Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/5

Kitambaa cha gome la mti kilichochapishwa

Sammlung Braun
r 2018 / 18379
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18379
Kichwa
Kitambaa cha gome la mti kilichochapishwa
Vipimo
Upana: 95cm, Urefu: 112cm
Nyenzo
Rindenbast,
Nguo
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_739a782f-b532-4611-b168-bd652232874e
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uainishaji
Nguo/Vitambaa  
Uzalishaji
Wakati
mpaka ca. 1920
Mtu
  • Mtu, haijulikani (Mtengenezaji)
Mahali
  • Bukoba
Acquisition:
Wakati
ca. 1904 - ca. 1920
Mtu
Mahali
  • Tansania
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
Mahali
  • Stade
Scientific use:
Wakati
2023-06-14
Maelezo
I: Sawasawa asante ngoja tuendelee na picha nyingine nina picha nyingine hapa imesajiliwa kwa namba 2018_18379_1 hebu angalia unaweza kutuambia hiki ni kitu gani? R: Hii naona ni kanga au kitenge eeh na hii kanga kama kitenge inavaliwa na wake zumbe, mke jumbe I: Mke zumbe wake wa? R: Wakubwa I: Wakubwa eeh R: Maana hapo ilikuwa ni vimarekani tu watu wote vimarekani ukifunga kimarekani basi ndiyo nguo za wakati huo I: Kimarekani ndiyo kikoje? R: Hizi ni nzuri ni paprini nzuri marekani ile ya zamani ile ni nyeupe lakini imekaa na nyuzi nene nene yani ni hafifu sasa hivi zimeboreshwa ndiyo mtu ukipatiwa kipande chako ukifunga hapo shingoni nguo kama hizi zinamtaka wake wa wakubwa kama wajumbe I: Wajumbe R: Eeeeh I: Na nguo kama hiyo kwa jumbe ilikuwa na jina maalumu au walikuwa wanaziitaje? R: Nguo za wake zumbe I: Nguo za wake zumbe? R: Eeeeh nguo za wake zumbe I: Makabila gani walikuwa wakivaa? R: Wasambaa I: Wasambaa? R: Eeeeh I: Na walikuwa wanavaa wakati gani nguo kama hizo wake zumbe? R: Walikuwa wakivaa wakiawa wanatoka kwa wake zumbe labda kuna sherehe kuna harusi kwa jumbe mkuu muende eeh wanavaa nguo zao eeh hata kesi zilikuwa zinamalizwa na majumbe na wake zumbe yani mke jumbe na yeye ni jumbe I: Ni jumbe? R: Eeeeh ukienda na wewe umevaa nguo za wake zumbe na wewe unaheshimika sana maana walikua wanavaa watu wenye uwezo I: Unakuwa unaheshimika? R: Eeeeh I: Kwahiyo kwenye kusuluhisha kesi walikuwa wanavaa hizo? R: Eeeeh I: Sawasawa na kwa sasa vazi kama hilo linaendelea kutumika? R: Sasa hivi kila mtu anavaa wake zumbe hapa hahhaha I: Sawasawa kwahiyo walikuwa wanatumia tu kuvaa kwa ajili ya shughuli maalum au zilikuwa na matumizi mengine na kusuluhishia kesi kama ulivosema? R: Ndiyo hivyo kama kusuluhishia kesi na kwenye mambo yao zamani watu wanaoza wanafanya shughuli zao kwa pamoja za raha za furaha lazima wanavaa nguo zao nzuri ee katika sherehe mbali mbali I: Sawasawa na ili avae vazi hili kwenda kwenye hizo shughuli maalum ambazo walikuwa wanafanya wake zumbe walikuwa wanavaa na nguo gani nyingine ni nguo gani nyingine zilikuwa zinaenda sambamba na vazi hili? R: Hizo zitakuwa labda nyingine atajifunika na nyingine atavaa na ndani atavaa na nguo nyingine kama kawaida I: Kama nguo gani walikuwa wakivaa kwa ndani kabla hawajajifunika hii? R: Nguo za ndani sanasana zilikuwa nguo za kifua eeh haya magauni kuja kutokea badae lakini nguo za kifua au za kiunoni ndiyo anajifunika I: Zilikuwa na majina maalum nguo hizo? R: Yani ilikua gauni, au fulana I: Ilikuwa hakuna? R: Ilikuwa ni kidogo sana mpaka sisi tunakuwa ukishafunga kanga yako humu mabega nje aaah shughuli zako zote unamaliza ee I: Sawasawa watu gani walikuwa wakitengeneza hizi walikuwa wakiwatengenezea wakezumbe ni akina nani hasa? R: Naona kutakuwa na wataalamu hivyo hivyo kwasababu kila kitu na utaalamu wake na haiwezekani wote muwe mnajua mtengeneze nguo zake zumbe hapana wako mafundi wao maalumu eeh I: Labda kwa kipindi kile cha utawala wa mkoloni unadhani zilikua zinatengenezwa maeneo yao au zilikua zinaletwa kutoka nchi nyingine? R: Walikuwa wanatengeneza wenyewe I: Na unaweza ukatuambia walikua wanatengeneza kwa kutumia vitu gani? R: Huo wakati wa wakoloni walikua wanatumia Ngozi I: Ngozi? R: Nguo zao zilikua zinatengenezwa na ngozi I: Ngozi za mnyama gani? R: Wanyama walikuwa wengi ila sasa hivi wanyama wameondoka walikuwa wengi ilikuwa mtu ukitoka wanapita hapa ukizunguka nyuma unawakuta wanyama wengi totauti na hivi sasa wanyama siyo wengi I: Na hii inaonekana imechorwachorwa imewekwa nakishi nakishi walikua wanatumia kitu gani kuchorea? R: Walikuwa wanatumia vigongo eeh yani wakiweka alama wakigonga vinatoka urembo wanaotaka I: Kwahiyo walikuwa wanatumia ngozi? R: Eeeeh I: Wake zumbe? R: Eeeeh

chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023, Interview No. 18
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Amani
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1906-06-04, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 47 (44)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1908-08-23, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 52 (56-57)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1908-07-25, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 52 (36)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1909-04-10, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 53 (43-50)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1908-08-23, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 52 (56-57)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1908-07-30, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 52 (39-40)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1909-04-10, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 53 (45)jifunze zaidi

Rejeo la ndani la kitu

Kitambaa cha gome la mti kilichochapishwa

Kitambaa cha gome la mti kilichochapishwa

r 2018 / 18380
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Kitambaa cha gome la mti kilichochapishwa

Kitambaa cha gome la mti kilichochapishwa

r 2018 / 18378
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Kitambaa cha gome kilichochapishwa

Kitambaa cha gome kilichochapishwa

r 2018 / 18364
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Kitambaa cha gome kilichochapishwa

Kitambaa cha gome kilichochapishwa

r 2018 / 18389
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Kitambaa cha gome la mti kilichochapishwa

Kitambaa cha gome la mti kilichochapishwa

r 2018 / 18391
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:52:09+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji