Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).
chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.
I: Nina picha hapa imesajiliwa kwa namba 2018_18302_001 hebu angalia unaweza ukafahamu hicho ni kitu gani?
R: Kishoka
I: Wanaita nini?
R: Kishoka
I: Kishoka?
R: Eeeeh
I: Ni kikabila gani hicho kishoka?
R: Hata wasambaa wanaita hivo kishoka siyo aina ya kaghembe kuna kale kaliko kaa hivi sasa huyu amekaa hivi siunamwona hivyo alivyo bwana kuna kile kijembe kilicho kaa hivi hasa huyu amekaa hivi hiki ni kishoka
I: Kishoka?
R: Eeeeh
I: Kwahiyo kinaitwa kishoka?
R: Eeeeh kishoka
I: Ni watu wa utamaduni gani wanatumia kishoka?
R: Hata wasambaa wanakitumia hiki
I: Wasambaa?
R: Eeeeh
I: Na kinapatikana zaidi mikoa gani?
R: Katika mikoa niliyoona ni hii mikoa ya Tanga
I: Tanga?
R: Eeeeh
I: Maeneo gani?
R: Wilaya ya muheza tarafa ya Amani ndiyo nilikionea hiki
I: Kinatumikaje kishoka?
R: Hiki kama kwa kukatia
I: Kukatia nini?
R: Wengine watu wanatumia kama silaha saa nyingine usiku mtu anatembea nacho kimsaidie kama silaha
I: Lakini kilitengenezwa kwa madhumuni yapi?
R: Hiki utakuta kuna wengine kuni ndogo ndogo hizi za vibanzi, vibanzi anapasua na haka haka kashoka
I: Unapasulia kuni?
R: Eeeeh hizi ndogondogo
I: Sawasawa
R: Maana hivi viko aina mbili
I: Ndiyo
R: Aina hii kuna mwingine naye hiki kimekaa hivi kwa mfano hata wanao panda minazi vile vipandio vyake vile wana
I: Tuzungumzie kwanza hiki hii unayoiona
R: Hii ni kama shoka
I: Hiyo ni shoka
R: Eeeeh
I: Kwahiyo inatumika kukatia kuni?
R: Eeeeh kukatia sehemu yoyote inayosumbua unaweza ukakata na haka na kakakata vizuri sana eeh
I: Kwahiyo wasambaa, wabondei wote wanatumia hiki
R: Eeeeh wote wanatumia hiki eeh
I: Ni watu gani hasa wantumia mashoka kati ya wanaume au wanawake wa umri gani katika jamii?
R: Hiki mimi nilivoona hata vijana walikuwa wanatumia eeh
I: Hakizingatii umri hiko?
R: Hakizingatii umri saa nyingine mtu anatumia kama silaha eeh
I: Hata wanawake pia?
R: Eeeeh wanatumia hiki
I: Na kwa mawazo yako unadhani inaweza ikafika wakati shoka likawa halina kazi tena katika matumizi ya sasa?
R: Kishoka hiki
I: Kuna tofauti kati ya kishoka na shoka?
R: Tofauti eeh
I: Kishoka?
R: Unatumia kwa mkono hivi
I: Kinakuwa ni kidogo?
R: Eeeh kidogo kama hiki
I: Aaaaah unadhani inaweza kufika wakati kishoka kinaweza kikafika wakati kisitumike tena?
R: Kama hiki hapa hukioni kwa watu hiki hapa hakionekani
I: Kwanini hakionekani?
R: Unajua jinsi gani wanavyo songa mbele uelewaji kimazingira wakati mwingine hivi hapa havitumiki vinakaa ndani tu eeh
I: Mazingira ya kivipi kwamba kitu hiki kisitumike?
R: Hivi hapa kama uharibifu wa misitu unakuta hiki utakitumia wapi kinakaa tu kama vile kumbu kumbu ndani
I: Kwahiyo kutokana na misitu kuharibiwa kikakosa matumizi?
R: Ndiyo kimekosa matumizi kinakaa kama kumbukumbu tu
I: Na ili utumie kishoka unatakiwa uwe na kitu gani kingine?
R: Sana sana uwe na panga eeh uwe na panga sasa sehemu ambazo ngumu unatumia panga lako sehemu ndogo ndogo zile unaweza ukatumia haka
I: Sawasawa na kishoka kilikuwa kina umuhimu gani hasa kwa watu wa kabila la kisambaa?
R: Unajua saa nyingine umuhimu saa nyingine wewe mwenyewe upenzi wa kile kitu eeh upenzi wa kile kitu kwamba bado uko moyoni mwako basi utakitumia ila ukikiona cha nini weka kando bwana eeh inatengemea jinsi gani unavokipenda
I: Kwahiyo umuhimu unakuja kulingana na unavokipenda?
R: Ndiyo unavokipenda
I: Sawasawa na kishoka bado kina tengenezwa kwasasa kuna watu bado wanatengeneza?
R: Sijaona kwa saivi
I: Kwahiyo utengenezaji umepotea kabisa?
R: Umepotea
I: Labda ukivuta picha ni miaka mingapi ulikuwa ukiona bado vinatengenezwa mzee [Anonym]?
R: Kwasababu hata hao wahunzi wanaotengeneza hivi hapa siwaoni tena kwa siku hizi za karibuni eeh
I: Kwanini?
R: Muda wake umeshasogea mbele
I: Muda umepita?
R: Muda umepita eeh
I: Sawasawa wanaotengeneza vishoka ni watu gani hasa kati ya wakike na wakiume?
R: Wakiume
I: Kwanini wakiume?
R: Unajua wenzetu wa kike kuna baadhi ya shughuli fulani niza wanaume tu tulikuwa hatuingiliani kwenye zile shughuli
I: Kitu gani kilikuwa kinafanya zisiingiliane?
R: Unajua tamaduni zile tabia sanasana wana mind kwamba hiyo bwana siyo kazi yako hii kazi niya mwenyewe niya huyu kazi hiyo watu walikuwa hawaingiliani kwenye shughuli kila mtu anafanya za kwake
I: Sababu kubwa hasa ilikuwa ni nini ukiachia maumbile ya kike na kiume kulikuwa na sababu nyingine?
R: Sana sana na uwezo
I: Uwezo wa kinamna gani?
R: Uwezo ule uchukue hiyo chuma uchome jikoni uchukue nyundo udesign unavotaka uchome udesign unavotaka nini na nini mwanamke anakuambia hiyo mimi hapana na ndiyo maana wanafanya wanaume
I: Uwezo unamaanisha nini mzee [Anonym]?
R: Unajua hii hapa unaweza ukakuta lichuma tu hapo limetupwa pale ukoke moto ukichome kile chuma ukidesign mpaka upate picha hii ni muda
I: Ilikuwa haizingatii mtu ana nguvu kiasi gani kutengeneza kishoka hebu tuelezee hapo mzee [Anonym]?
R: Unajua sanasana hii haitumii nguvu nyingi kwasababu moto ndiyo unaotumia unalainisha kwa moto
I: Sawasawa na waliokuwa wanatengeneza kishoka ni watu wa umri gani hasa kwa kipindi hicho?
R: Unajua ujuzi saa nyingine unaweza ukaupata ujuzi mapema mno kutokana na wewe mwenyewe unavyojituma unaweza ukaupata ujuzi ule wa mbele huko lakini sanasana utakuta wakati huo wanaofanya shughuli hii ni umri wa kati ndiyo wanafanya kazi ya kutengeneza kishoka
I: Wakuanzia miaka mingapi?
R: Miaka 30s au 20s kwenda mbele huko lakini mtu akishafikia umri kwenda miaka 70 huko anasema kazi bwana hiyo siiwezi
I: Kwasababu ameishiwa nguvu?
R: Saa nyingine kuishiwa nguvu ila kuwaachia wengine nao wafanye ili waweze kupa ridhiki pia eeh
I: Na unaweza ukafahamu ni nyezo gani zilikuwa zinatumika kutengeneza kishoka mzee [Anonym]?
R: Kishoka sanasana ni vyuma hivyo upate na nyundo upate na mpini huu eeh
I: Mpini wa mti wowote?
R: Eeeeh mti wowote ule ambao unavumilia ambao hauvunjiki vunjiki kirahisi unatumika kutengenezea
I: Mti mgumu?
R: Ndiyo mti mgumu
I: Sawasawa na material au nyenzo zilizokuwa zikitumika kutengeneza kishoka zilibadilika miaka ilivokuwa inaenda au zilibaki hizohizo tu chuma na mpini wa mti peke yake au kuna mabadiliko?
R: Eeeeh hivyo ndiyo vinavyotumika sanasana
I: Hakuna mabadiliko labda kwenye kutengeneza kishoka kwenye nyenzo zinazotumika mzee [Anonym]?
R: Mambao yanavobadilika hizi hapa ukipata labda spring zake hapo ukapata cherehe yake anakereza pale tayari kashamaliza
I: Kwahiyo inatumika kwa maana kutengeneza kwa chuma kwa chuma ama?
R: Chuma kwa chuma
I: Na kishoka kama hiko kwa hali ya sasa kinaweza kikauzwa shilingi ngapi?
R: Hiki
I: Eeeeh
R: Inategemea mtu anaweza akakuambia hata elfu 20 bwana
I: Hhahhahha
R: Eeeh sikapoteza muda wake kafanya kila kitu kadesign na nini anaweza akakuambia elfu 20 au elfu 15
I: Kwa mfano kwa muheza hapa ulikuwa unaweza ukapata maeneo gani ukivuta picha labda miaka miwili mitatu iliyopita?
R: Sanasana masokoni unavikuta vinauzwa sokoni
I: Soko lolote tu?
R: Eeeeh soko lolote lile unavikuta
chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023, Interview No. 04 mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
Amani
Nyalaka
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 46 (3)jifunze zaidi
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:13:33+01:00
Maoni
Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.