Wakati
2023-10-03
Maelezo
I: Sawasawa asante ngoja tujadili picha moja ya mwisho ili tukaendelee na majukumu mengine nina picha nyingine hapa ambayo imesajiliwa kwa namba 2018_18238_1 hebu nikumbusheni jina la hiki kitu?
R1: Sasa hiki kitu ni kama desturi moja ya kimasai wakati mtoto anaanza kukua kutoka kwenye utotoni na kuelekea kwenye kijana kwenda kutahiriwa anaweza sasa akavalishwa hiki kikaninginizwa tu hapa shingoni anavaa siku ya kwanza ya pili siku nyingine inatolewa wanapewa watoto wengine siyo kitu ya kudumu nacho baada tu ya kuvalishwa lakini inavaliwa kwa kipindi hicho.
I: Siku akiwa anaenda wapi?
R1: Siku ile akiwa anaenda kutahiriwa yani kuna aina ya mifugo baadhi ambayo zinasindikiza kama mbuzi ambo wanaitwa lailibono sasa mkishatoka wanaita orikitukubene ndiyo siku hiyo unatoka sasa unavalishwa hii baada ya mbuzi kuchinjwa ikisha chinjwa hii miti inatolewa sasa yani kwa tafsiri nyinyi mnasema ni udongo lakini hatujakuta hizo tumekuta njia yake ya kuendeleza ni kama tunda la miti ulani.
I: Mti huo unaitwaje?
R1: Olikimogiki sasa ndiyo inapekechwa sasa ikishapekechwa inawekwa ile uzi hadi inakamilika.
I: Uzi gani ulikuwa unatumika kuweka?
R1: Yani ni igonoti ngozi iliyokwanguliwa ngozi ya kondoo.
I: Ngozi ya kondoo?
R1: Eeeeh ikishaanza kuwekwa anavaa baada sasa ya kwenda kutahiriwa yani siku hiyo unaimbiwa ukiwa nayo unalala usiku na siku hiyo unaimbiwa bila kuvaa nguo moja ila tu hiki kipo shingoni.
I: Huna nguo yoyote?
R1: Huna nguo hata moja unapingwa na baridi mpaka asubuhi saa kumi na mbili unaelekea pale uangaliwe ujasiri wako kama utaweza kukubali ile kisu upingwe tu bila kunungunika na bila sindano hasa ndiyo siku hiyo unatolewa yote hayo yalikuwa yanafanyika kupima ujasiri wako ulionao.
I: Kwahiyo ilikuwa ni kwa ajili ya vijana wa kiume tu?
R1: Eeeh yoyote wa kiume hata wasichana ila wasichana hawatoi nguo kwanza hawaruhusiwi na hawaimbiwi kabisa.
I: Anayeimbiwa niwa kiume tu?
R1: Eeeh wa kiume tu yani unateswa tu ili kupata hasira ili kama una hasira kabisa yani unadamka asubuhi uwe unangangana na ile kisu eeh ya yule jamaa anayetahiri na haitakiwi sindano aa unabaki hivyohivyo saa kumi na mbili au sa moja moja ndiyo sasa uonekana kwamba unaweza huogopi kisu.
I: Kwahiyo akisha tahiriwa hiyo anavuliwa?
R1: Eeeeh anatolewa.
I: Siku hiyo hiyo?
R1: Eeeh anatoa hii anapewa malaiyoni.
I: Namba mbili ilikuwa ina umuhimu gani?
R2: Unajua zamani vijana kama hajatahiriwa anakaa sana kwa vijana ndiyo wanafanya vitu vingine vya ajabu ajabu anaua ua vitu hovyo hovyo kwahiyo hiyo ni kitu kilichokuja kufaa hii akiamka asubuhi kuna maji fulani anaoshwa na hii maji fulani akioshwa na maji fulani ndiyo anatoa hii.
I: Maji gani hayo?
R2: Haya ni maji ambayo haichemshwi yanakuwa ya baridi lakini kuna chuma fulani anapoweka haya maji.
I: Chuma hiyo inaitwaje?
R2: Inaitwa endolu wengine wanaita ondido anapoweka anavooshwa na haya maji baridi na atatoa hizi vitu au wakisema vitu vya watoto sirudii tena kufanya maana chochote ulichofanya wakati wa utotoni ndiyo anasema anaomba msamaha leo anaviacha wakati bado hajatahiriwa sasa hivi anakuja kuingia kwenye uwanaume fanya kazi yoyote hiyo yote maana unakuta akipita paka vitu vingine haviliwi ndiyo atakuwa ameoshwa siku hiyo hutakiwi ukiwa mwanaume kila kitu ule ule lakini usile kitu ambacho hakiliwi katika jamii yetu ya kimasai maana ni dhambi kwako maana hiyo katika sisi wamasai kwa mila yetu tunasema tunajaribu kuacha vitu vilivyofanywa na vijana.
I: Khaa historia ndefu hahhha kwahiyo ilikuwa ni kama kumuosha kumtakasa na yale yote aliyofanya?
R2: Kabisa.
I: Akitoka hapo anakuwa mweupe?
R2: Kabisa kabisa mweupe.
I: Sawasawa na wanaowaosha ni watu gani?
R1: Sasa hiyo kuosha ni sio mtu mkubwa ambaye ametahiriwa ile maji ambayo inawekwa ile kitu kama shoka aina ya ulimi wa shoka na chuma ambacho kina mpini kidogo wa kijiti sasa ile maji ni kwamba ni kama sindano fulani lakini haina sindano ni kama ile pedoli ya baskeli ichongwe kabisa iwe ni kama chuma yenye ukali kabisa sasa ile inachukuliwa yale maji yanatundikwa kwenye baridi.
I: Kwenye mti au kwenye nini?
R1: Juu ya nyumba na yanalindwa na mtu, mtu anawekwa wakulinda yale maji yani yanawekwa kuanzia sa mbili ya usiku yanapingwa na baridi mpaka saa kumi na mbili ya asubuhi na hayachemshwi yani kitu chake kinachofanyia kuweka yale maji kwenye friji ni ile chuma baada sasa ya kutoka kwenda nje ya boma kutahiriwa unaenda nje ya boma kidogo yale maji unamiminiwa kuanzia kichwani na haitakiwi kusema yani kusikia kwamba niya baridi yani wewe tu uone kama maji ya moto kwahiyo hutakiwi kunungunika wala kufanyaje alafu ile safuria unaipiga teke moja yani ukishamaliza kumiminiwa na yule kijana mguu mmoja unaambiwa unapiga na mguu huu tu.
I: Mguu gani?
R1: Mguu wa kushoto ndiyo unaotumika katika kupiga sufuria huwezi ukapiga na mguu wa kulia.
I: Maana yake nini kupiga na mguu wa kushoto?
R1: Yani hivyo vitu ni kama uhalifu fulani wa vitu ambavyo havina maana ulivyovifanya ukiwa utotoni kama kuua kitu ambacho hakifai kuua umekitesa na kukiua bure ni kheri uue kitu ambacho kinaliwa lakini kama umeua kitu ambacho hakiliwi au kama punda hauli nyama na umeua paka hauli nyama, pundamilia hauli nyama, na umeua sasa ndiyo unajaribu kuyasafisha hayo yote umetoka kwenye hilo group la kufanya ujinga unaelekea sasa kwenye group la waerevu unapiga sasa teke safuria na mguu wa kushoto unakimbilia sasa kwa yule dakitari anaeenda kukutahiri sasa ndiyo taratibu za hivyo vitu katima mila na desturi katika jamii yetu ya kimasai.
I: Sawasawa na hizo walikuwa wanatengeneza wakina nani?
R1: Hii ni mama anatengeneza na maji ni mama anayelinda mpaka asubuhi yale maji ya kulala nje kutoka saa mbili usiku anayalinda pale yalipowekwa mpaka saa kumi na mbili asubuhi ndiyo anamkabidhi anayehusika hatakiwa kuondoka na kuyaacha yenyewe maana hayatakiwi kuguswa kabisa.
I: Mama ndiyo analinda mpaka aje sasa mzee mmoja wa kuchukua na kwenda kumkabidhi layoni wa kummiminia yule mtu.
I: Mpaka sasa bado vinatumika hivi?
R1: Hiyo inatumika kabisa.
I: Sawasawa.
R1: Kwasasa hivi unajua wanawatoa watu kwa group kwahiyo sahivi bado miaka mitatu ndiyo waanze tena maana unajua magroup ya rika yakitolewa inaweza ikawekwa kuanzia miaka sita mpaka saba yani watu wamekatwa hakuna kutahiriwa tena hadi miaka mingine ya kutahiri itakapofika.
I: Mpaka miaka sita ikifika tena?
R1: Ndiyo mpaka miaka saba ikifika tena watu wameshaanza kukua wameshatanuka akili kidogo hilo group na lenyewe sasa ndiyo wananza sahivi wanatoa tena garanteen ya miaka mitatu kutahiriwa au ,miaka minne kutahiriwa hilo group lingine tena ikishafika miaka minne yani watu wa mila wanajua kwamba sasa hivi tunako elekea tushatahiri watu miaka minne mfululizo wanaenda kuingilia watoto wadogo ambao hawafai kutahiriwa ilibidi tufunge kabisa moja kwa moja mpaka miaka mingine ili watu wakue vizuri nawakomae kiakili ndiyo waweze kutahiriwa tena.
I: Sawa labda tumalize na namba tatu hebu tupe historia kidogo ya olimokogiki naam karibu sana namba tatu?
R3: Unajua hawa wameshaeleza vizuri kwasababu wanawatengeneza wakati wa kutahiriwa kwahiyo hawa wameshaeleza.
I: Sawasawa namba nne ni hivyohivyo au kuna cha kuongeza.
R4: Wameelezea vizuri kwasababu wamepitia hali moja ambayo inaitwa olimokogiki ambayo wanavaa kipindi wakati huyu kijana anatahiriwa wa kimasai kwasababu inakuwaga mara mbili wakati sasa anaenda kutahiriwa kuna dume linachinjwa hapo tayari imeshabarikiwa naya pili ambayo ndiyo olimokogiki ndiyo inatumika ambayo ni dume la kondoo ndiyo sasa inafanyika hapo ili uweze kwenda kutahiriwa kwahiyo hapo wameelezea vizuri kwasababu unatumia hiyo mpaka ile siku unatahiriwa mwisho unakaa nayo siku mbili inakuwa kazi yake imeshaisha kabisa kwa wakati huo eeh.
I: Kwahiyo hilo dume la kondoo linachinjwa kabla ya kutahiriwa au baada ya kutahiriwa namba nne hebu tuambie?
R4: Kabla hujatahiriwa yani siku hiyo kama ni jana ndiyo dume la ng’ombe limeshabarikiwa sasa hii siku ya pili ndiyo linachinjwa hili dume la kondoo ambalo linatumika siku moja hiyo siku unaenda siku ya tatu unaingia kwenye kutahiriwa ndiyo mila na desturi za jamii ya kimasai zilivyo.
I: Sawasawa asante sana namba nne umeongea kidogo taarifa ndiyo maana ya kufanya kwenye kundi kama hivi mwingine akisahau mwingine anakumbushia sawasawa basi mimi nichukue fursa hii kuwashukuru tumejadili picha nyingi kidogo na muda umekimbia najua kuna nyingine zimebaki lakini tutaendelea kwasababu tuna makundi mengine yanayofuata naamini tunaweza tukapata taarifa hizo kwahiyo mimi niwashukuru kwa muda wenu asanteni sana na kwa maelezo mazuri mimi nimetokea kuipenda hii kazi maana najua mila na desturi za watu sahivi kwahiyo nashukuruni sana kwa muda wenu.
R: WOTE: Sawa.
I: Asanteni sana.
R: WOTE: Haya.
chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 06
mwandishi: I: Mohamed Seif, R1-4: Anonymous
Mtu
-
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
-
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali