Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/1

Kitambaa chenye muundo wa tarizi nyekundu

Sammlung Braun
r 2018 / 18361 b
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18361 b
Kichwa
Kitambaa chenye muundo wa tarizi nyekundu
Vipimo
Upana: 201cm, Urefu: 201cm
Nyenzo
Nguo
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_cdfa60f6-2f12-4046-80aa-fa75fd52a910
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uainishaji
Nguo/Vitambaa  
Uzalishaji
Wakati
mpaka ca. 1920
Mtu
  • Mtu, haijulikani (Mtengenezaji)
Acquisition:
Wakati
ca. 1904 - ca. 1920
Mtu
Mahali
  • Tansania
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
Mahali
  • Stade
Scientific use:
Wakati
2023-06-13
Maelezo
I: Sawa hapa hizo nyingine umeshindwa kuzitambua hapa nimeshika picha iliyosajiliwa kwa namba 2018_18361_b hebu angalia unaweza kutambua ni kitu gani hiki mama [anonymous]? R: Hiki hapa ni kanga I: Hiyo ni kanga? R: Hii ni kanga ambayo imetengenezwa vizuri sana I: Ni kanga iliyotengenezwa vizuri sana? R: Eeeeh I: Unaweza ukatuambia kanga zinatumiwa zaidi na watu wa utamaduni gani? R: Kanga wakina mama ndiyo wanapenda kuvaa kanga I: Kama vile? R: Wasambaa, wapare, yani sasa hivi ni kila kabila I: Kila kabila? R: Eeeeeeh wanavaa kanga I: Kwa miaka ya nyuma? R: Kwa miaka ya nyuma ni wasambaa I: Wasambaa? R: Eeeeh I: Kwanini ilikuwa zaidi ni wasambaa? R: Kwasababu ndiyo nguo ambazo pia zina urahisi ee I: Urahisi upi? R: Wa bei I: Hebu tuambie kanga matumizi ya kanga? R: Matumizi ya kanga ni kuvaa, yani kama kuna harusi unavaa kanga hizi kanga hizi siyo za kutumia nyumbani wanavaa kwenye harusi kama kwenye ngoma basi ndiyo wanavaa hizi kanga hizi I: Kwanini unasema kanga hizi siyo za kutumia nyumbani? R: Kwasababu nyumbani siwanavaa vinaitwa vitenge kaniki lakini zamani walikuwa wanavaa kaniki kwahiyo hizi ni special kwenye maharusi, kwenye ngoma, lakini sanasana za hapo nyumbani wanavaa kaniki I: Kaniki? R: Walikuwa wanavaa kaniki I: Kwahiyo kanga zilikuwa zina matukio maalum? R: Eeeeheee matukio maalum ndiyo mtu anavaa kanga I: Kaniki ndiyo yakushindia nyumbani? R: Eeeeh kaniki ya kushindia nyumbani lakini hizi ni kwenye matukio maalumu ndiyo wanavaa hizi kanga I: Kanga? R: Eeeeeh I: Na kanga ilikua ikivaliwa ukivuta picha miaka hiyo ya kipindi hicho ambacho nyinyi sasa mnawaona wazazi wenu, mabibi zenu walikuwa wanatumia zaidi wanawake wa umri gani zaidi kanga? R: Hizi kanga hizi hata hivyo walikua wanatumia watu wenye uwezo ama huna uwezo huwezi kununua kanga eeh I: Uwezo wa namna gani? R: Kipesa maana zinauzwa ghali labda kama utapewa zawadi lakini sanasana zamani hizo walikua wanavaa makaniki I: Makaniki? R: Eeeeh I: Kwahiyo ukivuta picha kwa miaka 1900 iliyopita unaweza ukavuta picha kanga hizo walikuwa wakivaa watu gani kipindi hicho? R: Wakati wa huko nyuma ambapo mimi pia sinilikuwa sijazaliwa ni wale watu ambao wenye uwezo ndiyo wanavaa hizi kanga hizi lakini kama huna uwezo wa kununua huwezi kuvaa kanga unavaa kaniki ndiyo nguo zilikuwa zinavaliwa zamani I: Zinavaliwa zamani? R: Eeeeh kwenye 1968 ndiyo tuwasichana hapo tumeolewa pia ndiyo hizi kanga watu walikua wanavaa hizi kanga I: Lakini walikuwa ni wachache? R: Lakini walikuwa wachache lakini sasa hivi ndiyo hivo kanga kila mtu anavaa ni vazi kila mtu anaweza kununua I: Labda tuzungumzie hadhi ya mtu aliyekuwa akivaa kanga kipindi hicho ilikuwaje yani mtu akivaa kanga alikuwa anaonekanaje katika jamii? R: Yani mtu huyo anaonekana kuwa ni mtu wa hali ya juu sana I: Aaaaah R: Eeeeh I: Hali ya juu sana mwenye hadhi kubwa? R: Mwenye hadhi kubwa lakini kama huna hadhi hii kanga hata wewe mwenyewe ukiangalia unaona kama ilikua inavaliwa na watu wenye hadhi eeh watu ambao wamesoma sana maana ukisoma sana wanapata hela kwahiyo wananunua kanga hizi au kama ni wake wa wafalme wanavaa hizi kanga I: Wake wa viogozi? R: Eeeeh wake wa viongozi hapo nimekosea wa viongozi wanavaa hizi kanga lakini hapo zamani watu walikuwa wanavaa kaniki I: Kaniki? R: Eeeeeeh I: Na waumri gani walikuwa wakivaa zaidi kanga kwa kipindi hicho? R: Wasichana wa makamo kama miaka 20 na kuenedelea juu lakini miaka 50 huko siyo sana kwenye kuvaa kanga I: Na matumizi ya kanga yapoje hivi sasa ukilinganisha na mika hiyo ya 60s unaweza kusema kanga bado inaendelea kutumika? R: Sasa hivi I: Ndiyo R: Sasa hivi zinatumika sana kanga saivi wanashona, wengine wanafunga, eeh kwahiyo saivi ndiyo zinatumika sana kuliko huko mwanzo I: Kuliko mwanzo? R: Kwasababu zamani zilikuwa haziko nyingi japokuwa sikukutwa lakini zamani zilikuwa siyo nyingi halafu ni gahali eeh lakini sasa hivi kanga kila mtu anavaa I: Anavaa kila mtu? R: Eeeh kila mtu anavaa tena hata hizo kaniki zimepotea I: Mambo yamebadilika? R: Yamebadilika sana I: Kaniki zimepotea kanga zimepatikana? R: Zimepatikana kanga, vitenge watu wanavaa sasa hivi lakini hata hapo mwanzo zilikuwa nzuri sana hata mimi nimezipenda I: Umezipenda? R: Eeeeh I: Kwa kipindi hicho kanga zilikuwa zinatoka wapi? R: Mimi naona kwa huku Tanzania sijui kama labda huko Dar es salaam lakini huku zilikuwa hazipatikani eeh I: Kwahiyo zilikuwa zinaletwa? R: Zinaletwa labda kutoka nje mhh walikua wanaleta kutoka nje lakini wakagi huo naona zilikua adimu sana I: Sawasawa na kwa sasa hivi ni maeneo gani wanatengeneza kanga Tanzania kama unajua sehemu wanatengeneza? R: Tanzania ni sehemu nyingi urafiki Dar es salaam kuna viwanda vingi tu vinatengeneza kanga na vitenge I: Na unaweza ukatambua kanga zinatengenezwa kwa kutumia nyenzo gani ni vitu gani vinatumika kutengeneza kanga? R: Kanga I: Eeeh R: Zinatengenezwa na pamba, mimi naona ni pamba I: Ni pamba? R: Eeeeh ndiyo nyenzo zinatengenezea kanga I: Na pamba kwa Tanzania zinazalishwa mikoa gani? R: Mikoa mingi tu I: Miwili ambayo unaifahamu? R: Nafahamu Mwanza, na Tanga I: Sawa labda unadhani inaweza ikafika wakati kanga ikawa haina thamani kwa jamii za watu ulizozitaja kwa maana ikawa haihitajiki tena kutumika? R: Aaaaaaa itakuwa inatumika tu I: Kwanini? R: Hahahhahahhhah I: Hahahahahha unadhani kwanini itaendelee kutumika? R: Itaendelea kutumika kwasababu ni vazi la kina mama eeh hata akina baba pia wanashona mashati I: Siku hizi mashati ya kanga? R: Eeeeh hizi kanga sasa hivi kuna kanga nzito alafu kama vitenge kwahiyo hii haitapotea tena kanga haiwezi kupotea I: Sawa labda umeangalia hiyo kanga na ukasema inaonekana ni nzuri sana ukiikuta leo dukani kama kama hiyo au ikaletwa ukaambiwa inauzwa wewe utakuwa tayari kununua kwa shilingi ngapi? R: Sasa hivi kanga wananunua kwa shilingi elfu kumi na tano, kumi na saba I: Kumi na saba? R: Eeeeh kanga nzito I: Kanga nzito? R: Eeeeh I: Bila shaka na hii itakuwa nzito maana imetengenezwa kipindi hicho R: Eeeeeh mimi nikiletewa nitainunua hahahahah I: Hahahahah sawasawa basi mama [anonymous] mimi nishukuru kwa hivi vichache ulivovitambua umetupatia maelezo ya kutosha kabisa R: Sawa I: Asante sana kwa ushiriki wako R: Na mimi nashukuru vingine nimekosea kosea lakini nisameheni I: Ni kawaida huwezi ukatambua kila kitu R: Ni siku nyingi sana I: Ni kweli R: Ni miaka mingi

chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023, Interview No. 14
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Amani

Rejeo la ndani la kitu

Kitambaa chenye muundo wa tarizi nyekundu

Kitambaa chenye muundo wa tarizi nyekundu

r 2018 / 18361 a
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:42:01+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji