Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/3

Bangili ya shanga

Sammlung Braun
r 2018 / 18207 a
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18207 a
Kichwa
Bangili ya shanga
Vipimo
Urefu: 18cm, Upana: 10,5cm
Nyenzo
Kioo shanga
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_b3aba1f7-1c19-4c1e-a7ce-9767e6f22c3f
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uainishaji
vito vya kikabila  
Uzalishaji
Wakati
mpaka 1906-05-26
Mtu
  • Person (Mtengenezaji)
Mahali
  • Tansania
Kununua / Uuzaji
Wakati
1906-05-26
Maelezo
"„Jumamosi 26. Mwezi wa tano 1906 [imepigwa mstari] [njiani na Dr [7] Lenz kutoka kwenye meli ya mvuke bandarini Dar es Salaam hadi ""Meiller-Shamba"" tukaendelea hadi ""Waldschlöschen"" [8], kupitia makazi ya wazawa, wakati wa kurudi kupitia sokoni kuelekea meli ya mvuke] [...] Nimekwenda melini na kweli kulikuwa an ujumbe ""urudi haraka mavuno ya karanga yamemalizika."" nifanyaje kabla ya tarehe 7. Mwezi wa sita hakuna meli ya mvuke. Nikaenda makao makuu ya utawala nikaagizwa nisafiri Mikindani nikaangalie mengi yawezekanavyo. Nikifurahiahatimaye kuwa na mwelekeo nikatembea kurudi. – Barbarani nikakutana na mwanamume aliyekuwa anauza vitu kadhaa [u. 15].: Meli kubwa iliyochongwa na kifuu (?) imetengenezwa na fundi bei yake ilikuwa Rupie 2 halafu mitumbwi miwili midogo imetengenezwa kutoka nusu ya tunda ya baobab kushoto na kulia na viambatanisho vinavyoelea majini dann [mchoro wa ] boti hizo za wazawa huitwa ""Ngarawa"" [orofdha. na. Karl Braun 74]. Pia vinyago viwili kwa ajili ya Pepo Goma, kila moja kimewekewa kauri (kila moja = 1 Rupie) [mchoro] [Orofdha. na. Karl Braun 75], pambo kubwa la kichwa lenye manyoya na shanga za kioo = 6 Rup. [mchoro] [orofdha. na. Karl Braun 76] & bangili tatu kwamatumizi yale yale = 5 Rup [Orofdha. na. Karl Braun 77]. Nimetapeliwa na hivi vitu kwa maneno ya mkazi wa hapa aliyekuwepo melini akisema vitu hivyo vyanunuliwa kwa Rupie 1 ila sikuamini jioni melini"" [Utafsiri] [7] daktari au mwenye phd [8] kasri ndogo msituni"

chanzo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 47 (15)
mwandishi: Karl Braun
Mtu
  • Mtu, haijulikani (Mchuuzi)
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mnunuzi)
    GND Explorer
Mahali
  • Dar es Salaam
Malipo
Wakati
1906-05-26
Maelezo
"77. Bangili ya shanga za kioo nyeusi nyeupe na nyekundu . / Daresalam mwezi wa tano 1906 / 3 = 5 Rp. / TB 47,15 / juu na chini imewekewa nyoya nyeupe [mchoro]" [Utafsiri]

chanzo: Museen Stade, r 2018 / 18566
mwandishi: Karl Braun
Mtu
Nambari za hesabu za zamani
  • 77
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
  • Hansestadt Stade (Mkopeshaji)
  • Museum Schwedenspeicher (Mkopaji)
    GND Explorer
  • Bohmbach, Jürgen (* 1944) (Mkopeshaji)
    GND Explorer
  • Gerd Mettjes (Mkopeshaji)
Mahali
  • Stade
Scientific use:
Wakati
2023-09-15
Maelezo
I: Nina picha ya mwisho mzee [anonymous] hapa kwa siku ya leo imesajiliwa kwa namba 2018_18207_3 hebu iangalie hii R2: Hii imetengenezwa kwa ajili ya mikono I: Hiyo inaitwaje? R2: Emustai engaena na engaena maana yake ni mkono sasa inatengenezwa alafu inakuja kufungiwa hapa kwenye mkono au kama ni ndefu inaweza kuwa mkanda wa kiuno ukauvaa kiunoni R3: Ila hii niya mkono I: Eeehe mzee [anonymous] ili nyingine ulituambia ni mshono wa ngao huu ni mshono wa nini hebu tuambie? R2: Hii ni kurembesha tu ili ipendeze rangi hizi alizoweka eeh huoni amechanganya rangi aina kama tatu au nne nyekundu, nyeusi, na nyeupe I: Kwahiyo hizi zilikuwa zinavaliwa na watu gani wa kike au wakiume mzee [anonymous] hebu tuelezee? R2: Inavaliwa na kila mtu R3: Lakini sanasana ni vijana watu wadogo wadogo lakini mzee hawezi kuvaa hii kabisa ni vijana wadogo tu I: Vijana wadogo wadogo kuanzia miaka mingapi? R2: Hawa wa sasa kuanzia miaka 16, 20 wanavaa lakini sisi kama wazee hatuvai hizi kabisa tushavuka huko I: Wazee hawavai? R2: Hapana lakini huzuiliwi ila unajizuia mwenyewe I: Kutokana na rika lako? R2: Eeeeh sasa mambo ya watoto utaenda kuyafata fata I: Kwahiyo hii walikuwa wanavaa wanaume na wanawake au wanavaa jinsia gani hasa mzee [anonymous]? R2: Hasa inavaliwa na wanaume R3: Ila hata wanawake wanavaa I: Emustani Engaena? R2: Eeeh Emustai Engaena I: Engaena ndiyo mkono? R2: Eeeeeh na unajua hata kwenye kiuno bwana inakaa kama ni ndefu inavaliwa na kiunoni emborosi I: Emboross ndiyo kiuno? R2: Eeeh ndiyo kiuno I: Kwahiyo ikiwa fupi niya mkono? R2: Eeeeh niya mkono I: Ikiwa ndefu ya kiuno? R2: Eeeeh ya kiuno I: Na hii walikuwa wanashona na shanga na kitu gani? R2: Na kamba fulani na ngozi lakini hii imetengenezwa tu kibiashara siyo, ile yenyewe ambayo imetengenezwa yani hii imetengenezwa kwa kuuzwa au kupingwa picha eeh lakini siyo, ile yenyewe sasa hivi hii bwana ukiihitaji haki ya Mungu ukisema hapa nishonee nikapige picha alafu niende nikaonyeshe unatengenezewa kitu ambacho ni kizuri kinashonwa vizuri na kwa ustadi mkubwa I: Kwahiyo hii ilikuwa ni ngozi ya mnyama gani hii? R2: Ng’ombe I: Niya ng’ombe? R2: Eeeh ngozi ya ng’ombe I: Kwahiyo wanavaa vijana wote wa kike na wakiume? R2: Eeeeh I: Emustani engaena? R2: Au emborosi I: Emboross ndiyo ya kiuno? R2: Eeeh shanga yya kiuno, atakusumbua lakini mambo ya ushanga ushanga muulize hayo ndiyo mambo yao I: Basi mzee [anonymous] mimi nikushukuru kwa ushiriki wako maelezo yako yamekuwa niya muhimu na tija kubwa kwasababu umeweza kutambua vitu na kuvieleza kwa undani zaidi kwasababu ni vitu ambavyo vinagusa moja kwa moja mila na desturi za kabila lako kwahiyo mimi nishukuru nichukue muda huu kukushukuru kwa muda wako na pia kwa kuitikia wito maana hii ni heshima kubwa kwetu najua una majukumu mengi makubwa sana nashukuru sana asante sana R2: Haya

chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 02
mwandishi: I: Mohamed Seif, R2, 3: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Mnazi
Scientific use:
Wakati
2023-10-04
Maelezo
I: Nina picha nyingine hapa ambayo imesajiliwa kwa namba 2018_18207_3 hii pia mliitambua mnaweza mkanikumbusha jina lake? R1: Hii inaitwa engomesha I: Hiyo inatumikaje? R2: Engomesha wanavaa wote kijana anavaa na morani anavaa kwasababu zote ni ushanga ambao wote wanaweza wakavaa I: Wanavaa kipindi gani? R2: Binti au upande wa kike wa binti akiwa binti msichana lakini hata akifika ile hatua ya kuwa seikiki bado anaweza akavaa lakini morani upande wa wanaume morani anavaa tu akiwa morani akishaacha umorani anaacha I: Wanavaa sehemu gani? R2: Mkono wa chini I: Kwa mkono wa kulia au wakushoto? R2: Mikono yote I: Ni kwa ajili ya urembo tu au ina maana nyingine? R2: Haina maana R1: Pia wanavaa kwasababu yeye mwenyewe anataka urembo yeye mwenyewe anaonyesha mikono yake yote in urembo akishika fimbo anakuwa kapendeza lakini haina maana nyinginme mbaya nikupendeza kwake tu I: Labda ni kwa ajili ya kuvutia morani wakati wa kucheza? R1: Eeeh kama anapendeza basi na macho yako yanaona I: Namba tatu unataka kuongezea kitu? R3: Ni hivyo hivyo tu I: Labda mnaweza mkaniambia hii aina ya mishono hii inaitwaje namba moja hebu tuambie jina la huu mshono? R1: Hii imeshonwa kwa uzi tu enopini ya kawaida kwasababu kama ni kitu ambacho kimesukwa hakionekani hizi uzi lakini kama unaona kitu ambacho kimeshonwa na enopini inaonekana enopini maaana ndiyo hii ambayo inaonekana ndani ya hii I: Unaweza ukatambua kwamba imeshonwa kwa nyenzo gani haswa ni kitu gani na kitu gani kimetumika kushona hiyo engomesha namba moja hebu hebu tuambie nyenzo zilizotumika kushonea R1: Hii imeshonwa kwa enopini hii ambayo umemwambia namba moja ng’ombe ana enopini ya kukaa ndani ya nyama kwenye mkonga ile ngozi nyeupe anakuja kutoa kuna mstari mmoja anatoa kitu kinaitwa enopini mtu ambaye anaweka kwenye fimbo anaweka juu ya bati itakaa siku mbili, au siku tatu itakauka baada ya kukauka itakuja kutengenezwa ili aje kushonea hivi vitu imeshonwa na enopini R2: Inashonwa na enopini tu hakuna shanga I: Ukiangalia vizuri inaonekana kama kuna ngozi, ngozi unaweza ukajua kwamba ni ngozi ya nini? R1: Hiyo ni ngozi ya ng’ombe au ya kondoo kwasababu ng’ombe ana ngozi nzito kondoo au mbuzi wana ngozi nyepesi kuna watu wengine wanatengeneza ngozi ya mbuzi wanatengeneza na kisu basi inatoa kwasababu ngozi yake ni nyepesi na ndiyo hii anashonea hii engomesha mpaka inakamilika

chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 10
mwandishi: I: Mohamed Seif, R2, R1: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Kimokouwa
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566 (77)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1906-05-26, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 47 (14-16)jifunze zaidi

Rejeo la ndani la kitu

Meli ndogo

Meli ndogo

r 2018 / 18324 b
Rejeo la ndani la kitu
Mazingira/Muktadha wa upataji/Upatikanaji
Meli ndogo

Meli ndogo

r 2018 / 18324 a
Rejeo la ndani la kitu
Mazingira/Muktadha wa upataji/Upatikanaji
Bangili ya shanga

Bangili ya shanga

r 2018 / 18397 b
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Mask iliyofanywa kwa vipande vya wicker na shells za cowrie

Mask iliyofanywa kwa vipande vya wicker na shells za cowrie

r 2018 / 18491
Rejeo la ndani la kitu
Mazingira/Muktadha wa upataji/Upatikanaji
Bangili ya shanga

Bangili ya shanga

r 2018 / 18516 a
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Bangili ya shanga

Bangili ya shanga

r 2018 / 18516 b
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Bangili yenye shanga

Bangili yenye shanga

r 2018 / 18520
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Mask iliyotengenezwa kwa vipande vya kusuka na shells za cowrie

Mask iliyotengenezwa kwa vipande vya kusuka na shells za cowrie

r 2018 / 18522
Rejeo la ndani la kitu
Mazingira/Muktadha wa upataji/Upatikanaji
Vazi la kichwa lenye manyoya na shanga

Vazi la kichwa lenye manyoya na shanga

r 2018 / 18527
Rejeo la ndani la kitu
Mazingira/Muktadha wa upataji/Upatikanaji
Apron ya shanga

Apron ya shanga

r 2018 / 18517
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:53:32+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji