Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/1

Chuma cha Kisu

Sammlung Braun
r 2018 / 18298
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18298
Kichwa
Chuma cha Kisu
Vipimo
Urefu: 33cm
Nyenzo
Chuma
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_b8ebbb5d-8cc2-4434-8cc4-8c5e6e426a0f
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uainishaji
Werkzeuge  
Uzalishaji
Wakati
mpaka ca. 1920
Mtu
  • Mtu, haijulikani (Mtengenezaji)
Mahali
  • Tansania
Acquisition:
Wakati
ca. 1904 - ca. 1920
Mtu
Mahali
  • Tansania
Malipo
Mtu
Nambari za hesabu za zamani
  • 295
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
Mahali
  • Stade
Scientific use:
Wakati
2023-06-10
Maelezo
I: nataka nikuulize maswali kidogo, hapa nimeshika picha iliyosajiliwa kwa namba 2018_18298_001, babu hebu tumambie ni kitu gani hicho R: hii ni kama nyengo lakini hii ni jamii ya panga, inatumika kama panga, huu huku ni mpini na hiki ni chuma kimechongwa sasa mpini wake umefanana na ule wa nyengo, mpini wake ukishauchonga hii inachomwa moto halafu unachomeka kule, kisha unachomoa tena ukishakuwa tayari kuna mti unatoa matone yake ni kama asali, unachomwa au ngozi inachomwa inaingizwa kule kwenye tundu sasa ukiingiza hii inashika moja kwa moja mle mwenye mpini, lakini ni panga hili I: kikwenu mnaliitaje R: panga I: ni hivyo hivyo panga R: ni panga hakuna tofauti I: wabena wanaita hivyo hivyo panga, R: ni panga tu hili I: sawa, na ni watu wa mikoa gani haswa wanatengeneza mapanga ya namna hiyo R: ni kuanzia iringa kwenda njombe, makete, hata mbea vinatumika hivi I: na ikishatengenezwa hivi inakuwa kama nyengo na inatumikaje R: kufyeka kama hivi kukata miti I: mpaka leo linatumika R: hakuna I: kwa nini R: zimepotea zamani I: kwa nini imepotea R: si ni kisasa sasa I: na ukitaka kutumia panga hilo unatakiwa uwe na kitu gani kingine kutumia pamoja nalo R: hili ni fupi, uwe na hiyo nyengo na jembe I: kwa hiyo vinatumika pamoja, na wanaotumia zaidi mapanga ya namna hiyo ni jinsia gani R: hii ni kwa wote, maana kilimo cha kutumia haya ni kwa wote ni zana za wote, sio kwamba ni wanaume tu ni wote, akienda kulima sasa atatumia nini, manake majembe kwenda dukani hayapo ni haya ya mila I: ilikuwa ni miaka gani hiyo ama unakumbuka R: ni miaka mingi I: hukumbuki ulikuwa na miaka mingapi kipindi hicho mnatumia mapanga namna hiyo R: sisi tumekuwa tunayaona I: kwa hiyo wazee walikuwa wanatumia toka zamani R: ni kutoka zamani ndio asili yao, sisi tulikuwa tunayaona lakini waliokuwa wanatengeneza walikuwa ni wazee wa zamani I: wa kama miaka mingapi hivi R: kwa kuwa ni wazee wazamani inaweza kuwa kama kwenye miaka 40 na kuendelea I: watoto walikuwa wanatumia mapanga kama haya R: atakapofanya kazi chombo kama kipo ndani ya nyumba lazima atumie, atatumia chombo gani I: kwa hiyo waliokuwa wanatengeneza ni wanaume R: ni wanaume tena wa umri sio kijana, kwa mfano kama kufua vile vyuma, huku wanakofua hakupiti wanawake I: kwa sababu gani R: si ni wazee wana miko yao ya kufua vyuma wakizingatia asilia, hata mtoto mdogo haendi huko I: ni wazee wa umri R: ni wazee wa umri kulikuwa kuna masharti sio hivi hivi , huko wanakofua vyuma hakupiti mwanamke, hakupiti mtoto mdogo awe wa kuime au wa kike ni mwiko I: na walikuwa wakipita ni kitu gani kitatokea R: sijui wenyewe ni siri yao hiyo, hawawezi wakakuambia mpaka ufikie umri wao ndio waeleze, utakapokaribishwa kule wanatengeneza ndio utakapo julishwa I: na ukiangalia hilo panga lilikuwa linatengenezwa kwa chuma na kitu gani kingne R: kitu kingine kama, ni kama sasa wanasema unachukua masufuria mabovu unakwenda kuyeyusha ndio wanatengeneza hiyo I: ulisema unachomeka kwenye mti R: ee unachonga mti, si kama vile nyengo, sasa lazima uchome uungue iingie kwenye mti I: ni mti gani ulikuwa unatumia kuchomekea panga R: kule zaidi sana ni huu ulanzi, unachonga ndio unachomeka hivi, I: kwa nini ni mti wa ulanzi R: ulikuwa unatumika na ni mti mgumu I: na panga la namna hii likiletwa leo unaweza ukalinunua kwa shilingi ngapi R: bei ndio nisiseme uongo, huwezi kujua, bei utakayoambiwa na fundi mwenyewe ndio utakayo toa

chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research, Interview No. 10
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Amani
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 46 (3)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1909-08-08, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 53 (107)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1905-10-10, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 46 (3)jifunze zaidi
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:13:44+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji