Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/6

Kofia nyeupe yenye tarizi

Sammlung Braun
r 2018 / 18373
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18373
Kichwa
Kofia nyeupe yenye tarizi
Nyenzo
Nguo
Fasihi
Braun, Karl Suaheli-Mützen, mit 12 Textfiguren nach Zeichnungen des Verfassers, Der Erdball, 1931, GVK
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_0f7dd804-e559-4b8b-b63e-bbab88acb2c7
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uainishaji
Nguo/Vitambaa  
Uzalishaji
Wakati
mpaka ca. 1909-04-10
Mtu
  • Mtu, haijulikani (Mtengenezaji)
Kununua / Uuzaji
Wakati
1909-04-10
Maelezo
"Jumamosi 10. Mwezi wa nne 1909 [imepigwa mstari] Asubuhi nimeendelea kuufanyia kazi mzigo mkubwa wa mimea kwa ajili ya Berlin. Mchana mafaili. – Najaribu kukusanya vitu vyote ambavyo Wasuaheli [sic] huvinunua kwenye maduka ya Wahindi kama mahitaji yao. Kwa lengo hilo nimewafanya akina „Boy“ waandae orodha kwanza na hapo nikakuta vitu vingine ambavyo hata sivijui. Leo nimepata :kofia ya kituruki yenye rangi nyekundu iliyopauka imetengenezwa na kitambaa gandamizo chekundu huitwa kwa kisuaheli: kofia stambuli huku juu ina mpini mdogo [u. 46] inasemekana kwa kibonei [?]: huitwa shuju [?]. Kofia ya aina hiyo hugharimu hela 50 hapa Amani. Tanga hununuliwa kwa hela 25. Pia nikanunua kofia nyeupe ya kawaida. Imetariziwa na nyuzi nyeupe aina hii huitwa kofia ya eherhani [?] [inadhaniwa r 2018 / 18373]. Maana yake kofia iliyotengenezwa kwa cherehani. Hapa moja inagharimu nusu rupie, kule Tanga kama hela 30. / kofia kama ile yenye jina hilo hilo ila imeshonewa upinde wenye mapambo ya nyuzi nyeusi hapa inagharimu hela 75 pale Tanga hela 50 Mapambo hapa [?] kwa N* [1] ni mistari inayoingiliana vimeshonwa kiholela kwa mashine [michoro mitatu yenye umakini ya mistari ya mshono] Ikiwa kofia imekeketwa huitwa kofia ya someno [?], kofia iliyoshonwa [?] kamwe si laini kofia ya futo / kofia maridadi na ya thamani huitwa kofia buibui (shajara 52, u.39) na hulipiwa Rupien kadhaa. Pia nimenunua nguo kadhaa: [u. 47] [mchoro wa rangi] Kitambi, kitambaa chenye rangi nyingi kilichofumwa. Hutengenezwa India au inawezekana Uingereza. Mistari yenye rangi nyingi hutengenezwa na mapambo ya nyuzi zenye rangi zilizofumwa. Rangi kuu ni zambarau tepe nyembamba zenye rangi ya machungwa – manjano, nyeupe rangi ya ndimu nyeupe nyekundu na nyeupe zimefumwa kwa pambo lililopo hapa kila mstari hutengenezwa kwa nyuzi mbili. [mchoro wa rangi] pambo la juu huchukua nusu ya upana wote na linajirudia upande mwingine [?]. upana wote ni 106 cm, urefu 212 cm. Bei hapa Amani ni 1 rupie. Kitambaa huvaliwa na wanauma kiunoni. Kitambi kingine upana 16 cm b 168 kina upinde mwekundu katikati kuna sehemu zilizozungushwa na nyuzi za manjano, zenyewe ziliundwa kwa nyuzi nyekundu na nyeusi [?]. Kati ya upinde mwekundu na eneo la ndani kuna / [u. 48] [mchoro wa rangi na mwandishi] mstari wa wima mweupe. Kitambaa hicho pia huvaliwa na wanaume kiunoni na moja hugharamia 1 rp. 25. / Shuka au kitambaa cha kiunoni na upinde wa kawaida mweusi na mwekundu. Urefu 172 upana 89 cm, bei hapa Amani hela 60. [mchoro mdogo wa rangi] / shuka ya kawaida zaidi linagharamia hela 50 ni kitambaa, upana 98cm na urefu 186 cm lang. Upinde ni [masahihisho] mistari mwekundu kijani na zambarau. Bei ni hela 50. [mchoro mdogo wa rangi] / Pia nimepata ubani tofauti tofauti: [...] [u. 50] [mchoro wa rangi] pana [...] [?] (shajara 52, u. 59) Kikoi kina upinde wenye rangi nyingi. Vitambaa hivi vinasemekana kuwa maridadi zaidi. upana 95 cm urefu 168 cm bila upinde wa nyuzi zinazoning‘iniya urefu wa hizo ni 10 cm." [Utafsiri] [1] The N-word (N*) is a highly racist term used to refer to Black people. The term originated in the context of "racial" theories and is closely linked to the history of slavery and colonialism. In the transcription of original sources, it has not been reproduced but instead marked as a racist, derogatory, and offensive term.

50 Heller (für Europäer), 25 Heller (für lokale Bevölkerung)

chanzo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 53 (46)
mwandishi: Karl Braun
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mnunuzi)
    GND Explorer
  • Mtu, haijulikani (Mchuuzi)
Mahali
  • Amani
Urithi
Wakati
kutoka 1934-07-10
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mkusanyaji)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mmiliki wa awali)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mmiliki wa awali)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
kutoka 1997
Mtu
  • Hansestadt Stade (Mmiliki wa awali)
  • Museum Schwedenspeicher (Mmiliki wa awali)
    GND Explorer
Mahali
  • Stade
Malipo
Wakati
kutoka ca. 1909-04-10
Maelezo
“125. Kofia nyeupe ya Boy's / Kofia nyeupa [?], Kofia ya cherehani [?] / kazi ya cherehani / Amani, duka la wahindi 10. mwezi wa nne 1909 = hela 30 / TB 53,46. / mapambo hapohapo / Kofia ya someno [?] = kofia yenye mapambo kama msumeno pembeni ([...] [?] kofia)" [Utafsiri]

chanzo: Museen Stade, r 2018 / 18566
mwandishi: Karl Braun
Mtu
Nambari za hesabu za zamani
  • 125
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
Mahali
  • Stade
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1906-06-04, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 47 (44)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1908-08-23, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 52 (56-57)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1908-07-25, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 52 (36)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1909-04-10, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 53 (43-50)jifunze zaidi

Rejeo la ndani la kitu

Kofia nyekundu

Kofia nyekundu

r 2018 / 18369
Rejeo la ndani la kitu
Kuhusiana na
Kofia nyeupe yenye muundo matundu

Kofia nyeupe yenye muundo matundu

r 2018 / 18372
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Kofia nyeupe yenye tarizi nyeusi

Kofia nyeupe yenye tarizi nyeusi

r 2018 / 18385
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana

Rejeo la ndani la kitu

Kofia (Fes) - Staatliche Museen zu Berlin

Rejeo la ndani la kitu
ist ähnliches Objekt
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:51:55+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji