Wakati
2023-06-09
Maelezo
I: Hebu tuangalie hii imesajiliwa kwa namba 2018_18396_b, hebu angalia unaweza ukafahamu hicho ni kitu gani?
R: Huu ni mkeka
I: Huo ni?
R: Mkeka
I: Angalia vizuri
R: Nilivohisi kama mkeka
I: Kama mkeka
R: Eeeeh pia niseme nimeshindwa kutambua
I: Nakusikiliza
R: Huu mimi nahisi ni mkeka lakini sasa hivi viungo ungo hivi vimeletwa na nini maana hivi huu ni mkeka huu amesuka na minyaa na rangi tofauti kaunganisha unganisha eeh
I: Ukiunganishwa ndiyo unakuwa mkeka?
R: Ni ukindu
I: Haujaunganishwa ukiwa haujaunganishwa?
R: Ni ukindu
I: Hahahahahahah huu ni?
R: Humu katikati kumbe hakujaungwa bado
I: Hakujaungwa bado
R: Basi sawa
I: Kwahiyo huo ni nini mama?
R: Ukindu
R: Ukindu
R: Eeeeh
I: Ukindu ni jina la kabila gani ukindu?
R: Ukindu kwa kisambaa tunaita misaa
I: Misaa?
R: Eeeeh
I: Maana yake nini msaa?
R: Msaa ni huu mti ambao una hivi vitu eeh
I: Ni makabila gani wanatengeneza ukindu?
R: Wasambaa, wabondei, wakwizu, watu wa bara wengi tu wanatengeneza wabena, wahehe, wanyakyusa, ni kazi zao hizo
I: Kwahiyo mikoa ambayo inapatikana sana ukindu ni mikoa gani hasa?
R: Mkoa wa tanga
I: Mkoa wa Tanga
R: Eeeeh
I: Tanga sehemu gani hasa unapata ukindu?
R: Sehemu za magunga hizo kule kwetu Lushoto ipo na humu Amani pia ipo lakini Zaidi sehemu za wagunda hapo ndiyo sana
I: Na ukindu unatumikaje?
R: Ukindu unatumika kwa mikeka, unatumika kwa vikapu, mikoba, vitu kama hivo ndiyo ukindu unatumika
I: Na hadi sasa unatumika?
R: Mpaka sasa unatumika
I: Na ukindu unaweza ukawa na matumizi tofauti na kutengenezea mikeka?
R: Tofauti yake
I: Eeeeh
R: Mikeka ni vikapu nafikiri vitu viwili
I: Mkeka na vikapu
R: Eeeeh na makofia haya
I: Kofia?
R: Eeeeeh
I: Na nikina nani hasa wanatengeneza?
R: Zaidi akina mama
I: Akina mama
R: Eeeeeh
I: Wa umri gani?
R: Wa umri wa miaka ishirini na tano, thelathini, arobaini, sitini na kuendelea watu wazima sana ni kazi zao
I: Kwanini ni kina mama nani watu wakubwa?
R: Sehemu kubwa wanatengeneza wakichoka na shamba mtu amekaa amepumzika ana kazi hii anatengeneza pia inambadilisha yani ule upweke yuko mwenyewe ana jisikia tu kufanya ile kazi anaona kama inamchangamsha eeh unachangamka hutapata uvivu wakulala lala hovyo kwahiyo inachangamsha mwili eeh
I: Kwa mawazo yako inaweza ikafika wakati kwamba ukindu ukawa hauhitajiki kutumika tena kwa watu wa makabila uliyoyataja?
R: Huu kupotea kabisa siyo rahisi japo sasa hivi imetokea vitu vya kisasa lakini huu kwasababu watu wanao vitengeneza watu tunasema ni wazee lakini wanavijana wanao waigiza wasichana kwahiyo hautapotea sana hautapotea kwa mikoa yote
I: Watu wanaendelea kutengeneza?
R: Kwasababu hivo vikapu ni endelevu na makofia vitu vyote hivo vinaendelea eeh
I: Na ili ukindu utumike uanze kuutengeneza unatakiwa uwe na kitu gani kingine?
R: Ukindu ili uutumie unapanga tatu uje uuanike kwenye jua ukauke uwe na pini au sindano ya kuchongea kuiweka sawa ndiyo unaanza kutumia sasa ukimaliza na uzi unaoshonea unaanza kuunganisha huo mkeka
I: Sawasawa na ukindu una umuhimu gani kwako au kwa watu wa utamaduni uliowataja?
R: Kutumika
I: Una umuhimu gani?
R: Huu una umuhimu kukalia, na kwenye shughuli
I: Shughuli kama zipi?
R: Shughuli za harusi, shughuli za misiba na wengine wanapamba kwenye vyumba vyao wanaweka ukutani ee ndiyo inayotumika zaidi
I: Sawasawa
R: Kwa njia nyingine kwa wasiokuwa na kubadilisha kuita mkeka kuna vitanda pia vilivokua vinatengenezwa kwa ukindu
I: Kwa ukindu
R: Eeee
I: Vitanda hivo vinaitwaje?
R: Vitanda vile vinaitwa vitanda vya kamba na kamba zake zile zilikuwa zinaitwa supatu kwa kisambaa eeeh
I: Eheee
R: Mnakwenda kutafuta supatu nitengeneze kitanda eeh ni vitanda vinavotumika sana mpaka sasa kwenye kulazia maiti vinatumika sana na hivyo vitanda vya aina hiyo
I: Kwanini wanatumia kulazia maiti sana?
R: Yani kama sasa ni utamaduni wanaona ni urahisi hata wakimuosha ni kwamba hawapati usumbufu maji kwenda kwenye mbao ni kama ni utamaduni wa hivyo vitanda yani hata visikosekane kwenye kijiji visikosekane itapatikana msiba lazima nani anacho lazima atafutwe eeh
I: Kwahiyo ni sehemu ya utamaduni?
R: Ndiyo
I: Kwahiyo inamaanisha utaendelea kutumika kwasababu bado matumizi yake yapo
R: Vitaendelea kwasababu matumizi bado hayatakoma eeh
I: Na ukindu unatengenezwa kwa vifaa gani na vifaa gani?
R: Hivi vifaa hapa ni ukindu tu unaoendelea mpaka patokee mkeka ni ukindu na kamba
I: Ukindu na kamba?
R: Kamba yenyewe yaweza kutumika ile ile ya ukindu au kamba ya mkonge
I: Mkonge?
R: Eeeeh kamba ya mkonge
I: Sawasawa na nyenzo zinazotumika kutengeneza ukindu zimekuwa zikibadilika au miaka yote ni hizohizo?
R: Aaah tuseme miaka yote haijawahi kubadilika
I: Haijawahi kubadilika?
R: Haibadiliki na kibao
I: Kibao?
R: Kibao wakati wakuunda unatumia kibao kuvingirisha hii kamba kushona mpaka ule mduara unaotegemea sasa umetosheka unatumia kisu kukata
I: Ahhaa kukata?
R: Eeeeh
I: Na ukindu unathamani gani ukikadiria kwa mfano huo ukindu unaouona kwenye picha ukiletwa sokoni unaweza ukauzwa shilingi ngapi?
R: Ukindu sasa hivi unathamani ukindu zamani kichanga kama kichanga hivi kinaweza kikauzwa mia tano lakini sasa hivi kichanga cha ukindu kinafikia shilingi elfu moja
I: Elfu moja?
R: Eehh
I: Kwahiyo hicho ambacho kimeshasukwa hivo kinaweza kikauzwa shilingi ngapi?
R: Duara moja
I: Kimesukwa kimewekewa rangi kama hivo unavoona
R: Ni shilingi elfu thelatini mpaka elfu arobaini eeh unatumika hata kutunza maharusi vinafikia hata arobaini elfu
I: Sawasawa basi asante tumepata maelezo mazuri sana kwenye ukindu hahahhaha
R: Hahahahhah umetosheka
I: Eeeeh sasa tuchukue picha yetu ya mwisho siku ya leo
R: Ndiyo
chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023, Interview No. 03
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
-
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
-
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali