Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/2

Kibuyu ca kuhifadhia maziwa

Sammlung Braun
r 2018 / 18329 a
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18329 a
Kichwa
Kibuyu ca kuhifadhia maziwa
Vipimo
Urefu: 28cm, Kipenyo: 9cm
Nyenzo
Bottle gourd
Fasihi
Baumann, Oscar Durch Massailand zur Nilquelle, Reisen und Forschungen der Massai-Expedition des deutschen Antisklaverei-Komite in den Jahren 1891 - 1893, 1894, GVK
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_4b42ca78-ad14-4bba-9815-b6938ba70253
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uainishaji
Vyombo/hifadhi (kazi ya jikoni)  
Uzalishaji
Wakati
mpaka ca. 1905-10-10
Mtu
  • Person (Mtengenezaji)
Mahali
  • Bukoba
Mchango
Wakati
1905-10-10
Maelezo
"Jumanne 10. Mwezi wa kumi 1905 [imepigwa mstari] Kuna vitu viwili vya kimila [...] [?], alizawadiwa Max: kijiko cha mbao kilichochongwa kutoka kampuni ya Silva kijijini Amani [mchoro] [orodha. na. Karl Braun 32] / upinde na mishale mitatu (imenunuliwa kwa Boy (Rup. 1). / chombo cha maziwa = Kibuju kutoka Uganda, zawadi kutoka kwa Geh. Rat [1] Stuhlmann, alichokileta [...] [?] kutoka safari zake. Kilitengenezwa kwa mbao na kupakwa [...] [?] laini. Mfuniko umesukwa [...] [?]. Chombo kinaning’iniya kwenye wavu uliosukwa. [mchoro chombo na maelezo] chombo cha maziwa cha mbao cha Watussi. Baumann, O. Durch Massailand z. Nilquelle, Berlin 1894, u. 207. [orodha. na Karl Braun 33, 33a] – jioni matembezi Kwozalalla. – [...]" [Utafsiri] [1] Cheo cha kitawala."

chanzo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 46 (3)
mwandishi: Karl Braun
Mtu
  • Stuhlmann, Franz (* 1863 † 1928) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • unknown actor (Mpokeaji)
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mpokeaji)
    GND Explorer
Mahali
  • Amani
Malipo
Wakati
kutoka 1905-10-31
Maelezo
"33. Chombo cha maziwa = kutoka Uganda. Kibuyu chenye umbo cha chupa / zawadi: Kiongozi wa kitawala / Dr. F. Stuhlmann (kinatoka kwenye safari na Emin Pascha) / Amani 10 mwezi wa kumi. 1905 / [mchoro] / [imeongezewa kwa wino mwekundu] 1 Rp."

chanzo: Museen Stade, r 2018 / 18566
mwandishi: Karl Braun
Mtu
Nambari za hesabu za zamani
  • 33
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
namo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
  • Hansestadt Stade (Mkopeshaji)
  • Bohmbach, Jürgen (* 1944) (Mkopeshaji)
    GND Explorer
  • Gerd Mettjes (Mkopaji)
Mahali
  • Stade
Scientific use:
Wakati
2023-06-20
Maelezo
I: Na picha hii imesajiliwa kwa namba 2018_18329_1 hebu angalia picha hii unaweza kutambua hicho ni nini? R: Hiki kwa mimi ninavoona ni aina ya either niseme buyu au ubao mwembamba ila nafikiria ni ubao mwembamba walioigisha kama buyu maana tuna tunaliwekea maji tunaita mabuyu ambayo hata wamasai wanayatumia ndiyo ninayohisi either ni hiyo au zile mbao nyembamba zinaitwa plaudi wanazifanyia utafiti kuweka glasi na hii kama kibuyu cha kuwekea maji hiyo nahisi hivo au lakini hii haswa nahisi ni buyu maana kama ingekuwa ni ufinyazi au ubao ungekuwa siyo hivi eeh mimi nahisi hivi na hii picha nahisi kwamba ubunifu huu ulikuwa hapa Zigi. I: Watu wakabila gani walikuwa wakitengeneza hii? R: Hao walikuwa ni watu mchanganyiko wa makabila mbalimbali ya huko nyuma ambapo kuna Wasambaa, na Wanyamwezi na Wagogo ndiyo ambao wanatumia vitu hivi vya asili kwa asilimia kubwa sana. I: Wazigua, Wasambaa, Wagogo, na Wanyamwezi? R: Ndiyo waliokuwa wanatumia vitu hivi na hapa kwenye eneo letu hili walikuwepo hao makabila yote mchanganyiko kwahiyo hivi vitu hivi sivishangai ambao sasa hivi wameboresha zaidi vinapatikana kwa Wamasai pamoja na Wagogo eeeh. I: Ndiyo hahhahaaa. R: Eeeeeh sisi tumeacha tunatumia hivi vitu vya kisasa vya plastic vya udongo. I: Na walikua wanaliitaje hasa kikabila kwa Wasambaa? R: Sisi Wasambaa tunaita boma. I: Boma? R: Eheeeee yani boma siyo boma la zizi boma ni asili ya mmea unapandwa unakuwa tunaita vibuyu eeh. I: Sawasawa. R: Maana kuna buyu lile la mti na hili buyu la mmea kama maboga. I: Kama maboga? R: Eeeeh ndiyo unazaa vitu ambavyo vikikomaa tunaviondoa uchafu kule ndani ni kiwekezo either cha kunywea maji au kuwekea maji au maziwa hii ndiyo maana hivi tunaita ni vifaa vilivyotumika kwa ajili ya matumizi ya maji au chakula humu unaweza kutia maziwa yakaganda, au unakwenda mbali unakwenda shamba unatia pure. I: Pure? R: Eeeeh chakula pure zinakaa hapa unaweka pale unakwenda unalima ukichoka unakula hivi vitu hivi na ukichoka hivi au maji na hii glasi yake unalima umechoka unaona kiu unachukua kibuyu chako hicho unatia kwenye glasi unakunywa. I: Unakunywa? R: Eeeeh taratibu ya maisha ambayo hata wababa wa sasa hivi huko wenzetu Wamasai hivi vitu wanavitumia sana mpaka sasa hivi mila zao kidogo tumestaarabika kwasababu tuko Pwani eeh hatuvitumii sana. I: Tumepata mabadiliko. R: Eeeeh mabadiliko. I: Hahahaha. R: Tunatumia vitu vya kisasa. I: Na matumizi walikuwa wanatumia jinsia gani hasa hizo buyu? R: Hivi vitu jinsia hizi mbili mke na mume ndiyo vitu haswa wanawake ndiyo wanao vitengeneza na kuhifadhia maana ndiyo waandalizi wanaume wakiandaa kama ni maji, maziwa, au tongwa wanaweka humo. I: Mhhhh. R: Eeeeh wanaviandaa anampa bwana ake akienda shambani asipate tabu ni kwamba niletee maji huko. I: Wanawake ndiyo waliokuwa wanaviandaa sana. R: Eeeeh wanawake ndiyo wanaandaa na kuvitengeneza kwa ajili ya kuhifadhia vitu vitakavyo wafaa wakati wa shughuli zao eeh. I: Kwahiyo waliokuwa wanatengeneza ni wanawake au ni wanaume? R: Wanaotengeneza ni wanaume. I: Wanaume? R: Ehee wanawake ndiyo wanapewa ndiyo wanahifadhia hayo maji au maziwa au tunaita tongwa maana tongwa nafikiri nyinyi vijana mnazisikia tu. I: Tunazisikia tu. R: Eeeh mnasikia tu lakini ndiyo ilikuwa chai hatuitumii sisi tulikua tunatumia uji au tongwa ndiyo kifungua kinywa. I: Tongwa? R: Eeeeeh unafanya kazi umechoka unamimina kutoka humo imewekwa tongwa lako unakunywa. I: Mhhh. R: Eeeeh. I: Ni wanaume wa umri gani walikuwa wakitengeneza mabuyu kama haya? R: Umri kwasababu zamani mtu mdogo ukiambiwa ni mdogo ana miaka 20s na kitu. I: Miaka 20 na kitu? R: Eheee hao ndiyo wenye kazi hizi za uhunzi huu wa kutengeneza hivi vifaa wakijua hivi kwa mama zao vitawasaidia wao na baba zao kwa kuwekea vitu kama hivi. I: Mhhh. R: Eeeeh. I: Unadhani kitu gani kilipelekea kwa jamii za watu wa pwani kuacha kutumia vifaa vya namna hiyo? R: Unajua kila watu mnavyoendelea kutembea unajifunza vitu vya namna hii kwanza vikianguka vinavunjika kama walivokuwa wanatengeneza hivi vikombe vya udongo lakini ona sasa hivi wamebadilisha vya plasitic ambavyo hata uangushe haviharibiki hivyo wameacha maana hiki ni aina ya kibuyu kikikuponyoka tu tayari kimeshakufa ndiyo maana watu vikatoweka. I: Hahahahhaha. R: Wakaingia kwenye ya kisasa kuchukua vikombe vya udongo au vya plastic ndiyo maana huku kwasababu sisi watu wa mwambao watu ndiyo tumeanza kustaarabika maana wageni wakija na meli na ndege wa kwanza kutuona ni sisi. I: Hahhahhah. R: Kwahiyo kumkaribisha hivi vitu hivi atavishangaa maana huenda ikawa kwao havipo lakini vipo huoni kwamba akaona kwamba tukawathamini kwenye mambo haya kuna watu wa sitaarabu usipowapa hivi vitu ndiyo hivyo tumeacha vimetoweka sana vimebaki tu baadhi mpaka sasa hivi vipo wamo wanao vitumia vibuyu bado vipo kabisa tena zaidi kwenye tambiko aah hivi kwenye tambiko ndiyo ambavyo tunatumia pamoja na kata ila sasa hivi kuna kata hizi za plastic lakini tunacho huko nyumbani kwangu kata ninayo ya nazi. I: Mnazi? R: Nazi ile inatengenezwa unaitia mpini ambayo hiyo zamani hata msikitini ndiyo tulikuwa tunatumia kuchukua udhu ambayo mimi sasa hivi tunategemea kata haya hapo nyumbani hata ukitaka nikuonyeshe nakuonyesha I: Na buyu lipo? R: Buyu sina I: Mhhhh R: Eeeeeh I: Lakini ni vitu vinavyoenda sambamba? R: Vizuri sana yani hii katika tambiko kwa mbondei, mzigua ni lazima hii itumike au kata ya maji hivi vitu hivi tunavijua kwenye mila zetu I: Ndiyo R: Eeeeeh na mimi ndiyo maana hiyo bila ya kata ni iko hapo kwa ajili ya tambiko na kiti hiki cha ubao ambacho kina miguu mitatu kigoda I: Kigoda? R: Eeeeh mimi humu nyumbani kipo I: Lazima kipatikane? R: Hicho sikikosi hahahha I: Hahahaha R: Maana nicha mila eeh I: Kwahiyo kutumia kibuyu cha namna hiyo lazima uwe na kata au unaweza ukatumia peke yake? R: Unaweza kutumia hichi hichi tena kama upo peke yako unatumia badala ya kuwa na glasi unabandika mdomo pale unajinywesha eeh lakini kama kwa kuwa sasa ustaarabu umeenea unachukua bwana hebu nipe kikombe nitie haya maziwa au tongwa langu maana hilo tongwa wengine mpaka sasa hivi tunatumia I: Na labda kwenye mila unaweza ukatuambia buyu linatumikaje kwenye mila? R: Buyu linatumika kwa kuweka ile imani iliyotuingia kwamba hayo maji kuyachukua ukiyatia humu unamaanisha kwa sababu zamani dini ni mustaarabu umeingia lakini kwa mila yetu iliyokuwa imetujaa moyoni ya imani kwamba tukifanya hivi Mungu pia anasikia basi imani ile tumeishika mpaka sasa hivi mila ndiyo maana inaendelea kudumu kwamba tufanye hiki kitu hiki faida yake ni hii tumesikia mpaka tumeona mpaka sasa hivi tunaihisi hivyo eeh I: Kwahiyo kwenye mila ni kitu gani kilikuwa kinawekwa humo ndani na kinatumikaje? R: Humu either ni maji au kwa makabila mengine maziwa au tongwa tunayozungumza hili unatandika kuna majani fulani either ya mgomba aina ya mgomba unaweka hapo unatambikia kwa yale ambayo hisia yako inajisikia kwamba kuna mila yetu fulani hii inatakiwa hivi unakwenda pale unaomboleza yeye sijui ni nani, ni nani unaona tatizo hili haliondoki tunaomba ukalifungulie baraka ili tatizo lisitokee basi mkweli baada ya muda Mungu anajalia lile tatizo lililokuwa linaondoka kwahiyo ndiyo maana unaambiwa mila ni mwisho kwa sababu inasaidia jamii kutoa kwenye matatizo kwenda kwenye hali nzuri eeh mimi kwa ukubwa wangu ndivyo ninavyoelewa I: Nilikuwa nataka kufahamu tumeshatia maji kwa baadhi ya makabila kama ulivyosema au maziwa au tongwa humu ndani umeshatandika majani yetu ya mgomba kinachofanyika hapo ni kitu gani? R: Hapo inategemea either ni maji tupu au ni hilo tongwa au ugali uliochanganywa na asali ndiyo unaumwagia pale chini unazungumza hayo maneno I: Ambayo ulikuwa umeyahifadhi? R: Eeeeh ambayo ulikuwa umeyahifadhi humo ndani eeehe unaumwagia kidogo kidogo pale huku unanuia I: Huku unanuia? R: Eeeeh huku unanuia kwamba bwana tunaona tatizo hili basi wewe fulani ni nani tunaomba hili tatizo kama hili ndiyo linalo tusumbua tunaomba kwamba likanyamaze I: Kwahiyo hapo mnakuwa mnawataja mababu? R: Mababu I: Waanzilishi wa ukoo? R: Waanzilishi wa ukoo kwamba wewe fulani uliyekuwa ukipata tatizo unafanya kama hivi tuko hapa twakutumia hizo salamu ubariki hayo maombi yetu kwamba hichi tunachokiona kiishe kweli hiyo mila ina matokeo yake yale matatizo uliyokuwa unayapata yanatoweka hii ndiyo maana ya kutumia dhana hizi ambazo hata sasa hivi tunazikumbuka kwamba ndiyo hizo zilikuwa zinatusaidia kwenye matatizo yakitufikia au chombo hiki tukiwa tuna kiu maji tunahifadhi humo au hilo tongwa au hata asali wakati mwingine eeeh I: Na kwa maeneo labda ya Amani sehemu gani ninaweza nikaenda nikavikuta hivi? R: Hivi ninaweza nikakuambia kuna sehemu hii ya Amani sehemu ya Shebo I: Shebo? R: Hii unaweza ukaipata Meseya kati I: Ndiyo R: Ambapo panaitwa Bomubomu unaweza ukaipata halafu Makanya I: Makanya? R: Ambapo inachanganyika na kwa Mdimu hivi vitu huwezi ukavikosa huwezi ukatembea ukasema unataka kibuyu hapa alafu ukakikosa hivyo vitu vinapatikana I: Na huku hasa ni makabila gani yalikuwa yakitumia hiki? R: Ni Wasambaa, Wazigua wamechanganyikana sasa hivi hata Wabena hivi wanavitumia sana eeh I: Na Wabena walikuwa wanatumiaje? R: Hawa mimi haswa haswa walikuwa wanatumia kwenye pombe I: Kwenye pombe? R: Pombe wanapenda sana kuweka hapa wanaita Ulanzi I: Ulanzi R: Ehee I: Wanahifadhi au wananywea? R: Wanahifadhi nyingine ndiyo kwenye glasi kama hii wananywea maana hivi vitu hivi wanavitengeneza sana yani wanaviiga watu sasa hivi wanahisia ya kutengeneza hivi vitu vya asili kwa nyenzo hizi za plastic au nailoni, nailoni wanautundu sana wa kuchonga vitu kwa ajili ya watalii waje waone kwamba hapo zamani tulikuwa hivi I: Mhhh R: Eeeeeeh I: Na hapo nyuma ni vitu gani vilikuwa vinatumika kutengenezea hivyo vifaa? R: Hivi kwanza ni kisu, alafu kuna aina ya chuma ila laini, laini inaitwa kombeo ndiyo ambayo ule uchafu anaukomba akikunja hivi kwenye kibuyu anakwaruza kule ndani maana nako si kuna pango wanakwaruza kuruu, kuruu yanaondoa yale mauchafu yanayobakia karibu na hili ganda la nje ambayo ni nene kuondoa uchachu yani ukiweka vile inachachuka haraka inaharibika haraka lakini ukishaweka usafi namna hii inakaa haiharibiki ile ladha yake I: Sawasawa na hii glasi ilikuwa inatengenezwa kwa nyenzo gani hasa? R: Hii mimi nahisi kama siyo muanzi ni aina ya mti wanauchonga hivi halafu ndiyo wanatumia hilo kombeo eeeh ili iwe nyembamba ee I: Ni miti gani ambayo inaweza kutumika kutengenezea glasi kama hizi? R: Kuna mti mkuzu I: Mkuzu? R: Maana ni laini kuna mti unaitwa mfufu I: Mfufu? R: Ehee kuna mti mfufu, mkuzu, miti hiyo ndiyo walikuwa wanaiona mwepesi alafu kuna huu mti ulikuwa unatengeneza vitanda vyetu vya asili vya kamba ulikuwa unaitwa muheti I: Muheti? R: Eeeeh muheti nayo ni milaini siyo migumu I: Na labda turudi katika uhalisia wa sasa hivi maana imebakia katika matumizi ya mila ukikuta kitu kama hicho kinauzwa sokoni wewe unaweza ukakinunua kwa shilingi ngapi? R: Walikuwa wanaita nkhasi I: Nkhasi R: Eeeeeh nkhasi I: Ndiyo maana yake nini glasi au? R: Eeeeh I: Ni Kisambaa hicho hahha R: Ninke iyo nkhasi yangu aho eeh I: Hhahhahha R: Eeeeh bwana hivi vitu vimetumika huko mpaka sasa hivi vinatumika baadhi eee watu bado wanavitumia I: Na nkhasi kama hizi kati ya wanaume na wanawake wa umri gani hasa? R: Umri haswa watu wa umri wa wakati huo vijana wenye miaka 20s unajua ndiyo maana sasa hivi wanazaa na miaka kumi na nne, kumi na tatu lakini zamani miaka 29, 30 ndiyo wanaanza kutumia lakini kwa hivi vilikuwa na watu wa miaka kuanzia 30 na kwenda juu eeh I: Ambao tayari wana miji yao R: Eeeeh wana miji yao na wanawafundisha watoto wao hebu niletee kibuyu changu hapo na maji hapo anakuja anamimina anakunywa akikosa, ile kata eeh ninayo bwana hapo ndani kata ya mnazi ninayo mtaiona mimi nikifanya mila zangu ndiyo hiyo ninayoitumia eeeeh I: Sawasawa tuthaminishe hiko kibuyu na hiyo nkhasi? R: Kwa sasa hivi I: Ndiyo kwa sasa hivi R: Kwa sasa hivi watu wanaita ni vitu vya utalii na mila I: Utalii na mila? R: Eeeeh maana mtu anakuwa anachukua kwa mila hapa kati 4000, 5000 hukosi eeh kutokana sasa hivi fedha haina thamani zamani ukiambiwa shilingi hizo I: Ni hela nyingi? R: Ni hela kubwa sana kwahiyo hivi ndivyo kwa elfu 5000, 4000 hukosi I: Sawasawa basi kwa leo tutakuwa tumeishia hapa na hizi picha mbili ulizoweza kuzitambua nadhani tutakutembelea tena wakati mwingine R: Mimi nipo karibuni sana mimi kama Mungu atatujalia maana tunazungumza hatujui ya mbele kama tuko hai basi utakuja nitakukaribisha I: Basi asante sana kwa muda wako R: Mimi nashukuru Mungu na atujalie I: InshaAllah R: Atupe umri mpaka hapo utakapo kumbuka kuja basi umenikuta alhamdulillah kama huku nikuta hao utakao wakuta kama una dodoso basi utaendelea nao karibuni sana I: Asante sana R: Haya asante

chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023 / Interview No. 27
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Amani
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 46 (3)jifunze zaidi

Rejeo la ndani la kitu

Ladle ya kuni

Ladle ya kuni

r 2018 / 18505 b
Rejeo la ndani la kitu
Kuhusiana na
Kikombe cha mbao

Kikombe cha mbao

r 2018 / 18329 b
Rejeo la ndani la kitu
Kuhusiana na

Rejeo la ndani la kitu

Milchgefäß - Staatliche Museen zu Berlin

Rejeo la ndani la kitu
ist ähnliches Objekt

Milchgefäß - Staatliche Museen zu Berlin

Rejeo la ndani la kitu
ist ähnliches Objekt
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:13:30+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji