwa bahati tu. Umetengenezwa kwa ajili ya mwanamfalme Adalbert v. Preußen. Nimeupata kwa msaada wa utawala wa kata. (= 10 Rupie) 22. 3 Vitana vinavyotumiwa na wanawake wazawa kuchana nywele. Vina mapambo ya kawaida ya kuchonga.Havikupatikana madukani. Tulivipata tu kwa msaada wa Boy mmoja [u. 69) (kimoja 40 pesa) [mchoro] Felix von Luschan. Beiträge zur Völkerkunde d Deutsch. Schutzgebiete. Berlin 1897. (Dietrich Reimer) u.61-63. T. 42, 43, 44. [u. 69] Pia niliweza kununua [...] [?] 3 [...] [?] manyoya ya [?] tumbili mabega myeupe [...] [?] kutoka [...] [?] mkeka wa Mao. Nimenunua kila ngozi yenye manyoya kwa 2 Rup. 50 Pesa, [...] [?] rahisi zaidi [...] [?] Rupie 3 [...] [?] Pesa kwa kila mnyama huyu. – [...]" [Utafsiri]

chanzo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 44 (68)
mwandishi: Karl Braun
Mtu
  • Person, weiblich (Mchuuzi)
  • Person, männlich (Mshiriki)
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mnunuzi)
    GND Explorer
Mahali
  • Tanga
Malipo
Wakati
kutoka 1905-02-24
Maelezo
"22. Chanuo cha mbao / 40 Pesa / Tanga 24. mwezi wa 2. 1905 / Ratzel, F. Völkerkunde, Bd. I, Leipzig 1887, u. 447 / TB. 44, 68 / [mchoro unalingana na 2018 / 18470 ] / [imeongezewa kwa wino mwekundu] 1 Rp." [Utafsiri]

chanzo: Museen Stade, r 2018 / 18566
mwandishi: Karl Braun
Mtu
Nambari za hesabu za zamani
  • 22
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
Mahali
  • Stade
Scientific use:
Wakati
2023-06-08
Maelezo
I: Sawa asante hii tumemaliza hii na hapa nimeshika kifaa kingine ambacho kimesajiliwa kwa namba 2018_18470_AC hebu angalia unaweza kutuambia hiki ni kifaa gani? R: Haya ni machanuo I: Chanuo? R: Eeeeh I: Hizo ni chanuo hizo? R: Hizi ni chanuo I: Ziko tofauti unaweza ukatuambia kila moja inaweza ilikua na jina lake tofauti kulingana na aina au zote tu ni chanuo jina lake ni moja? R: Zote hizi ni chanuo I: Hebu unaweza ukatuambia kwa kilugha zinaitwaje kwa Kisambaa labda? R: Shanuo I: Shanuo ahaa Kisambaa inaitwa Shanuo sawa na watu gani wanatumia machanuo? R: Wanawaake I: Wanawake wanatumia kufanyaje? R: Kucha nywele na wakati akisukwa linapitishwa chanuo hapa anapitishiwa anaambiwa ashike upande huu kwasababu huwezi ziacha hivyo I: Sawasawa na watu wa tamaduni gani wanatumia zaidi machanuo? R: Wanawake I: Makabila gani hasa? R: Ahaa shanuo I: Haina kabila maalumu shanuo R: Eeeeh I: Kabila gani lenye wanawake wanaotumia machanuo zaid? R: Wasambaa I: Kwanini wanatumia hizi? R: Madukani unaweza ukakuta ni bei gali I: Na machanuo yanapatikana mkoa gani hasa maeneo gani? R: Hata hapa Amani yanapatikana I: Yanapatikana hata hapa Amani? R: Eeeeeh I: Watu wanayatengeneza? R: Eeeeeh I: Eeeeh ehh R: Unapata I: Kwahiyo hayana maeneo maalumu kwamba lazima usafiri uende mkoa fulani kutapata kwa wingi? R: Shanuo unaenda dukani unakuta chanuo ya plasitic size kama unazoziona hapa I: Kwahiyo wanatumia Zaidi wanawake? R: Eeeh wanawake I: Wanawake wa rika gani? R: Hawa wanawake wanaojipenda I: Wanaojipenda kuanzia umri gani? R: Umri unaomeza mate I: Umri unaomeza mate ndiyo umri gani? R: Ukimuona mwanamke amefikia umri wa kumeza mate anajipenda sana I: Umri wa kumeza mate yani ni umri wa anakuwa na jicho la husuda kuanzia miaka kumi na nane hivi hahahahahhahahah R: Hao ni watoto hao I: Miaka ishirini ishirini, ishirini na tano? R: Mhhh I: Kwako wewe umri wa kumeza mate ni umri gani? R: Aaaaa I: Mzee alikuwa hatari hahahhahah R: Umri wa kumeza mate ni kuanzia miaka ishirini naaa kuendelea eeh I: Akipita hapo mate lazima umeze kwanza hahhaha sawa mambo ya mzee [anonymous] hahahha ulikua mchezaji mzuri? R: Sana I: Mzee [anonymous] unadhani itafika wakati machanuo hayo ya design hiyo uliyoyashika yakawa hayatumiki tena? R: Unajua ni jinsi mtu anavopenda mwenyewe I: Labda kulingana na mabadiliko ya saivi umesema kuna machanuo yanakuja ya plastiki R: Eeeeh I: Unadhani machanuo haya ya ina hii inaweza kufika kipindi yakawa hayapatikani wala hayatumiki tena na akina mama? R: Inawezekana kwa wakati huu eeh I: Kwanini unadhani inawezekana kwa wakati huu? R: Hapa sinimeonyesha bwana huyu ni mtoto huyu yupo makamo kidogo huyu amekuwa mzee kidogo I: Kwahiyo zimetofautishwa kulingana na umri R: Ndiyo I: Kwahiyo hilo dogodogo nila mtoto? R: Eeeeeeh au [anonymous] wewe unasemaje I: Mimi nimesimamia pale pale kwenye kumeza mate? R: Hahahahahha I: Sasa nafikiri na kwenye vichwa watu wako tofauti R: Eeeh I: Mzee [anonymous] mtu atumie chanuo kuna kitu kingine anatakiwa kuwa nacho wakati anatumia chanuo? R: Ni mafuta tu I: Mafuta? R: Eeeeh basi I: Mfuta unayatumiaje? R: Mafuta unampaka kwenye nywele unachukua chanuo unachana unashika I: Na mantiki yakutumia mafuta ndipo utumie chanuo ni ipi? R: Ni kulainisha nywele I: Kulainisha nywele ili R: Chanuo ipite vizuri I: Mhhh kwahiyo mtu anapopaka mafuta alafu anachana ili chanuo lipite vizuri lisikwame Kwame kwahiyo ili utumie chanuo lazima upake mafuta R: Eeeeh I: Sawasawa na unadhani kuna umuhimu wa kutumia chanuo? R: Inategemeana na uko vipi wengine hawatumii mafuta anaoga tu alafu anachana nyewele bila mafuta tu I: Kwahiyo inategemea na aina ya nywele ya mtu R: Eeh I: Wewe ushawahi kutumia chanuo au mkeo ashawahi kutumia chanuo? R: Mke wangu anatumia chanuo I: Sawa na kwa hapa Amani umesema vinatengenezwa maeneo gani wanatengeneza? R: Wapo watu humu wanachonga chonga I: Ni maeneo gani mengine ulitembea kipindi hicho ukakuta zinatengenezwa hizi chanuo? R: Chanuo I: Eeeeh hizi chanuo ni maeneo yapi ulikuta watu wanatengeneza? R: Monga I: Monga ehee kwahiyo Monga kuna sehemu wanauza? R: Sokoni I: Unafikiri wanazouza wanazitoa wapi pale? R: Sasa nakuta kibao kimeanguka kinaenda kuchongewa chanuo anamwambia fundi huyo hebu niangalizie hichi ninaweza nikapta chanuo basi wanapatana bei I: Kwahiyo ni mbao zinatumika kutengenezea? R: Eeeeh I: Sawasawa na ukiangalia hiyo chanuo jinsi ilivotengenezwa kwa umaridadi kama huo kwa hali ya sasa hivi mtu chanuo kama hili anaweza kununua kwa shilingi ngapi? R: Hii kwa elfu kumi I: Hii kuanzia shilingi elfu kumi umesema mbao ndiyo zinatengeneza chanuo kuna namna nyingine nyenzo zingine zinaweza kutumika kutengenezea chanuo? R: Hapana ni mbao tu I: Ni mbao tu? R: Eeeh I: Nyenzo zake zinakuwa hazibadiliki toka miaka hiyo mpaka leo? R: Eeeeh I: Mhh sawasawa kwa hapa Amani ni Monga ndiyo unaweza ukapata machanuo? R: Eee I: Na sehemu gani nyingine unaweza ukapata machanuo? R: Kwa hapa Amani ukipita mitaani humu unaweza ukamkuta fundi mchongaji wa mbao na mchongaji wa chanuo

chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023 / Interview No. 01
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Amani
Scientific use:
Wakati
2023-06-08
Maelezo
I: Sawa nina picha nyingine hapa imesajiliwa kwa namba 2018_18470_a-c, hebu angalia unaweza ukatambua hiki ni kitu gani? R: Chanuo I: Naam R: Chanuo I: Chanuo maana yake nini chanuo R: La kuchania nywele I: La kuchania nywele? R: Eeeeh ndiyo tunavoita sisi, Wenye misuko yao wanatumia sana hizi I: Kilugha linaitwaje labda kwenye lugha ya kikwenu kabila gani kwani? R: Kwa kisambaa tunaita I: Shanuo? R: Wenzetu nao wanasema fumuo I: Fumuo? R: Eeeeh niletee fumuo yangu hapa I: Na mashanuo yanazalishwa Zaidi mikoa gani? R: Tuseme Bonde pia wengine wanachonga hizi, lakini tunasema wamakonde ndiyo wana mambo haya I: Sawasawa R: Hizi ndiyo za kizamani kabisa eeh I: Kwahiyo unaweza ukatuambia matumizi ya chanuo? R: Shanuo I: Inatumikaje shanuo? R: Unafumulia nywele zako fundi ukimuita akikusuka bila hii huwezi kusukwa I: Kwa ajili ya kusukia na kufumua nywele? R: Eeeeh I: Na watu gani wanatumia sana mashanuo? R: Wanawake wote I: Wanawake? R: Eeeeh I: Haina umri hiyo? R: Aaaaa haina umri I: Sawasawa unadhani inaweza ikafika wakati machanuo ya namna hiyo yakawa hayatumiki tena? R: Yatatumika kama mimi hii siwezi kununua mpira niache hii hapana I: Kwanini huwezi kuacha hiyo ya mbao? R: Mimi naona ni bora Zaidi I: Kuliko ya mpira? R: Eeeh kuliko ya mpira I: Sawasawa ili uweze kutumia chanuo unatakiwa uwe na kitu gani kingine? R: Aaa hii hii tu yenyewe lakini sasa hii kwa kweli za kizamanini nzuri sana kwasababu hata kama una mba ukichukua kitana huku kudogo ni kama kitana I: Huko kudogo ni kama kitana? R: Eeeh ni kama kitana I: Kwahiyo huko kukubwa? R: Unafumulia eeh kama ni kubwa nywele, nah uku kudogo Kukwangulia mba, Eeeh hata kama unanyoosha nywele I: Sawasawa kwenye makabila yenu chanuo lina umuhimu gani? R: Umuhimu ni huko kuchania nywele wakati wa kusukwa eh I: Na bado vinatengenezwa mashanuo haya ya design kama hiyo? R: Ya design kama hii wameacha wanatengeneza ya upade mmoja I: Ya upande mmoja? R: Eeeeh I: Unadhani kwanini wameacha kutengeneza hayo ya pande mbili? R: Naona wale wenyewe ambao ni wabunifu wa hizi naona sijui hawapo tena I: Sawasawa na ni watu gani wanatengeneza mashanuo? R: Zaidi wamakonde ndiyo walikuwa wanatengeneza I: Wamakonde? R: Eeeeh na hata humu humu pia wapo wengine I: Wakike au wakiume? R: Wakiume I: Wakiume? R: Eeeh I: Kwanini yanatengenezwa na wanaume na wakati wanatumia wanawake? R: Ilikuwa ni kazi ya kina baba hiyo I: Hahahahah ilikuwa ni kazi ya kina baba? R: Eeeeh I: Na unaweza kujua kwamba ni kitu gani kilitumika kutengenezea hayo machanuo? R: Miti kama mipingo, mifenesi eeh I: Miti?’ R: Eeeeh I: Kwanini mipingo na mifenesi? R: Waligundua tu wenyewe I: Hivi kwa sasa hivi kuna nyenzo nyingine inaweza kutumika kutengenezea machanuo kama haya? R: Naona hamna I: Kwahiyo ni mbao tu na hiyo miti tu hakuna nyenzo nyingine inaweza ikatumika? R: Hamna I: Ukiangalia hayo machanuo jinsi yalivo nakishiwa yakiletwa kwenye soko la sasa hivi yanaweza yakauzwa shilingi ngapi ngapi? R: Mpaka elfu tatu unaweza ununue I: Haya ya upande mmoja kwani yanauzwa shilingi ngapi? R: Elfu mbili, elfu moja miatano I: Kwahiyo haya yanaweza yakauzwa hadi shilingi elfu tatu R: Eeeeh I: Sawasawa haya asante R: Haya

chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023 / Interview No. 06
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Amani
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1905-02-24, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 44 (68)jifunze zaidi

Rejeo la ndani la kitu

Sega / Chanuo la mbao

Sega / Chanuo la mbao

r 2018 / 18229
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Sega ya mbao

Sega ya mbao

r 2018 / 18363
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Chanuo la mbao

Chanuo la mbao

r 2018 / 18493 a
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Chanuo la mbao

Chanuo la mbao

r 2018 / 18493 d
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Chanuo la mbao

Chanuo la mbao

r 2018 / 18493 c
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana

Rejeo la ndani la kitu

Kamm - Staatliche Museen zu Berlin

Rejeo la ndani la kitu
ist ähnliches Objekt

Kämme - Staatliche Museen zu Berlin

Rejeo la ndani la kitu
ist ähnliches Objekt

Kikwemuro - Staatliche Museen zu Berlin

Rejeo la ndani la kitu
ist ähnliches Objekt
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:32:45+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji