Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/3

Mkanda wa shanga

Sammlung Braun
r 2018 / 18542 b
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18542 b
Kichwa
Mkanda wa shanga
Nyenzo
Kioo shanga
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_0b239bf0-9e53-4e78-896d-d3fca9534ba1
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uainishaji
Vito vya mwili na nguo (nguo za wanaume)  
Vito vya mwili na mavazi (Nguo za wanawake)  
Uzalishaji
Wakati
mpaka ca. 1907-02-05
Mtu
  • Person (Mtengenezaji)
Mahali
  • Tansania
Kununua / Uuzaji
Wakati
1907-02-05
Maelezo
"Jumanne 5. Mwezi wa pili 1907 [imepigwa mstari] Karani mgeni amefika nimekutana naye kwa muda mfupi tu anapaswa kuweka orodha ya vitu vilivyopo sawa ila hawezi akafaulu [u. 2] Max amenunua mkanda wa kiMasai: 2 Rp. 50. Mapambo ya shanga juu ya ngozi ya ng’ombe.Shanga zilizotumika zina rangi zilizokolea nyeupe zambarau nyekundu kijani. Mapambo ni mstari wa kawaida wenye umbile wa msumeno: Urefu 71 cm / Upana 4 ½ cm. [Mchoro wenye umakini wa mapambo] Geh. Rat [1] Stuhlmann ameleta vitabu vya safari na picha za India & Italia, zilizoangaliwa jioni." [Utafsiri] [1] Cheo cha kitawala.

chanzo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 49 (2)
mwandishi: Karl Braun
Mtu
  • Mtu, haijulikani (Mchuuzi)
  • unknown actor (Mnunuzi)
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mkusanyaji)
    GND Explorer
Mahali
  • Amani
Malipo
Maelezo
"84. Mkanda wa Maasai / mapambo ya shanga yaliyoshonwa kama msumeno kwenye ngozi nyeupe, zambarau, nyekundu, kijani. urefu 71 cm, upana 4 ½ cm. / 2 ½ Rp. Amani 5. mwezi wa pili. 1907 / TB. 49,2 / [mchoro]" [Utafsiri]

chanzo: Museen Stade, r 2018 / 18566
mwandishi: Karl Braun
Mtu
Nambari za hesabu za zamani
  • 84
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
Mahali
  • Stade
Scientific use:
Wakati
2023-09-15
Maelezo
I: Sawa tunaenda kwenye picha nyingine ambayo imesajiliwa kwa namba 2018_18542-1 hii mlisema inaitwa? R1: Ingimeta I: Ingimeta hii ya kwanza hapa R1: Eeeh hii ya kwanza I: Sawa hii ingimeta inatumikaje? R2: Hii niya wasichana na ndiyo mkanda wao ukishafikisha miaka 9 msichana anatengenezewa hii anaanza kuivaa na ndiyo mkanda wake kabisa I: Hii ya emutha R1: Hii emutha emborosi anaifunga kiunoni ndani yake wanavaa wanawake wa kawaida tu ndiyo wanavaa I: Kuanzia umri gani hii ya kufunga kiunoni? R1: Kuvaa akiwa na miaka 10, 15, 20 ila akishafika umri wa kuolewa anaacha zote mbili anaingia kwenye utu uzima eeh anaenda ukubwani kwahiyo havai tena hizo anawaachia watoto ndiyo wavae I: Kuna nyingine anavaa tofauti na hizo? R1: Mkanda, sikioni na ushanga I: Kwahiyo hizi ni bado akiwa binti? R1: Bado ni msichana ukimkuta nayo hii bado ni mtoto bado hajaolewa I: Kwahiyo utoto unaisha akiwa na umri gani? R2: Akiwa na miaka 15, 20 sema akipata bwana wake anaachana na hii I: Kwahiyo hii ingimeta inavaliwa nje? R1: Eeeeeeh I: Lakini emutha emborosi? R1: Inavaliwa ndani I: Sawasawa nani kwa ajili ya wasichana tu? R1: Wasichana tu I: Sawasawa na ilikuwa na umuhimu gani hasa? R1: Ni mapambo tu ni urembo tu msichana anavaa ile anapendeza kijana akiona sijui atamfata hahaha I: Hhahahha kwahiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kuwafanya wapendeze? R2: Ndiyo I: Na kuvutia kwenye jamii R2: Ndiyo I: Sawasawa bado zinatumika hivi sasa? R1: Mpaka leo zinatumika I: Wanaotengeza hizi ni akina nani? R1: Ni akina mama ni mafundi tena sasa hivi ndiyo wameongeza kuboresha wanatengeneza vizuri zaidi siyo kama huko nyuma saa hivi wakitengeneza wanatengeneza kitu kizuri sana na bora I: Wakina mama kuanzia umri gani ndiyo wanaanza kutengeneza hizi? R1: Yani kuanzia miaka 20 yani hii haina kiwango ni ile ufundi tu wa kujua hata akijua na miaka 15 basi anatengeneza unaweza ukakuta mkubwa lakini hajui kutengeneza ni ule ufundi tu umri wowote unaweza ukatengeneza I: Na hizi zilikuwa zikitengenezwa kwa kutumia nini? R2: Ngozi I: Ngozi? R2: Eeeh hii ni ngozi hii sasa hivi hapa siunaona ni ngozi imegeuzwa huku juu ndiyo inayotumika I: Alafu hii ni shanga? R2: Ni shanga hizo I: Alivochanganya changanya hizo rangi ilikuwa kuna maana yoyote? R1: Yeye sianatengeneza mapambo shanga inawekwa sehemu yake hii sehemu yake na hii pia sehemu yake I: Kwahiyo ilikuwa yakuifanya ipendeze zaidi? R1: Ipendeze zaidi kama hii sahivi siunaona hii I: Ndiyo R2: Hiyo bado ina urembo hivyo hivo I: Na ngozi ni ngozi ya aina gani? R1: Ni ng’ombe I: Emutha emborosi? R1: Eeeeh ushanga wa kiunoni I: Lakini sasa mke wangu kashatoka kwenye huuu umri hahhhaha R1: Hahhahhah ukitaka hii sianavaa kwa ndani wewe unakwenda kumshika shika mke wako hahaha I: Sawasawa na hizi sasa mtu akitaka kununua atazinunua kwa shilingi ngapi? R1: Hii sasa hivi engimeta inauzwa kuanzia elfu sabini ukikuta ambayo imeshonwa eeh ila fundi yupo hapa kwetu ukimwambia mama nataka kitu kama hiki unishonee ni elfu sabini kama ni hela kama ni mbuzi mbarika inayofikia makamu lakini kama ni hela ni elfu sabini sasa hivi ndiyo inauzwa hivyo I: Kwahiyo sasa watoto wakiwa kwenye umri wa wasichana wanaowanunulia hizi ni akina nani kwenye jamii? R2: Mzazi wake I: Wa kike au wa kiume? R2: Wa kike haswa mama yake au au mtoto anaweza kwenda kwa baba yake kwamba baba hebu ninunulie basi mama yake atakwenda kumtengenezea kwasababu wanaume hawajui kutengeneza na kama mke hajui inabidi umuite anaye jua ili amutengenezee vizuri akishamaliza msichana wako anaenda kuvaa sasa I: Hela nyingi sana elfu sabini? R1: Eeeh hii elfu sabini I: Na hii emutha emborosi shilingi ngapi? R1: Hii ushonaji wake siyo wa muda mrefu kama hii hii inachukua siku tano tu anakuwa kashamaliza I: Siku tano inakuwa imeisha? R1: Hata wiki imeisha lakini hii mpaka miezi miwili yote hiyo anaitumia katika kutengeneza tu hiyo I: Ndiyo maana inauzwa bei nyingi sana? R2: Ndiyo maana unaweza ukaweka hii ukishamaliza mwenyewe akasema ibadilishwe awekewe anaoupenda ndiyo maana inakuwa ngumu kidogo I: Na hii naona ni shanga na hii inatengenezwa na ngozi pia emutha? R2: Kuna nyingine inatengenezwa na ngozi kuna nyingine inasukwa sukwa tu na kamba huoni sasa hivi kama hii siyo ngozi imesukwa tu eeh I: Ni kamba gani wanatumia kusuka? R1: Manila fulani unanunua dukani nyembamba eeh I: Lakini hii niya miaka ya 1905 kamba zilikuwa zinapatikana? R1: Wanajua bado kuna kamba au labda ngozi I: Hebu iangalie mzee [anonymous] vizuri hizo kamba zinaweza kuwa kamba za nini kama unaweza kuzitambua? R1: Si kuna hii mkonge wananyofoa kwanza wanatoa ganda yake ya nje alafu nyuzi zake ndiyo wanatengenezea hii wanashonea

chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 01
mwandishi: I: Mohamed Seif, R1, R2: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Mnazi
Scientific use:
Wakati
2023-09-28
Maelezo
I: Sawa nina picha nyingine hapa ambayo imesajiliwa kwa namba 2018_18542_1 hebu ishikeni hiyo hiyo ni nini? R1: Hii ni Engimeita I: Hiyo ni Engimeta Emboross? R1: Eeeeh Engimeita Emboross ya msichana ya kufungia nguo I: Na hiyo nyingine? R1: Inaitwa Surutiai I: Kwahiyo hii ni kwa wale wasichana ambao bado hawajaolewa? R1: Eeeeeeh I: Akishaolewa anaiacha R1: Eeeeh anaitoa hii niya wa mama I: Surutiai? R1: Eeeh yani anazunguka hivi akifika hapa anashikanishwa kwa hapa anafanya hivi huoni kwa hapa imeachana I: Wakina mama kuanzia umri gani? R1: Kuanzia mtoto alivoolewa kama miaka 20 ndiyo anavalishwa mpaka anakuwa mzee anakuwa ameivaa tu I: Mama [anonymous] unayo hii? R2: Eeeh lakini sasa hivi imechakaa nimeiacha kwasababu sasa hivi haitumiki katika jamii yetu tena I: Kwahiyo inavaliwa shingoni yenyewe? R1: Eeeeh I: Hiyo surutiai inatengenezwa kwa kutumia nini? R1: Yani hiyo wanatengenezewa mwanamke ambaye anaolewa ambaye ashakuwa mama akishaolewa bwana wake ndiyo anamnunulia I: Na hiyo inatengenezwa kwa ngozi pia? R1: Eeeeh ni ngozi ya ng’ombe kama hizi sababu hujuitoi toi unavaa tu I: Na hiyo mtu akitaka kutengenezewa anatengenezewa kwa shilingi ngapi? R1: Hizi wanashona kwa elfu themanini na tano I: Na umuhimiu wake ilikuwa ni huu tu urembo au kulikuwa kuna maana nyingine mama [anonymous] hebu tuambie R1: Hii ni urembo tu ili ajulikane kwamba ameshaolewa I: Kwahiyo ilikuwa ni utambulisho kwamba huyu kaolewa? R1: Eeeeeh I: Kwahiyo mtu akiona hiyo anajua huyu ameshaolewa? R1: Eeeeeh

chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 03
mwandishi: I: Mohamed Seif, R1, R2: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Mnazi
Scientific use:
Wakati
2023-09-29
Maelezo
I: Nina picha nyingine hapa imesajiliwa kwa namba 2018_18542_1 hebu iangalie bibi [anonymous] hiyo inaitwaje? R2: Engimeta imeshona na ngozi ya ng’ombe kamba yake hii ya kufungia mana [anonymous] anafunga na kamba ya ng’ombe sasa hivi unachukua hii I: Na hiyo wanavaa wanawake? R2: Ni wasichana tu I: Wa kuanzia miaka mingapi? R2: Kuanzia hawa kwenda juu I: Akiolewa haivai tena hiyo R2: Havai akifika tu kwa bwana anaitoa anampa mtoto wa boma hiyo anaendelea kuvaa yeye mtoto I: Kwahiyo kazi yake kubwa hasa katika mila na desturi za kimasai ni ipi kwa vijana wa kike ambao hawajaolewa? R2: Hajaolewa ndiyo hii na hii niya shingoni I: Ina umuhimu gani kwa vijana wa kike ambao hawajaolewa? R2: Ni kama urembo akitaka kwenda kijijini au unaenda sikukuu pale Kisima anavaa hii anaenda nayo I: Emustai Orubusi niya shingoni? R2: Eeeeh alafu hii Engimeta I: Emustani Engimeta? R2: Eeeeh Orubusi niya kuvaa tu shingoni I: Na Emboross inatofautigani na hiyo Engimeta? R2: Hii anafungia nje kama hii ile nyingine ile anaweka kwa ndani I: Hiyo ndiyo inaitwa Emboross? R2: Eeeeh I: Kwahiyo Emboross ni ndani? R2: Eeeeeh I: Engimeta ni nje ya nguo R2: Eeeeh I: Kwahiyo ile ya ndani anavaa ndani kabisa kwenye mwili R2: Eeeh kwenye mwili na hii anavaa shingoni tu I: Sawa asante R2: Hii imesukwa tu na manila I: Na huu mshono wa Engimeta unaitwaje? R2: Huu unaitwa Engimeta Orobela I: Na hii ya shingoni mshono wake unaitwaje? R2: Unaitwa Naigenda I: Bibi [anonymous] nakumbuka ulisema kwamba hii wanavaa ambao hawajaenda tohara hebu tuelezee? R2: Ni ambao hawajaolewa I: Aha ni ambao hawajaolewa? R2: Eeeh hii kama mtoto ameolewa anaacha kwa mama akishaolewa hiyo anakuwa haivai tena anaacha I: Anamwachia mdogo wake? R2: Eeeeh anafungia mkanda wa ngozi ambao hauna ushanga I: Aha akishaolewa anafunga mkanda ambao hauna ushanga? R2: Eeeeh anaenda kwa bwana maana ashaolewa I: Kwahiyo hii pia ni kiashiria kwamba huyu binti hajaolewa bado mama [anonymous] hebu tuambie hapo? R2: Eeeeh I: Hahhahah R2: Akiona tu ipo hii anajua bado huyu hajaolewa kwahiyo ni kama kitambulisho kwenye jamii ya kimasai I: Sawasawa basi mimi nataka niwashukuru kwa muda wenu na maelezo mazuri mliyonipatia asanteni sana na wakati mwingine pia msichoke kuniona nimerudi hapa naombeni mnipokee hahahha R1 & R2: Tunakukaribisha kwa mikono miwili I: Asante sana R (WOTE): Tunashukuru baba I: Asanteni

chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 05
mwandishi: I: Mohamed Seif, R1-3: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Mnazi
Scientific use:
Wakati
2023-10-03
Maelezo
I: Sawa tumalize na picha ya mwisho ambayo imesajiliwa kwa namba 2018-18542_1 namba moja karibu R1: Asante hii tunaita engimeta I: Engimeta? R1: Eeeeh engimeta ni wasichana tu ndiyo wanafunga I: Ndiyo wanafunga? R1: Eeeh kabila la kimasai siyo sasa hivi tumekuwa mchanganyiko sasa hivi ni wasichana walikuwa wanavaa hii I: Walioolewa au ambao hawajaolewa? R1: Hawajaolewa na hawajatahiriwa I: Hawajaolewa au hawajatahiriwa? R1: Eeeh msichana akishatahiriwa anaacha hiyo kitu anamuachia mdogo wake hata funga tena maana ameshatahiriwa nina maana kusema siyo sasa hivi maana tumekuwa changanyikeni sasa hivi maana sasa hivi mtu yoyote anaweza akafunga hii lakini kwa mila ya kimasai ni msichana ambaye hajatahiriwa ndiyo alikuwa anatakiwa afunge hii na siyo mtu mwingine yoyote alikuwa anaruhusiwa kuivaa I: Na anaifunga nje ya nguo au ndani kwenye mwili? R1: Nje I: Nje ya nguo? R1: Eeeh zamani kama nilivokuambia tulikuwa tunavaa ngozi msichana zamani maana walikuwa wanawaacha wasichana hadi wanakuwa wakubwa msichana anaweza akafika miaka 20 hajatahiriwa anaingizwa jando kama ni msichana alikuwa anafungia ile ngozi kwa juu siyo kwa ndani unafunga unakunja ngozi yako unafungia hapa unatembea kwahiyo hata ukiwa unatembea inaonekana I: Na ilikuwa na maana gani kuvalisha hivo? R1: Sana sana ni urembo kwa mila ya kimasai ilikuwa ni urembo wa wasichana walikuwa wanavaa lakini ina maana yake maana kwanini basi ukishatahiriwa unaacha haufungi tena unamwachia mdogo wako I: Kwahiyo ilikuwa ni kitambulisho kwamba huyu bado hajatahiriwa katika jamii yenu hii ya kimasai? R1: Eeeh bado hajatahiriwa I: Na hiyo walikuwa wanatumia ngozi ya mnyama gani? R1: Ng’ombe I: Na kwanini ni ngozi ya ng’ombe? R1: Ngozi ya ng’ombe ndiyo ngumu inaweza ikadumu hawapendi sana kutumia ya mbuzi maana ya mbuzi ni nyepesi kwahiyo tulikuwa tunatumia ngozi ya ng’ombe zinadumu sana kwa muda mrefu I: Na hivi sasa bado zinatengenezwa hizi? R1: Zinatengenezwa I: Na wanavaa bado? R1: Sasa hivi hawavai tena siyo sana ukawakuta sema kuna sehemu moja moja bado wao wanashikilia mila kwa sasa wasichana wanafunga hivo kama mimi ninavoangalia kwenye mitandao naona kabila la watu wa chalinze bado wanavaa ambao sisi tunaita lumbwa kwahiyo wanatumia bado kabisa I: Sawa basi mimi nishukuru kwa muda wenu na kwa hiki ambacho tumeweza kukijadili na tumetmia takribani dakika thelasini na saba toka tumeanza mazungumzo yetu lakini nishukuru kwa muda wenu na maelezo mazuri ambayo mmetupatia hakika wanasema ukitaka kujifunza ukutane na watu wazima na ndiyo maana tukaomba tukutane na watu wazima kama nyinyi kwahiyo mimi niwashukuru sana kwa muda wenu asanteni sana R1: Asante pia kama mimi nashukuru maana kumbe kuna vitu kumbe bado vipo sisi tulikuwa tumeshasahau kama hizi Ndalama tumeshasahau lakini leo umekuja umetukumbusha kwa kweli tumekumbuka mbali eeh I: Mmekumbuka asili yenu R1: Tumekumbuka asili yetu I: Sawasawa basi asanteni sana R: WOTE: Karibu sana I: Haya

chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 07
mwandishi: I: Mohamed Seif, R1-3: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Longido
Scientific use:
Wakati
2023-10-04
Maelezo
I: Kuna picha nyingine hapa ambayo imesajiliwa kwa namba 2018_18542_1 na hii pia ni engimeta hiyo hiyo? R1: Eeeh engimeta ndiyo hiyo hiyo ameshakueleza kama hii inafanana na ile ya kwanza orekelaa ni lazima I: Hiyo ndiyo orekelaa? R1: Ndiyo hiyo ndiyo orikelia hiyo ya chini hii ni engimeta na hiyo ni ngozi ambayo bado haijawekwa ushanga na hiyo orikelia ambayo orikelia ni kijana ndiyo anavaa mfano sasa hivi mimi mwenyewe nina kija wangu ambaye nimempeleka jando ambaye ametahiriwa wote amemaliza kabla kuna kijana wa kimasai anavaa nguo hii nyeusi bado hajaenda jando lakini anajiandaa kushona vitu ambavyo anastahili kama anatoa nywele kuwa morani itafaa ndiyo hiyo orikelia zamani orikelia ina muundo sana sana hakuna mama ambaye ametahiri kijana ambaye hajakaa chini kushona orikelia ndiyo kitu cha kwanza ambacho ni kitu ya kuimbia hapa morani anaenda kuimba anavaa kama hii lakini ni kubwa lakini haitawekwa vitu vingi kama hii anashona huko na ngozi sasa hivi kwasababu ni muundo mwingine wa ushonaji umekuja inaweza kusukwa akaenda kushona kama muundo wa sasa hivi maana ushonaji wa sasa hivi hauna ngozi ndani anashona kisasa ya sasa hivi ambayo anasuka kitu ambacho kinaitwa olicheka kama ambayo mama huyu anavaa hii ndiyo olicheka unaweza kushona pembeni anabandika hapa kwenye ngozi mwenyewe anavaa hivyohivyo lakini hii ya kijana na hii niya msichana ndiyo tofauti yake hiyo I: Kwahiyo orikelia hii niya wavulana? R1: Wavulana ambao kama wanatahiriwa mama yake anakaa anajiandaa anashona anaweka chini anashona kitu kingine kinaitwa maradipi ushanga wa kiunoni kitu kinaitwa ndalama ya mguu vitu vidogo dogo hivi maana kijana wakati anatoa nywele anakuja kupakwa udongo anaweka mkaa kidogo hapa kichwani anavaa siku hiyo hiyo anakunywa chai, anakula mchele, anavaa vitu kama hivyo kwasababu ametoka jando kwahiyo vile vitu vyote alivyotengenezewa na mama yake anavivaa I: Kwahiyo orikelia ilikuwa inavaliwa shingoni? R1: Eeeh shingoni I: Na unaweza ukajua mshono huu unaitwaje? R1: Sasa hivi huo mshono unaitwa olicheka sasa hivi muundo wa sasa hivi kwahiyo mtu ambaye anaenda kutafakari atakaa chini atashona kitu kabla hajaweka ngozi anaweza kushona hii baada ya kumaliza atapasua ngozi atakuja kubandika lakini anashona kwanza nje ya ngozi ndiyo unaitwa olicheka I: Kwahiyo hii olikelia ilikuwa na maana gani kwa kijana hasa namba moja hebu tuambie maana yake? R1: Ni kwa ajili ya kwenda kuimba I: Kwa ajili ya kuimba tu? R2: Lakini hata akitahiriwa kijana mama yake kabisa anajua ametahiriwa kijana anashona orikelia ana maana sana ya kwenda kuimba maana zamani morani anajenga kitu muhimu akitoroka hata kama baba yake anazuia amwambie nenda kachunge mbuzi anasema kha kwasababu amenipa kazi mimi sikai naenda kuimba na morani naenda kuimba sehemu fulani au naenda kunywa kitu kinaitwa ngibo kwa wasichana kwa mfano huyu kijana ana rafiki yake ambaye wanapendana anatoa maziwa ambayo mama yake aliandaa anaweka kwenye kibuyu anaenda kuimba na morani anavaa hiyo orikelia hii ni kwasababu anaenda kunywa ngibo ya rafiki yake R3: Orikelia ni kitu muhimu sana kwa kijana wa kiume ni sawa na ile engimeta kwa msichana kwamba ni kitu muhimu ambayo mama yake anatakiwa amshonee yule kijana wake anapoanza kuwa mtu mzima kwamba amemaliza jando sasa ndiyo kitu cha kwanza yani ushanga wa kwanza mama yake kumshonea ambayo ndiyo kitu chake cha kuimbia muhimu sana eeh kwa upande wa wanaume I: Na yeye anavaa kwa muda gani tumeona hii engimeta akiolewa haivai tena amekuwa mama orikelia inakuwaje? R2: Ni kitu muhimu kwamba atavaa kwa muda mrefu inavyoonekana mpaka atakapo fikia ile hatua ambayo ya kuwa mzee akishafikia hatua ya kuwa mzee havai tena anaacha anaachia mwingine mdogo aendelee kuvaa yeye sasa anakuwa ashaingia kwenye rika linguini la wazee sasa

chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 10
mwandishi: I: Mohamed Seif, R1-3: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Kimokouwa
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566 (77)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1906-05-26, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 47 (14-16)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1907-02-05, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 49 (2)jifunze zaidi

Rejeo la ndani la kitu

Mkanda wa shanga katika muundo wa zigzag

Mkanda wa shanga katika muundo wa zigzag

r 2018 / 18205
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Mkanda wa shanga

Mkanda wa shanga

r 2018 / 18398 b
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Mkanda wa shanga

Mkanda wa shanga

r 2018 / 18398 a
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Apron ya shanga

Apron ya shanga

r 2018 / 18412
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Asili ya data ya kitu
Museen Stade Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:53:42+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji