Wakati
2023-09-09
Maelezo
I: Basi asante tuendelee na picha nyingine, hapa nina picha nyingine imesajiliwa kwa namba 2018_18472_1, hebu angalia unaweza ukatambua hucho ni kitu gani?
R: Hiki kinakuwa kama hicho hicho ‘‘Kiko’’ lakini sasa kimerembeshwa zaidi, unaona kuna mahali pakushika hapa, unaona hapa hamna kamba, mtu anaweza kuweka kidole hapa ndani unaona pana tundu, sasa kimrembeshwa zaidi ili kuvutia wateja, lakini sasa hapa pa kuwekea pamekwenda upande, naona hapa palipokwenda upande unaweka mkaa hapo juu
I: Kwa hiyo hapo juu ndio pa kuwekea mkaa
R: Hapa ndipo pa kuwekea mkaa na unashika hapa
I: Nadhani viko hivi kwa sababu hapo kama unavyoona ndio hiki hapa
R: Sasa shida hapa kwa nini hii imekwenda hivi na mkaa utakaaje hapo maana kimelala hivi
I: Labda ni dizaini
R : Hiyo ni dizaini yao tu
I: Na inaonekana kama sura ya mtu hivi
R: Na hiki wameweka kama bunduki kama hapa pakuminya hivi, wakiweka kama bunduki
I: Kina sura ya mtu halafu ‘‘Kiko’’ kama bunduki, unadhani kimelengwa zaidi kuuziwa watu wa namna gani labda
R: Hiki ni kwa kuuziwa watu matajiri
I: Kwa kipindi kile cha miaka cha wamishionari, unadhani walilenga watu gani
R: Hiki kimelengwa kutumiwa na wazungu, lakini kichwa kipo si hiki au wana maana unaweka mkaa na tumbak hapa juu maana kichwa si hiki huku wamerembesha, lakini ni hicho hicho ‘‘Kiko’’, kimerembeshwa kwa ajili ya kupata bei kubwa
I: Na ukikiangalia hicho unadhani kilitengenezwa kwa kutumia nini
I: Hiki naona wametengeneza wazungu, sisi hatuwezi kutengeneza hivi kwa sababu kina vitu vingi vya kurembesha huku, sisi wanarembesha lakini sio kama hivi, hapa zaidi ni wazungu wamewaletea waafrika wakinunue
I: Na huo unadhani ni mti wa mpingo au udongo kama ulivyosema ukikiangalia vizuri
R: Huu ni mti wameuchonga wakaweka maringo wakafanya hivi wakafanya hivi, kwa sababu kuna vitu fulani vinavyofanya hivi ili kipendeze, hicho unashika hapa unaweka kidole hapa unashika hivi unavuta hivi, lakini kuwekea mkaa unaweka hapa, lakini sasa hiki ‘‘Kiko’’ wamekibinua kidogo
I: Sasa kwenye kuvuta pengine labda mtu lazima alale kidogo au
R: Hapana ni dizaini yao, maana mtu hawezi akavuta akiwa amelala
I: Na hivyo jinsi kilivyo unadhani kingeletwa sokoni kuuzwa kikakutana na mtu ambaye ni mtumiaji wa ‘‘Kiko’’, kingeweza kuuzwa shilingi ngapi
R: Kingeweza kuuzwa kama shilingi elfu 15 kwa sababu kimerembeshwa sana
I: Na kwa kipindi hicho unadhani kilipendezeshwa kwa ajili ya kuwavutia wazungu au waafrika
R: Hiki ‘‘Kiko’’ kimeletwa na wazungu ili kuvutia waafrika wanaovuta tumbaku, hata tumbakua walikuwa wanaleta hilo la kwao lakini sio kali kama la kwetu, la kwetu ni kali kwa sababu wanatengeneza wenyewe
chanzo: Amani-Stade Project / Mlalo Field Research, Interview No. 05
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
-
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
-
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali