Wakati
2023-10-03
Maelezo
I: Sawa nina picha nyingine hapa imesajiliwa kwa namba 2018_18267_1 hebu iangalieni hii mnaweza mkaniambia ni nini hii?
R3: Hii ndiyo nilikuwa nasema hata kijana wangu anatengeneza hizi ni nondo na nondo ambazo unatwanga mpaka inatokea hivi alafu huku unatwanga inaviringika inakuwa kali alafu anatafuta mti mzuri ambapo atakavo pekecha hapa hii iingie hapa mpaka ifike hapa inaingia ndani ya ule mti alafu huku chini anaweza akaweka chuma nyingine ile ya kawaida ya mkuki ili iwe na chuma huku na huku ili ukifika mahali unaweza ukakita chini haukiti upande huu unakita kwa chini alafu unaweka ngozi nyembembe hapa kwa juu na unafunga vizuri ikiwa mbichi inakamata vizuri inakaukia hapo hapo mkuki tayari unaweza anza kutumika kwa kujilinda na maadui mbalimbali
I: Na mkuki kwa kimasai unaitwaje?
R3: Embere ila hii ni nyerembe hii lakini nyerembe ni kama huu ambao ni mpana lakini kwa ujumla inaitwa embere lakini ikaitwa nyerembe kwasababu ya hii shape yake ni tofauti na hii ya kawaida hii ya kawaida ni mirefu alafu mwembamba lakini nyerembe ni hii fupi ambayo inakuwa ni pana ndiyo wanaita nyerembe
I: Ile mirefu inaitwaje?
R3: Emberesirwa kwasababu ni mfupi mweupe ambayo ile ni special kwa vijana hawa ambao ni morani
I: Morani?
R3: Eeeeh Morani peke yake
I: Inakuwa ni mirefu sana?
R3: Mirefu kama futi tatu na kitu
I: Ile chuma yake?
R3: Ndiyo ile chuma yake tu
I: Ni kama futi tatu?
R3: Eeeh kama futi tatu ni ndefu siunaona hata wewe ukisimama inakupita kwasababu ni ndefu sana
I: Na kazi yake hasa hii ilikuwa ni nini
R3: Ni silaha tu ya kujihami ila sasa wanatofautisha ya morani naya wazee, wazee wanatumia vitu kama hivi vya kizee zee lakini wale wanatumia ambayo shoo yake ni nzuri nani mikuki ya vijana ni ndefu alafu nyeupe kila saa inasuguliwa inakuwa nyeupe akija kule akifanya hivi inamulika mulika eeh sasa akiwa na mkuki namna hiyo dah wasichana wakiona wanasema aaah basi ndiyo hivo tena
I: Hahhha emberesirwa
R3: Eeh emberesirwa hii ni nyerembe alafu kuna nyerembe special ambayo imetengenezwa kwa mikuki ya kawaida lakini hapa haijafanywa hivo imewekwa yenyewe inaingia kwenye mti inashikilia pale na ile nayo ni nyerembe pia maana hata mikuki ya kawaida hiyo haitumiki kwenye mti ila inaingia upande wa juu na upande wa chini
I: Na mti uliokuwa unatumika kutengenezea mikuki ya namna hii inaitwaje namba tatu hebu tuambie?
R3: Mikuki ya vijana wale morani sasa nitakupeleka mbali sisi wamasai tuna rika mbalimbali kuna rika hii kuna rika hii alafu kuna nyinyi sasa wa morani wale ambao ndiyo wamorani hasa wanaomiliki katika jamii yao mikuki yao ni mweupe alafu mpini ni mweusi sasa wanapokuja kupata rika lingine maana wanafuatana hii rika kubwa na hii ndogo hawa wa rika ndogo hawaruhusiwi kubeba mkuki wenye mpini mweusi ukikutwa umebeba mkuki mweupe na mpini mweusi na wewe ni rika ndogo unapingwa na ule mkuki unakatwa ule mti hauruhusiwi kwasababu wewe bado ni rika dogo na hili rika kubwa wao wanaonyesha kwasababu wameshapewa idhini ana control familia nzima ni morani wanafahamika ni wakubwa wao wanaweza kuweka mikuki yao mipini mweusi na wanabeba mikuki mweupe lakini yule asiye na mkuki mweupe anabeba nyerembe pia lakini siyo mara nyingi hizi nyerembe mara nyingi zinatumika na wazee na vijana wale ambao hawajapata tohara na hawa vijana wadogo ambao hawajapata tohara wanapata wale wakubwa mikuki yao ni mweupe lakini miti ni fimbo kama hii maana hujaruhusiwa hawa wakiwastop kwenye umorani na kuingia kwenye stage ya wazee sasa ndiyo wataingia nafasi ile wataanza kuweka mikuki yao miti mweusi ndiyo utaratibu tulio nao hata ukiwauliza hawa watakuambia hivo
I: Kwahiyo nyerembe inatumiwa na vijana na wazee?
R3: Eeeeeh na wazee mikuki mweupe na mirefu niya morani na wanaweka miti mweusi ukiona mkuki wa morani mweusi ujue ni senior, jonior hawezi kuweka mti mweusi mpaka wafikie stage ya kuwa seniour kuna wakati wanaendelea hawa wanakuwa stage ya wazee ambao wanakuwa junior bado hawajafikia uzee lakini wametoka kwenye morani hawa ndiyo wanaingia wanakuwa senior ndiyo peke yao wanaruhusiwa kupata hali hiyo
I: Kwahiyo ile ya morani umesema inaitwaje?
R3: Hii ya morani inaitwa Emberesirwa
chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 08
mwandishi: I: Mohamed Seif, R1, R2: Anonymous
Mtu
-
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
-
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali