Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/5

Suruali nyeupe

Sammlung Braun
r 2018 / 18386
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18386
Kichwa
Suruali nyeupe
Nyenzo
Nguo
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_9a2d6d5c-32a6-49ea-b16b-27ac3405a9a5
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uainishaji
Nguo/Vitambaa  
Uzalishaji
Wakati
mpaka ca. 1908-08-23
Mtu
  • Mtu, haijulikani (Mtengenezaji)
Mahali
  • Muheza
Kununua / Uuzaji
Wakati
1908-08-23
Maelezo
"Jumapili 23. Mwezi wa nane 1908 [ime pigwa mstari] nimesafisha picha zangu – Leo nimepata sketi ya mwanamke inayoendana na suruali inayoelezwa u. 36 imetengenezwa na kitambaa cha kawaida cheupe [mchoro] shingoni mkononi na kwa chini kumewekwa kitambaa kilichokunjwakunjwa Kifuani juu chini, shingoni na mgongoni kwa juu [u. 57] kuna mapambo ya nyuzi za njano na nyeusi zilizowekwa na washonaji Waswahili kwa kutumia cherehani. [michoro makini miwili ya mapambo yakiwa na maelezo ] utepe kifuani urefu 31,5 cm, upana 5,5 cm / utepe shingoni upana 4,5 cm / mapambo ya mgongoni ni nyota ya kawaida mistari myeusi kwa nje mistari ya manjano kwa ndani. nimeilipia 1 rp. 5. Tena nikapata suruali ya mwanamke kama nilivyoionesha u 36 ila na rangi tofauti u. 36: Sikuwa na rangi stahiki rangi ya machungwa yangu ingepaswa kuwa pinki nyote nyeusi zimeshonwa kwa juu. Kitu chenyewe kimeunganishwa na mistari mingi. Nimelipa 1 rp. 25. Jioni nyumbani kwa Prof. Vosseler mkusanyiko: [u.58] Prof. Zimmermann & mke wake, Lommel, Prof Vosseler, Raab, Daktari rasmi Dr England na mimi." [Utafsiri]

1,25 Rupien

chanzo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 52 (57)
mwandishi: Karl Braun
Mtu
Mahali
  • Amani
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
Mahali
  • Stade
Scientific use:
Wakati
2023-06-12
Maelezo
I: nina picha nyingine hapa imesajiliwa kwa namba 2018_18386_001, hebu angalia ni kitu gani hiki R: hii ni suruali I: ni suruali gani R: ni suruali kama zile za kike zenye urembo humu I: inaitwaje suruali ya namna hiyo R: inaitwa pajama I: ilikuwa inavaliwa zaidi na watu gani R: sana sana wahindi I: sawa, ilikuwa inapatikana zaidi katika mikoa gani R: mkoa wa tanga ndio walikuwa wanavaa sana hizi nguo I: ni miaka gani, unaweza ukafahamu mwaka R: kuanzia mwaka 68 kuja chini mpaka sasa hivi bado wahindi wanazitumia hizi nguo I: na pajama ilikuwa inatumikaje R: pajama sana sana wahindi walikuwa wanatumia kulalia au kutembelea mle mle ndani wanawake wa kihindi I: ni wanawake wa kihindi wanavaa pajama R: ee I: ni wanawake tu R: ni wanawake tu wanaume walikuwa hawatumii nguo hizo, wanawake wa kihindi ndio walikuwa wanavaa suruali hizo

chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023, Interview No. 12
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Amani
Scientific use:
Wakati
2023-06-12
Maelezo
I: Nina picha nyingine hapa imesajiliwa kwa namba 2018_18386_001 hebu angalia unaweza ukafahamu ni kitu gani hichi? R: Hii kama suruali ina flaizi kabisa hapa kama nguo ya kulalia na ina miguu I: Mzee [anonymous] umefanya kazi dukani unaweza kuona ni nini hiyo? R: Hii kama suruali hii I: Suruali hiyo inaitwaje ina jina maalumu labda? R: Siyo suruali ya kulalia I: Suruali ya kulalia inaitwaje? R: Kwa kweli sifahamu I: Kwa siku hizo ilikua inaitwaje? R: Sijui pajama I: Pajama? R: Eeeeh nguo ya kulalia I: Ishikilie picha yako bado hatujamaliza hahhha suruali hizo aina ya pajama zilikuwa zinavaliwa na watu gani hasa? R: Sisi tulikua hatuziwezi hizi ni wale watu wenye nafasi zao I: Kama watu gani labda? R: Wanaume wa kijerumanmi wanavaa lakini sisi hatujiwezi zilikua hazijafika kwetu walikua wanavaa wenyewe hao wenye hali nzuri nzuri suruali maalum kwa ajili ya kulalia ndiyo hizi zilikuwa zinavaliwa I: Ndiyo hizo R: Eeeeh I: Na unaweza ukadhani zilikuwa zinatokea wapi nguo kama hizo? R: Mara nyingi walikua wanatoa huko kwao nje ingawa pamba walikua wanalima huku lakini zinaletwa kutoka nje kwao kwetu bado kipindi hicho I: Kwahiyo ilikua inaitwa pajama? R: Eeeeeh pajama I: Ni kilugha gani hicho? R: Hii nimeikuta lakini walikuwa wakitumia sana wafanya biashara wa kiarabu I: Wa kiarabu? R: Na ndiyo walikuwa wafanya biashara wakubwa wa nguo kama hizi walikuwa wakiuza sehemu mbalimbali I: Wa nguo kama hizo? R: Eeeeeeh walikua wanauza vitu vingi nguo nini na kuna jamaa walikuwa wanaitwa mahara walikuwa wanatembeza mitaani hata wanawakopesha watu na baadae ndiyo wanakuja kuchukua hela eeh I: Sawasawa R: Kama saivi ndiyo wamachinga I: Zamani walikuwa wanawaita? R: Mahara I: Ni waarabu hao? R: Eeeeh waarabu hao I: Ndiyo walikua wanatembea nguo kama hizo? R: Eeeeeeh I: Ni miaka gani kama unakumbuka? R: Ahaa ni siku nyingi sana I: Ni siku nyingi sana? R: Mimi kuwaona hawa niliwaona wakitembea nipo wilaya ya Handeni sehemu moja inaitwa Mgambo ndiyo walikuwa wanatembeza hizi nguo hizi hao mahara hao lakini ni miaka mingi 1956 I: Mwaka 1956? R: Eeeeeh I: Kwahiyo walikuwa wanatoka nchi gani hawa waarabu? R: Hao waarabu walikuwa humu humu nchini wanafanya biashara lakini waliona kwamba hizi nguo wakikaa pamoja hawatapata hela kwahiyo wanatembeza kwa kukopesha alafu baadae wanafata hela zao lakini walikuwa humuhumu nchini nao na biashara zao walikuwa wakifanyia humu humu I: Wao walikuwa wakizipata kutoka wapi? R: Kutoka nje pia waarabu walikuwa wengi sana I: Na wewe ushawahi kununua kama hiyo? R: Mimi wakati huo nilikuwa sijiwezi bado mdogo mwaka 1956 bado sijaweza kununua hiyo nguo I: Na watu waliokuwa wanavaa hizo ni watu wa jinsia gani hasa? R: Hizi I: Eeeh R: Hizi wanavaa sanasana wanaume lakini siyo kwa ajili kutembelea mitaani ni kwa ajili ya kulalia tu I: Ni kuanzia umri gani? R: Watu wazima makamo ya kawaida I: Miaka 50, hivi R: Eeeeh unavaa hii I: Kwa hivi sasa nguo kama hiyo pajama bado zinatumika? R: Saivi hamna mtu siana vaa bukta Lake I: Hahahhaha siku hizi watu wanatumia bukta? R: Kulikua na majina hata yale kama mabukta sasa ndiyo walikuwa wanavalia yale walikua wanaita teitei I: Tei, tei? R: Eeeh tei, tei I: Na pajama ilikuwa inatumika na kitu gani kingine alikua unavaa pajama tu basi au kuna nguo nyingine ilikua inaendana na pajama? R: Mara nyingi wanavaa hizohizo tu huku juu wanavaa vifulana vyembamba vyembamba nguo ya kulalia inakuwa hivo maana ukivaa ikitokea tatizo usiku inakusaidia ila usipovaa utachelewa kujifunga utatoka tu eeeh I: Na waliokuwa wanatengeneza ndiyo huwezi ukafahamu? R: Hawa jamaa waliotawala diyo walikuwa wanatengeneza I: Wajerumani? R: Eeeeh wajerumani nguo zote walikuwa wanatengeneza wao si huku washafungua biashara ya pamba na pamba ikitoka hapa siina safirishwa sasa zinaenda zinatengenezwa na zinarudi tena huku huku I: Kwahiyo hapa nchini kulikua hakuna mkoa unatengeneza nguo kama hizo? R: Kiwanda kulikua hakuna huku bado na viwanda walikuja kuweka wao na kwavile wao wanataka masilahi yaende kwao I: Kwahiyo ilikua inatumika pamba kutengenezea? R: Eeeh ilikua inapelekwa nje inatengenezwa haya mavazi huko alafu sasa inaletwa huku I: Sawasawa labda pajama kama hiyo kwa leo hii ukiikuta inauzwa unaweza ukainunua shilingi ngapi? R: Hii I: Eeeeeh labda kwa nakishi, nakishi iliyoko nayo R: Kwa bei wakati huo ilikua ni ndogo tu lakini ilikuwa na thamani lakini hii ya sasa unaweza ukaona kitu ni ghali kwa mfano ukichukua andazi shilingi mia kwa mwaka 1972 ni gunia zima huwezi kulila I: Hahahha kwa pesa yetu ya sasa ithaminishe R: Hii tufanye shilingi elfu 6 au 7 I: Elfu 6 au 7 R: Kwasababu thamani yake iko chini

chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023, Interview No. 13
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Amani
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1906-06-04, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 47 (44)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1908-08-23, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 52 (56-57)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1908-07-25, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 52 (36)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1909-04-10, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 53 (43-50)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1908-08-23, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 52 (56-57)jifunze zaidi

Rejeo la ndani la kitu

Vazi / sketi ya kucheza

Vazi / sketi ya kucheza

r 2018 / 18375
Rejeo la ndani la kitu
Kuhusiana na
Suruali nyeupe

Suruali nyeupe

r 2018 / 18376
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:51:59+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji