Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/1

Kisu na ala

Sammlung Braun
r 2018 / 18290
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18290
Kichwa
Kisu na ala
Vipimo
Urefu: 58cm
Nyenzo
Chuma
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_b698dad6-aa3a-4d53-a465-03e76b43c852
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uzalishaji
Wakati
mpaka ca. 1920
Mtu
  • Person (Mtengenezaji)
Mahali
  • Tansania
Acquisition:
Wakati
ca. 1904 - ca. 1920
Mtu
Mahali
  • Tansania
Malipo
Wakati
ca. 1904 - 1920
Mtu
Nambari za hesabu za zamani
  • 297
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
Mahali
  • Stade
Scientific use:
Wakati
2023-09-15
Maelezo
I: Sawasawa nina picha nyingine hapa imesajiliwa kwa namba 2018_18290_1 hebu shika mzee [anonymous] unaweza kutuambia hiyo ni nini? R2: Hii ni sime I: Kimasai mnaiitaje? R2: Arabanga na hii ni ala yake na hii alalemu au arabanga I: Arabanga ndiyo sime? R2: Eeeeeh I: Na Alalemu? R2: Hii Arabanga ni sime alafu hii ni nyumba yake I: Nyumba yake inaitwaje kwa kimasai? R2: Enjahuru I: Na kazi yake hii hasa ilikuwa ni nini? R2: Ni kutunza tu hii sime isidondoke au isimkate ni hiyo tu I: Na sime kazi yake hasa mlikuwa mnaifanyia nini? R2: Ina kazi nyingi unaweza ukakuta miba inaweza ikakuchoma unaweza kuona fimbo unatumia kukatia na kama huna panga ila una kitu cha kukata unakata kwa kutumia sime unachomoa tu unakata yani ni mbadala wa panga I: Sawasawa na kwa maeneo haya ya Lushoto ni maeneo gani unaweza ukapata sime kama hii kwasasa? R2: Hapa bwiko ipo nyingi tu I: Bwiko? R2: Eeeh Mkomazi hapo kuna mnada siku ya jumatano alafu na sehemu za Mombo pia unaweza ukapata I: Wanaotengeneza ni kina nani? R3: Ni wengi sana waarusha wanaleta ni biashara hiyo na sisi tunanunua pale R2: Hata mimi naweza kutengeneza hii I: Sawasawa kutengeneza hii unatengeneza kwa kutumia nini na nini labda mzee [anonymous] hebu tuambie? R2: Unatengeneza kwa kutumia maana nilivyotengeneza mimi nimetumia mashine nilipunguza kwanza unene nikapasua panga alafu ndiyo nikachukua tupa kama tatu ndiyo nikatengeneza sasa sime I: Kwahiyo inakuwa hii yenye makali ni chuma ya aina gani unatumia? R2: Ni panga tu unachukua panga alafu unapasua kwa kutumia msumeno au na mashine ya umeme I: Ni panga? R2: Eeeh ni panga I: Alafu huku kwenye mshikio huku? R2: Hapo tunapasua pamoja na miti yake alafu sasa ndiyo unaanza eeh unapasua unaweka miti eeh hii ni miti ukiamua kutoa hiyo miti alafu ndiyo unatengeneza upya tena unafanya hivyo kama unashindwa unapasua zile miti za panga kwa pande zote mbili alafu inabakia hii ya katikati ambayo ina msumari R3: Alafu siumeona kuna ngozi fulani imevalishwa basi ni mkia wa ng’ombe huo ndiyo unaotumika I: Mkia wa ng’ombe? R3: Ndiyo unauchomeka ili uimarike zaidi hata ukikata kwenye mti ikikauka inashika hasa ukikata miti haipasuki inakuwa steal inaimarika I: Kwahiyo ni mti wowote tu unaweza ukawekea? R2: Eeeh unaweza ukawekea I: Na hii ala yake mnatumia ngozi ya nini? R3: Ng’ombe au mbuzi I: Kwanini ngozi ya ng’ombe au mbuzi? R2: Inakuwa imara ya kondoo hapana kwasababu ni nyepesi sana inapasuka haraka lakini ya mbuzi ni steal naya ng’ombe ndiyo mwisho kabisa kwasababu ngozi ya ng’ombe ni ngumu kuliko ya mbuzi na kondoo I: Kwahiyo ukikosa ya ng’ombe unachukua ya mbuzi? R2: Eeeh ya mbuzi eeh lakini haikai ya ng���ombe ndiyo nzuri I: Sawasawa na mnashona na uzi wa namna gani? R2: Tunatumia uzi kama inayotengenezwa hii ya sulphate unatoa sulphate uzi unatengeneza alafu unashona na sindano I: Kwahiyo mpaka leo mzee [anonymous] unatengeneza hizi? R2: Natengeneza haina shida I: Nikitaka unitengenezee kama hii unaweza ukanitengenezea kwa shilingi ngapi mzee [anonymous] hebu tuambie? R2: Hii sasa kama unataka nitakuuzia kwa pesa ndefu I: Shilingi ngapi? R2: Nitakuuzia kwa shilingi elfu sabini I: Sawasawa na waliokuwa wanatumia hii ni vijana wa kiume tu? R2: Hata sisi hata mimi ninayo ya kwangu nyumbani eeh I: Kina mama hawaruhusiwi kutumia? R2: Sanasana ni wanaume wanatumia wanawake hapana hawaruhusiwi kabisa kutumia ni wanaume tu I: Hawatumii sime wanawake? R: Eeeeeh I: Kwanini kina mama hawatumii sime? R2: Wanawake ni mtu wa kukaa nyumbani sasa hizi ni silaha mtu anatembea porini na muda mwingine unatembea usiku ni silaha ya kukulinda wewe ukikutana na mnyama mbaya au na majangili huko basi unapambana nao I: Sawasawa kwahiyo wakina mama hawatakiwi kabisa kugusa? R2: Ndiyo I: Na kwenye maswala ya mila na desturi za kimasai maana kila mtu naona ana sime usipokuwa nayo kuna shida? R2: Hakuna shida kama huna siyo lazima I: Haina ulazima? R2: Ni kwa kupenda mtu haina ulazima kwamba kwanini usiwe nayo hakuna bwana ni kupenda tu kwa mtu I: Labda kwenye mila na desturi za kimasai kuna hadhi yake mtu ukishika au ukiwa na sime kiunoni na vitu vingine? R2: Haina ulazima lakini kwa vijana inapendeza uwe na sime kwahiyo sanasana kwa kijana huwezi kwenda bila shime kwasababu kwanza ni silaha kwa upande wa silaha alafu inapendeza kijana akifunga kiunoni

chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 02
mwandishi: I: Mohamed Seif, R1-3: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Mnazi
Scientific use:
Wakati
2023-10-03
Maelezo
I: Sawasawa nina picha nyingine hapa imesajiliwa kwa namba 2018_18290_1 namba moja karibu R1: Hii ni Sime au alalemu na hii ni ala yake ambayo anaweka enchashuu na hii ni kamba yake ya kufungia engene na hii Sime mpaka sasa naonyesha niliyonayo kiunoni ina kazi nyingi kwamfano moja ukihamisha mifugo kupeleka sehemu kama orijoo au maboma mapya unatumia kutengenezea boma, kukata masanzu ya kutengenezea boma naya pili ukija kukutana na chakula kama nyama unaitumia pia kukata kata ili uweze kula kwahiyo ndiyo kazi zake za hii Sime lakini pia namna ya utengenezaji wa ala hii ala haitengenezwi tu hivihivi kuna aina ya miti wanaita olitimaroi sasa wanachonga ile miti kwa huku ya saize ya hii Sime yake alafu ukishachonga unatafuta ngozi ya ng’ombe mbichi unakuja sasa unaanza kuishonea sasa ndiyo itakuwa ala ya hiyo Sime I: Na hiki ni chuma gani kinachotumika kutengenezea? R2: Hii ilikuwa niya mkuki ilikuwa ni ncha ya mkuki ilikuwa imechongwa ili itengenezwe hiyo Sime ni ndefu na ninyembamba na katika kupigana na huwa wakitaka kupiga kitu kwa umbali hasa wale wenzetu wa huko ndiyo wanaotumia Sime ya staili hii ni ndefu sana ni nusu ya hii meza ukikaa hapa utakuta yenyewe iko kule sasa wao akichomoa hii anakanyaga kidogo inabendi akitoa inaenda vibaya lazima itakufuata vibaya kwahiyo hao ndiyo wanatumia hii na kwa kawaida Sime yoyote ambazo tulizonazo huwa wapo wajuzi wanachonga panga alafu inatokea Sime lakini hawa vitu viwili wanatumia nondo wanatwanga nondo mpaka inatokea hivi au wanatumia vyuma vingine ambavyo ni vigumu na bapa wanatwanga alafu wanachonga wanachonga inatokea Sime kama hii kwahiyo wanatumia nondo katika kutengeneza Sime kama hii I: Sawasawa na huo mpini wake? R2: Na huo mpini ni kama huo mti walivyokuambia wanauchukua wanakata alafu wanapasua alafu wanachonga wanachonga alafu wanaacha inakauka alafu wanakuja wanachonga inakuwa nyembamba alafu wanakuja wanaweka pamoja wanapima Sime ilivyo ndefu alafu wanapima ngozi mbichi ya ng’ombe alafu wanaishonea alafu wanamwagia maji ya moto alafu wanachukua yale mnyoya alafu wanachukua rangi nyekundu wanapaka I: Inakuwa ala tayari? R2: Eeeeh I: Huu mkono niwa kushikia? R2: Huku kwenye mkono inakuwa na vitundu, vitundu alafu wanachongea vijiti ambavyo ndiyo mpini wakishachongea wanaweka na msumari wake wanafunga alafu wanachukua sasa mkia wa ng’ombe ile sehemu nyembamba wanatoa ile ngozi wanavalisha hapa alafu wanafunga na uzi sasa ukiona utaona kama ina misitari kwasababu wamefunga na uzi na inakauka ikiwa na msitari na baadae ikikauka wanatoa wanakata huku vizuri wanafunga vizuri tayari kabisa kwa kuanza kutumika I: Na waliokuwa wanafanya kazi hizi ni wanaume? R3: Ni wanaume hii ni kazi ya wanaume tu siyo wanawake na wanawake hawajui kabisa kuhusu hii I: Ni wanaume kuanzia umri gani R3: Ukishakuwa kijana yoyote ambaye amepata tohara lazima atanunuliwa Sime na baba yake sasa siku hizi hawatengenezi wao isipokuwa wananunua mnadani ikiwa imeshatengenezwa na ala tayari lakini utengenezaji wa ala wanajua kutengeneza wenyewe kwahiyo inayonunuliwa inakuwa ni Sime tu I: Bado zinatengenezwa hivi sasa Sime kama hizi zinapatikana kwenye meneo ya kwenu hapa namaba tatu tuambie? R3: Hizi nyembamba hizi sidhani ila kwa wakenya zinapatikana kwasababu wanapenda kutumia hizi lakini kijana wangu anatengeneza Sime kama hii hata hawa wazee wanaweza wakatengeneza ila wazee hawawezi kutwanga vyuma I: Nguvu zimepotea kidogo? R3: Nguvu zimepotea I: Sawasawa na ka mfano Sime kama hii kwa mfano ikiletwa sokoni inaweza ikauzwa shilingi ngapi? R3: Sime ya kawaida kama hii inaweza kuuzwa elfu ishirini au elfu ishirini na tano inategemea tu na muuzaji I: Sawasawa R3: Hata mnadani ukienda unazikuta zipo

chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No.08
mwandishi: I: Mohamed Seif, R1-3: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Longido
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1909-04-05, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 53 (43 )jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566 (123)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1905-02-24, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 44 (68)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Baun, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1905-02-24, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 44 (68)jifunze zaidi
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:41:32+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji