Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/1

Marimba

Sammlung Braun
r 2018 / 18263
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18263
Kichwa
Marimba
Vipimo
Upana: 44cm, Urefu: 50cm
Nyenzo
Mbao
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_5953695d-8942-479d-ac93-75dca73924bf
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uainishaji
Vyombo vya muziki  
Uzalishaji
Wakati
mpaka ca. 1920
Mtu
  • Mtu, haijulikani (Mtengenezaji)
Mahali
  • Tansania
Acquisition:
Wakati
ca. 1904 - ca. 1920
Mtu
Mahali
  • Tansania
Malipo
Wakati
kutoka ca. 1920
Mtu
Nambari za hesabu za zamani
  • 260
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
Mahali
  • Stade
Scientific use:
Wakati
2023-06-09
Maelezo
I: Naomba nichukue picha nyingine, hapa nina picha imesajiliwa kwa namba 2018_18663_1, hebu angalia unaweza ukafahamu hicho ni kitu gani? R: Hii ni mianzi I: Hiyo ni mianzi jina lake ni mianzi? R: Vijiti vya mianzi I: Vijiti vya mianzi? R: Eeeeh I: Kilikuwa na jina maalumu? R: Ni mianzi tu I: Kwanini imeungwa ungwa? R: Hapa wameunga ni kama ngoma hapa wameunga hapa wanapiga hapa inalia mlio I: Mlio? R: Mlio eeh I: Vilikua vinatumika kwenye ngoma? R: Eheee I: Labda jina la moja kwa moja jina Lake Kinaitwaje? R: Yani jina Lake Niseme nilivoona hapa wanaita marimba I: Marimba? R: Eeeeh I: Mhh hahahahahah marimba R: Eheee ukipiga nde nde nde vinalia hivi I: Watu wautamaduni gani marimba? R: Yani sanasana wasambaa I: Wasambaa? R: Eeeeh wasambaa, wabondei eeh wametumia sana hivi vitu I: Kwahiyo kilikua kinapatikana zaidi kwenye mikoa gani hasa? R: Mkoa wa Tanga I: Mkoa wa Tanga maeneo gani hasa? R: Sana sana hata humu Amani maana ngoma hizi zilitumika sana I: Kwahiyo kilikua kinatumika wakati wa ngoma? R: Eeeeh wakati wa ngoma na zamani vijana hata wanangoma tu za kila siku zao za jumamosi wanasheria kwamba jumamosi tunakwenda kucheza ngoma eeh ndiyo hivo I: Eee marimba? R: Ndiyo hahhahha R: Hata huko Lushoto zilikuwepo I: Zilikuwepo? R: Eeeeh I: Sawa sawa na ni watu gani hasa walikuwa wakitumia marimba? R: Watu wote wake kwa waume I: Watu wote? R: Vijana hasa I: Wakuanzia umri gani? R: Kuanzia umri wa miaka kumi na sita, kumi na nane na ishirini na kuendelea mpaka thelathini na tano I: Kwanini walikuwa vijana zaidi? R: Vijana waliona kama starehe yao wana dansi kama sasa hivi I: Ilikuwa starehe yao? R: Ndiyo ilikuwa starehe yao I: Kwahiyo vijana wa kike na wakiume walikuwa wanatumia? R: Eeeeh naona hivi hata sasa bado vinatumika sana hasa huko Bonde vinatumika mpaka sasa hata kwenye sherehe wanasherehe wanatumia kwenye harusi wanatumia wanacheza eeh I: Na unadhani inaweza ikafika wakati marimba ikawa haitumiki tena? R: Naona kuna sehemu haita koma I: Kwanini unadhani haito koma? R: Kwasababu kama mpaka sasa inaendelea na hawa wanaokuwa siwanaikuta nawao wanaiendeleza I: Sawasawa na ili marimba itumike ilikuwa inapaswa itumike na vitu gani vingine kwa pamoja ili ifanye kazi? R: Kuna ngoma, I: Kwahiyo marimba inaendana na ngoma? R: Eeeh unatkiwa uwe na ngoma I: Kulikua kuna ngoma maalumu au ngoma yoyote ulikua unaweza kutumia na marimba? R: Siyo kama hizi ngoma za shule wana ngoma zao walizounda I: Ngoma za vikundi vya kiutamaduni? R: Eheee ngoma za vikundi vya kiutamaduni I: Kwenye tamaduni za wasambaa marimba ina umuhimu ga ni kwao? R: Hizi marimba zina umuhimu tuseme kwenye tamaduni za kisambaa walitumia ngoma hizi Zaidi sana zilikuwa za wabondei lakini hata kwa wasambaa ngoma walikuwa wanatumia ngoma sana eeh kwenye shughuli zao za hapo zamani kuna tamaduni ya wasichana wamekuwa wanafanyiwa ngoma vijana wakiume msichana akijifungua wanatumia ngoma eeh I: Sawasawa na marimba bado zinatengenezwa R: Kwa humu tambarare humu Bonde nikihesabu ni hili eneo la kutoka hapa kwenda kule kote Lushoto huko tunaita Bonde zinatumika I: Na bado zinatengenezwa? R: Ndiyo bado zinatengenezwa I: Sawasawa R: Kwasababu hata mwaka jana tu hapa nimezikuta huko kwa mdimu I: Kwa mdimu? R: Eeeeh I: Kwa mdimu wapi? R: Hapa kwa mdimu hapo kisiwani na huku ng’ambo eeh bado zipo wanazicheza I: Sawa na ni watu gani walikuwa wakizitengeneza zaidi marimba? R: Hawa ni wanaume vijana haswa haswa eeh I: Vijana wale ambao wanazitumia R: Eeeeh wanazitengeneza ndiyo I: Sasa na unadhani marimba zilikuwa zinatengenezwa kwa kutumia nini hasa? R: Marimba sasa wanatengeneza kwa kutumia mti ya mianzi I: Mianzi? R: Eeeeh I: Kwahiyo ni mianzi na vitu gani vingine vinatumika? R: Mianzi na hizi kamba ni waya waya hizi I: Kamba na waya wa kawaida au? R: Hizi ni waya za kawaida ni waya hizi sio kamba ni waya hizi I: Ni waya? R: Eeeeh I: Sawasawa unadhani vimekuwa vikibadilika au toka miaka na miaka ni hizo hizo a u zilikuwa zikibadilika badilika vifaa vya kutengenezea marimba? R: Kubadilisha wanaweza kubadilisha na kamba sasa hivi wanaziita manila sehemu nyingine unakuta manila sehemu nyingine unakuta waya ee I: Sawasawa labda kwenye mazingira yetu ya sasa marimba inaweza ikauzwa shilingi ngapi? R: Kwasasa? I: Eeeeh R: Hizi nyuzi? I: Hiyo marimba yenyewe R: Hiyo marimba kwa sasa kama mtu anatengeneza anachukua elfu kumi na tano hata ishirini inategemea I: Elfu kumi na tano hadi ishirini? R: Eeeeeh

chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023, Interview No. 03
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Amani

Rejeo la ndani la kitu

Xylophonplatten - Staatliche Museen zu Berlin

Rejeo la ndani la kitu
ist ähnliches Objekt

Xylophonplatten - Staatliche Museen zu Berlin

Rejeo la ndani la kitu
ist ähnliches Objekt
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:37:26+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji