Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/3

Taa ya bati

Sammlung Braun
r 2018 / 18314 b
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18314 b
Kichwa
Taa ya bati
Vipimo
Urefu: 9,5cm, Kipenyo: 4,7cm
Nyenzo
Chuma
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_9989a2bd-6693-44b1-b91f-86334255ef9c
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uainishaji
Utunzaji wa nyumba  
Uzalishaji
Wakati
mpaka ca. 1909-03-31
Mtu
  • Mtu, haijulikani (Mtengenezaji)
Mahali
  • Tansania
Ethnolojia
  • Swahili  
Kununua / Uuzaji
Wakati
1909-03-31
Maelezo
"Jumatano 31. Mwezi wa tatu 09 [imepigwa mstari] Asubuhi nimeanza kupangua badhi ya vitu vya Bwana Prof Vossler [?]. – kwenye maabara nimepanga mimea. Mchana mafaili. Nimepata taa nne ndogo zinzotumiwa na Waswahili Wahualuli [?] hutengenezwa na fundi kwa kutumia bamba jeupe. 4 hugharimu hela 36 kwenye duka la Wahindi. Mfuniko wa juu wenye tundu la utambi waweza kutolewa.Inashangaza ilivyotengenezwa imara. Kwa kazi ya mikono inachukua muda sana kugonga na kuchomelea kitu kama hicho [orodha la vitu. na. Karl Braun 122]. – Bwana Schulze & Manneschmidt walikuja kwangu kwa ajili ya chakula." [Utafsiri]

9 Heller / piece

chanzo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 53 (42)
mwandishi: Karl Braun
Mtu
Mahali
  • Amani
Malipo
Wakati
kutoka ca. 1909-03-31
Maelezo
"122. Taa za bati za Waswahili. Hutengenezwa na wafua mabati wa Kihindi kutoka kwa bati kuukuu, taa za mafuta ya taa na kadhalika. Hujazwa utambi wa pamba na mafuta ya taa / Amani, duka la Kihindi. 31 Machi 1909 / 1 pc = 9 heller / TB 53.42 / 20 heller [imeongezwa kwa herufi nyekundu] / [mchoro]" [Utafsiri]

chanzo: Museen Stade, r 2018 / 18566
mwandishi: Karl Braun
Mtu
Nambari za hesabu za zamani
  • 122
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
Mahali
  • Stade
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1909-03-31, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 53 (42)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566jifunze zaidi
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T14:59:30+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji