Wakati
1909-04-10
Maelezo
"Jumamosi 10. Mwezi wa nne 1909 [imepigwa mstari] Asubuhi nimeendelea kuufanyia kazi mzigo mkubwa wa mimea kwa ajili ya Berlin. Mchana mafaili. – Najaribu kukusanya vitu vyote ambavyo Wasuaheli [sic] huvinunua kwenye maduka ya Wahindi kama mahitaji yao. Kwa lengo hilo nimewafanya akina „Boy“ waandae orodha kwanza na hapo nikakuta vitu vingine ambavyo hata sivijui. Leo nimepata :kofia ya kituruki yenye rangi nyekundu iliyopauka imetengenezwa na kitambaa gandamizo chekundu huitwa kwa kisuaheli: kofia stambuli huku juu ina mpini mdogo [u. 46] inasemekana kwa kibonei [?]: huitwa shuju [?]. Kofia ya aina hiyo hugharimu hela 50 hapa Amani. Tanga hununuliwa kwa hela 25. Pia nikanunua kofia nyeupe ya kawaida. Imetariziwa na nyuzi nyeupe aina hii huitwa kofia ya eherhani [?] [inadhaniwa r 2018 / 18373]. Maana yake kofia iliyotengenezwa kwa cherehani. Hapa moja inagharimu nusu rupie, kule Tanga kama hela 30. / kofia kama ile yenye jina hilo hilo ila imeshonewa upinde wenye mapambo ya nyuzi nyeusi hapa inagharimu hela 75 pale Tanga hela 50 Mapambo hapa [?] kwa N* [1] ni mistari inayoingiliana vimeshonwa kiholela kwa mashine [michoro mitatu yenye umakini ya mistari ya mshono] Ikiwa kofia imekeketwa huitwa kofia ya someno [?], kofia iliyoshonwa [?] kamwe si laini kofia ya futo / kofia maridadi na ya thamani huitwa kofia buibui (shajara 52, u.39) na hulipiwa Rupien kadhaa. Pia nimenunua nguo kadhaa: [u. 47] [mchoro wa rangi] Kitambi, kitambaa chenye rangi nyingi kilichofumwa. Hutengenezwa India au inawezekana Uingereza. Mistari yenye rangi nyingi hutengenezwa na mapambo ya nyuzi zenye rangi zilizofumwa. Rangi kuu ni zambarau tepe nyembamba zenye rangi ya machungwa – manjano, nyeupe rangi ya ndimu nyeupe nyekundu na nyeupe zimefumwa kwa pambo lililopo hapa kila mstari hutengenezwa kwa nyuzi mbili. [mchoro wa rangi] pambo la juu huchukua nusu ya upana wote na linajirudia upande mwingine [?]. upana wote ni 106 cm, urefu 212 cm. Bei hapa Amani ni 1 rupie. Kitambaa huvaliwa na wanauma kiunoni. Kitambi kingine upana 16 cm b 168 kina upinde mwekundu katikati kuna sehemu zilizozungushwa na nyuzi za manjano, zenyewe ziliundwa kwa nyuzi nyekundu na nyeusi [?]. Kati ya upinde mwekundu na eneo la ndani kuna / [u. 48] [mchoro wa rangi na mwandishi] mstari wa wima mweupe. Kitambaa hicho pia huvaliwa na wanaume kiunoni na moja hugharamia 1 rp. 25. / Shuka au kitambaa cha kiunoni na upinde wa kawaida mweusi na mwekundu. Urefu 172 upana 89 cm, bei hapa Amani hela 60. [mchoro mdogo wa rangi] / shuka ya kawaida zaidi linagharamia hela 50 ni kitambaa, upana 98cm na urefu 186 cm lang. Upinde ni [masahihisho] mistari mwekundu kijani na zambarau. Bei ni hela 50. [mchoro mdogo wa rangi] / Pia nimepata ubani tofauti tofauti: [...] [u. 50] [mchoro wa rangi] pana [...] [?] (shajara 52, u. 59) Kikoi kina upinde wenye rangi nyingi. Vitambaa hivi vinasemekana kuwa maridadi zaidi. upana 95 cm urefu 168 cm bila upinde wa nyuzi zinazoning‘iniya urefu wa hizo ni 10 cm." [Utafsiri]
[1] The N-word (N*) is a highly racist term used to refer to Black people. The term originated in the context of "racial" theories and is closely linked to the history of slavery and colonialism. In the transcription of original sources, it has not been reproduced but instead marked as a racist, derogatory, and offensive term.
50 Heller (für Europäer), 25 Heller (für lokale Bevölkerung)
chanzo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 53 (46)
mwandishi: Karl Braun
Mtu
-
Braun, Karl (* 1870 † 1935)
(Mnunuzi)
GND Explorer
-
Mtu, haijulikani
(Mchuuzi)
Mahali