Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/5

Suruali nyeupe

Sammlung Braun
r 2018 / 18376
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18376
Kichwa
Suruali nyeupe
Nyenzo
Nguo
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_067f894e-86c7-43d6-a60d-b6363eea0028
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uainishaji
Nguo/Vitambaa  
Uzalishaji
Wakati
mpaka ca. 1908-07-25
Mtu
  • Mtu, haijulikani (Mtengenezaji)
Mahali
  • Muheza
Ethnolojia
  • Swahili  
Kununua / Uuzaji
Wakati
1908-07-25
Maelezo
"Jumamosi 25. Mwezi wa saba 1908 [imepigwa mstari] kushughulikia mafaili. Nimepata suruali ya mwanamke wa Suaheli wa tabaka ya juu Nimeinunua dukani [duka] kijijini kwa 1 rp. 50. Imetengenezwa kwa kitambaa cheupe kitokacho mguu kwa chini hufunikwa na mikunjo. Juu ya kifundo cha mguu umeingizwa kwa kutumia nyusi za rangi kitambaa chenye giza zaidi. Upana wake ni kama mikono miwili. Yote ni kazi ya cherehani ya washonaji wahindi. Mara nyingi hata Wazawa hushona kutumia mashine. Hasa Muhesa vitu hivyo hutengenezwa [1] Kitamba kinatoka D.O.A.G [2]. Pia kuna suti kamili kama nilivyoona juzi kwenye ngoma ya wanawake [ngoma ya wanawake] Vitambaa vyeusi huvaliwa na wanawake wenye hedhi. –" [Utafsiri] [1] Wakoloni waliamini wazawa hawawezi kazi ya kitalamu pia wakazuia wazawa wasitumie mashine yoyote. [2] Shirika la wafanyabiashara wajerumani waliotaka kufanya biashara Afrika Mashariki

1,50 Rupien, (1,25 Rupien, betrifft r 2018 / 18386)

chanzo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 52 (36)
mwandishi: Karl Braun
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mnunuzi)
    GND Explorer
  • Mtu, haijulikani (Mchuuzi)
Mahali
  • Amani
Malipo
Wakati
kutoka ca. 1908-07-25
Maelezo
“92. Suruali ya kucheza ngoma kwa wachezaji wa kike. Nyeupe, imewekewa udarizi, mara nyingi zaidi kwa mashine. Suruali inafika hadi chini mguuni,mguu unafunikwa na mapambo yaliokunjwa yaliyowekwa juu.Suruali hizo hutengenezwa Muheza, Kwa ajili ya wacheza ngoma wa kike wanaosafiri kutoka soko moja hadi jingine. / Amani 25. mwezi wa sita 1908. / 1 Rp. 50. & 1 Rp. 25 / TB. 52, 36.57 angalia pia 97 / [mchoro]" [Utafsiri]

chanzo: Museen Stade, r 2018 / 18566
mwandishi: Karl Braun
Mtu
Nambari za hesabu za zamani
  • 092
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
Mahali
  • Stade
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1906-06-04, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 47 (44)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1908-08-23, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 52 (56-57)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1908-07-25, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 52 (36)jifunze zaidi

Rejeo la ndani la kitu

Suruali nyeupe

Suruali nyeupe

r 2018 / 18386
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Vazi / sketi ya kucheza

Vazi / sketi ya kucheza

r 2018 / 18375
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:51:51+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji