"Alhamisi 22. Mwezi wa pili 1906 imepigwa mstari] Kupitia Sembe-Muhesa [?] nimepata miiko 12 inashangaza jinsi mafundi wazalendo [fundi ]wanavyoweza kubadilisha muundo au mapambo Yote huchongwa kutoka kipande kimoja [imepigwa mstari): [mchoro na taarifa ya urefu] 48 cm / Mapambo kwenye tepe nyeusi ya kati ni maduara nyeupe na doa nyeupe kwenye eneo iliyochomwa yamewekwa kwa umakini mkubwa mpambaji lazima amepata ala ya musiki kutoka ulaya akafurahishwa na mapambo yake ala hiyo ikatumika kotekote. [mchoro] Hapa pana maduara [mchoro yenye umakini] meupe kwenye eneo nyeupe. Mistari mikubwa ni myeusi mikato ya umbo wa v ni myeupe. [u.89] [michoro kadhaa ya vitu a-g, vingine na michoro yenye umakini na miandiko:] [mchoro kijiko na mchoro yenye umakini] a /majozi ma5 duara-doa / majozi ma5 ya duara-doa / nyeupe kwenye nyeusi / upande wa pini [mchoro wenye umakini mpini wa kijiko] b / pia mpini kwa chini [mchoro wenye umakini mpini wa kijiko] / mapambo ya duara iliyobadilishwa: zote nyeupe kwenye eneo jeusi pia kuna mistari mitatu ya duara inayopakana[mchoro kijiko] d / kijiko cha pande mbili / duara nyeupe kwenye eneo jeusi/ vivyo hivyo [mchoro kijiko] upande [mchoro kijiko] e / kijiko na mpini uliopindwa / mapambo ya duara kama hapo juu [mchoro wenye umakini mpini wa kijiko] f / vivyo hivyo, ndogo zaidi eneo la mpini lililokunjwa kwa upana zaidi [mchoro wenye umakini mpini wa kijiko] g / vivyo hivyo ila sehemu iliyopindwa ina umbile tofauti [...]" [kijiko 62 ama. r 2018 / 18482 (kitu 2) sawasawa na mchoro e kwenye shajara] [tafsiri]
chanzo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 46 (98) mwandishi: Karl Braun
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).
chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.
I: Haya sawa nina picha nyingine hapa imesajiliwa kwa namba 2018_18545_001 hebu angalia unaweza ukatambua hicho ni kitu gani?
R: Mwiko wasambaa wanaita wiko
I: Wiko?
R: Eeeeh
I: Wiko kazi yake ni nini?
R: Wiko kazi yake mimi nilikua ninaona wakipika pure basi ndiyo vijiko hivyo
I: Ndiyo vijiko?
R: Eeeeh
I: Kwahiyo vilikua vinatumika kwenye pure tu peke yake au hata kwenye vitu vingine wiko ulikua unatumika?
R: Hata kwenye vitu vingine hata wakipika supu walikua wanatumia
I: Wiko?
R: Eeeeh wiko
I: Kwahiyo ilikua inatumika kama kijiko?
R: Eeeeh
I: Siyo cha kupikia?
R: Hapana
I: Aaah hicho siyo cha kupikia
R: Ndiyo
I: Ni watu wa makabila gani wametumia sana hiyo wiko?
R: Mimi nimeona Zaidi kule Lushoto kwa wasambaa na wambugu
I: Wasambaa na wambugu kwa mkoa wa Tanga?
R: Eeeeh
I: Sawasawa kwahiyo ilikua inatumika kwenye uji au kulia pure?
R: Ehh pure hata wanapenda kutumia kwenye vitu vya kunywa kunywa kwa wenzetu kule vitu kama supu supu
I: Ni jinsia gani walikua wakitumia Zaidi wiko?
R: Naona Zaidi ni wasambaa na wambugu
I: Wakike au wakiume?
R: Wakike
I: Kuanzia umri gani?
R: Hawana umri yani kama ndiyo matumizi yao
I: Sawasawa kwa mawazo yako inaweza ikafika kipindi kwanza huo wiko bado unatumika saivi au hautumiki tena?
R: Kwa kule Lushoto ndani ndani bado unatumika
I: Lakini utumiaji umepungua?
R: Umepungua saivi
I: Unadhani ni kwasababu gani utumiaji wa wiko au kijiko cha asili umepungua kwenye jamii yenu?
R: Ni kule kwenda na wakati umekuja kama wewe nitakupa wiko kweli hahahahhahaha inakuwa haiwezekani
I: Kwanini?
R: Labda upende mwenyewe na nitakueleza huu ni wiko ukitaka kuutumia unatumia
I: Kwahiyo saivi kuna kitu gani cha usasa ambacho kimeondosha matumizi ya wiko?
R: Aaah ni hivi vijiko
I: Vijiko vya chuma?
R: Eeeeh
I: Aaaah sawasawa na ili utumie wiko lazima uwe na supu au pure au kitu gani kingine ndiyo uweze kutumia wiko?
R: Matumizi niliyokuwa nayaona ni hayo tu
I: Pure zilikuwa zinawekwa kwenye kitu gani kingine ili uweze kutumia wiko?
R: Kulikuwa na bakuli ya udongo
I: Kwa kipindi hicho kipindi cha miaka ya hamsini hamsini kurudi nyuma kulikuwa na bakuli za udongo zilikuwa zinapatikana pia?
R: Eeeeh
I: Sawasawa bado vinatengenezwa kwa sasa kwa maeneo ya Lushoto?
R: Kwa makame ukienda hukosi
I: Makame?
R: Ndiyo, Makame Lushoto eeeeh! Huko hukosi
I: Lushoto huko?
R: Eeeeh
I: Sawa sawa na ni watu gani walikuwa wakitengeneza wiko kati ya wakike au wakiume?
R: Wakiume
I: Wakiume?
R: Ndiyo
I: Kwanini wakiume ndiyo walikuwa wakitengeneza wiko?
R: Sijui hahahah labda ndiyo wenyewe wataalamu
I: Wa umri gani walikuwa wakitengeneza?
R: Mimi niliwakuta tu wababa pale sokoni
I: Wakuanzia umri gani ukiwa kadiria?
R: Kuanzia miaka hamsini
I: Sawasawa na wiko unatengenezwa kwa kutumia kitu gani?
R: Mbao tu
I: Mbao?
R: Eeeeeh
I: Bakuli hilo?
R: Eeeeh bakuli la udongo wa mfinyazi nikisaga pilipili zangu naweka mwenyewe nakula hivo yani
I: Kwahiyo wiko mwenzake ndiyo huyo
R: Eeeeeh
I: Sawasawa kwahiyo inatengenezwa kwa mbao?
R: Eeeeh
I: Na ukiangalia design ilivonakishiwa wiko wa kipindi hicho ukiletwa katika mazingira yetu ya sasa unaweza ukauzwa shilingi ngapi?
R: Buku, buku jero tunanunua
I: Shilingi elfu moja, elfu moja mia tano?
R: Eeeeeh
chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023, Interview No. 06 mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T14:59:07+01:00
Maoni
Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.