Wakati
2023-10-03
Maelezo
I: Ni kweli niliishika mimi ni nzito sana sawa nina picha nyingine hapa ambayo imesajiliwa kwa namba 2018_18204_1 kuna mmoja wenu aliitambua hii ehe namba mbili hebu tuambie kwa jinsi ulivoiona ukaielewa?
R2: Unajua watu wa zamani wanakula nyama porini
I: Kwanza kabla hujaendelea hiyo kwa kimasai inaitwaje?
R2: Hii hapa inaitwa olitwala na hii hapa ni mkanda ndiyo wanaweka milima mizima zamani wanaweka kwenye milima tuseme ndiyo wameiba ng’ombe sehemu fulani wanashika hizi kamba hivi ukishika hivi watakuja watu kumuokoa wanasikia ambae yupo Luzilwa anasikia ujue ameiba ng’ombe watu wote ndiyo wanaamka lakini wale wanaoenda kukamata ng’ombe kurudisha anaweka na kengele zao mguuni na wapo na pembe nyingine basi atakuwa anasikia kama kengele fulani hivi mbali kunavitu vingine vinalia vuu, vuuu, vuuu pembe yani walikuwa wanafuraha kubwa sana hata kwenda kuua samba huko porini wanaweka hapa wanakuja hiyo ni vitu vya kimila na desturi za zamani maana hivyo vitu vipo sana katika jamii yetu hii ya kimasai vipo sana
I: Anafunga kwenye paja?
R2: Eeeh kwenye paja
I: Kwahiyo kazi yake kubwa ni kama ishara?
R2: Ni kama ishara
I: Kupeana tarifa?
R2: Eeeeh
I: Kwahiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kwenda kuua simba na kufuatilia mifugo na kazi gani nyingine ilikuwa inatumika?
R2: Hata kuiba ng’ombe
I: Waliokuwa wanaenda kuiba ndiyo wanavaa hivyo?
R2: Aaaa hao walioiba hawavai lakini tuseme mtu aliyekuja kutoka Ngorongoro kusema anakuja kuiba ng’ombe ya Longido kuja kuiba ng’ombe ya Longido kwahiyo watu waliofuata Longido ndiyo wanaitana kwa kutumia hii kengele lakini anapofuata ng’ombe akienda kumkuta ng’ombe anamkamata anaweka kengele zao mguuni watakuwa wazee wanavyokaa nyumbani atasema hawa ndiyo wameshika ng’ombe maana wanasikia kengele zao zile eeh wamerudisha ng’ombe kwenda kutafuta simba ndiyo wanawawekea kengele hawa wakina mama na wazee kwamba leo ndiyo wameua simba hawa ndiyo simu kama simu ambazo zilikuwa zinatumika kipindi hicho cha zamani
I: Kwahiyo ambao hawajaua simba walikuwa hawatakiwi?
R2: Watakuja tu kumuona lakini atakuja kimya kimya maana hana furaha maana hiyo niya furaha kabisa
R1: Sasa hii ni ishara ya furaha yani ipo mara mbili maana unajua kwenye wizi kuna kengenle mara mbili kuna ile ya mdomoni puuu kuna mlio fulani pekee wa kupiga na pia hii iko hivo hivo lakini hii inaweza ikaingia mara mbili kwa mfano kwenye hiyo furaha tuseme kama ng’ombe wakimpata wakishaua yule simba na kurudi nyumbani vijana hawajajua wanaweza wakafurahi lakini kama watu wamejua hawa furahi yani hawataweka kwenye paja maana ni kimya kimya mpaka tu maana watu wameliwa na simba ameuliwa lakini simba amemkwaruza mtu awe ana damu au amekufa au amemjeruhi tu hii haivaliwi hii tunavalisha wale watoto wadogo pale akitaka kuanza kunyanyuka yani mtoto mdogo kitu ambacho sasa zile ambazo viatu vyenu mnavyonunulia watoto wakikataa kutembea sasa wewe unakuwa unamvalisha kinavyofanya tii, tii, tii inakuwa inamsaidia mtoto kuweza kunyanyuka na kuanza kutembea tembea kuna mabobo yao yalikuwa yanafungwa yawasaidie wale watoto kutembea kwa urahisi kama watakuwa wanasua sua katika kutembea kwahiyo kihalisia tunaona ni kama mkanda tu ule wa kufungia mdomo wa kengele
I: Na ilikuwa hiyo kengele inatengenezwa kwa kutumia nini na nini namba moja hebu tuambie hapo?
R1: Kengele hii ni ngozi lakini hizi huwa wamasai wananunua tu kutoka kwenye zile makereketwa au kwenye wale watu wa machuma chuma sasa wanaweka gololi ndani ndiyo zinatoa kelele
I: Kwahiyo kwa watoto walikuwa wanavaa watoto wa kike na wakiume wote wanavaa katika jamii?
R1: Mtoto mdogo ambaye anakataa kutembea anavalishwa ili imsaidie aamke aanze kutembea inakuwa ni hivyo
I: Inaitwa olitwala ndiyo kengele hiyo?
R2: Eeeeeh
chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 06
mwandishi: I: Mohamed Seif, R1, 2: Anonymous
Mtu
-
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
-
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali