Wakati
2023-06-14
Maelezo
I: sawa, asante tumepata maelezo ya kibobo na stori nyingi ndani yake, tuna picha nyingine hapa imesajiliwa kwa namba 2018_18527_1, hebu angalia unaweza ukatambua ni kitu gani hiki
R: hiki kulikuwa na ngoma zamani zinachezwa na mabinti kama hivi, kwa kipare tunasema 'mueka', anachezwa ngoma, kwa kisambaa wana namna zao wanasema 'dawau unyago', yani anapitishwa unyago, sasa watoto wa jumbeau aliyefanya vizuri sana alikuwa anavalishwa kitu kaa hiki
I: inaitwaje hiyo
R: hii ni kofia lakini ilikuwa inaitwa 'ivungah', hicho ni kipare, 'adokwa ivungah’, yani huyo ameshinda ndio anavalishwa ambavyo wameboresha sasa hivi wanasema amevalishwa taji, kisambaa wanasema tu kofia au 'azaikwa taji', sasa hivi vinakuwa vimelala humu, basi akiletwa kule anatembea namna hii wanapiga vigelegele, hivi vigelegele wanaita 'ngagha' kwa kipare, wazaramo wanasema 'nkheghe' akipigiwa hivyo kwanza ameshinda vitu vyote
I: kwa hiyo ni makabila gani walikuwa wanatumia kofia kama hizo
R: wapare, lakini pia hata wambugu, hata wasambaa walikuwa wakitumia kama hivi wakifanya hayo matambiko, sasa hivi vilikuwa vinatengenezwa halafu vinauzwa...
I: vilikuwa vinauzwa zaidi mikoa gani
R: ni huko lushoto ninakokuambia, kule same, gonja maore kuna masoko kule, kwa mfano kuna soko linaitwa ‘kwekanga’, halafu kuna soko linaitwa ‘baga’ na ‘kwemakame’, ndio masoko ambayo yalikuwa vinauzwa vitu hivyo, na pale mazinde kuna soko lilikuwa linaitwa ‘mshangai’,
I: mzee [anonymous] hao mabinti waliokuwa wanavalishwa hiyo, walikuwa ni mabinti wa kuanzia umri gani
R: kuanzia miaka 18, 20ambao ndio hao wanachezwa hizo ngoma
I: na kuchezwa walikuwa wanachezwa baada ya kuwekwa ndani
R: ee
I: ndani walikuwa wanawekwa kwa muda gani
R: wiki au mwezi, inategemeana na nafasi ya yule mwenye mtoto
I: na taji au kofia kama hilo bado inatumika kwa sasa
R: hapana
I: kwa nini unadhani haitumiki
R: zile mila na tamaduni na wale waliokuwa wanazithamini wengi wamekufa na wengi hawakurithi
I: na ili kofia hiyo itumike kuna kitu kingine ambacho kilikuwa kinapaswa kuwa sambamba anayevaa kofia hilo labda anatakiwa awe na kitu kingine cha kuendana na hiyo kofia
R: ndio
I: ni vitu gani
R: mavazi, kunaandaliwa gauni ambalo linashonwa moja refu mpaka huku, lakini mtindo wake lilikuwa linaitwa 'mshono wa mwamvuli' yani ukitimiza hivyo anaambiwa 'ula ni mgothi', lakini ndani ya hivyo vitu ninavyokutajia vikikosekana na vipambopambo vingine havimo 'ni mgothi yani ula atekoloshe', yani hakutimiza, na wasambaa wanasema 'simtuja, ukimuona mtu wa mana mya atala ngoma a mwanae, itimize, nainosiabigo waa, osiemteme vikoja', maushanga makubwa yana punje kubwa na makoja mengine kokwa zake ni nene kama vile matunda damu, basi yale ndio yalikuwa yanatumika kwenye mila zinazoendana na hii
I: na waliokuwa wanatengeneza haya mataji kwa ajili ya mabinti walikuwa ni wa jinsia gani na kuanzia umri gani
R: ni wanaume, ila kwenye hayo ninayokuambia makoja, hayo yanatengenezwa na wanawake, kwa sababu inafikia hatua ni ya kuenda kumpima shingo wanapima wanawake wenyewe, mengine ni ya kuvaa kiunoni anaenda kupima mwanamke, lakini wale wa zamani zinaweza zikawa hamsini hapa akipiga mguu hivi zenyewe zinalia...
wote: wanacheka
I: mzee [anonymous] hebu tuambie ni vitu gani vilikuwa vinatumika kutengenezea hiyo taji
R: kunatumika manyoya ya kuku, manyoya ya ndege na hizi kamba kamba hizi kuna miti mingine ilikuwa inachunwa porini kuletwa kuja kuunganishwa...
I: ni miti gani
R: kuna mti unaitwa 'ifyofyokoo',au 'minyambo' ndio inachunwa na inasukwa sukwa, yani hiyo miti yenyewe ukiichuna ukiianika kwenye jua inakuwa na rangi yake, ukiianikia ndani inakuwa na rangi kama nyeusi na nyingine zilikuwa zinachukuliwa ule mkia wa ng'ombe yale manyoya yake yanasukwa
I: kwa hiyo kuna hizo kamba, kuna manyoya na kitu gani kingine?
R: na hizo nywele za mkia wa ng'ombe
I: na hivi vyeupe vyeupe ni nini
R: hizi ndio hizo kamba ninazokuambia, zinaanikwa zinatofautishwa zinaboreshw kwenye kuziandaa, huku ni manyoya ya kuku, ya ndege na nini ndio vitu hivi vilivyojaziwa jaziwa, lakini hizi ni kamba ambazo zimeandaliwa kwa mfumo wa aina yake...
I: naona kama kuna vitu vya duara duara
R: hivi vya duara duara hapa ndani ndio hivyo tunavyosema ‘vikoja’
I: na kofia kama hii kwa wale wanaofahamu umuhimi wake, ingeletwa katika mazingira sasa hivi ingeweza kuuzwa shilingi ngapi
R: hizi zilikuwa zina bei, kwa sasa hivi ninaweza nikakuambia elfu kumi au hata ishirini, hizi zilikuwa zina mzunguko mrefu sana
I: na ilikuwa binti asipovaa hivyo hajakamilika
R: ndio maana nikakumbia (...anaongea kilugha...) basi ni vitu kama hivyo
I: lile jukumu la kununua hivi nani
R: ni baba na ndio anayemuambia mama aende aandae hivyo anampa hela, lakini baba ndio mwenye maandalizi yote ya kuandaa, inaweza ikauzwa ng'ombe ikaenda tafuta vitu hivi na vinginevyo
I: na ilikuwa ni heshima akivaa
R: ee ni heshima, huyo mtoto hata ukienda kuposa, ukifanikiwa ukikaa na wenzako wanasema 'tha uyu ne mgothe avae aingia ao avae hekoloke' yani; huyu mwanaume naye ni mzima maana amekubalika pale', yani hapo huwezi kuenda ovyo ovyo, lakini siku hizi binti akionekana 'oyaa, vipi wewe pita naye huyo mwanangu'
wote: wanacheka
chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023, Interview No. 19
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
-
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
-
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali