Wakati
2023-06-09
Maelezo
I: basi asante ngoja tuchukue tena picha nyingine, hapa nina picha nyingine ya kingine kifaa ambayo imesajiliwa kwa namba 2018_18346_001, hebu angalia unaweza ukatambua ni kitu gani hicho
R: hii ni nyengo ndio kama ile niliyokuambia kwamba anaweka mpini mkubwa halafu anatumia kufyeka
I: umewezaje kuitambua
R: nimeweza kuitambua kwa sababu nimewaona wengine kama ile ya kwanza wamechomeka kwenye mti kama hii ndio wanafanya vitu na nyingine ziko kama hivi hivi za kufyekea
I: nyengo ya namna hiyo inatumiwa zaidi na watu wa makabila gani
R: hii nyengo hii naona ni ya watu wa iringa ambao wako huku, kuna mmoja mmoja bado wanazo hizi
I: unaweza ukataja majina ya hayo makabila
R: wabena
I: kwa hiyo wabena ndio wamezitumia zaidi nyengo hizi
R: na wahehe
I: na unaweza ukanieleza kidogo matumizi yake kwa uzuri zaidi
R: matumizi yake hii ni kufyeka pori, maana hii unaweza kufyeka huku umesimama tofauti na pnga au fauno, unafyeka huku umeinama
I: unadhani kwa nini imetengeezwa na mpini mrefu kiasi hicho
R: hapo sasa siwezi kuelewa nafikiri labda ni urahisishaji tu kwa yeye mwenyewe .
I: na ni jinsia gani hasa walikuwa wakitumia nyengo hizo kubwa
R: ni jinsia ya kiume
I: kwa nini wanaume
R: wanatumia wnaume kwa sababu zaidi inatumika kufyekea msitu , na msitu sana sana unafyekwa na wananaume ni tofauti na kufyeka, sasa ukiingia kweny pori unakuta wanaume ndio wanatangulia kwanza
I: ni umri gani hasa wanaotumia nyengo kubwa za namna hii
R: hata wakubwa
I: wa umri gani ukikadiria labda
R: niliwaona mimi ni kuanzia miaka45
I: kwa nini wa umri huo
R: sijajua inawezekana huko iringa labda na watoto pia wanatumia, kwa huku nilioina ni umri mkubwa kwa hapa kwetu
I: na kwa mawazo yako unadhani inaweza ikafika wakati nyengo ya namna ikawa haitumiki tena kwa watu wa kabila hilo la wabena ulilolitaja
R: watu wa kabila hili hizi wanaziona kama jadi na wao, kusema kweli hizi kuziacha ...kuna moja wapo hapa alikuwa nazo...
I: tukimaliza hapa tutaenda kwake tukazione
R: sawa sawa tutakwenda kuuangalia,niliwahi kumuona nayo hii tena atakwenda kutuonyesha
I: kwa hiyo ni sehemu ya jadi
R: ee ni sehemu ya jadi na wao kwa sababu hizi wamezileta wao wabena ndio tunawaona nazo, sisi wote tunaiga tunaweza tukanunua au tukachonga, unampelekea fundi unamwabia nichongee hiki chuma unitengenezee kama nyengo , na anakutengenezea kama hivyo unaweka mpini na ukatumia
I: na ili utumie nyengo kubwa ya namna hiyo unatakwa uwe na kitu kingine
R:ni nyengo tu, kwa sabab hii inatakiwa ushike na mikono miwili, kwa hiyo kama unakitu kingine kinakuwa hakina nafasi
I: wabena bado wanatengeneza nyengo za namna hiyo
R: kwa hivi sasa nafikiri bado wanaendelea, hapa naona wameacha labda kama mtu kama unashida nayo kwa ajili ya msitu, unamuona fundi, unamuagizia chuma chochote unamuona fundi anakutengenezea
I: na wanaotenegeneza hizo nyengo kubwa ni watu wa jinsia gani
R: hizi kwa sababu zimetoka huko nafikiri wazee wanafahamu wa kibena, ni wakubwa tu na sidhani kama watoto pia wanatengeneza
I: ila kwa huku umesema kuna mafundi wanatengeneza
R: huyu kijana anatengeneza
I: ni mbena
R: ee
R2: hii ni mundu
R: mundu si ndio panga
R2: sawa lakini hii kwa kilugha ukisema mundu wanaelewa ni hii yenye mpini mrefu
wote: anha
R2: ni ya kufyekea kwenye bustani tunaitumia hiyo
I: mundu, ni kilugha gani hicho
R2: mundu ni kiswahili lakini kule kwetu mundu tunasema ni nyengo
I: ni kibena hicho
R2: ee nyengo, nyengo hii hapa kwa lugha ya kibena, kihehe wanaita nyengo, wakinga wanaita 'sidavala'
I: inatumikaje nyengo ya namna hii
R2: hii ni kwa kufyekea magugu kama unataka kulima kwenye mabonde hivi, unafyeka
I: kwa nini inampini mrefu
R2: kama unakofyeka ni shamba kama inamiba isikuchome ndio maana unafyeka kule unavuta, hii ndio yenyewe
I: hebu tuambie ni jinsia gani wanatengeneza nyengo
R2: wanaume,wanatenegeza wazee zamani
I: wa umri gani
R2: wa umri mkubwa, ya huku wanafua vyuma ndio hizi, unaweza kuwa na chuma bovu bovu unapelekwa kwa fundi anakwenda kufua anatengeneza inakuwa hii
I: na wanao tuma zaidi ni wakike au wa kiume
R2: wakiume, hata wa kike kufyeka, hii inatumika kwa watu wote
I: na unaweza ukaniambia ni vitu gani vinatumika kutengeneza nyengo
R2: ni vyuma vilivyoharibika unapeleka kwa mafundi ndio wanatengeneza
I: ni chuma peke yake au kuna kitu kingine
R2: zile za zamani kabisa wanatengeneza vyuma vinachemka wana mashine
I: vitu vilivyokuwa vimetumika kutengenezea nyengo zamani kwa sasa ni hivyo hivyo ama wamebadilisha siku hizi
R2: wamebadilisha, sasa hivi si chuma wanaunganisha
I: nyengo kama hiyo ukiikuta sokoni kwa sasa hivi unaweza ukainunua kwa shilingi ngapi
R2: kwa bei ndio haijulikani nisisemem uongo, bei atakayokuambia itabidi mpatane lakini kwa huku hakuna hizi zinatoka nyumbani bara huko
I: ni mikoa gani hasa wanatengeneza
R2: kuanzia iringa kwenda njombe kwenda mpaka kote mpaka upanga, makete, ukinga, hizi kule ndio zinatumika sana hizi
chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023, Interview No. 10
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous, R2: Anonymous
Mtu
-
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
-
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali