Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/2

Kikapu cha kusuka

Sammlung Braun
r 2018 / 18316
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18316
Kichwa
Kikapu cha kusuka
Vipimo
Urefu: 18cm, Upana: 20cm
Nyenzo
Fiber ya mimea
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_8688f17c-9881-4db8-a8e6-18ebbbb531f4
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uainishaji
Vikapu  
Uzalishaji
Wakati
mpaka ca. 1908-10-02
Mtu
  • Person (Mtengenezaji)
Mahali
  • Tansania
Ethnolojia
  • Shambaa  
Acquisition:
Wakati
1908-10-02
Maelezo
"Ijuma 2. Mwezi wa kumi 1908 [imepigwa mstari] nimeshughulikia mafaili na kusoma vitabu vipya. Jioni nilitaka kufanya kazi lakini nikaitwa barazani kwa Manneschmidt mashine ya kuchezesha musiki ya Bwana Raab ilicheza na watu wengi sana wamekusanyika. – nilimruhusu Walimu na Dandi alifanya tena kwangu [?]. – Nimepokea vitu vya mila: Kigoda cha Wakamba, [u. 74] kimechongwa kutoka ubao mmoja mwekundu kina miguu 3 [orodha. na Karl Braun 99]. Pia kikapu kidogo kilichosukwa na kisichoruhusu maji kupenya cha Washambala. Kwenye lugha ya watu hao huitwa Tanguhu na hutengenezwa na Ukundu [?] Phoenix reclinata Iaeg. [?] [orodha.na. Karl Braun 100]. Kwa kigoda na kikapu nikalipa Rp 1. Kwenye ukusanyaji wangu kuna kikapu kinachofanana kimesukwa na hakiruhusu maji kupenya kinatoka kwa WaBurundi. Kimesukwa na pambo la kawaida jeusi [orodha. na. Karl Braun 100 [sic]]. [michoro miwili na miandiko] kikapu cha Washambaa / kikapu cha Barundi [masahihisho]. Kikapu cha Barundi [masahihisho ] nikapata kutoka kwa Bwana Didtfurth kule Kenge (v. u. 14) Pia nina kikapu kizuri cha Washamba wanamobebea kuku inafunikwa kwa wavu juu [mchoro] [orodha. na. Karl Braun 101]." [Utafsiri]

chanzo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 52 (74)
mwandishi: Karl Braun
Mtu
  • Mtu, haijulikani (Mfadhili)
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mpokeaji)
    GND Explorer
Mahali
  • Amani
Malipo
Wakati
kutoka 1908-10-02
Maelezo
"101. Tundu, kikapu cha kuku, sehemu ya juu inayozibika kwa wavu wa kamba, kwa ajili ya kuku. Shambala / Amani 2 Okt. 1908 / TB 52.74. / [mchoro]" [Utafsiri]

chanzo: Museen Stade, r 2018 / 18566
mwandishi: Karl Braun
Mtu
Nambari za hesabu za zamani
  • 101
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
Mahali
  • Stade
Scientific use:
Wakati
2023-06-09
Maelezo
I: Haya, hii ya mwisho ukishindwa hii basi tutakuwa tumeishia hapa, haya hii ni picha imesajiliwa kwa namba 2018_18316_001, hebu angalia unaweza ukafahamu hicho ni kitu gani? R: Hiki ni kikapu kilichotengenezwa na matete I: Kikapu kilichotengenezwa na matete? R: Eeeeh I: Kikabila inaitwaje kikishakuwa kimetengenezwa hivo? R: Kitezu I: Kitezu? R: Eeeeh kitezu I: Maana yake ni nini kitezu? R: Kitezu hiki maana yake ni kikapu bali hiki kimeenda mfano wa mkoba eeh I: Na kikapu hiko kimekuwa kikitengenezwa na watu wa utamaduni gani hasa? R: Hiki haswa na wabena I: Wabena R: Wahehe watu wengi wa bara wabena na wahehe I: Wabena na wahehe R: Ndiyo I: Na kilikuwa kikitumikaje? R: Hiki kilikua kinatumika sana kuhifadhia unga ndani ya nyumba eeh kama tunavohifadhi kwenye ndoo sasa hivi hiki sanasana kilikuwa cha unga ndani I: Cha kuhifadhia unga R: Lakini sasa naona hiki kina uwazi uwazi I: Kina matundu makubwa kidogo hiki R: Kina matundu makubwa kidogo hata kwendea shamba kuvuna mboga, mahindi vinatumika hivi I: Kwahiyo kina matumizi mengi? R: Eeeh I: Na watu gani walikuwa wakitumia sana? R: Yani hiki watu wa bara kuanzia wabena, wahehe haya makabila gani haya wangoni I: Wabena, wahehe na wangoni R: Na hawa wafipa hivi vitu ndiyo vinatumika sana eeh kwa wasambaa hivi hapana siyo sana hamna labda anunue tu lakini siyo asili yetu hii I; Sawasawa hapa kuna wabena kwani? R: Eeeeh wengi tu I: Itabidi tupate mbena mmoja R: Hapa wapo bali zaidi ya hapa ni kwenye kuhifadhia unga na kwendea kenye mboga maana tuliletewa hata sisi tuliolewa na wabena tuliletewa zawadi eeh I: Na ndiyo mlikua mnatumia kufanyia hivo? R: Eeeeh tulikuwa tunatumia wanakuletea kikubwa cha kuhifadhia ndani na kidogo cha kuchotea unga ndani kuja jikoni eeh I: Na wewe ulishawahi kutumia? R: Eeeeh nimeshawahi kutumia I: Wewe ulitumia kwa muda gani? R: Ah vinadumu hivi eeh hata vingine vidogo wametuletea tunawekea sadaka kanisani eeh I: Kwa matumizi ya sasa? R: Eeeeh I: Lakini kipindi hicho ilikua ni kuhifadhia unga na kwenda kuvunia? R: Eeeeh kwenda kuvunia yani hiki kikubwa chakuvunia na hiki kingine cha matumizi ya ndani hivi vidogo tuliletewa hata sisi na wamama wakibala walituletea viko kanisani hapo tulikua twawekea sadaka kwahiyo sasa hivi sasa tumeacha tu kwa ajili kuna mifumo ya kisasa wametengeneza vya mbao eeh lakini hivi vitu zaidi ni vya kibala I: Vya kibala? R: Eeeeh I: Kati ya wanaume na wanawake akina nani wanatumia zaidi? R: Ni wanawake I: Wanawake? R: Eeeeh I: Umesema kinaitwaje? R: Kitezu I: Kitezu: R: Eeeeh ni mkoba wa kikapu yani kwa mbena atajua jina lake sasa zaidi eeh I: Sawasawa na kwa mawazo yako inaweza ikafika wakati kikawa hakihitajiki tena? R: Hivi havitapotea I: Kwasababu gani? R: Kwa kupotea vinaweza vikapotea kwa hii mikoa ambayo sisi tunaletewa lakini kwa kule bara havitapotea sana kwasababu hivi vifaa wanavyo wenyewe hii minyaa wanayo, na matete haya wanayo na ufundi wanao eeh I: Na ili kutumia hicho kitezu unatakiwa uwe na kitu gani kingine? R: Tena hapa ni kutumia tu hii peke yake maana hapa unavitembeza tu vyenyewe na kidole hiki eeh bali kwa ila kutengeneza lazima pawe na kisu na huku juu kutakuwa na sindano ya kukazia lakini huku ni kamba zenyewe ndiyo zinazozunguka mpaka zikafanya hivi I: Sawasawa na waliokuwa wanatumia zaidi ni wanawake au hata wanaume pia? R: Hata wanaume kama kipo ndani mwanaume ila kwa utengenezaji ni wanawake I: Watengenezaji ni wanawake? R: Eeeeh I: Na wanawake wa kuanzia umri gani wanatengeneza zaidi? R: Miaka kumi na tano, kumi na sita na kuendelea mpaka miaka hamsini sitini mpaka sabini kama mimi I: Kwanini wanawake? R: Kwasababu kinatumika sana ni kazi za jikoni eeh I: Kazi za jikoni? R: Ndiyo I: Sawasawa na umesema vinatumia matete, kitu gani kingine kimetumika kutengenezea hicho kitezu? R: Hapa kukazia huku juu imetumika sindano hizi kubwa za kushonea magunia I: Sindano R: Na uzi I: Uzi? R: Eeeeh I: Sawasawa labda vitezu vya sasa hivi ambavyo mnaletewa ambavyo vinatumika hadi makanisani utofauti na material yaliyotumika kutengenezea au nyenzo? R: Havina tofauti bali vya zamani ni imara Zaidi I: Kwanini vya zamani ni imara Zaidi? R: Wale watengenezaji zamani akitengeneza kitu sianatengeneza ngumu lakini sasa hivi anatengeneza kitu kiishe upesi ni biashara ili aendelee kutengeneza kwahiyo wako kibiashara zaidi I: Sawasawa hasa ukiangalia kitezu hicho cha miaka hiyo ya elfu moja mia tisa miaka mia iliyopita kikiletwa katika masoko yetu ya sasa kinaweza kikauzwa shilingi ngapi? R: Hiki sasa hivi kinaweza kikauzwa elfu kumi mpaka kumi na tano eeh I: Aha R: Kumi mpaka kumi na tano I: Kumi mpaka kumi na tano? R: Eeeeeh I: Sawa mimi nishukuru kwa ushiriki wako wa siku ya leo umetusaidia taarifa nyingi sana kwahiyo tushukuru sana kukubali ushiriki wako asante sana R: Asanteni na nyinyi I: Haya asante

chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023, Interview No. 03
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Amani
Scientific use:
Wakati
2023-06-10
Maelezo
I: Hapa mkononi mwangu nina picha imesajiliwa kwa namba 2018_18316_001 hebu angalia picha hii unaweza kutambua ni kitu gani hicho? R: Hiki ni kikapu kilichoshonwa na baadhi ya mimea cha kitamaduni I: Kikapu? R: Eeeh kikapu I: Jina lake ni kikapu tu R: Unaweza kusema mfuko au kikapu I: Mfuko au kikapu? R: Eeeeh I: Unaweza ukauhusianisha na utamaduni wowote wa kabila Fulani labda? R: Eeeeh ndiyo I: Ehee mhhh R: Kwenye utamaduni wa kipare walikuwa wanashona vitu kama hivo kutumia mimea ambayo inaota kwenye vitivo au niseme kando kando ya mito I: Inaitwaje mimea hiyo? R: Kwa jina la kipare? I: Eeeeh hilohilo jina la kipare R: Majia I: Majia? R: Eeeeh I: Na hicho kikapu kikishatengenezwa hivyo kinaitwaje kwa kipare? R: Kwa kiapare mbinda I: Mbinda? R: Eeeeh I: Hhahahaha mbinda maana yake ni nini? R: Ni mfuko wakuekea either vyakula ukienda shambani umechuma maharage umeweka au umechuma mboga unaweka wakati Fulani walikuwa wanashona vidogo kwa kuchumia kahawa shambani I: Kuchumia kahawa? R: Unakivaa alafu unaweka kahawa I: Kahawa? R: Eeeeh I: Nani wapare peke yake walikuwa wanafahamu au kuna kabila lingine walikuwa wakitumia vitu kama hivo? R: Eeeh kwa makabila mengine siwezi nikafahamu eeh lakini nadhani kwa wachaga na wapare hawako tofauti sana eeh nadhani hata wao walikuwa wanatumia vitu kama hivi eeeh I: Sawasawa na mikoa mabayo kinaweza kikapatikana Zaidi ni wapi ni mikoa gani hasa naweza kuitaja? R: Mikoa ya Iringa, niliona kule wanatumia vitu vya kushona wanaita matete I: Matete? R: Eeeh matete wanashona vitu kama hivi vikapu na vyombo vidogo vya kuwekea either maua na vitu mbalimbali I: Na kwa Iringa wanitaje? R: Ndiyo hiyo wanaita matete hii mimea hii I: Inayotumika kutengenezea inaitwa matete? R: Ndiyo I: Kikishatengenezwa kikawa kama hicho kinaitwaje? R: Kwa kweli siwezi jua I: Sawasawa na umesema walikuwa wanatumia wapare kwenda kuwekea vitu ni vitu gani hasa walikuwa wanaweka huku? R: Hapa tulikuwa tunaweka vitu vya aina nyingi unaweza ukaweka kahawa, unaweza ukaweka maharage yani vitu vya aina nyingi ambavyo vyote unaweza kuweka na visimwagike eeh kwenye mbinda I: Na watu wa umri gani na jinsia gani walikuwa wakitumia kifaa hicho? R: Kifaa hiki ni wazee, ni kwamba ni kifaa ambacho kinatumika ndani ya nyumba kwahiyo umri wote wanatumia I: Jinsia zote? R: Eeeeeh jinsia zote ni watoto, haya watavitumia kwa ajili ya kwenda kuchumia kahawa au kwenda kuchumia mboga I: Kilikuwa kina umuhimu gani Kwa watu wa kabila hilo la kipare? R: Kilikuwa na umuhimu kwasababu ndiyo chombo pekee ambacho mtu unaweza kukitumia katika kazi za shamba ukawekea vifaa vyako I: Kifaa hicho bado kinatengenezwa hivi sasa? R: Bado wanatengeneza I: Na wanatumia? R: Na wanatumia I: Kwa mfano ukienda upareni maeneo gani unaweza ukakipata? R: Kule upareni kule sehemu za Vudee, vudee nyika, vudee milimani, unaweza ukapata na wapo watu wanatengeneza I: Na wanaotengeneza ni watu wa jinsia gani? R: Wanaotengeneza hivi vifaa saivi ni watu wenye umri kuanzia miaka sabini na kuendelea I: Wa kike au wakiume R: Wakike hadi wakiume wanaweza kutengeneza I: Kwahiyo hiki nilijua kwamba kinatengenezwa na wanawake tu R: Wanaume na wanawake lakini Zaidi Zaidi ni wanawake I: Wanawake? R: Eeeeh wanawake ndiyo wanaotengeneza hivi kwa ajili ya kwenda kuuza kwa wasioweza kutengeneza I:Ulisema mimea inayotumika upareni ulisema inaitwaje? R: Majia I: Majia tofauti na majia ni kitu gani kingine kinatumika kutengeneza kifaa hicho? R: Aaaa kwa kweli hapana I: Ni majia tu peke yake? R: Eeeeh I: Kwahiyo hizo nyenzo zinazotumika kutengeneza kifaa hicho hakija badilika wanatumia hivyo hivyo? R: Wanatumia hivyo hivyo isipokuwa sasa hivi siyo wengi I: Ndiyo R: Ni wachache sana I: Wachache sana kwanini saivi wamekuwa wachache? R: Kwasababu sasa hivi wanatumia mifuko fuko hii na wakati ule walikuwa yani hicha kifaa ndiyo kilikuwa kifaa kikubwa kabisa ambacho kinatumika kwa kazi hizo I: Ukiangalia hicho kikiletwa mazingira yetu ya sasa kwenye usasa wetu kinaweza kupewa thamani gani kama kinauzwa sokoni? R: Ukweli kwa yule anayejua maana yake na umaarufu wake anaweza akakiona kina thamani kwake I: Tuchulie mfano mtu ambaye amekiona kina thamani kwake anaweza akakinunua shilingi ngapi? R: Kifaa kama hiki unaweza kuuziwa elfu tano na kuendelea I: Sawasawa asante tumemaliza hiyo tuchukue picha nyingine R: Sawa

chanzo: Amani-Stade Projct / Amani Field Research 2023, Interview No. 07
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Amani
Scientific use:
Wakati
2023-06-08
Maelezo
I: Na picha ya mwisho kwako kwa siku ya leo na picha hii imesajiliwa kwa namba 2018_18316_001 hebu angalia unaweza ukafahamu ni kitu gani hicho? R: Hiki ni jamii ya kikapu lakini kinatumika sana kwenye mikoa ya bara I: Mikoa ya bara? R: Eeeeh I: Kinaitwaje? R: Sijui wanakiitaje kwavile mama huko bara unamuona hajakusalimia kaweka unga wake humo I: Mikoa gani hiyo hasa? R: Iringa na Njombe I: Na njombe ahhh Iringa na Njombe ndiyo wanatumia kuwekea unga? R: Unga I: Ila jina lake ndiyo hulijui? R: Silijui kwa kweli I: Ni makabila gani hasa? R: Wabena, wakinga I: Wabena na wakinga? R: Eeeeh I: Iringa na njombe R: Eeeeh I: Vilikuwa vinatumika kuwekea unga tu peke yake au kilikuwa na matumizi mengine? R: Mimi Zaidi nilikuwa naona wanabebea unga I: Sawasawa na watu gani sanasana walikuwa wanatumia kubebea unga jinsia gani? R: Wanawake I: Wa umri gani? R: Watu wazima I: Kuanzia umri gani? R: Tuseme kuanzia miaka hamsini kupanda juu eeh I: Unadhani bado kinaendelea kutumika kwa kiasi kikubwa? R: Hivi wanaendelea navyo I: Asee R: Eeeh I: Sawasawa na ili utumie hiko lazima uwe na unga au unaweza ukatumia kitu kingine chochote kingine? R: Sijui hawa wenzetu wa bara lakini sanasana naona wanawekea unga Zaidi I: Sawasawa kwa mawazo yako unadhani kifaa hicho kinatengenezwa katika mikoa uliyo itaja hadi saivi? R: Eeeeh kule bado wanavitumia I: Bado wanavitumia? R: Eeeeh I: Na wanaotengeneza hivo ni jinsia gani hasa? R: Mimi sijui kule kwao I: Sawasawa kwa Tanga hakuna? R: Eeeh I; Hata hapa Amani hakuna wanaotengeneza? R: Hakuna I: Unaweza ukatambua kitu gani kimetumika kutengeneza kifaa hicho? R: Matete Fulani hivi I: Matete? R: Eeeh I: Yanaitwa matete? R: Eeeh matete Fulani hivi I: Na kitu gani kingine ukiachia matete? R: Sijui kwa kweli najionea tu vitungwa I: Hahahha vitu vya watu hivo hahhha R: Eeeeh hahahahahah mikoa ya wenzetu I: Naukikiangalia hicho kwa mazingira yetu yasasa kinaweza kikauzwa shilingi ngapi thamani yake garama ya thamani yake inaweza ikawa shilingi ngapi? R: Hiki siyo sawa na vikapu vyetu hivi vinaweza viwe juu I: Kwani vikapu vya kawaida unanunua shilingi ngapi saivi? R: Vikapu vyetu vya kawaida kuna vya elfu mbili, elfu tatu, elfu nne eeh I: Kwahiyo ukikilinganisha na vikapu vyetu vya sasa na hicho kinaweza kikawa shilingi ngapi? R: Wanaweza wakakuambia elfu sita I: Elfu sita? R: Eeeh I: Sawasawa basi asante mama kwa siku nya leo tutakuwa tumeishia hapa picha ziko nyingi ila hatuwezi tukamaliza leo R: Sawasawa hahahhaha I: Nashukuru sana kwa ushiriki wako R: Haya baba asante

chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023, Interview No. 06
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Amani
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1908-11-02, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 52 (86)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1908-10-02, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 52 (74)jifunze zaidi
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:37:47+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji