Wakati
2023-06-13
Maelezo
I: Sawasawa asante tunaenda na picha nyingine hapa ambayo imesajiliwa kwa namba 2018_18261_11 hebu angalia vizuri mzee Gorge unaweza ukatambua ni kitu gani hiko hapo kwenye picha?
R: Hiki bila shaka wakati ule hiki kilikuwa ni chombo cha mziki
I: Kinaitwaje?
R: Hiki kinaitwa marimba
I: „marimba“?
R: Eeeh
I: „marimba“ ilikuwa inatumiwa zaidi na watu watamaduni gani Zaidi hebu tuelezee vizuri mzee [Anonym]?
R: Tena „marimba“ hata ukiangalia mpaka sasa hivi kuna watu bado wanatumia kwenye mziki marimba
I: Labda tukihusianishe na kabila ni makabila gani hasa walikuwa wanatumia „marimba“ kama unayajua?
R: Sasa hivi huku wasambaa wanatumia „marimba“ lakini sasa hivi tunasikia wazaramo wana ngoma na wanatumia hizi marimba
I: „marimba“?
R: Eeeeh
I: Kitu gani kimekuwezesha kutambua hivyo ni vipande vya „marimba“?
R: Hivi vipande vya mbao vilivyo chongwa kwahiyo „marimba“ ukivipandika hivi ukaweka hizi kamba zake hizi ndiyo zinatune ule mlio wa dotilasofa…….. eeh
I: Inaleta sound?
R: Eeeeeh
I: Na kwa kabila lenu mlikuwa mna „marimba“ pia?
R: Sisi wazigua kwa kweli tulikua tunatumia vinubi na njuga
I: Aah vinubi na njuga?
R: Eeeeeh
I: Kwahiyo jina hili kwa makabila haya uliyoyataja inajulikana kwa jina hilohilo „marimba“ au kuna jina lingine?
R: Eeeh „marimba“ hata kwa Kiswahili ni marimba
I: Kwahiyo ni „marimba“ „marimba“?
R: Eeeeh marimba
I: Sawa na „marimba“ unaweza ukajua ilikuwa inasambazwa upande wa mikoa gani hasa hasa hebu tutajie?
R: Walikuwa wanacheza sanasana mikoa ya bara walikuwa wanatumia ngoma na njuga lakini „marimba“ yalikuwa ya pwani
I: Pwani?
R: Eeeh tunaona wazaramo, wasambaa, mkoa wa Tanga na wadigo hivi vitu pia wanavyo hivyo wanavitumia
I: Sawasawa kwahiyo ilikua ni kwa matumizi ya kutoa burudani tu au kulikuwa na matumizi mengine?
R: Bila shaka ilikuwa nikutoa burudani
I: Burudani hahahha kutoa sauti tofauti tofauti?
R: Eeeh
I: Na unadhani waliokuwa wanapiga „marimba“ walikuwa niwa jinsia gani hasa katika jamii iliyokuwa inatumia „marimba“?
R: Wanaume nafikiri mara nyingi ndiyo walikuwa wanapiga „marimba“ eh hata kule Lushoto walikuwa wanamwita Shauri sijui Shauri naye pia alikuwa na ule mdumange wake akarikodi mpaka redio Tanzania alikuwa anatumia „marimba“ hizi eeh kupiga ngoma ya mdumange hiyo ndiyo kazi ya marimba
I: Mdumange eeh sawasawa nakumbuka mdumange hahhahha kwahiyo wanaopiga „marimba“ ni wanaume?
R: Ndiyo
I: Wakuanzia umri gani haswa?
R: Aaah vijana
I: Vijana?
R: Eeeeh ambao wanajifunza toka wadogo wakichipukia wanakuwa bingwa wa kupiga hizi kwenye jamii
I: Kwa mawazo yako unafikiri inaweza ikafika wakati „marimba“ yakawa hayahitajiki tena kutumika katika tamaduni za watu ulio wataja?
R: Aaaaa yani zinaweza zikatumika maana yake ustaarabu bado haujaenea nchini kote kiasi cha kutumia vyombo vya technolojia ya sasa eeh sahivi ni juzi naangalia hapa kwenye TV bado kuna watu wanamfahamu mwalimu Julias Kambarage Nyerere ndiyo raisi wa Tanzania hahahhahahaha
I: Hahahhahaha ndiyo raisi kwahiyo itachukua muda?
R: Eeeh itachukua muda
I: Sawasawa na ili mtu atumie „marimba“ anahitaji kuwa na kitu gani kingine ambacho vinaendana sambamba kwamba kikiwepo hiki na kitu fulani lazima kiwepo ili aweze kutumia „marimba“ vizuri?
R: Nafikiria hapa kwa sasa hivi zamani walikuwa wanaweka humu kama nguo lakini siku hizi wanaweka kama sponji fulani eeh na hizi zinashikwa na kamba na huyu naye tune anatune zake alafu lile boksi la chini sasa linajenga na mbao pia nalo sidhani kama kuna kitu kingine kinatakiwa zaidi ya mbao, kamba
I: Na hiyo ilikuwa inapingwa peke yake au kuna nyingine inaenda sambamba na matumizi ya „marimba“?
R: Ndiyo hivo kuna vitu Fulani wanaita kuna makopo fulani wanapiga kochooo kochoo, kocho, kochoo
I: Manyanga?
R: Eeeeh manyanga hahhahhaha
I: Hhahhahhah manyanga kwahiyo ukipiga „marimba“ lazima upige na manyaga vuyote vinaenda sambamba?
R: Eeeeh huku wanaimba
I: Na ngoma?
R: Na ngoma
I: Sawasawa kwa leo zinaweza kuwa zinatengenezwa hizi kwa baadhi ya sehemu unaweza ukapata?
R: Mpaka sasa hivi vipo hata pale misitu ukienda wale wamwera wanapiga zile siwanazo pale kwa rasi
I: Sawasawa na waliokuwa wanatengeneza ni wanaume?
R: Eeeeh ndiyo wanatengeneza
I: Kwanini wanaume?
R: Unajua mila na desturi mpaka unajua kuna makabila mengine mpaka leo wanawake wanajihusisha kwenye vitu fulani fulani eeh wanaume wanavitu vyao na wanawake wana vitu vyao wanawake saa nyingine hawaruhusiwi kujiingiza kwenye vitu ambavyo vinaonekana ni vya kiume kiume
I: Sawasawa
R: Kwahiyo huu utamaduni bado upo
I: Bado upo?
R: Eeeeh
I: Sawa na unaweza kutuambia nyenzo au material zilizotumika kutengenezea „marimba“ mzee [Anonym]?
R: Hizi ni mbao na kamba na hizi kamba siyo lazima ziwe hata kuna kamba za msituni wanatengeneza ndiyo zinakuwa laini maana yake zamani mikonge ilikuwa haipo kwahiyo walikuwa wanatumia kamba zao za msituni nafikiri mpaka leo kamba za msituni bado zipo watu wakubwa wanafanya hivo vitu
I: Na ni mbao za mti gani hasa zilikuwa zikitumika zaidi?
A: Bila shaka wana mbao zao hawatumii kila mbao
I: Siyo kila mbao?
A: Eeeeh sisi kule nyumbani hivi vitu hivi kuna mti mmoja wanauita mfuleta
I: Mfuleta?
A: Eeeeh huo mfuleta ndiyo ulikuwa unatumika
I: Mti inasound tofauti
A: Eeeeeh sawa kabisa mfuleta huo unakuwa ni mwepesi kiasi kwamba
I: Na nyenzo hizi zimekuwa zikibadilika ama zimekuwa ni hizo hizo?
A: Nafikiri hazijabadilika ndiyo hizohizo za enzi ya zamani lakini ilikuwa miaka hiyo miaka 100 iliyopita kwa maana nyuingine hii picha ilipingwa miaka
chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023, Interview No. 16
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous, A: Aloyes Mkongewa
Mtu
-
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
-
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
-
unknown actor
(Mshiriki)
Mahali