Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/1

Mfuko uliotengenezwa kwa manyoya

Sammlung Braun
r 2018 / 18300
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18300
Kichwa
Mfuko uliotengenezwa kwa manyoya
Vipimo
Urefu: 29cm, Upana: 25,5cm
Nyenzo
Ngozi
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_95e9e778-de2c-420f-8c28-a977e4ff33e9
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uainishaji
Vyombo/hifadhi (kazi ya jikoni)  
Uzalishaji
Wakati
mpaka ca. 1920
Mtu
  • Mtu, haijulikani (Mtengenezaji)
Mahali
  • Tansania
Acquisition:
Wakati
ca. 1904 - ca. 1920
Mtu
Mahali
  • Tansania
Malipo
Mtu
Nambari za hesabu za zamani
  • 155
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
Mahali
  • Stade
Scientific use:
Wakati
2023-06-09
Maelezo
I: Hapa ninapicha nyingine ambayo imesajiliwa namba 2018_18300_1 hebu angalia unaweza ukatambua ni kitu gani hicho? R: Ni mfuko uliotengenezwa na aina ya Ngozi I: Ni mfuko ulio tengenezwa na ngozi unaweza ukafahamu jina la mfuko huu? R: Mh hapana I: Hapana R: Eeeeh I: Unaweza ukahusisha na tamaduni za watu gani mfuko huu? R: Labda wanaoweza kutengeneza vitu kama hivi niseme labda wamasai I: Wamasai? R: Eeeeeeh I: Mikoa gani wanapatikana Zaidi watu hawa? R: Mikoa wanayopatikana wamasai mikoa ya Kilimanjaro, mikoa ya Tanga, I: Unaweza ukafahamu matumizi ya mfuko huu? R: Matumizi ya mfuko huu ni kuwekea vitu mbalimbali eeh I: Kama vitu gani vinaweza vikahifadhiwa huku? R: Kama ni mwanamke ni mkoba wa kusafiria unaweka vifaa vyako vya aina zote unavyotaka kusafiri navyo I: Sawasawa nani jinsia gani wanaweza wakatumia mfuko wa aina hiyo kwenye jamii ya kimasai? R: Hapa ninaweza sema jinsia ya kike eeh na wenye umri kuanzia miaka kumi na nane na kuendelea I: Unadhani inaweza ikafikia kipindi kifaa hicho kikawa hakina thamani na kutumika tena katika jamii ya kimasai? R: Sidhani kwasababu hiki kifaa hakiwezi kikatoka thamani kwasababu ni kifaa ambacho kina umuhimu kwao siyo kwao tu hata kwa wengine kwahiyo huwezi kama sisi wanawake huwezi ukatoka bila mkoba maana yake hapo nitaweka vitambulisho vyako utaweka sijui kalamu zako vitu vya aina mbalimbali tuseme hela zako utaweka hapo kwahiyo hiki sioni kama hakina thamani kina thamani wakati wote I: Thamani wakati wote kwa mantiki hiyo kinaendelea kutumika hivi karibuni umewahi kuona mikoba kama hiyo inaendelea kuzalishwa? R: Kwa kweli sijawahi kuona sijawahi kuona kwasababu muda mrefu niko huku na hizi wan apenda kuzalisha watu wa mikoa ile ya Kilimanjaro kwa upande wa wamasai I: Nawanaotengeneza ni wamasai wa kike au kiume Zaidi Zaidi? R: Kwa kweli sijawahi kuwaona ila nimewahi kuona wakiwa wanauza I: Wanauza? R: Eeeeh sasa sijajua wanaotengeneza ni mwanamke au mwanaume I: Sawasawa umetaja nyenzo iliyotumika kutengeneza hao kwamba ni ngozi ni nyenzo gani nyingine unaona imetumika hapo? R: Mimi siwezi kujua I: Tukipe thamani tukikadirie thamani ya huo mkoba umeletwa umeenda sasa hivi ukaukuta ukaupemda unaweza ukaununua shilingi ngapi? R: Hapa hata elfu kumi nanunua I: Kwanini? R: Kwasababu ngozi ni kitu ambacho kinadumu kwa muda mrefu alafu hakiishi thamani yake I: Kwahiyo hata ikikaa miaka mia ijayo kitaendelea kuwa na thamani ile ile? R: Eeeeeh ukiwa mtunzaji I: Kama ni mtunzaji? R: Eeeeeh

chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023, Interview No. 03
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Amani
Scientific use:
Wakati
2023-09-15
Maelezo
I: Ahaa historia hiyo hahhha sawasawa zimebakia mbili tunamalizia na nimeshika picha nyingine hapa imesajiliwa kwa namba 2018_18300_1 mzee [anonymous] na mzee [anonymous] kinaitwaje hiki kwa kimasai? R1: Oribene I: Oribene ni kikapu? R1: Eeeh ni kitu cha kubebea vitu hii wakina mama wanaweka hapa na hii inakuwa mgongoni anatembea nayo I: Kamba inawekwa kichwani alafu R1: Mama anatembea tu kama kawaida ipo mgongoni ama unawekea vitu vyako kipindi hicho vitu kulikuwa hamna huoni imewekwa kama wanasema kifungo osegerai I: Inaitwa osegerai R1: Unafungua pale unaweka vitu vyako vyote na hii imeshonwa kwa kutumia ngozi hiyo nimeiona sana hiyo eeh imepotea tu juzi juzi kwenye miaka ya 1980-1988 ni juzi juzi tu vikaja masafleti hii ikaachwa I: Na ilikuwa inatumiwa na wanawake tu? R2: Ni wanawake tu au kama mzee unashonewa unaweka ndani unaweka dawa ya ng’ombe kipindi hiko hakuna pochi unaweka na ukiweka ndani hakuna mtu anayegusa hiyo unakuwa umehifadhi I: Ilikuwa ni ngozi ya mnyama gani? R2: Ng’ombe na kondoo na mbuzi yani ngozi yoyote tu na hii imenyolewa kabisa tena sanasana ni ile ngozi ya ndama kwasababu ndiyo laini kidogo huwezi linganisha na ngozi ya ng’ombe mkubwa I: Na waliokuwa wanatengeneza hivi vikapu oribene ni wakina nani? R2: Ni wakina mama I: Kuanzia umri gani? R2: Umri kuanzia miaka 20 mtu akiwa na shida ya kikapu analeta ngozi anakata anaikunja katikati maana hii tumeiona anaanza kushona mbembeni huku anashona hadi anamaliza tayari kikapu kinakamilika I: Kwasasa hivi havipo tena? R2: Havipo ila kama ukitaka unatengenezewa kama zitakuwa zinahitajika lakini sasa hivi hakuna I: Sawasawa na umesema ni kwa ajili ya kuwekea vitu vidogo vidogo tu ndani? R1: Eeeeh I: Sawasawa nani ngozi hata hii kamba ni ngozi pia? R1: Ni ngozi yote I: Hiki kifungo ndiyo umesema kinaitwa? R1: Osererai I: Sawasawa, na hivi walikuwa wanavipata wapi vifungo? R1: Kwenye bahari ni vingi hivyo I: Baharini? R1: Eeeeh ni nyingi sana ukienda Tanga unaokota tu lakini kwenye mnada kule Arusha wanauza lakini hii sanasana inapatkana kwenye bahari I: Sawasawa kwasasa hivi nikitaka kutengenezewa kama hii ninaweza nikatengenezewa kwa shilingi ngapi mzee [anonymous]? R2: Inategemea utakavyo kwenda kuongea na hao wanaotengeneza mimi siwezi kukuambia inatengenezwa shilingi ngapi kwasababu mpaka niwaeleweshe watu wajue watake hapo ndiyo nitakuelewesha ndugu yangu lakini nikwambie wanatengeneza kitu Fulani na wakti mtengenezaji siyo yeye I: Hahahha unaweza kusema bei hii alafu kule ikawa ni tofauti? R2: Eeeeh inakuwa ni udanganyifu I: kwahiyo ngozi ya ndama ndiyo inatumika? R1: Ndiyo ni nyepesi kidogo

chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 01
mwandishi: I: Mohamed Seif, R1, R2: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Mnazi
Scientific use:
Wakati
2023-09-28
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Mnazi
Scientific use:
Wakati
2023-09-29
Maelezo
I: Nina picha nyingine hapa imesajiliwa kwa namba 2018_18300_1 hebu bibi iangalie hiyo inaitwaje hiyo? R2: Hii inaitwa Olbenee I: Olbenee? R2: Eeeh ya kubebea kama anaenda sokoni anabebea hii chakula kila kitu anaweka hapa sukari yako, unajaza hapa unaweka kichwani unaenda bila shida yoyote kwahiyo hii ilikuwa inasaidia kubebea vitu I: Huo mkanda ndiyo unaweka kichwani R2: Eeeeh huu mkanda ndiyo unaweka hapa Olbenee inakaa mgongoni basi tayari na safari inaendelea I: Olbene hahha R2: Eeeeh alafu hii ni Esikirai I: Hiko kifungo hicho? R2: Eeeh Esikirai I: Na hiyo inatengenezwa kwa kutumia ngozi ya mnyama gani? R2: Ya mbuzi I: Kwanini ngozi ya mbuzi? R2: Ndiyo nzuri inatoa I: Hhahaha R2: Eeeeh walikuwa wanatumia kuanzia zamani hata mtu anataka sasa hivi kama anataka anashona tu ya ngozi na ngozi ya ng’ombe haifai niya mbuzi tu ndiyo inayotumika kutengenezea hiyo I: Niya mbuzi tu? R1: Eeeh kwasababu ndiyo laini I: Inakuwa ni laini kuichonga vizuri? R1: Eeeh I: Olbenee? R2: Eeeh Olbenee I: Na wanaotumia Olbenee ni wanawake au wanaume? R2: Wanawake I: Wakuanzia umri gani? R2: Kuanzia sisi sasa hivi hata mtu yoyote anabebea I: Kuanzia miaka 30? R2: Eeeh na kuendelea I: Na wanaotengeneza ni kina mama pia? R2: Eeeh ni akina mama I: Mwanaume hawezi kutengeneza au haruhusiwi? R2: Hapana hawezi I: Kwahiyo umuhimu wake ulikuwa nikubebea vitu? R2: Eeeeh I: Ukienda sokoni? R2: Kama unaenda safari yako unabeba oribene kama unaenda kuleta mwali ndiyo unaenda kuweka chumba yote ya mwali hapa I: Ukienda kuleta mwali unaweka vitu vyake hapa? R2: Eeeh anabeba mgongoni R1: Kibuyu nini unaweka hapa unaenda na mwali wako I: Sawasawa na ilikuwa kwenye mila na desturi za Wamasai ilikuwa inachukua nafasi gani? R2: Hii ni mila ya zamani tena kama unabebea chombo chako hapa hakinyeshewi na mvua kabisa yani I: Maji hayaingii hapo R2: Hapana I: Sasa hivi wanatengeneza hizo? R2: Eeeh kama mtu unataka wanatengeneza I: Mpaka mtu akitaka lakini R2: Eeeeh I: Kwahiyo siku hizi mkienda kuchukua mwali hamtumii tena hizo mama [anonymous] hebu tuambie hapo? R2: Wanatumia lakini siyo wote lakini si mabegi ndiyo yamejaa dunia imebadilika tumeacha mambo ya kale sisi zamani tukienda kwenye sherehe unavaa ngozi ya mbuzi basi unaenda kwenye sherehe sasa hivi mtu unachukuwa nguo nzuri unavaa unapendeza ndiyo unaenda kwenye sherehe R1: Akiamua hata sahivi hadi keshokutwa ashaishona anaenda kuletea mwali lakini sasa hivi wanasema ngoja tuache kwasababu hawajui kushona Olbene na mbadala wake umeshapatikana I: Kwahiyo mtu akitaka umtengenezee kama hiyo bibi Katepoi unaweza ukatengeneza kwa shilingi ngapi? R2: Hii baba tena ngozi ya mbuzi sasa hivi sinaenda kununua maana siku hizi wazee hawachinji mbuzi nyumbani kama zamani, zamani wazee wanachinja kila siku mbuzi mama kama amejifungua anachinja au wazee wanajazana kwenye boma wanachinja wanapata ngozi ya mbuzi sasa hivi buchani tu ndiyo unaenda kununua ngozi unakuja kukwangua hiyo nywele nitoe zote labda kama amesema nisitoe nywele kama anasema nisitoe nywele nanunua tu nakuja kutengeneza kabisa mpaka nashona mpaka inakuwa oribene lakini kama anasema toa manyoya yake ni kazi sasa I: Kazi nyingine? R2: Eeeh maana unatafuta mti unaisimamisha hii alafu anatafuta ile kama shoka ndiyo unakwangua mpaka ile nywele yote inaisha ikishaisha sasa ndiyo unaanza kuitengeneza sasa Olbenee

chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 05
mwandishi: I: Mohamed Seif, R1-3: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Mnazi
Scientific use:
Wakati
2023-10-03
Maelezo
I: Sawa nina picha nyingine hapa ambayo imesajiliwa kwa namba 2018_18300_1 hebu ishike tumpe namba mbili na yeye atuambie unaweza kutuambia ni kitu gani hicho mama kwa kimasai kinaitwaje? R2: Olbenee I: Olbenee ni nini? R2: Ni mfuko tu wa kubebea vitu Olbenee sasa ilikuwa inatengenezwa kule ilikuwa inatumika pia kwa uelewa wake zinatumika kutengenezea pombe ya kienyejo unaweka maji unaweka zile dawa za kutengenezea pombe alafu unafunika inawekwa mahali inaanza yenyewe kujipika hiyo pombe ndiyo hizo dawa ambazo zinawekwa zile mizizi ya alovera ile mizizi ya alovera inawekwa ndani alafu zinaanza kujipika I: Ndiyo inakuwa pombe? R2: Eeeeh inakuwa pombe na itakuwa inajipika yenyewe inatoa sauti ya du, du, kwahiyo kumbe inatumika kutengenezea pombe kwahiyo ndiyo kazi yake hiyo I: Kwahiyo ilikuwa ni kwa ajili ya vitu lakini pia kwa ajili ya kutengenezea pombe pia hiyo Olbenee? R2: Eeeeh I: Namba tatu unataka kuongeza kitu kwenye Olbenee? R3: Huu mfuko zamani ulikuwa unaitwa Olbene Olimokora yani zamani hii ilikuwa inawekwa tu pombe inaletwa asali maana zamani kulikuwa hakuna sukari ni asali ndiyo inatumika unaweza kuleta debe la asali unamiminia unaleta debe tano za maji au sita maana ni kubwa unaweka na hizo dawa nyingine zinawekwa ndani sasa inaachiwa tu maana inatundikwa inawekwa kamba pale, pale kila mahali kamba inawekwa juu ya nyumba sasa inabaki sasa inaning’inia hivi eeh sasa unasikia inachemka yenyewe maana ikiiva inanyamaza haiendelei tena kufanya hivo inanyamaza ndiyo maana yake I: Na ilikuwa inatengenezwa kwa kutumia nini? R3: Ngozi ya ng’ombe I: Na waliokuwa wanatengeneza hizi Olbenee walikuwa ni jinsia gani hasa wa kike au wakiume kwenye jamii? R1: Olbenee jinsia ambayo walikuwa wanatengeneza ni wanaume I: Wa kuanzia umri gani? R1: Ni wazee walibuni wao kitu kama hiki maana hii ilikuwa inatumika kabla hawajajua kwamba kuna vibuyu vilikuwa vinaota linaota likibuyu kubwa ambayo inaitwa orimosori kabla hawajapata hivyo vibuyu ndiyo hii walikuwa wanatumia hii kuloweka pombe zao kipindi hicho zamani I: Na waliokuwa wanatumia ni kina mama peke yao au na kina baba pia walikuwa wanatumia hiyo oribene? R1: Wa baba ndiyo walikuwa wanaloweka hamna mama anayeloweka pombe ni kina baba ndiyo walikuwa wanaloweka pombe maana wao walikuwa wanajua kiasi cha asali itakayoingia maji kiasi gani inawekwa wao ndiyo walikuwa wanatengeneza hakuna mwanamke alikuwa anatengeneza pombe ni wababa ndiyo walikuwa wanatengeneza na wao siku ya kuja kuonja kutext kama imekuwa tayari au bado ni wao I: Na ilikuwa inakaa baada ya muda gani kufahamika kwamba imekuwa tayari? R1: Wakitengeneza hii kubwa inaweza ikachukua mwezi mmoja kubwa lakini na kuna ambayo inaweza ikachukua mwezi maana wanatengeneza ile origino ya asili siyo kitu chepesi hapana maana wao walikuwa hawatumii kuuza walikuwa wanatumia kwa manufaa yao kama mtu alikuwa na sherehe ndiyo wanaloweka pombe kuingiza watoto jando ndiyo walikuwa wanatumia au kama msichana anaolewa ndiyo walikuwa wanatumia eeh kwahiyo walikuwa wanatumia kwa manufaa yao

chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 07
mwandishi: I: Mohamed Seif, R1-3: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Longido
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:35:49+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji