Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/1

Mkanda wa shanga katika muundo wa zigzag

Sammlung Braun
r 2018 / 18205
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18205
Kichwa
Mkanda wa shanga katika muundo wa zigzag
Nyenzo
Kioo shanga
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_6b069950-3a97-4fc5-b52c-139ca76b3a45
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uainishaji
vito vya kikabila  
Uzalishaji
Wakati
mpaka ca. 1920
Mtu
  • Person (Mtengenezaji)
Mahali
  • Tansania
Acquisition:
Wakati
ca. 1904 - ca. 1920
Mtu
Mahali
  • Tansania
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
  • Hansestadt Stade (Mkopeshaji)
  • Museum Schwedenspeicher (Mkopaji)
    GND Explorer
  • Bohmbach, Jürgen (* 1944) (Mkopeshaji)
    GND Explorer
  • Gerd Mettjes (Mkopaji)
Mahali
  • Stade
Scientific use:
Wakati
2023-09-15
Maelezo
I: Nina picha nyingine hapa imesajiliwa kwa namba 2018_18205_1 hebu mzee [anonymous] iangalie hii? R2: Hii ni Engimeta I: Inaitwa Engimeta R2: Tunasema elong’ongoi I: Engimeta au elong’ongoi? R2: Aaaa ni mshono tu huo I: Mshono ndiyo unaitwa Elong’ongoi? R2: Eeeeeh I: Engimeta? R2: Engimeita ondoye yani ya wasichana imeshonwa kwa alama ya kingao I: Ina maana gani hiyo alama ya kingao? R2: Ni mtu anapenda kuweka alama hiyo anaweka ili apendeze I: Urembo? R3: Eeeh au ni ile ya kufunga hapa kwenye kiuno au kufungia nguo hapa ni ngozi ya zamani maana zamani ilikuwa wasichana wanavaa ngozi na hii inafungwa juu ya nguo ndivyo ilikuwa inafungwa hivyo I: Ni kwa ajili ya wasichana tu? R2: Eeeeh ni wasichana tu I: Kwasababu gani walikuwa wanatumia wasichana tu? R2: Nikuonekana kwamba ni alama ya wasichana maana wakina mama haifungwi hivi ni wasichana tu ndiyo wanafunga haya na ni msichana ambaye bado hajaolewa tu ndiyo wanaofunga hivyo I: Kuanzia miaka mingapi? R2: Kuanzia miaka 17 R3: Tena miaka 17 ni mkubwa ni miaka 13, 14, 15 maana sasa miaka 17 sianaelekea kwenda kwa bwana eeh I: Kwahiyo akishaolewa haivai tena hii? R2: Haivai tena kwasababu ameshakuwa mke wa mtu haifai tena hii I: Kwahiyo mzee [anonymous] umesema ni mshono wa ngao? R2: Mshono wa ngao elong’o I: Kwanini ilikuwa inatengenezwa kwa mshono wa ngao? R2: Imetengenezwa kwa kupenda au kurembesha kuchukua hiyo na hii ya ngao I: Kwahiyo akishaolewa havai tena? R2: Havai tena I: Kwahiyo walikuwa wanatengeneza kwa kutumia shanga na kitu gani kingine mzee [anonymous] hebu tuambie? R2: Wametumia shanga na hii anayoshonea ni ngozi ambayo imewambwa vizuri ikawa laini ndiyo sasa unatengeneza hii sasa alafu na kutengeneza nyuzi za aina fulani ndiyo anasukia hapo eeh I: Ni ngozi ya mnyama gani ilikuwa inatumika? R2: Ya ng’ombe I: Ni ng’ombe peke yake? R2: Eeeeh ni ngombe peke yake I: Kwanini ng’ombe peke yake? R2: Hakuna nyingine yenye ngozi kama hii kwasababu mbuzi haifai na kondoo haifai kutumika kutengenezea I: Na waliokuwa wanatengeneza hizi ni kina mama au wakina baba? R2: Wakina mama R3: Mama anamtengenezea msichana wake anamshonea lakini baba ananunua huu ushanga anampa mama I: Baba analeta ushanga mama anatengeneza? R2: Eeeeeeh ili msichana wake aoenekane na mwenzake I: Ili apate bwana haraka au? R3: Hata kama hakumpata lakini apendeze na kitu kizuri hakijifichi I: Kwahiyo jukumu la utengenezaji wa hii ilikuwa nila baba na mama? R2: Eeeeeh I: Baba analeta shanga R2: Mama anatengeneza anapewa msichana I: Sawasawa na akishaolewa hii anaiacha? R2: Anaiacha kwa mama yake na kama ana mdogo wake anamuachia kama hana anamuachia tu mama ili ushanga utumike kwa matumizi mengine I: Na gharama yake hii inaweza ikawa shilingi ngapi mzee […]? R2: Inategemea na wakati huo ilikuwa pesa ndogo ila sasa hivi imekuwa pesa nyingi I: Na shanga sasa hivi zinauzwa kwa kiasi gani? R: Hatujui kwa sasa hivi ni shilingi ngapi I: Kwani sasa hivi hazitengenezwi hizo? R2: Wanatengeneza kama biashara maana ukienda Mgagao unakuta zimetengenezwa zinauzwa pia I: Kwahiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kupendezesha? R3: Eeeh na Mgagao ukienda kununua ni laki moja I: Ukiwa umekamilika? R3: Eeeeh laki moja I: Kwahiyo walikuwa wanatengeneza wakina mama umri gani hasa? R2: Inategemea ufundi wa mtu R3: Alafu na hawa wa mama marika kwasababu wale wazee sana hawatengenezi kwanza macho yao hayaoni I: Kwahiyo mpaka leo vinatumika hivi? R2: Vinatumika

chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No.
mwandishi: I: Mohamed Seif, R2: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Mnazi
Scientific use:
Wakati
2023-10-04
Maelezo
I: Nina picha nyingine hapa ambayo imesajiliwa kwa namba 2018_18205_1 hii kuna mmoja wenu aliitambua pia inaitwaje hii? R3: Engimeta I: Nani anaweza kutuambia engimeta inatumikaje? R2: Hii engimeta ni mama ndiyo anashona na enopini ndiyo anashonea msichana kwahiyo unashona kama niya msichana wako unashona hiyo unaweka lukaria alafu unampa msichana avae. I: Msichana ambaye ameolewa au ambaye hajaolewa au msichana kwa kimasai ni yule ambaye hajaolewa? R2: Ni msichana ambaye hajaolewa. I: Anaivaa sehemu gani? R2: Kiunoni. I: Anavaa kiunoni? R2: Eeeeh. I: Kwa ndani ya mwili au nje ya mwili? R2: Anavaa nje ya nguo. I: Na unaweza kutuambia huo mshono unaitwaje? R2: Hauna jina huu mshono. I: Anavaa mpaka muda gani akiolewa bado anaendelea kuivaa hiyo engimeta au anaachana nayo? R2: Akishaolewa siyo msichana tena kwahiyo anaitoa. R3: Engimeta mama ukishamzaa binti utamuangalia akishafikia umri wa miaka 10 utaona kwamba huyu anahitaji kuwa na engimeta kwahiyo unaanza kuandaa ngozi yako na kukata ili umtengenezee engimeta ukishatoa kiasi ya kiuno chake unaishonea ushanga alafu unampa anavaa akishafika ule umri wa kuwa siangiki sasa siyo binti tena na hafai kuvaa tena hiyo engimeta kwasababu sasa nimaandalizi ya kuolewa sasa anaacha nyumbani yeye anaenda kuolewa. I: Anamwachia nani? R3: Msichana mwingine ambaye ni mdogo wake. I: Kwahiyo akiolewa haiendi nayo kwa mume wake? R3: Eeeh haendi nayo. I: Ilikuwa ina umuhimu gani engimeta? R1: Engimeta ina maana kadhaa engimeta msichana akiwa mkubwa haruhusiwi tena kwenda sehemu inaitwa esoto kwenda kuungana na morani bila engimeta hiyo ndiyo maana yake katika jamii ya kimasai. I: Inaitwaje? R1: Esoto, na esoto ni sehemu ya mkusanyiko wa morani na wasichana, msichana kama anenda kulala na morani anaweza kutoa ile engimeta ataiweka juu ya kitanda kuna mbao ambayo iko juu ya kitanda zamani sisi ambavyo ilikuwa nyumba ya matope siyo sasa kwa ambaye ana ya majani au mabati hapana zamani kuna nyumba za matope ambayo inatengenezwa inawekwa matope na majani hivi na unafunika na matope huyo msichana anaenda kuiweka kwenye kitanda ambacho analala naye na morani pamoja hairuhusiwi msichana ambaye amekuwa kwenda kulala na morani lakini awe na engimeta inatakiwa iwe inaninginia kwenye kitanda kwahiyo engimeta hakuna mama ambaye anaona mtoto wake amekuwa lazima anatoa ngozi yake anapasua anatoa hii ngozi anashonea msichana wake engimeta baada ya kumaliza anafanya kama hivyo namba tatu anaweka udongo ambao unaitwa lukaria anatengeneza lukaria alafu anaweka kwanza mafuta ndani siyo nje ya shanga ndani ya ngozi ataweka lukaria ataweka kamba nyingine ndefu itakuwa tayari anampa mtoto wake avae hairuhusiwi kama mtoto amekuwa ameenda kwa mume wake haruhusiwi tena kuvaa ushanga kama waswahili maana waswahili sasahivi mwanamke ambaye ni mwanamke wa mtu anavaa ushanga ndani ya sketi ndani ya kiuno lakini wamasai hawaruhusiwi mpaka sasa hivi kwahiyo ina maana sana kwa msichana wa jamii ya kimasai hii engimeta. R3: Engimeta ina mambo mengi mazuri na engimeta ina umuhimu mwingi kwa mfano pia kwa wanaume wanavopelekwa jandoni akiwa bado hajawa morani akiwa kwenye stage ya sipolio sasa ndiyo ameshaenda tu jando sasa lazima avae engimeta na hiyo ndiyo inamfanya sasa huyu mwanaume kuonekana tayari ameshaenda jando na amekuwa na vile vile kwa msichana akivaa anaonekana pia amekuwa mkubwa kwahiyo ina baraka kama hizo katika vijana wa jamii hii ya kimasai. I: Kwahiyo hiyo inavaliwa na mtu ambaye ameshaenda jando? R3: Kwa wanaume ndiyo anavaa akienda jando lakini kwa wasichana ni kwamba ni ile hali ya kuonekana tu amekua lakini hajafanyiwa tohara na morani akishatolewa nywele spolio na yeye anarudisha hii. I: Kwahiyo akisha nyolewa anavua hii? R3: Eeeeh. I: Na umesema inavaliwa juu ya nguo? R3: Eeeh juu ya nguo. I: Ni nguo aina yoyote anaweza akavaa? R3: Eeeeh nguo yoyote kama orekelaa maana orekelaa ni ngozi maana kuna watu wanavaa ngozi anafunga kiunoni. R1: Kwasababu zamani sisi kama tunavaa engimeta na orekelaa tunaenda sikukuu hatutavaa nyingine juu hivi hata kama ana matiti kiasi gani anavaa ushanga anavaa orekelaa hapa kiunoni na anaweka engimeta ili aende kwenye sikukuu kwahiyo ina maana sana katika jamii yetu hii ya kimasai. I: Bado hii inatengenezwa mpaka sasa hivi? R1: Mpaka sasa hivi. I: Na inatumika kwa utaratibu huo huo mlioueleza? R1: Kabisa. I: Kwahiyo wanaoshona hii ni wakina mama? R1: Ni mama. I: Mama yake na binti? R1: Mama yake binti au kama yeye mwenyewe ana kazi nyingine anaweza kumuomba rafiki yake amsaidie kumshonea binti yangu engimeta analeta na ushanga wenyewe wanasaidia kushona lakini wanasaidiana tu siyo kwa namna nyingine tunasaidia tu kama kazi nyingine kwenye jamii.

chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 10
mwandishi: I: Mohamed Seif, R1, 2: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Kimokouwa
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1906-06-04, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 47 (44)jifunze zaidi

Rejeo la ndani la kitu

Mkanda wa shanga

Mkanda wa shanga

r 2018 / 18542 a
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Mkanda wa shanga

Mkanda wa shanga

r 2018 / 18542 b
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Mkanda wa shanga

Mkanda wa shanga

r 2018 / 18398 a
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Mkanda wa shanga

Mkanda wa shanga

r 2018 / 18398 b
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Apron ya shanga

Apron ya shanga

r 2018 / 18412
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:51:44+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji