Wakati
2023-06-13
Maelezo
I: Sawasawa asante tumemaliza hizi twende kwenye picha za vitu hapa mkononi mwangu nimeshika picha ambayo imesajiliwa kwa namba 2018_18288_3 hebu angalia unaweza ukatuambia hicho ni kitu gani?
R: Hii kwa hivi vijiti vyake haieleweki sasa hii ni chuma au kitu fulani kama vile boga lakini hiki kimeonekana kama vile ni chuma ambacho kina vyumba viwili ndani ambavyo hivi naona vitakuwa vimefungwa na hii kamba au kama siyo kamba ni waya huu wa juu hiki chuma kitakua kina tundu hapa kwahiyo hivi vitakuwa vimefungwa kiasi kwamba hiki kikitingishwa hivi vitakuwa vinagonga kwenye fremu vitakuwa vinalia kama kengele
I: Kama kengele?
R: Eeeh lakini wenyewe wenyeji wanautamaduni wakuzitengeneza hizi kengele kwa ajili ya kufunga kwenye mifugo yao kama ng’ombe, mbuzi, hivi vitu vipo wanafunga kwenye shingo kwahiyo mbuzi akitembea vinalia kara, karaaa, kara kwahiyo inakuwa ni rahisi kujua mifugo yako iko sehemu gani
I: Kwa mfano kwenye lugha yako ni msambaa eeh?
R: Mimi nimzigua
I: Mzigua?
R: Eeeeeh
I: Kengele kama hizi kwa kilugha chenu kizigua mnaziitaje?
R: Tunaita mmanga
I: „mmanga”?
R: Eeeeh
I: Maana yake?
R: Yani „mmanga” ndiyo hilo jina lake maana yake kengele ya ng’ombe
I: Kengele ya ng’ombe?
R: Eeeeh
I: Ni kwenye ng’ombe tu inatumika au unaweza ukatumia kwenye matumizi mengine hebu tuambie?
R: Unaweza ukatumia hata kwenye punda wamasai wanawake kwenye punda kwenye mbuzi kwahiyo una kundi kubwa la mbuzi wewe utasikia zile kengele utajua kundi langu la mbuzi lipo upande fulani
I: Aaaah kufatilia
R: Eeeeh kufwatilia
I: Tofauti ya kabila lako na wamasai ni kabila gani lingine linatumia kengele za namna hiyo kwenye jamii?
R: Sijatafatilia kuzunguka kwa wenyeji sana lakini nimefika mimi mpaka kule kwa wamasai ngorongoro nimefika kule ngorongoro utamaduni wa hivi bado wanao na hili lazima liwe la chuma ili liwe linatoa sauti lazima liwe la chuma tumefika kule tumekutana na makundi mengi ya mifugo tukakuta kuna hizi kengele za namna hii
I: Sawasawa na unadhani inaweza ikafika wakati kifaa hiko kikawa hakina matumizi tena kwenye jamii?
R: Sasa hivi bwana nafikiria kwa technolojia iliyokuwepo kwa sasa hivi hiki nicha muda mrefu sana yani mimi huyu ng’ombe wangu anakifaa Fulani ambacho bwana mifugo anaweza kumtrace
I: Aise
R: Eeeeh kwa ile hereni yake aliyovishwa hapa ndiyo wanakifaa wanaweza wakasema huyu ng’ombe wanaweza wakafatilia direction huyu ng’ombe yuko wapi na kumpata bila shida yoyote yani
I: Yuko wapi?
R: Eeeh
I: Kwahiyo maendeleo ya kitechnolojia?
R: Yamesaidia sana hahahha
I: Hahahaha
R: Eeeh yamesaidia sana
I: Kwahiyo hata kwenye jamii zetu inaweza ikafika wakati hizi zikawa hazina tena matumizi kwa jamii?
R: Nafikiri hata sasa hivi sidhani tungekuta kule kwa wamasai ambapo technolojia kwao technolojia kama hiyo sidhani kwamba serikali inawafikishia hata kwenye matangazo ya juzi kusajili ng’ombe kulikua kunatangazwa kila siku kusajili ng’ombe kusajili mifugo kunatagazwa kila siku na serikali sajili mifugo yako ili ujulikane una mifugo mingapi na pia yani hata ikiibiwa utajua ng’ombe wanaitrace tu vizuri kupitia hiyo technolojia
I: Sawasawa na kasasa unadhani kengele za namna hii zinatengenezwa kweli au ndiyo hivo kwasababu ya technolojia?
R: Vijijini kabisa kama hivo nilivokuambia kule ngorongoro nimeenda mwaka 2019 mpaka saivi ni miaka miwili mitatu nimeshapita lakini nafikiri bado nimezikuta bado wanatumia sana kuweka kwenye mifugo yao
I: Na wanaotengengeneza hizi ni watu wa jinsia gani hasa kwa mawazo yako hebu tuelezee mzee [Anonym]?
R: Kuna wahunzi sehemu nyingi hata nyumbani kwetu wapo wahunzi ndiyo wanohusika kutengeneza
I: Wa kike au wakiume?
R: Wakiume wanatumia zile njia za asili za kuchoma hivi vitu kwa moto ili chuma kiweze kulainika
I: Kuanzia umri gani ndiyo wanatengeneza vitu kama hivyo?
R: Wanajifunza kuangalia toka wako vijana akishafikia umri wa kujitambua tu kwamba hichi kitu ninachokifanya ni kitu gani maana yake na tahadhari zake maana moto wake ni mkali sana hawezi akatumia kijana ambaye tu ni mdogo inawezekana uwe na akili zako tu nzuri ndiyo unaweza ukatumia
I: Labda tukienda kwa makabila bado wanatumia hivyo vitu pengine kama unaenda kuuza unaweza ukaiuzaje unaweza iuza shilingi ngapi?
R: Kwa sasa hivi
I: Eeeeh
R: Eee kwasasa hivi yani ukisema labda tuangalie thamani yake kwa sasa hivi kwa mfano mimi nikikuambia mfano mshahara wangu mwaka 1975
I: Tulete kwenye uhalisia wa sasa hivi hizo za zamani tuziache tuzungumzie uhalisia wa sasa hivi tuziconvert hizo fedha za zamani kuja kwenye uhalisia wa sasa hivi inaweza ikawa ni shilingi ngapi?
R: Yani tunaangalia sasa thamani ya hichi chuma
I: Ndiyo hahahhahha
R: Kwa mfano thamani ya chuma hichi kwasasa hivi
I: Ndiyo
R: Sijui kwa kweli itakuwa ni shilingi ngapi maana yake hii kwa mfano sasa hivi mtu akiwa nacho kitakuwa kama skrepa atakiuza kwa bei ya kilo shilingi kadhaa maana haijui thamani yake kabisakwamba ni chuma ndiyo ila kinatumikaje hajui na akikiokota hawezi akakifanya matumizi haya yaliyokuwa yakifanywa kwa wakati huo atakiuza kama skrepa lakini kwa bei ya hiyo thamani yake toka wakati huo mpaka sasa hivi itakuwa yani ni kubwa wakati huo ukithaminisha shilingi hiyo ya Tanzania na dola ilikuwa shilingi ngapi kwasababu dola kila siku ina thamani kwa maana hiyo ukipata shilingi ya Tanzania ya mwaka huu utaambiwa dola imepanda kiasi gani mpaka saivi
chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research, Interview No. 16
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
-
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
-
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali