Wakati
kutoka 1909-08-19
Maelezo
"Alhamisi 19. Mwezi wa nane 1909 […] Bwana Laming amenizawadia ukanda wa shingo ya mbwa wa Washambaa, wanautumia wakienda na mbwa kuwinda nguruwe Ukanda huo unabeba kengele kubwa iliyochomelewa kwa mikono huitwa „gongongo“ Hutengenezwa kwa vyuma chakavu kama vile vifaa vya kulimia, majembe au vitu vya vyuma vinavyouzwa kwenye duka la Wahindi. Hivivitu hupigwa kwa nyundo halafu kipande cha duara hutengenezwa na kupindwa katikati huwekwa risasi ya chuma. Kamba ya kumfungia mbwa kengele hutengenezwa kwa „malamba“ yaani majani makavu yanayoning‘iniya nje kwenye shina ya migomba.Pia kutoka kwa Bwana yule yule nimepata mfuko wa ugoro wa Washamba. Umetengenezwa na gozi ya swala iliyoondolewa manyoya (pala). Ngozi inachunwa inasafishwa na kujazwa majani halafu inkaushwa.Baadaye hukunjwakunjwa kwa mikono ili ilainike halafu hupakwa mafuta ya Kwenne (Telfairia pedata) kuilainisha zaidi (inaendelea Kitabu. 54) [...]" "(inaendelea kutoka kitabu 53) gunia hilo liko wazi upande moja upande wa pili kuna utepe wa ngozi ya nyati kwenye sehemu ya utepe unaoning’inya kuna kifundo kinachoweza kusukumwa kwa kutumia mzunguko wa shaba utepe huu unavutwa kufunika sehemu ya gunia iliyo wazi. Hivyo gunia linafunikwa na laweza kubebwa mabegani kutumia utepe.“ [Utafsiri]
chanzo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 53 (132)
mwandishi: Karl Braun
Mtu
-
Braun, Karl (* 1870 † 1935)
(Mpokeaji)
GND Explorer
-
unknown actor
(Mfadhili)
Mahali