Wakati
1906-06-04
Maelezo
"Jumatatu ya pentkosti. 4. Mwezi wa sita 1906 [imepigwa mstari] [u. 40 . safari ya kikazi Kilwa, mchana mgeni wa Mkaguzi wa kilimo Bwana Knorre na mke wake: KB [Karl Braun] anapata habari nyingi kuhusu kilimo cha wazawa (mimea) orodha ya mimea na matumizi yake] [u. 44] Pia nikapewa vitu vya kimila, nilivyovipokea kwa furaha: 1) kutengenezwa kwa vijiti vya mtama [masahihisho] mtumbwi [?], ulitengenezwa na mvulana mdogo. 2) ala ya kupulizia kutoka milima ya Matumbi. Faneli ya sauti imetengenezwa kwa kutumia kibuyu [mchoro] 3) upinde wa Wazawa kutoka milima ya Matumbi 4) mishale 10-12 yenye sumu. 5) mikanda miwili ya shanga inayovaliwa na wasichana wadogo. [u. 45] 6) kimori kimoja cha wanawake wazawa inapendeza kiasi kimetengenezwa na shanga zenye rangi toauti. 7) mifuko miwili iliyosukwa iliyotengenezwa na mvulana kwa ajili ya tumbaku ya babake. 8) ngozi ya chui. Jioni tumekaa na wengine kwa Hauck." [Utafsiri]
chanzo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 47 (44)
mwandishi: Karl Braun
Mtu
-
Braun, Karl (* 1870 † 1935)
(Mpokeaji)
GND Explorer
-
unknown actor
(Mfadhili)
-
unknown actor
(Mfadhili)
Mahali