Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/1

Ncha ya mkuki au ncha ya Lance

Sammlung Braun
r 2018 / 18307
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18307
Kichwa
Ncha ya mkuki au ncha ya Lance
Vipimo
Urefu: 29cm
Nyenzo
Chuma
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_e45c79a0-1c09-4c34-a5e3-b576994dabcb
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uainishaji
Silaha (Vita/Kijeshi)  
Uzalishaji
Wakati
mpaka ca. 1920
Mtu
  • Mtu, haijulikani (Mtengenezaji)
Mahali
  • Tansania
Acquisition:
Wakati
ca. 1904 - ca. 1920
Mtu
Mahali
  • Tansania
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
Mahali
  • Stade
Scientific use:
Wakati
2023-10-03
Maelezo
I: Nina picha nyingine hapa imesajiliwam kwa namba 2018_18307_1 namba moja karibu tukusikie na wewe huu unatofauti yoyote na uliopita? R1: Zinafanana ila hii kwasababu hii inaitwa engerembe ila hii sasa ni nyerembe nyingine lakini ni sawa tu na ile engerembe yoyote kwahiyo nyerembe tu I: Kwahiyo na hii ni kwa ajili ya vijana ambao hawajatahiriwa na wazee? R1: Eeeh vijana ambao hawajatahiriwa na wazee R3: Ila kuna makabila ambao wanatumia hii hamna cha wazee hamna cha vijana wanatumia vyote kama wasonjo ila huku kwetu kuna tofauti sana na mkuki na morani na ile appearance ya mkuki wenyewe kwamba ina mti mweusi katikati najua huyu ni senior morani yule ambae anabeba mkuki mweupe lakini huyu ni junior kwahiyo appearance ndiyo inatofautisha senior na jonior I: Hahhahaa sawasawa na mti uliokuwa unatumika kutengenezea? R3: Kuna ngoja kidogo wanakata iliokomaa kabisa I: Ngoja kidogo? R3: Eeeeeh I: Ni mti huo unaitwa ngoja kidogo? R3: Eeeeeh ambao una miba, miba upo kama huu wanaita ngoja kidogo au oiti sasa wanatafuta ile iliyonyooka na kukomaa wakikata pingili namna hii wakipasua katikati kuna ile sehemu ya ndani sasa wanachonga na hata hii migunga hii hata na yenyewe inayo wanaita nderesiri wakakata nayo wanakuta ina sehemu kama hiyo na ndiyo wanayochukua wanatumia katika kutengenezea I: Kwahiyo mgunda na oiti? R3: Eeeeeh na wengine wantumia mpingo I: Mpingo wa Lushoto Lushoto huko Tanga? R3: Hata huku kuna sehemu upo na ukipatikana unakata ni nyara ya serikali unaweza ukachukuliwa hatua

chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 08
mwandishi: I: Mohamed Seif, R1-3: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Longido
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T14:58:11+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji