Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/1

Rungu

Sammlung Braun
r 2018 / 18318
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18318
Kichwa
Rungu
Vipimo
Urefu: 56cm
Nyenzo
Mbao,
Chuma
Fasihi
Merker, Moritz Masai, Ethnogr. Monographie e. ostafrikan. Semitenvolkes, 1910, GVK
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_499a802a-aef3-423b-a0d7-3806e3f9ede1
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uzalishaji
Wakati
mpaka 1909-04-05
Mtu
  • Person (Mtengenezaji)
Ethnolojia
  • Massai  
Kununua / Uuzaji
Wakati
1909-04-05
Maelezo
„Jumatatu 5. Mwezi wa nne 1909 [imepigwa mstari] Kwenye maabara asubuhi nimefanyia kazi mzigo wa mimea, mchana mafaili. – nimepata rungu zuri liliochongwa lilizungishwa na misumari ya shaba. (= 1 Rp. 50) mapambo ya kuchonga ni kama yale yanayopatikana kwa N* [1] wa hapa hasahasa kwenye vitu vya ""Lewa"". Kigeni kwangu yalikuwa mapambo yale ya mawimbi na pinde. Mnyama ni kenge (Kenge [?]) kama wanavyoishi porini. Mpini umegongeshwa na fedha au shaba nyeupe kwa chini. Kitu hicho ni kuukuu kina rangi ya kawia iliyokolea na kinatoa harufu ya mafuta amabayo wa Masai wanayapaka kwenye vitu vyao. Kwa vyovyote vile umetengenezwa kwa umakini usio wa kawaida (mchoro na vipimo 36 cm, 20 cm. Kofia mbaja masai wetu wa farasi aliyeniuzia kitu hicho akadai ni fimbo ya sultani wa ki Masai na kinaitwa ""es sēre"". Neno hilo linapatikana kwa Merker, Die Masai, Berlin 1904, u. 130 lakini hakuna picha ya fimbo kama hicho. Nategemea ikiwa Merker angeiona angeichora. Hayo yananifanya nifikiri kwamba pamoja na kwamba nimeinunua kwa Masai labda inatoka kwingineko. " [Utafsiri] [1] The N-word (N*) is a highly racist term used to refer to Black people. The term originated in the context of ""racial"" theories and is closely linked to the history of slavery and colonialism. In the transcription of original sources, it has not been reproduced but instead marked as a racist, derogatory, and offensive term.

chanzo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 53 (44)
mwandishi: Karl Braun
Mtu
  • unknown actor (Mchuuzi)
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mnunuzi)
    GND Explorer
Mahali
  • Amani
Malipo
Wakati
kutoka 1909-04-05
Maelezo
"123. Rungu,au fimbo ya sultani wa Masai = sere / limechongwa vizuri & na misumari & limepigwa karatasi ya bai nyeupe / Amani 5 mwezi wa nne 1909. / TB 53,44 (mchoro makini!) / 1 Rp 50. / [mchoro]" [Utafsiri]

chanzo: Museen Stade, r 2018 / 18566
mwandishi: Karl Braun
Mtu
Nambari za hesabu za zamani
  • 123
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
  • Hansestadt Stade (Mkopeshaji)
  • Museum Schwedenspeicher (Mkopaji)
    GND Explorer
  • Bohmbach, Jürgen (* 1944) (Mkopeshaji)
    GND Explorer
  • Gerd Mettjes (Mkopaji)
Mahali
  • Stade
Scientific use:
Wakati
2023-09-15
Maelezo
I: Sawa tumalize na picha ya mwisho ambayo imesajiliwa kwa namba 2018_18318_1 hebu mzee [anonymous] na mzee [anonymous] hichi ni nini? R1: Hii ni rung utu I: Ni rungu? R1: Eeeeh lakini sasa aliyekuwa ameitengeneza wanatengeneza kiaina kibiashara zaidi siyo haya marungu tunayo shika huko porini hii imetyngenezwa kwa ajili ya kuuzwa imekaa kibiashara zaidi I: Ni hiyo hiyo olgumaa? R1: Eeeh olgumaa I: Kwahiyo marungu kama hayo yanashikwa na mtu yoyote tu? R1: Eeeh I: Wakati naishika hiyo nilidhani inawezekana niya leigwanani? R1: Ya leingwanani ni ile nyeusi inachongwa tu nyeusi na nyeupe ila ukifika kwenye kikao ukikutwa nao unaulizwa hii umeishika kama nani wewe leigwanani hapo sasa ndiyo unasema hapana hii tu niliishika kama fimbo ya urembo maana leo leigwanani yupo mtu yoyote hatakiwi kuishika I: Hahhahha R1: Lakini kama ni mtaani nashika lakini laigwenani akikuona umeshika zaidi ya yeye unapingwa faini na hii inachongwa rasimi kwa malaigwenani na kuna mti fulani ndiyo unachongwa kwa ajili ya malaigwenani hizi tunazoshika wengine ni miti mingine siyo mti ambao laigwenani anachongewani tofauti unachongwa alafu inakabidhiwa rasimi sasa kama wewe ndiyo kiongozi eeeh I: Kwahiyo rungu kama hizi kwa rika nyingine ni kama fashion tum zee Majuka hebu tuambie hapo? R1: Hii sasa hivi hii imetengenezwa kwa biashara huoni ameweka weka mavitu vitu na laigwenani haweki hiyo ya kwake inatengenezwa na wzee anakabidhiwa anatafutwa yule fundi anatengeneza anachonga anatengeneza vizuri anakabidhi wazee waende wakampe huyu kiongozi aliyechaguliwa I: Sawasawa olgumaa? R1: Eeeeh olgumaa I: Hhahahhaa sawasawa basi mimi nichukue fursa hii kuwashukuru mzee [anonymous] na mzee [anonymous] nadhani tumejadili vitu vingi na muda umeenda na hatukuwa na maandalizi maalumu hatuwezi kuendelea kuwaweka hapa sana nashukuru kwa ushiriki wenu mmetupa taarifa muhimu sana R1: Ndiyo I: Asanteni sana R: Wote: Shukurani pia

chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 01
mwandishi: I: Mohamed Seif, R1, R2: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Mnazi
Scientific use:
Wakati
2023-10-04
Maelezo
I: Asante namba moja na namba mbili mimi nadhani kwasababu hii nyingine ulisema niya Kenya labda tuchukue muda kidogo wakuzungumza kidogo kwasababu nimeiona tuimalizie hii kwasababu kina mama wanatusubiria huko tuombe dakika chache tumalizie na picha hii imesajiliwa kwa namba 2018_18318_1 hebu namba mbili ishike maana wewe ndiyo uliitambua umeshaiona unaweza kutuambia hiyo ni rungu kwa hilo kabila walilikua nayo lilikuwa ni kabila gani? R2: Niliona wakati nilienda kenye mwaka 2004 kwa watu wanaitwa omijikenda Mombasa hii wanatumia kwa machief huko kwao macheif wakipewa mamlaka wanapokwenda kwenye kikao anakwenda na rungu yake kuzungumzia mambo mazito kuhusu jamii ya omijikenda kwahiyo hii ni rungu ya utawala I: Na kikwao huko omijikenda wanaiitaje hii? R2: Sikuuliza jina nilijua tu mimi ni rungu I: Na hiyo rungu inaonekana imechorwa inapicha ya mjusi kuna sehemu hapa haijaonekana vizuri lakini inapicha ya mjusi kwa pembeni ya ubavu wake sehemu mojawapo unaweza ukafahamu kwamba walikuwa wanamaanisha nini kuwepo huo mjusi? R2: Mimi nafikiri tu imewekwa kwasababu ni fimbo ya utawala na fimbo ya utawala lazima iwekwe vitu vya kulinda huu ni mjusi na huu mjusi nafikiri hata kwenye miko yao haishikwi na kila mtu hii niya kwasababu ya mfalme au kwasababu ya chief anayesimamia jamii ya omijikenda kwahiyo nafikiri sikuielewa sana lakina nafikiri niliona ni rungu tu ya utawala na hizi ni mapambo inawekwa vitu kama gold vidogo vidogo vichuma vinarundikwa ili iwe na urembo urembo I: Kwahiyo inawekwa vichuma? R2: Ndiyo I: Lakini yenyewe inatengenezwa kwa mti au ni nini hii? R2: Hii inatengenezwa na mpira aina ya plastiki lakini pia kuna aina ya miti inatengenezwa na aina ya miti ya kutengenezea mbao na asilimia kubwa ni black hata yenyewe ni black kwahiyo inawekwa hiyo ili irembeshwe I: Hivyo vichuma ni kwa ajili ya kurembesha? R2: Eeeeh ya kurembesha I: Waliokuwa wanatumia hiyo ni machief wa kiume? R2: Ni machief wa kiume R: Wakina mama hawashiki rungu hata mama Samia hashiki I: Kwahiyo hii ilikuwa pia ni sawa na hiyo ya laigwanani? R1: Ya laigwanani ni nyingine I: Sawasawa basi mimi nishukuru kwa muda wenu na kiukweli nimefaidi kwasababu nisingefika Kimokoa kuna taarifa ningezikosa ni nzito tumetumia muda mfupi lakini ni vitu vichache lakini taarifa tulizozipata ni nzito nadhani sijazipata sehemu zote nilizopita kwahiyo niwashukuru sana kwasababu kiukweli nimejifunza mengi kutoka kwenu na kama mtapendezwa pia ningependa kuona kama siyo mbali nyumbani hivyo vitu ambavyo vinafanana na vya kwetu ningeweza kuviona ningefurahi na kupiga picha ya kumbukumbu pia maana ndiyo tunahifadhi kumbukumbu hivi kwahiyo kama hamtojali na mtakuwa hamjabanwa na majukumu mengine mnaweza mkaturuhusu tukaenda tukaona na kupiga picha baada ya hapa lakini naomba mniruhusu nizime R1&2: Sawa I: Asanteni sana R1&2: Karibu

chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 09
mwandishi: I: Mohamed Seif, R1-3: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Kimokouwa
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1909-04-05, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 53 (43 )jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566 (123)jifunze zaidi
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:41:07+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji