Wakati
2023-06-10
Maelezo
I: nataka nikuulize maswali kidogo, hapa nimeshika picha iliyosajiliwa kwa namba 2018_18298_001, babu hebu tumambie ni kitu gani hicho
R: hii ni kama nyengo lakini hii ni jamii ya panga, inatumika kama panga, huu huku ni mpini na hiki ni chuma kimechongwa sasa mpini wake umefanana na ule wa nyengo, mpini wake ukishauchonga hii inachomwa moto halafu unachomeka kule, kisha unachomoa tena ukishakuwa tayari kuna mti unatoa matone yake ni kama asali, unachomwa au ngozi inachomwa inaingizwa kule kwenye tundu sasa ukiingiza hii inashika moja kwa moja mle mwenye mpini, lakini ni panga hili
I: kikwenu mnaliitaje
R: panga
I: ni hivyo hivyo panga
R: ni panga hakuna tofauti
I: wabena wanaita hivyo hivyo panga,
R: ni panga tu hili
I: sawa, na ni watu wa mikoa gani haswa wanatengeneza mapanga ya namna hiyo
R: ni kuanzia iringa kwenda njombe, makete, hata mbea vinatumika hivi
I: na ikishatengenezwa hivi inakuwa kama nyengo na inatumikaje
R: kufyeka kama hivi kukata miti
I: mpaka leo linatumika
R: hakuna
I: kwa nini
R: zimepotea zamani
I: kwa nini imepotea
R: si ni kisasa sasa
I: na ukitaka kutumia panga hilo unatakiwa uwe na kitu gani kingine kutumia pamoja nalo
R: hili ni fupi, uwe na hiyo nyengo na jembe
I: kwa hiyo vinatumika pamoja, na wanaotumia zaidi mapanga ya namna hiyo ni jinsia gani
R: hii ni kwa wote, maana kilimo cha kutumia haya ni kwa wote ni zana za wote, sio kwamba ni wanaume tu ni wote, akienda kulima sasa atatumia nini, manake majembe kwenda dukani hayapo ni haya ya mila
I: ilikuwa ni miaka gani hiyo ama unakumbuka
R: ni miaka mingi
I: hukumbuki ulikuwa na miaka mingapi kipindi hicho mnatumia mapanga namna hiyo
R: sisi tumekuwa tunayaona
I: kwa hiyo wazee walikuwa wanatumia toka zamani
R: ni kutoka zamani ndio asili yao, sisi tulikuwa tunayaona lakini waliokuwa wanatengeneza walikuwa ni wazee wa zamani
I: wa kama miaka mingapi hivi
R: kwa kuwa ni wazee wazamani inaweza kuwa kama kwenye miaka 40 na kuendelea
I: watoto walikuwa wanatumia mapanga kama haya
R: atakapofanya kazi chombo kama kipo ndani ya nyumba lazima atumie, atatumia chombo gani
I: kwa hiyo waliokuwa wanatengeneza ni wanaume
R: ni wanaume tena wa umri sio kijana, kwa mfano kama kufua vile vyuma, huku wanakofua hakupiti wanawake
I: kwa sababu gani
R: si ni wazee wana miko yao ya kufua vyuma wakizingatia asilia, hata mtoto mdogo haendi huko
I: ni wazee wa umri
R: ni wazee wa umri kulikuwa kuna masharti sio hivi hivi , huko wanakofua vyuma hakupiti mwanamke, hakupiti mtoto mdogo awe wa kuime au wa kike ni mwiko
I: na walikuwa wakipita ni kitu gani kitatokea
R: sijui wenyewe ni siri yao hiyo, hawawezi wakakuambia mpaka ufikie umri wao ndio waeleze, utakapokaribishwa kule wanatengeneza ndio utakapo julishwa
I: na ukiangalia hilo panga lilikuwa linatengenezwa kwa chuma na kitu gani kingne
R: kitu kingine kama, ni kama sasa wanasema unachukua masufuria mabovu unakwenda kuyeyusha ndio wanatengeneza hiyo
I: ulisema unachomeka kwenye mti
R: ee unachonga mti, si kama vile nyengo, sasa lazima uchome uungue iingie kwenye mti
I: ni mti gani ulikuwa unatumia kuchomekea panga
R: kule zaidi sana ni huu ulanzi, unachonga ndio unachomeka hivi,
I: kwa nini ni mti wa ulanzi
R: ulikuwa unatumika na ni mti mgumu
I: na panga la namna hii likiletwa leo unaweza ukalinunua kwa shilingi ngapi
R: bei ndio nisiseme uongo, huwezi kujua, bei utakayoambiwa na fundi mwenyewe ndio utakayo toa
chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research, Interview No. 10
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
-
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
-
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali