Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/1

Manyanga

Sammlung Braun
r 2018 / 18272
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18272
Kichwa
Manyanga
Vipimo
Urefu: 18cm, Upana: 21cm
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_bdf62fd5-33e8-4712-8ce5-7fef90fe2ca2
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uzalishaji
Wakati
mpaka ca. 1920
Mtu
  • Person (Mtengenezaji)
Mahali
  • Tansania
Acquisition:
Wakati
ca. 1904 - ca. 1920
Mtu
Mahali
  • Tansania
Malipo
Mtu
Nambari za hesabu za zamani
  • 275
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
Mahali
  • Stade
Scientific use:
Wakati
2023-06-09
Maelezo
I: Sawasawa haya asante hiyo tumemaliza nina picha nyingine hapa imesajiliwa kwa namba 2018_18272_001 hebu angalia unaweza ukatambua ni kitu gani hicho? R: Kikapu I: Kikapu? R: Eeeeh I: Kikapu kisambaa kinaitwaje? R: “ngahu” I: „ngahu“? R: Eeeeh hahahahhah I: Hahahahahah „ngahu“ ni watu gani wa utamaduni gani wanatumia „ngahu“? R: Watu wa Tanga I: Makabila gani unaweza ukaya taja? R: Hii kapu haina mdigo, msambaa, mbondei, mzigua I: Na unaweza kutuambia inatumikaje? R: Saa nyingine ukienda mashine unaweka mahindi yako na makopa yako unapeleka mashine unaweka kwenye kapu na safari mnaenda wanawake mnapeleka tunaita ushashi kumuangalia mzazi lazima pale kila mama anakuwa kabeba kapu yake I: Kwanini ilikuwa lazima uwe na kikapu ukienda kuangalia mzazi? R: Ndiyo utamaduni wetu tuseme eeeh I: Ni utamaduni? R: Eeeh I: Kwahiyo mtu hawezi kubeba hivi hivi bila kikapu? R: Saivi mtu na begi lake la mgongoni kaweka mfuko wake wa magufuli unga na sabuni hana habari na kikapu I: Kwa kipindi hicho ilikuwa ina hadhi gani kubeba kikapu kwenda kwa mzazi? R: Hadhi sasa ukienda pale unapokelewa kapu kama huna kapu unadharaulika sana kwahiyo lazima uwe nalo I: Kwahiyo ilikuwa unapewa hadhi kubwa ukibeba? R: Kikapu I: Na waliokuwa wanabeba Zaidi kikapu ni watu gani? R: Wasambaa I: Wa jinsia gani? R: Wabondei, wazigua, wasambaa wenyewe wa Lushoto I: Wakike au wakiume? R: Wa kike I: Kuanzia umri gani au mtu yoyote tu wa umri wowote anaweza akabeba kikapu? R: Anabeba I: Ilikuwa haijalishi umri? R: Hapana mtu ukienda safarini hivi si mgeni lazima uwe na kikapu chako tena zamani kilikuwa kinawekwa bahasha kabisa ukifika kikapu pale kinafunguliwa basi ndiyo furaha kwamba mgeni kaja I: Sawasawa na kwa mawazo yako unadhani kikapu kina nafasi kwa hali ya sasa? R: Ndiyo eeh I: Unadhani inaweza ikafika kipindi kikawa hakitumiki tena? R: Kwa hawa wenzetu wanaokuja miaka ijayo sidhani kama kitakuwa na hadhi tena I: Kwanini? R: Basi siwanaenda na wakati eeh wana vikapu vyao I: Vya aina gani? R: Manila hivi I: Aaaaaaa vya manila? R: Eeeh I: Kwahiyo hivo vinaenda vinapotea? R: Hivi vinapotea I: Na ili uweze kutumia kikapu ulikuwa unatakiwa uwe na kitu gani kingine? R: Ukiwa na kikapu ni muhimu tu ukiwa na kikapu I: Kikapu tu basi hakuna kitu ambacho lazima uwe nacho ndiyo uwe na kikapu? R: Kikapu unaweka zile zawadi zako unaziweka kwenye kikapu I: Kwahiyo kilikuwa kinatumika Zaidi unapoenda kumuona mzazi? R: Hata ukienda safarini mgeni unaenda lazima unabeba kikapu chako eeh I: Sawa sawa R: Unapoenda kumuona mgonjwa unabeba kikapu eeh umeweka vya kuweka humo na zawadi pia I: Vikapu kama hivo vinatengenezwa katika maisha yetu ya sasa hivi? R: Wanatengeneza sana wazigua I: Wazigua? R: Eeeh I: Handeni handeni huko? R: Eeeeh I: Ndiyo wanatengeneza sana R: Eeeeh I: Sawa na wanaotengeneza vikapu ni kina nani hasa ni jinsia gani na waumri gani katika jamii yenu? R: Siku hizi kwa vile wabunifu ni wengi hata wasichana mtu anasuka vikapu vyake hapo basi anakuja ananunua mtu anakwenda kuuza huko I: Kwahiyo saivi haijalishi umri? R: Hapana I: Wala jinsia? R: Hapana I: Labda miaka hiyo kikapu kilikua kinatumika kubebea vitu wakati unaenda kumuona mzazi walikuwa wakitengeneza watu wa jinsia gani kwa kipindi hicho na umri wao ulikuwa je hao waliokuwa wanatengeneza? R: Walikuwa ni wababa tu I: Kuanzia umri gani? R: Kuanzia miaka thelathini kwenda juu I: Kwenda juu? R: Eeeeh I: Unaweza ukafahamu ni nyenzo gani zinatumika kutengenezea kikapu? R: Kuna minyaa I: Minyaa ndiyo nini? R: Ule ukindu I: Ukindu? R: Eeeh kuna ule mwingine ule sijui wanaitaje I: Ukindu au minyaa? R: Ukindu sijui wanaita minyaa na kuna wengine wanasema mfuko wa mabamba I: Mfuko wa mabamba? R: Eeeeh ndiyo hiyo minyaa sijui I: Ni kitu gani kingine ni hiyo minyaa tu na ukindu basi? R: Eeeh hiyo tu I: Ndiyo hizo zilikuwa zikitumika kutengeneza kipindi hicho na sasa hivi zilikuwa zikibadilika au hazibadiliki? R: Eeeeh wanabadilisha I: Labda kwasasa? R: Vikapu unashika huku na huku vile vya ukindu labda nikuonyeshe fashion yake I: Utanionesha sawa bado ukindu unaendelea kutumika kutengenezea hivo ama? R: Ndiyo I: Hakuna material nyingine zinatumika? R: Vikapu wanatengenezea ukindu na makawa eeh I: Sawasawa R: Hiyo ipo kama ilivo I: Sawasawa nitapiga picha hizo sawa na kwa hicho jinsi unavokiona kikiletwa saivi kwenye masoko yetu ya kisasa kinaweza kikauzwa shilingi ngapi? R: Kuanzia elfu tano na kupanda juu I: Kuanzia elfu tano na kupanda juu kwasababu gani kinaweza kikauzwa elfu tano na kupanda juu? R: Saivi vina gharama yake saivi vinapatikana tuseme kwa shida

chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023, Interview No. 6
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Amani

Rejeo la ndani la kitu

Manyanga

Manyanga

r 2018 / 18279
Rejeo la ndani la kitu
Kuhusiana na
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:13:18+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji